Kuna ishu ya Mikocheni inahusu msichana aliyetapeliwa Pesa
Jumanne
ya February 03, leo inatokea Mikocheni Dar inahusu
msichana aliyetumwa na bosi wake kwenye kibanda cha huduma za simu ili
akamuwekee hela, akamuwekee hela kwenye simu yake ya mkononi na kukutana
na vijana ambao walimrubuni na kumtapeli fedha pamoja na simu.
Bosi huyo amesema kuwa alimpa shilingi
laki nne akamuwekee kwenye simu yake lakini baadaye alirudi na kumwambia
kuwa ameibiwa, hakuamini kwa kuwa haikuwa mara ya kwanza kumuagiza
msichana huyo, akakasirika na kutaka kumpeleka Polisi.
Msichana huyo amesema kuwa alikutana na
kijana mmoja ambaye alimuuliza kama anamfahamu mzee mmoja ambaye
alimtajia jina, yeye akasema hamfahamu, muda huo huo akatokea kijana
mwingine ambaye aliwaaambia kwamba wanaonekana kama wana matatizo,
akawaambia waongozane nae ili akawatatulie matatizo yao.
Walifika sehemu kijana wa kwanza
akaambiwa aache vitu vyake aende mbele kisha akarushe jiwe, akaenda
akarusha na kukuta vitu vyake viko salama, yule msichana naye akaambiwa
aache vitu vyake akarushe jiwe, akaenda aliporudi hakuwakuta wote
wawili.
Bosi wake alienda kwenye kibanda cha
simu alikomuagiza, msichana anayehudumia hapo akaema alimuona binti
huyo akipita akiwa ameongozana na vijana wawili lakini baadaye alirudi
akiwa analia, walipomuuliza aliwaambia kuwa ameibiwa.
Baada ya ushahidi huo bosi wake aliamua kumsamehe msichana huyo.
No comments:
Post a Comment