Ule ugonjwa wa kuvuja kwa nyimbo za
wasanii ambacho hazijakamilika au muda wake wa kutoka bado time hii
imemkuta Ney wa Mitego baada ya wimbo wake mpya uitwao Only One kuenea
kwenye mitandao mbalimbali.
Akiongea mapema leo alisema; “Mimi
sijawahi kuvujiwa na wimbo kiukweli kabisa labda kitambo sana kipindi
hicho nilikuwa sina nguvu kubwa yaani kujulikana, lakini kwa mara ya
kwanza imenikuta juzi, ni wimbo wangu mpya Only One ambao niliimba kwa
hisia zangu mwenyewe ukiangalia ni wimbo ambao upo kwenye maadhi ya
R&B nikasema nahitaji kuimba wimbo wa mapenzi, sikuweka akili kabisa
kama nitakuja kuutoa rasmi lakini mipango yangu ilikuwa kama nitakuja
kuutoa kwenye albam yangu inshallah Mungu akijaalia…
Sasa
nashangaa kuona wimbo umeshatoka bila ruksa yangu yaani upo tayari
kwenye mitandao, nahisi utakuwa ni utaratibu wa studio ndio chanzo cha
kuvuja kwa wimbo wangu….’alisema.
No comments:
Post a Comment