Idadi ya vifo iliyoripotiwa mpaka sasa kutokana na tetemeko la ardhi Nepal
Stori
ambayo kwa sasa imechukua headlines kwa wingi ni ile ya tetemeko la
ardhi lililotokea Nepal na kuua idadi kubwa ya watu karibu na milima ya Everest.
Idadi
ya watu ambao wamethibitishwa kufariki kutokana na tetemeko hilo
lililotokea siku ya jumamosi iliyopita imeongezeka na mpaka sasa ni watu
zaidi ya 4,500 waliofariki.
Serikali
ya nchi hiyo imesema zaidi ya watu 10,000 wamejeruhiwa.. Hali hiyo
imewaelea na Serikali imehitaji msaada kutoka mataifa mengine.
Waziri Mkuu wa Nepal, Sushil Koirala amesema mahitaji ya dharura yanayohitajika yakiwa ya mahema , chakula pamoja na maji.
Kwa habari na matuki yanayojiri kokote utayapata hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment