Uchambuzi huu kutoka magazetini unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wale ambao wanajiendeleza kielimu. Kituo kimesajiliwa na NECTA. Kituo pia kinatoa kozi za Kiingereza na Computer. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746
MTANZANIA
Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Sekondari ya Matui iliyopo Wilayani Kiteto, Mkoani Manyara Emmanuel Mbigima mwenye miaka 15 amefariki dunia baada ya kuchapwa viboko 12 na walimu wake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Christopher Fulme alisema mwanafunzi huyo alifariki dunia baada ya kuchapwa viboko na walimu wake watatu kutokana na kufeli somo la Kiswahili.
Mauaji hayo yalitokea juzi saa 4 asubuhi shuleni hapo na mwili wake kwa sasa unaendelea na uchunguzi.
Msemaji wa familia Emmanuel Ngowi alisema familia inataka kuona haki inatendeka juu ya kifo chandugu yao.
“Kwa
kifupi mtoto wetu alikuwa haumwi na hakuwahi kulazwa hospitalini,,
tunaomba haki itendeke kwani tunaona kuna mazingira ya kutaka kulindana
na huenda haki isitendeke” Ngowi.
Chama cha Walimu Kiteto kimelaani tukio
hilo na kutaka uchunguzi wa kina ufanyike ili kujua ukweli kuhusu kifo
cha mwanafunzi huyo.
NIPASHE
Madudu zaidi yameendelea kuibuka katika sakata la mabehewa feki 274 yaliyonunuliwa na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL),
na sasa imebainika kuwa kampuni iliyopewa zabuni ya kuleta mabehewa
hayo ndiyo iliyokuwa ya bei ya juu zaidi kuliko kampuni 10 zilizokuwa
zimeomba na haikuweka dhamana yoyote kama sheria ya manunuzi inavyotaka.
Imebainika pia kampuni ya Hindustan Engineering Ltd
ya India, ambayo ilishinda zabuni hiyo, ilibadilishiwa vigezo, vya aina
ya mabehewa kinyemela baada ya zabuni kutangazwa na wazabuni
kuwasilisha maombi yao.
Kwa mujibu wa taarifa za uhakika,
kampuni hiyo iliomba kuiuzia TRL mabehewa 174 yenye ‘rubber’ badala ya
‘spring’Sh. bilioni 32.8 wakati kampuni ya Baotou Beifang Chuangye Co. Ltd ya China ilikuwa tayari kuleta idadi hiyo ya mabehewa yenye viwango vinavyokubalika kwa Sh. bilioni 25.
Kampuni hiyo pia ilishinda zabuni hiyo
ambayo ilihusisha kuleta mabehewa mengine 100 ya mizigo ambayo ni ya
muundo wa matangi na yasiyofunikwa Sh. bilioni 18.5 wakati kampuni ya Baotou Beifang Chuangye Co. Ltd ya China iliyokuwa ndiyo yenye bei ndogo ilikuwa tayari kuleta idadi hiyo ya mabehewa kwa Sh. bilioni 13.09.
Kampuni hiyo pia ilishinda zabuni ya kuiuzia TRL
vipuri kwa thamani ya Sh. bilioni 4.4 baada ya kuirekebisha na taarifa
ya zabuni inaonyesha kuwa iliwasilisha zabuni iliyorekebishwa na
ilikubaliwa.’
Kampuni ya Baotou Beifang Chuangye Co.
Ltd iliomba kuleta vipuri hivyo kwa Sh. bilioni 4.46 wakati kampuni
nyingine kama Transnet iliomba kwa Sh. bilioni 5.6 wakati Modern
Industries iliyoshindwa kwa kutowasilisha dhamana iliomba kwa Sh.
bilioni 6.02.
Kwa ujumla taarifa zinaonyesha kuwa
kampuni ya Hindustan Engineering ililipwa Sh. bilioni 55.9 wakati
kampuni iliyokuwa ya bei ndogo kuliko zote ingeweza kufanyakazi hiyo kwa
Sh. bilioni 43.86 hatua ambayo ingeokoa Sh. bilioni 12.02 na
kutoitumbukiza nchi kwenye hasara hiyo ya mabehewa feki.
“Mabehewa
nyenye rubber hayawezi kabisa kwa namna yoyote ile kupita kwenye reli
yetu. Kilichotokea ni kwamba zabuni iliyotangazwa ilitaka wazabuni
walete mabehewa yenye spring ambayo ndiyo sahihi, lakini baadaye
inaonekana walibadilisha vigezo na kuielekeza kampuni waliyoipa zabuni
vigezo vipya ndiyo maana unaona mabehewa yaliyokuja hayafai,” alisema mmoja wa wataalam wa reli ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa kampuni ya
Hindustan Engineering Ltd haikuweka dhamana yoyote jambo ambalo ni
kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma na ilitaka ilipwe fedha yote
kabla ya kuingiza mabehewa nchini jambo ambalo TRL ilitekeleza.
Wakati mzabuni huyo akiweka masharti
hayo, kampuni nyingine zilizoomba ikiwamo iliyokuwa ya bei ndogo zaidi,
iliweka dhamana na ilitaka ilipwe kwa awamu hadi itakapokamilisha kazi
husika.
NIPASHE
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR- Mageuzi), David Kafulila,
amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kigoma kujibu
shtaka la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Hadija Nyembo.
Kafulila alifikishwa mahakamani hapo jana saa 3:00 asubuhi akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo, David Ngunyale, Wakili wa Serikali, Maryasinta Lazaro, alidai kuwa Mbunge huyo alitenda kosa hilo Agosti Mosi, mwaka 2013, katika Kata ya Nguruka, Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.
Wakili huyo alidai kuwa Mbunge huyo
alimtolea maneno ya matusi Nyembo kuwa hana maadili, ana akili finyu na
ni kiumbe dhaifu, kitendo ambacho kingesababisha uvunjifu wa amani.
Wakili Lazaro, alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba kupangwa tarehe nyingine ya usikilizwaji wa awali.
Hakimu Ngunyale alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Mei 19, mwaka huu.
Wakili wa Mbunge huyo, Danieli Rumenyela,
aliomba Mahakama hiyo kumpunguzia mteja wake masharti ya dhamana ili
kumalizia vikao vya Bunge ambavyo vinatarajia kuanza mwezi ujao.
Hata hivyo, Kafulila alikana shtaka hilo
na kukidhi masharti ya dhamana ambayo ni kuwa na mdhamini mmoja mwenye
barua ya utambulisho kutoka kwa Ofisa Mtendaji wa Kata na mali
isiyohamishika yenye thamani ya Sh. milioni mbili kisha kuachiwa.
Kafulila alidhaminiwa na Diwani wa Kata ya Katubuka (Chadema), Moses Bilantanye.
Kabla ya kufikishwa mahakamani jana,
Mbunge huyo alikuwa nje kwa dhamana ambayo alipewa na askari wa kituo
cha Polisi Kati baada ya kudaiwa kumtukana Mkuu huyo wa wilaya.
MWANANCHI
Katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
imeanza kuandikisha wapigakura kwenye mikoa ambayo ni ngome ya CCM na
kwamba ile yenye upinzani itaandikishwa kwa kulipua ili watu wengi wenye
sifa ya kupiga kura wasiandikishwe.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva amesema hilo ni jambo jipya kwake kwa kuwa hawakuangalia suala hilo wakati wa kupanga mikoa hiyo.
Akizungumza jana kwenye Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya kuwasili nchini akitokea
Marekani, Dk Slaa alisema wamegundua kwamba mwishoni mwa kazi ya
uandikishaji kwenye mikoa ambayo ni ngome ya vyama vya upinzani, watu
wengi hawataandikishwa.
“Tumegundua
hujuma zao, NEC wameanza kuandikisha wapigakura kwenye mikoa ambayo ni
ngome ya CCM. Huko wanajitahidi kuandikisha wapigakura wote na
wanachukua muda mrefu,” Dk Slaa
“Mikoa
yenye ngome ya Chadema na vyama vingine vya upinzani itakuwa ya mwisho
kuandikisha wapigakura na uandikishaji huo utakuwa wa harakaharaka ambao
utawaacha mamia ya watu bila kuandikishwa kwa sababu muda utakuwa
hautoshi,” Dk Slaa.
Alisema suala hilo linaweza kuvuruga uchaguzi, hasa ikizingatiwa kwamba mchakato wa uandikishaji umekuwa na sintofahamu nyingi.
MWANANCHI
Mlinzi wa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima
jana alijisalimisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa
mashtaka mawili ya kukutwa na bastola aina ya Berretta pamoja na risasi
20 kinyume na sheria.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Wilfred Dyansobera kuwa baada ya kuomba mahakamani hapo hati ya wito ya kumuita mshtakiwa George Mzava , jana alijisalimisha akiambatana na Wakili Peter Kibatala.
Akimsomea hati ya mashtaka, Kweka alidai
kuwa Machi 29 katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni A, akiwa na
wenzake Bihagaze na Milulu walikutwa na bastola aina ya Berretta yenye
namba ya siri CAT 5802 bila ya kuwa na kibali cha mamlaka inayohusika na
silaha na milipuko.
Alidai kuwa washtakiwa hao walifanya kosa hilo kinyume cha Sheria ya Silaha.
Wakili huyo wa Serikali, aliendelea
kudai kuwa siku hiyo ya tukio, Mzava akiwa na wenzake hao walikutwa
wakimiliki isivyo halali, risasi tatu za bastola pamoja na risasi 17 za
bunduki aina ya shotgun.
Mshtakiwa huyo baada ya kusomewa mashtaka hayo aliyakana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi bado haujakamilika.
MWANANCHI
Raia 12 wa Iran na Pakistan
wanaokabiliwa na shtaka la kuingiza nchini shehena ya mihadarati yenye
thamani ya bilioni 9 wamesema kuwa kama upepelzi wa kesi zao
haujakamilikni bora wapigwe risasi wafe kuliko kukaa mahabusu kwa muda
mrefu.
Walitoa malalamiko yao jana mbele ya hakimu Janeth Kaluyenda baada ya wakili wa Serikali Janeth Kitali kudai kuwa upelelezi wao haujakamilika na kesi imeahirishwa mpaka Mei 4.
Raia hao walikamatwa katika bahari ya
Hindi upande wa Tanzania wakiingiza shehena ya kilo 200.5 za dawa za
kulevya aina ya Heroin.
Kesi hiyo ipo mahakamani hapo kwa ajili
ya kusikilizwa na upepezi ukikamilika itahamishiwa mahakama kuu Tanzania
kanda ya Dar es salaam.
HABARILEO
Serikali imefanikisha kurejea nchini kwa
kundi la pili la Watanzania 14 wanaoishi Yemen, ambako kuna machafuko
ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Watu hao wameelezea jinsi walivyoteseka
na kuathirika kisaikolojia, huku wakiwataka Watanzania waliopo nchini,
kutojaribu kuichezea amani iliyopo.
Katika kuyanusuru maisha yao, Watanzania
hao waliogharamia chakula, malazi na usafiri wa kurejea nchini,
wamesema walilazimika kutangatanga kwa zaidi ya wiki mbili na hatimaye
kufanikiwa kurejea salama nchini.
Kurejea kwao jana, kumefanya watanzania waliorejea nchini hadi sasa kutoka Yemen kufikia 39, kati ya 64 waliopo nchini humo.
Wakizungumza na gazeti hili jana kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam baada ya
kurejea na ndege ya Shirika la Ndege ya Emirates, watanzania hao
walisema kama sio juhudi za serikali ya Tanzania, wana uhakika kwa sasa
wangekuwa wafu.
“Sina
cha kusema, kwa kweli naishukuru serikali yangu na Balozi wangu kule
Muscat, Oman alitusaidia sana, nilikuwa naishi Yemen mimi na familia
yangu ya watu 10, na hali ilipozidi kuwa mbaya niliomba msaada ubalozini
na walitusaidia na tumerejea nyumbani na familia yangu kwa gharama za
serikali, hili sio jambo dogo,” Sabri Abeid Almaghi.
Akisimulia hali halisi nchini Yemen,
Almaghi alisema tangu mwaka 2011 amekuwa akiishi nchini humo yeye na
mkewe na familia yake ya watu 10, akifanya biashara ya maduka ya kuuza
vipuri vya pikipiki na kwamba hali ya siasa ikachafuka na mapigano
yakaanza.
Alisema baada ya machafuko kutokea,
ilimbidi afunge maduka yake na kuhamishia vipuri vyote kwenye stoo moja
na kisha kurudisha maduka ya watu aliyokuwa amepanga na kuanza kutafuta
msaada ubalozini wa kurejea nyumbani.
“Kwa
kweli kule hivi sasa ni taabu tupu, hali sio nzuri kwanza uwanja wa
ndege ulifungwa, tukaambiwa muda unavyokwenda barabara nazo zitafungwa,
nilikuwa ninaishi mji uitwao Mukalla, baada ya kuona hali mbaya nilipiga
simu ubalozini, kuomba msaada na ndipo tukaanza safari ya kuondoka
Yemen kwa basi kwenda Muscat, tumechukua zaidi ya siku tano kusafiri,”Almaghi.
Aliongeza kuwa, kwa ujumla tangu
walipoanza safari ya kuondoka Yemen hadi kufika Tanzania wakiwa salama
jana, wametumia zaidi ya siku 15, jambo ambalo aliloelezea kuwa limempa
uchovu mkubwa hasa kwa kuwa alikuwa na watoto na watu wengine wa familia
yake.
HABARILEO
Kumeibuka vikundi vya watu jijini Dar es
Salaam vikidaiwa kujichukulia madaraka ya kukusanya ushuru katika vituo
vya daladala na kwa wafanyabiashara kwenye maeneo yasiyoruhusiwa hali
ambayo mamlaka zinazohusika na usimamizi zimeshauriwa kuingilia kati
kukomesha vitendo hivyo.
Kuhusu vituo vya daladala, lipo wimbi la
wapigadebe ambao wanadaiwa kuhodhi vituo hivyo kwa kulipisha ushuru
daladala, bajaj, pikipiki na hata magari ya watu binafsi yanayoamua
kupakia abiria vituoni.
Kwa upande wa wamachinga, suala hilo
linadaiwa kujitokeza zaidi katika eneo la Ubungo ambako liko kundi
linalojiita ‘Matembo’ linalodaiwa kulipisha ushuru wa Sh 500 kwa kila
mfanyabiashara ndogo aliye katika eneo hilo.
Vikundi vyote hivyo vilivyoamua
kujichukulia mamlaka ya kutoza ushuru, vinashutumiwa kutumia nguvu na
vitisho kujipatia fedha kutoka kwa wahusika. “Usipolipa shilingi mia tano, wanakufanyia fujo.
Wanakuvunjia meza. Ni wababe lakini hatuna jinsi ya kufanya. Tunawapa tu,”
alisema mmoja wa wafanyabiashara katika eneo la Ubungo karibu na kituo
cha zamani cha daladala aliyekutwa na mwandishi akizozana na wakusanya
ushuru hao.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo hilo
la Ubungo, wapo wafanyabiashara wapatao 200, hali ambayo inakadiriwa
kwamba, kikundi hicho hukusanya zaidi ya Sh milioni moja kwa siku kwa
kisingizio cha kufanya usafi.
Mmoja wa wafanyabiashara ambaye hakutaka
jina lake liandikwe gazetini, alisema, kikundi hicho kinaundwa na watu
wapatao saba ambao wamekuwa kero kubwa kwao.
“Hakuna
usafi wanaofanya,Hawa ni wezi tu, wameamua kujitengenezea njia ya
kuchukua fedha zetu, wao wamekaa tu wanasubiri kutulazimisha kuwapa
hela,” alisema.
Msemaji wa Manispaa ya Kinondoni, Sebastian Mholela
alipoulizwa iwapo wafanyabiashara katika eneo sanjari na watu
wanaotumia mwanya huo kujikusanyia fedha kwa kutoza ushuru, alisema
hawezi kukiri uwepo wa kikundi hicho.
Alisema anachofahamu ni kwamba, uwepo wa
wafanyabiashara hao ni kinyume cha sheria kwa sababu tayari
walishawaondoa na sasa wamerudi kinyemela.
Kil siku asubuhi na mapema tangakumekuchablog inakupa uchambuzi wa habari muhimu zilizoripotiwa magazetini, usiwe mbali nami ni hapa hapa kumekuchablog
No comments:
Post a Comment