Uchambuzi huu kutoka magazetini unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita wanaofanya mitihani ya Taifa na wale wanaojiendeleza. Kituo kiko na walimu waliobobea katika masomo. Pia kituo kinatoa kozi ya Kiingereza na Computer. Kituo kimesajiliwa na NECTA. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746
NIPASHE
Muuguzi mmoja wa zahanati ya Muungano,
Dodoma amekumbwa na kashfa nzito baada ya kudaiwa kumchapa viboko mama
mjamzito ambaye alikuwa na hali ya uchungu wa kujifungua na kusababisha
mtoto aliyetaka kujifungua kufariki akiwa tumboni.
Mwanamke huyo, Mariamu Maroda
amedaiwa kulazwa kwenye ICU kwa zaidi ya wiki moja, ambapo pamoja na
kufanyiwa upasuaji, hakufanikiwa kupata mtoto wake akiwa hai.
“Nilishuhudia
Lucy akimchapa Maroda viboko kwenye mapaja na mgongoni, akisema ana
uwezo wa kujifungua lakini anadeka tu, nilishindwa kuingilia nikihofia
asimdhuru zaidi mwanangu, ila nilihuzunika sana,” alisimulia mama mdogo wa Maroda, Joyce Charles.
Alisema muuguzi huyo alitumia fimbo tatu
kumchapa mgonjwa wake, fimbo zilipomalizika, alianza kumfinya mwanamke
huyo kwenye mapaja kwa kutumia rula.
“Kesho
yake saa 12:00 alfajiri, huku hali ya mgonjwa ikiwa mbaya, walitupatia
gari likatupeleka hospitali ya Mvumi Misheni, ambako walisema hali
aliyokuwa nayo mgonjwa wasingeiweza na kutuelekeza tumpeleke hospitali
ya rufaa, lakini walimpa mgonjwa chupa mbili za damu.. ukimuona, mwilini
ana alama za fimbo na kufinywa”— Joyce Charles.
Viongozi wa Hospitali ya Rufaa, wenye
mamlaka ya kuzungumzia suala hilo walionekana ‘kurushiana mpira’
walipotakiwa kuelezea suala hilo.
Hata hivyo, Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anatoria Mkindo alikiri kuwepo kwa mgonjwa huyo lakini Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Zainab Chaula alisema hakuwa na taarifa kuhusu Maroda.
Mdogo wa Maroda, Silika Mkwawi
amesema ingawa hakuingia kwenye chumba cha kujifunguli, dada yake
alipotolewa nje, muuguzi alimwambia kuwa alimchapa fimbo mbili tu, kwa
sababu ya kudeka kwake.
HABARI LEO
WATU 20 wamekamatwa na Polisi baada ya kumjeruhi askari aliyekuwa doria na mwenzake.
Kamanda wa Polisi Morogoro, RPC Leonard Paul amesema watu 20 watu hao walimshambulia kwa kumpiga na kitu butu kichwani askari wa jeshi hilo, Koplo Ramadhani
ambapo baada ya kupigwa alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa
wa Morogoro ambako amelazwa na anaendelea vizuri na matibabu.
Kamanda huyo amesema pikipiki
isiyofahamika namba za usajili iliyokuwa ikiendeshwa na Juma Abasi,
mkazi wa Mindu iligonga gari aina ya Isuzu Tipper kusababisha majeraha
kwa mpanda pikipiki huyo, chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa mwendesha
pikipiki kuingia barabarani bila kuchukua tahadhari.
Hata hivyo alisema ajali hiyo
ilishuhudiwa na askari hao waliokuwa doria na pikipiki maeneo hayo,
walifika eneo la ajali ili kutoa msaada na katika harakati hizo za kutoa
masaada ndipo askari Koplo Ramadhani alipopigwa na kitu butu kichwani na watu waliotokea eneo hilo na kuanguka chini.
MTANZANIA
Utafiti umeonesha kuwa wanaume wenye
umri kati ya miaka 40-50 wapo katika hatari kubwa ya kujiua kutokana na
msongo wa mawazo unaowatokea kwa sababu tofauti huku wengi wakikosa
washauri.
Utafiti huo ulifanywa Uingereza baada mzee mmoja kujiua siku yake ya kuzaliwa akiwa na umri wa miaka 44.
Utafiti unaonesha ndani ya wiki moja wanaume 100 hujiua huku idadi hiyo ikiizidi ya wanawake wanaojiua kwa zaidi ya mara nne.
Professa mmoja Kiongozi wa Kituo cha
Utafiti Chuo cha Glasgow amesema tabia ya kujiua ni tatizo la
kisaikolojia linalotokana na upungufu wa kiakili.
MWANANCHI
Mwili wa mwanafunzi wa kidato cha pili
aliyefariki kwa Manyara umezikwa jana huku Mchungaji wa Anglikana
akiwataka ndugu wakubaliane na hali iliyotokea.
“Tunaiomba Serikali namna ya walimu wanavhottoa adhabu.. kifo hicho kimesababishwa na uzembe”—Mchungaji Noel Bichima.
Ndugu na jamaa waliokuwa kwenye mazishi
hayo walionesha kusikitisha sana na kitendo cha mwanafunzi huyo kuchapwa
hadi kufariki wakisema kuwa ni ukatili.
Walimu watatu wamekamatwa wanashikiliwa na Polisi wakidaiwa kusababisha kifo cha mwanafunzi huyo.
MTANZANIA
Hali ya ulinzi katikati ya DAR
imeonekana sio ya kawaida baada ya Askari wa Jesh la Polisi kuonekana
kutanda huku wakiwa na silaha mbalimbali.
Baadhi ya maeneo ambayo imeonekana
ulinzi huo kuimarika ni pamoja na Mlimani City, Posta na Namanga huku
magari ya Polisi yakiendelea kuzunguka maeneo mbalimbali ya Jiji.
Gazeti la MTANZANIA liliwasiliana na Kamanda Kova ambaye amesema hali hiyo imetokana na operesheni maalum ya kupambana na uhalifu.
“Hii
inaitwa High Police Visibility tunajua kwamba uwepo wa mwonekano wa
Askari kwa wingi unasaidia kupunguza uwezekano wa kutokea uhalifu”—Kamanda Kova.
Kila siku asubuhi na mapema tangakumekuchablog inakupa uchambuzi wa magazetini kwa kina ambao unadhaminiwa na Kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga
No comments:
Post a Comment