Monday, April 27, 2015

KITISHO CHA UGAIDI NI BALAA KWA ASKARI KENYA

Tishio la ugaidi limeathiri vingi, huyu askari amejikuta akigeuka mhudumu wa afya Kenya !!

3d-abstract_other_soldier-in-sunset_27703
Kutokana na tatizo la hofu ya usalama Kenya jana tulisikia ishu ya walimu kugoma kwenda kufanya kazi maeneo ya kaskazini mwa Kenya.. kingine ilikuwa ishu ya wahudumu wa afya pia kukimbia maeneo hayo kutokana na hofu ya mashambulizi hayo pia.
Kaskazini mwa Kenya hali sio shwari sana, hii story inatoka maeneo ya Turkana ambako Afisa mmoja wa Polisi Alfred Lokori amelazimika kuchukua jukumu la kuwahudumia wenyeji wa eneo hilo katika kituo cha Afya cha Lomelo, kituo hicho hakina wahudumu kabisa.
sasa nimekuwa Askari mahali pengine na mahali pengine nimekuwa ni daktari “; Alfred Lokori.
Tukio kama hili liliripotiwa wiki iliyopita katika kaunti hiyohiyo ya Turkana ambako kijana mmoja alijitokeza kufanya kazi ya udaktari ambayo haifahamu kutokana na ukosefu wa wahudumu wa Afya katika eneo hilokutokana na kukosekana kwa usalama.
Hutopitwa na habri inayonifikia na nitakusogezea muda na wakato wowote hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment