Thursday, April 30, 2015

AKUTWA AKIWA HAI BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI KWA SIKU 5

Kijana mwingine kakutwa hai baada ya tetemeko kuangusha Hoteli Nepal, unajua kafukiwa siku ngapi??

Earthquake survivor Pema Lama, 15, is rescued by the Armed Police Force from the collapsed Hilton Hotel, a result of an earthquake in Kathmandu, Nepal April 30, 2015. REUTERS/Navesh Chitrakar
Pema Lama, ameokolewa baada ya kufukiwa na jengo lililokuwa Hoteli ya Hilton iliyoko Kathmandu, Nepal
Pole kwa watu wetu Nepal, stori kutoka huko ni za kusikitisha kwa zaidi ya wiki moja sasa hivi.. tangu limetokea tetemeko watu zaidi ya 5,000 wamefariki, wengine zaidi ya 10,000 ni majeruhi.. hii ni idadi kubwa sana ya watu.
Kingine kilichopewa sana headlines ni kuhusu kuokolewa kwa kijana mmoja, umri wake ni miaka 15.. Pema Lama amekutwa akiwa hai, alikuwa amefukiwa na kifusi kilichotokana na kuanguka kwa jengo la ghorofa ambalo lilikuwa ni hoteli.
Kijana huyu kapatikana siku tano baada ya kutokea kwa tetemeko hilo.
Hii imerudisha matumaini kwamba katika watu ambao hawajapatikana mpaka sasa huenda kuna watakaopatikana wakiwa wazima.. kingine ambacho kilikuwa stori kubwa sana kwenye vyombo vya habari duniani ilikuwa kupatikana kwa mtoto mchanga wa miezi minne.. mtoto huyo alifukuliwa toka kwenye kifusi akiwa hai siku ya Jumapili April 28.
adaptive-comp-template-two-way-1-762x428
Hutopitwa na habari yoyote inayonifia na niko tayari kukutumia muda na wakati wowote kupitia hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment