Mama alimmwagia mtoto wake maji ya moto
Leo inatokea Buguruni Dar inahusu mama ambaye
amekuwa na tabia ya kumtesa mtoto wake wa kiume kwa kumchoma na maji ya
moto kitendo kilichofanya majirani kushikwa na hasira na kuamua
kumsaidia kijana huyo kwa kumpeleka Polisi akatoe taarifa.
Majirani hao wamesema kijana mmoja
alipigiwa simu na mtoto huyo ambae ni rafiki yake na kumweleza kuwa
alimwagiwa maji ya moto saa tisa usiku na mama yake, wakampeleka Polisi
na kupewa PF3 ya matibabu.
Kijana huyo amesema kuwa mama yake
alimgongea mlango usiku na kumuuliza alikoweka pasi, akajibu kwamba
hajaiona na kuondoka baadaye alimgongea tena na alipofungua alimwagia
maji ya moto na kumtoa nje, halafu akafunga mlango.
Mjumbe ambaye amejitolea kukaa na kijana
huyo amesema kuwa sio mara ya kwanza mama huyo kufanya tukio kama hilo,
alishawahi kuwatibu watoto wake wawili majeraha ya moto ambao walienda
nyumbani kwake baada ya kuwachoma na mama yao, kwa sasa mama huyo
anashikiliwa kituo cha Polisi.
No comments:
Post a Comment