Hatua moja mbele Jeshi la Nigeria.. Waliotekwa na Boko Haram wameanza kuokolewa
Kampeni nyingi zimefanyika duniani kulaani tukio la wanafunzi wa kike zaidi ya 270 kutekwa na kundi la kigaidi la Boko Haram ni mwaka mmoja umepita, wasichana hao walitekwa toka Shuleni Jimbo la Chibok, Nigeria.
Rais aliyechaguliwa kuongoza Nigeria, Rais Buhari
moja ya vitu alivyosema ni kwamba hawezi kuahidi kwamba atahakikisha
wasichana hao wanapatikana ila atafanya jitihada zote mpaka wapatikane.
Good news ya leo ni kwamba Jeshi la Nigeria limesema limewaokoa wasichana 293 kutoka katika kambi za Boko Haram iliyoko katika msitu wa Sambisa, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Wasichana waliookolewa sio sehemu ya
kundi la wanafunzi waliotekwa Shuileni, hawa ni wengine ambao wlaikuwa
wakitekwa na Kundi hilo kila walipokuwa wakivamia vijiji mbalimbali vya
kaskazini mwa nchi hiyo.
Msemaji wa Jeshi la Nigeria amesema
wanawake hao na mabinti walikutwa katika kambi nne tofauti baada ya
Wanajeshi kuzishambulia kambi hizo.
No comments:
Post a Comment