Full time ya mechi za Real Madrid vs Atletico na Juve vs Monaco nimekuwekea hapa
Jijini Madrid, Spain Real Madrid wakiwa
Santiago Bernabeu walikuwa wakitetea ubingwa wao wa Ulaya kwa kucheza
dhidi ya wapinzani wao Atletico Madrid ambapo ilikua ni mechi ya pili
baada ya mechi ya kwanza kutoka sare tasa.
Tofauti na ilivyokuwa kwa mchezo uliopita
safari hii Madrid wakiwa na upungufu wa wachezaji muhimu wamefanikiwa
kupata ushindi wa 1-0 na wanazitoa shukrani kwa kijana wa kimexico Javier Hernandez Chicharito aliyefunga goli la ushindi dhidi ya Atletico na kuipeleka Madrid katika nusu fainali ya 37 ya michuano hiyo.
Kwenye mechi nyingine pia Juventus ya Italia imefanikiwa kuingia nusu fainali baada ya kupata ushindi wa jumla dhidi ya Monaco.
Kwa matokeo hayo FC Barca, Bayern Munich,
Real Madrid na Juventus ndio timu nne zilizoingia kwenye nusu fainali ya
UCL na ratiba ya mechi zao itapangwa rasmi Ijumaa wiki hii.
No comments:
Post a Comment