Magazeti yanaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga. Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na kwa wale ambao wanajiendeleza kielimu. Pia kituo kinatoa kozi ya Kiingereza na Computer. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746.
JAMBOLEO
Mtoto mwenye umri wa miaka 13 amekamatwa
usiku akiwa uchi kwa madai kuwa alikuwa akiwanga katika duka moja
lililopo kijiji cha mpunguti Mkoa wa Mbeya.
Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa
mtoto huyo ni mzoefu kwa kuwa wafanyabiashara wamekuwa wakipotelewa na
fedha katika amzingira ya utata ambapo walitenga mtego ili kubaini
upotevu huona kumbaini akiingia kwenye duka moja ambalo linadaiwa
kuzindikwa.
Taarifa za awali kutoka kwa wakazi wa
eneo hilo walidai taarifa za mtoto huyo ambaye alikuwa anaishi na bibi
yake aliyemfukuza kutokana na tuhuma za ushirikiana na kukimbilia
msituni kutokana na kukosa pa kuishi.
Inasemekana motto huyo aliishi misituni
kwa zaidi ya miezi mitano ndipo aliporejea na kuolewa lakini ndoa yake
haikudumu kutokana na maisha kuwa magumu na akaamua kuanza mbinu za
kichawi kwa kuibia watu.
Alianza kufungua kufuli za maduka kwa
kutumia kidole gumba huku akiwa uchi na alinaswa na kupelekwa kwenye
ofisi za kata ambapo anashikiliwa hadi sasa.
NIPASHE
Mwanamke mmoja ambaye alimpiga kichwani rais Nicolas Maduro kwa embe ameahidiwa nyumba mpya kutokana na matatizo yanayomkabili kufuatia tukio hilo la aina yake nchini Venezuela.
Rais huyo mwenye miaka 52 alikuwa
akienda basi kupitia kwenye kundi la watuwiki moja iliyopita kwenye moja
ya majimbo nchini humo na ndipo mtu mmoja katikati ya watu hao
alipotupa tunda hilo na kumpata.
“Marleny
Olivo alikuwa na tatizo la nyumba yake, na walimuita lakini mwanamke
huyo aliogopa na hakuamini kama ilikuwa ni kweli,Nimeidhinisha nyumba
kwa ajili yako kama sehemu ya misheni ya ujenzi wa nyumba nchini
Venezuela” alisema rais huyo MADURO huku akiapa kulila embe alilorushiwa na mwanamke huyo.
Tukio hilo limevuta hisia ya watu wengi kwenye mitandao ya kijamii nchini humo huku likiambatana na utani kila wakati.
NIPASHE
Watanzania waliokuwa wanaishi nchini
Afrika kusini jana wamerejeshwa nchini kufuatia mashambulizi ya wazawa
dhidi ya wageni yanayoendelea nchini humo.
Kundi hilo liliwasili jana majira ya saa 11 alfajiri katika uwanja wa ndege na shirika la ndege la Fastjet.
Taarifa iliyotolewa na kitengo cha
mawasiliano cha Serikali kupitia Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano
wa kimataifa kilisema watanzania hao walikuwa wakiishi katika kambi ya
dharura nchini humo.
Walisindikizwa kurudi nchini na ofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Elibahati Lowassa na zoezi lilisimamiwa na kuratibiwa na Ubalozi.
MWANANCHI
Wakati viongozi wajuu wa CCM wakiendelea
kulalamikia makada wanaowatuhumu kutumia fedha kujifagilia njia ya
urais, mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward Hoseah amesema taasisi yake inakusanya taarifa zote za wanachama wa chama hicho tawala wanaotuhumiwa kutumia mlungula.
Mara kadhaa viongozi wa juu wa CCM
wamekuwa wakiwaonya wanachama wao dhidi ya makada wanaotumia fedha
kujitengenezea mazingira mazuri ya kupitishwa na chama hicho kugombea
urais, lakini wameeleza kuwa hawawajibiki kuwaripoti Takukuru kwa kuwa
ni wajibu wa chombo hicho cha kuzuia na kupambana na rushwa kufanyia
kazi malalamiko hayo.
Jumatano, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nnauye
alisema Takukuru hawahitaji kupata mwaliko wa CCM ili kufanya uchunguzi
wa kukamata wagombea wanaotumia rushwa ndani ya chama hicho kwani
rushwa inayoendelea kwa sasa iko wazi.
“Kazi ya kuwafuatilia imeshaanza muda mrefu, tunazo taarifa zao za kutosha kwa kila mwanasiasa anayelalamikiwa,” Dk Hoseah
Dk Hoseah alisema kwa muda mrefu
Takukuru imekuwa ikifuatilia mienendo ya wanasiasa wanaotaka uongozi
kupitia chama hicho na ambao wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo vya
rushwa.
Alisema Takukuru kwa sasa inaendelea na
kazi yake ya uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo huku ikikusanya taarifa za
kila mwanasiasa anayeonekana kutuhumiwa na vitendo vya rushwa.
“Siyo
kwamba Takukuru haijaona wala haisikii malalamiko ya viongozi CCM.
Tunajua wajibu wetu na kazi ya kuwafuatilia imeshaanza,” Dk Hoseah.
“Sheria
ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 imekataza wazi kwamba, ni makosa
kutoa chochote kama zawadi kwa kundi la watu, vinginevyo ni kukiuka
sheria hiyo. Labda kama anaonekana kuwa na fedha nyingi basi ajenge hata
barabara kuliko kufanya hivyo.”
Dk Hoseah aliongeza kuwa sheria pia
inazuia kuanza kampeni kabla ya muda kupangwa rasmi na Tume ya Taifa
(Nec), kwa hivyo muda wa kampeni utakapoanza, itarahisisha kukusanya
taarifa zake na kuchukua hatua kwa wanasiasa hao.
MWANANCHI
Balozi wa zamani wa Tanzania kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN), Dk Augustine Mahiga
amesema anafuatwa na makundi ya watu wanaomshawishi achukue fomu
kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya CCM, lakini hajatoa
jibu.
Balozi Mahiga anaingia kwenye orodha ya
watu ambao wamejitangaza au wanatajwa kuwania nafasi hiyo ya juu kwenye
siasa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba utakaochagua Serikali ya Awamu
ya Tano.
Tayari makada 21 wa chama chake
wanatajwa kuwamo kwenye kinyang’anyiro hicho cha kumrithi Rais Jakaya
Kikwete ambaye anamaliza muda wake wa miaka 10 baada ya kuongoza nchi
kwa vipindi viwili, ambavyo ndio kikomo kwa mujibu wa Katiba.
Tayari makada 21 wa chama chake
wanatajwa kuwamo kwenye kinyang’anyiro hicho cha kumrithi Rais Jakaya
Kikwete ambaye anamaliza muda wake wa miaka 10 baada ya kuongoza nchi
kwa vipindi viwili, ambavyo ndio kikomo kwa mujibu wa Katiba.
Dk Mahiga, ambaye pia alikuwa mwakilishi
wa Katibu Mkuu wa UN nchini Somalia, alisema makundi hayo yalianza
kumfuata baada ya Rais Kikwete kutangaza kwenye sherehe za maadhimisho
ya kuzaliwa kwa CCM zilizofanyika Songea kuwa kama wanachama wanaona
kuna mtu anafaa kugombea urais na hajajitokeza, wamfuate na kumshauri
achukue fomu.
“Nimepata
makundi ya watu na mtu mmoja mmoja wakinishauri nichukue fomu ya
kuwania urais baada ya Rais Kikwete kutoa kauli kule Songea mkoani
Ruvuma, lakini bado sijakubali wala kukataa ushawishi huo,”
Lakini akaongeza kuwa kushawishiwa
kuchukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi hiyo nyeti kwa Taifa, ni jambo
moja, lakini kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho ni jambo jingine
akisema kuwa CCM ina mchakato na masharti ambayo ni lazima yatimizwe.
Hata hivyo, Dk Mahiga hakusita kumwaga sera zake iwapo atajitosa kuwania nafasi hiyo na kuchaguliwa kuongoza nchi.
“Nitaimarisha
demokrasia, kuongeza uwajibikaji, kuimarisha maadili, kuboresha
mwelekeo wa uchumi, kilimo, kuimarisha reli na kupambana na rushwa,” alisema balozi huyo ambaye ni mhitimu wa shahada ya umahiri ya sanaa.
MWANANCHI
Rais Jakaya Kikwete leo
atahudhuria sherehe za mwisho za Muungano na kukagua gwaride la 10 la
shughuli hiyo tangu aingie madarakani wakati wa maadhimisho ya miaka 51
ya Muungano yatakayofanyika kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.
Kikwete atahitimisha kipindi chake cha
miaka 10 cha kuongoza nchi mwishoni mwa mwaka huu baada ya kupatikana
kwa mrithi wa kiti kwenye uchaguzi mkuu ambao kikatiba unatakiwa
ufanyike mwishoni mwa Oktoba.
Tayari Kikwete ameshahudhuria sherehe za mwisho za Uhuru akiwa Rais zilizofanyika Desemba 9 mwaka jana.
Sherehe hizo zinafanyika April 26 kila
mwaka katika kumbukumbu ya kuunganisha mataifa ya Tanganyika na Zanzibar
yaliyoungana mwaka 1964.
MWANANCHI
Serikali imeanza kutimiza ahadi yake ya
kuyafuta mashirika na asasi zisizo za kiserikali, NGO, yakiwamo ya
kidini na kwa kuanzia imetangaza kusudio la kuzifuta asasi 24 katika
kipindi cha siku saba kuanzia jana.
Miongoni mwa asasi hizo ni taasisi mbili za dini ambazo ni Tanzania Muslim Social Community na Tanzania Christian Outreach Ministries ambazo zimepewa siku saba kujitetea.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Issack Nantanga aliliambia gazeti hili kuwa asasi zote zitakazothibitika kwenda kinyume na malengo ya kuanzishwa kwake, zitafutwa.
Nantanga pia alisema panga hilo
litazipitia pia asasi ambazo zimekuwa haziwasilishi kwa msajili ada ya
kila mwaka na taarifa za fedha zilizokaguliwa na wakaguzi waliosajiliwa.
“Haya
mashirika 24 ndio tumeanza nayo na ukaguzi unaendelea. Tumetoa muda wa
siku saba kuanzia leo (jana) kujitetea kwanini yasifutwe na wakishindwa
kufanya hivyo, yatafutwa rasmi,” alisema.
Mashirika mengine ni Mbezi
Juu and Salasala Woman Agricultural and Environmen Association, Waridi
Training Society, Vituka Machimbo Development Association na Gerezani Nguvukazi.
Mengine ni
Nyakasangwe Small Scale Farmers Association, Vitendo Trust Fund, Bahari
Beach Silvers and Woman Association, Owners Social Club na Magovent Development Association.
Kwa mujibu wa Nantanga, mashirika mengine yaliyomo katika orodha hiyo ni Hananasifu Quarters Women Association, Mburahati Barafu Development Community na The Movers Club.
Pia yamo Umoja wa Maendeleo ya Jamii
Mlima Mindu, Tabata Tujiimarishe Club, Umoja wa Wauza Miche Ubungo,
Kunguru/Kinzudi Development Association na Women & Environment
Association.
“Ukitazama
katika tovuti ya wizara utakuta tuna orodha ya mashirika 10,624
yaliyosajiliwa tangu 1953. Tutapitia moja baada ya jingine na
yatakayobainika kukiuka sheria yatafutwa,” alisisitiza.
Unahitaji chochote ninachokipataKila siku asubuhi na mapema tangakumekuchablog inakupa uchambuzi wa habari muhimu kutoka magazetini, usiwe mbali nami kila wakati kwa habari nying kemkem na za kusisimua zinazojiri pembe zote za dunia, ni hapa hapa
No comments:
Post a Comment