Ni zamu ya Mayweather!! Hivi ndivyo alivyokwenda kukagua ukumbi wa pambano…(Pichaz)
Siku mbili tu zimesalia kabla ya pambano la kimataifa la ngumi kati ya mastaa wawili Manny Pacquiao na Floyd Mayweather ambao watapanda ulingoni nakutegua kitendawili cha nani mkali zaidi.
Wakati homa ya pambano hilo ikizidi kupanda huku mabondia wote kila mmoja akimtambia mwenzake, jana tuliona PManny Pacquiao alivyowasili katika mji wa Las Vegas na familia yake pamoja na wapambe wake kwa mkwara, na leo ni zamu ya Floyd Mayweather ambaye ametumia muda wake kwenda kukagua ukumbi wa MGM Grand ambao utatumika kwa pambano hilo

Mayweather wakati anakwenda kutazama
ukumbi huo ulifurika mashabiki mbalimbali pamoja na camera za waandishi
wa habari hazikuwa mbali kuchukua tukio zima.
Pambano hilo linatajwa kuwa pambano la
kifahari zaidi duniani na ambalo viingilio vyake ni vikubwa
ukilinganisha na mapambano mengine yaliyowahi kufanyika duniani.
Hutpitwa na habari yoyote inayonifikia na niko tayari kukutumia muda wowote kupitia hapa hapa www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment