Kuku anatembea amebinua kichwa chini, imemshtua anaefuga.. Kisa nini?
Kama wengi tunavyofahamu kuku ni ndege
ambaye hutembea akiwa ameinua kichwa chake juu lakini katika mji wa
Kisumu nchini Kenya kuna tukio la kuku mmoja ambaye amewashangaza wengi
kwa kutembea shingo yake ikiwa imeelekea chini.
Tofauti na kuku wengine kuku huyo
anatembea kichwa chini na wakati mwingine anaruka kama anacheza
sarakasi.. mfugaji wa wa kuku huyo amesema tukio hilo linampa wasiwasi,
anahofu kumchinja kwa kuhofia shingo yake kupinda kama ya kuku huyo.
No comments:
Post a Comment