Uchambuzi huu wa magazetini unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga. Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita wanaofanya mitihani ya Taifa na wale wanaojiendeleza kielimu. Kituo kimesajiliwa na NECTA. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 7727246
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula
ametumia kifungo cha vigogo sita wanaowania urais ndani ya chama hicho
kuwatisha viongozi wa chini wasijihusishe na kampeni kabla ya muda
kufika.
Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya
kiongozi huyo kusema kuwa kanuni za uchaguzi za chama hicho zitawameza
makada wake wanaotumia fedha kuwanunua wapigakura kama maandazi.
Akizungumza na viongozi wa chama hicho katika Jimbo la Kigamboni, wilayani Temeke, Mangula alisema: “Mnafahamu tulichokifanya kwa wanachama sita walioanza kampeni kabla ya wakati.”
Alisema kanuni za chama hicho zinaruhusu
mwanachama kutangaza nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi
lakini haziruhusu kuanza kampeni kabla ya muda.
“Tuna
ushahidi kwamba mmeanza kutoa vitu na fedha, nawaonya ndugu zangu acheni
mambo hayo chama kina macho, kinawaona na kitachukua hatua,” alisema Mangula na kushangiliwa na viongozi wa chama hicho.
Alisema kamati ya maadili ya chama hicho
iliwabana kwa maswali magumu makada walioanza kampeni kabla ya muda
hadi wengi wao wakabaki midomo wazi.
Alisema walibaki midomo wazi kwa sababu
waliwahoji huku wakiwaonyesha ushahidi wa makosa waliyoyafanya na
shughuli walizozifanya.
“Kama watu hao maarufu tuliwapiga pingu
kwa miezi 12 kwa kuanza kampeni kabla ya wakati, tutashindwa vipi
kuwafungia nyie, tunafuata kanuni,” alisema Mangula.
Akifafanua namna Kamati ya Maadili anayoiongoza ilivyowabana kwa maswali viongozi hao, Mangula alisema; “tulipowaita
mmojammoja tuliwaonyesha siku, tarehe na saa na fedha walizotoa wakati
wakifanya kampeni kabla ya muda. Nadhani mnafahamu mtu mzima
anapobainika kufanya jambo baya ni lazima anabaki mdomo wazi.”
Waliopata adhabu hiyo ni mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Kilimo, Chakula na Kilimo, Stephen Wasira, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.
MWANANCHI
Wakati viongozi wa CCM wanaendelea
kupiga kelele bila ya kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya rushwa
wanavyodai vinafanywa na makada wanaotaka uongozi wa nchi, Takukuru iko
tayari kukisaidia chama hicho kikongwe kupambana na uhalifu huo kama
kitakuwa tayari kutoa ushirikiano.
Karibu viongozi wote wa CCM
wameshanukuliwa wakilalamikia kukithiri kwa vitendo vya rushwa ndani ya
chama hicho, hasa nyakati za uchaguzi, lakini wamekuwa wakieleza tu
kwamba wahusika watawajibishwa na vyombo vya maadili vya chama hicho,
licha ya vitendo hivyo kuwa vya uhalifu.
Juzi, akiwa kwenye vikao vya ndani na viongozi wa chama hicho wa Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangulla alisema fedha zinazotumiwa na makada kununua wanachama “kama maandazi”, zitakuwa kitanzi chao kwenye uchaguzi mkuu, akisisitiza kuwa wanachama hao watang’olewa.
Lakini wakati wasomi waliohojiwa na
Mwananchi wanahoji sababu za chama hicho kutowashitaki makada hao kwenye
chombo kinachojishughulisha na kupambana na rushwa, ofisa huyo wa
Takukuru amesema inawawia vigumu wao kuwashughulikia wahalifu hao bila
ya viongozi kutoa ushirikiano.
“Taasisi
iko tayari hata kama viongozi au wanachama watatuletea malalamiko hayo
leo (jana). Bila ushirikiano wa viongozi inakuwa vigumu kufuatilia,” Daniel Mtuka.
“Kwa
kesi ya rushwa kwa wagombea hao, ni vigumu kwani tuliwahi kukutana na
changamoto ya kushindwa kufanya kazi yetu miaka iliyopita tulipomnasa
mgombea fulani wa ubunge CCM ambaye pia alikuwa kiongozi wa chama. Sisi
tulidhani ni tatizo, lakini hali hiyo ikaonekana kuwa siyo tatizo,
akasema ni sahihi na ataingia kutekeleza ilani ya chama.”
Alisema kutokana na mazingira hayo ni
muhimu zaidi kupata ushirikiano wa chama ili kurahisisha kazi yao hasa
katika kipindi cha kuelekea uchaguzi ambacho kinatazamiwa kuwa na
matukio mengi ya rushwa kuanzia ndani ya vyama vya siasa.
NIPASHE
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),
imeanzisha utaratibu mpya wa mafunzo kwa vitendo kwa watendaji
wanaoandikisha wapigakura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa
kutumia mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR).
Jumla ya BVR kits 498 zitatumika kutoa
mafunzo hayo, lengo likiwa ni kurahisisha uandikishaji, baada ya awamu
ya kwanza kusuasua katika Mkoa wa Njombe.
Mafunzo hayo yatafanyika kwa mikoa minne
ya awamu ya tatu ya uandikishaji wapiga kura na yatakuwa endelevu ili
kuharakisha uandikishaji utakaoanza Mei 2, mwaka huu.
Mkurugenzi wa Nec, Julius Malaba, alisema Nec imeamua vifaa hivyo vitumike kwenye mafunzo ya vitendo kwa watumishi hao ili kuharakisha uandikishaji.
Awamu ya kwanza ya uandikishaji ilikuwa Mkoa wa Njombe, ya pili inayoanza kesho ni Mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Iringa na awamu ya tatu ni Dodoma, Mbeya, Katavi na Tabora.
Malaba alisema BVR 1,600 zilizowasili
katikati ya Aprili, mwaka huu, zitatumika kuandikisha katika mikoa ya
Iringa, Lindi, Mtwara na Ruvuma yenye watu wenye sifa ya kupiga kura
ifikapo Oktoba, mwaka huu ni 2,599,205.
Tangu Februari 23, mwaka huu, Nec
ilianza uandikishaji katika Mkoa wa Njombe wenye watu wenye sifa za
kupiga kura 392,634, lakini hadi uandikishaji unafika Aprili 18, mwaka
huu, walikuwa wameandikishwa watu 300,080 ikiwa ni tofauti ya watu
92,554.
Mkurugenzi huyo alisema BVR 1,600
zitakazowasili kati ya Jumamosi na Jumapili wiki hii, zitatumika kwenye
awamu ya pili ya uandikishaji wapiga kura.
Alisema kwa sasa mafunzo kwa vitendo kwa
idadi ya BVR zilizopo ni endelevu ili wakati wa uandikishaji kusiwe na
ucheleweshaji kama ilivyotokea kwenye Mkoa wa Njombe kutokana na ugeni
wa matumizi ya mashine hizo.
Aprili 2, mwaka huu, Mwenyekiti wa Nec,
Jaji mstaafu Damian Lubuva, alitangaza kuahirishwa kwa Kura ya Maoni kwa
Katiba inayopendekezwa kutokana na kushindwa kukamilika kwa daftari la
kudumu la wapiga kura na itatangazwa tena.
Alisema tarehe ya kura hiyo itatangazwa tena baada ya Nec kushauriana na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec).
Nec ilisema hadi wakati huo, serikali ilikuwa imetoa Dola milioni 72 za Marekani sawa na Sh. bilioni 13.
Vifaa hivyo vinanunuliwa na serikali
kupitia kampuni ya Lithotech Export ya Afrika Kusini ambayo imeingia
mkataba na Nec na inaviagiza China.
Taarifa zilizopatikana ndani ya tume
hiyo zinaeleza kuwa, kampuni hiyo ndiyo inayotoa muundo wa ndani (soft
ware) ya mashine hizo na kwamba utengenezaji wa mashine moja na kuweka
vifaa vyote muhimu inachukua wiki sita.
NIPASHE
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, ameanza ziara ya siku sita kwenye mikoa ya Tabora, Shinyanga, Mwanza na Kagera.
Ziara hiyo inalenga mwendelezo wa
uzinduzi wa programu ya FTP maalum kwa ajili ya mafunzo ya uzalendo kwa
vijana, shughuli ambayo amekuwa akiifanya tangu Januari mwaka huu.
Taarifa kwa vyombo vya habari jana iliyotolewa na Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene, ilisema ziara hiyo aliianza jana katika Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora.
Alisema ziara hizo zitaambatana na
mikutano ya hadhara wilayani Bariadi, Shinyanga kabla ya kwenda wilayani
Ukerewe, mkoani Mwanza.
Maeneo mengine atakayozindua programu
hiyo ni Bukoba Mjini kisha Kyerwa na kwamba katika maeneo yote
wamelialika Jeshi la Polisi kutoa elimu ya ulinzi shirikishi na polisi
jamii.
Makene alisema pia, wameialika Taasisi
ya Kupambana na kuzia Rushwa (Takukuru) ili kutoa elimu ya kupambana na
kuzuia rushwa hasa wakati wa uchaguzi.
Aidha, alisema viongozi wengine wajuu
wa chama hicho wataendelea na programu ya uzinduzi wa mafunzo ya
kukiandaa chama kushinda dola na kuiongoza serikali, kwenye mikoa ya
Tanga, Shinyanga na Mbeya.
Alifafanua kuwa Makamu Mwenyekiti Taifa Bara, Prof. Abdallah Safari,
atakuwa Korogwe Mjini na kuzindua mafunzo hayo kwa viongozi wa Korogwe
mjini na vijijini kisha kufanya mkutano wa hadhara Korogwe mjini.
Alisema, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, atazindua mafunzo wilayani Bariadi na pia atakuwa na mkutano wa hadhara Bariadi na Maswa.
Kadhalika, alisema Naibu Katibu Mkuu
Zanzibar, Salum Mwalimu, atazindua mafunzo hayo wilayani Mbalizi na
kufanya mkutano wa hadhara Njombe mjini.
MTANZANIA
Shilingi ya Tanzania imeporomoka kwa kasi katika miezi ya karibuni kiasi cha kutishia kuyumba kwa uchumi wan chi.
Katika takwimu za benki kuu ya Tanzania BoT za Januari 2 mwaka huu, dola moja ya Marekani ilikuwa ikiuzwa kwa wastani wa sh. 1586.
Mwishoni mwa mwaka jana dola ilifikia
sh. 1600 ingawa katika maduka mbalimbali ya kubadilisha dola moja
ilikuwa ikinunuliwa kwa wastani wa sh. 18000.
Hata hivyo kwa siku za karibuni dola
imepanda kwa kasi na hivi sasa inauzwa kwa wastani wa 1950 jambo ambalo
limeongeza maradufu gharama ya bidhaa zinazoingizwa nchini kutoka nje
ambazo hununuliwa kwa dola za Marekani.
Pamoja na sababu nyingine zinazotajwa
kusababisha hali hiyo, hatua ya wahisani kugoma kutoa fedha za misaada
hususan ya bajeti inayofikia trilioni moja, inatajwa kuwa moja ya
sababu ya kuporomoka kwake.
MTANZANIA
Baba mzazi wa kiongozi wa ACT –wazalendo, Zuberi Kabwe, amesema pamoja na misukosuko ya kisiasa inayompaya motto wake, Mungu ndiye anayemsimamia.
Amesema kwamba kwa kuwa yeye ndiye mzazi
wa mwanasiasa huyo amekuwa akimuombea mar azote, ikiwa ni pamoja na
kipindi alichokuwa mwanachama wa CHADEMA.
“Mwanangu alibezwa na hata kuonekana
kuwa si lolote katika chama awali na kupewa majina mbalimbali,
aliambiwa hata akitoka CHADEMA hatakuwa na athari zozote, lakini sasa
kila Mtanzania anashuhudia kinachoendelea”.
“ACT
ni chama kidogo lakini kinaongoza mitaa na vijiji na kimefanikiwa kuwa
na wanachama wengi, sasa najiuliza hivi hawa waliokuwa wanasema hana
madhara, inakuwaje wanamkebehi Na hata kumuhofia?.
Anasema aliumia baada ya mwanaye
kufukuzwa CHADEMA lakini sasa dunia yote inashuhudia hali halisi ilivyo
kutokana na maono ya kijana wake.
Kila siku asubuhi na mapema tangakumekuchablog inakupa uchambuzi wa yote yaliyoandikwa magazetini, ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment