Ishu ilikuwa ni ugomvi wa wapenzi, ukawashwa moto mkubwa na kuchoma mpaka ghorofa na maduka..
Jamaa mmoja alifika kwenye duka lililoko
kwenye jengo hilo na kummwagia mpenzi wake petrol aliyokuwa amebeba, halafu akajimwagia na yeye mwenyewe, akawasha moto wote wakaanza
kuungua.. mashuhuda wamesema kisa ni mgogoro wa kimapenzi waliokuwa nao.
“Akaanza kuwasukuma wateja waliokuwa katika M-Pesa akawaambia wacha nihudumiwe ndio akawasha kiberiti“, shuhuda aliyekuwa eneo la tukio.
Msichana huyo alifariki eneo hilohilo la
tukio, jamaa ambaye alimlipua nae akapata majeraha makubwa na
kupelekwa Hospitali ya Kericho, watu wengine wanne walijeruhiwa huku
maduka kadhaa ya dawa na vitabu yakiteketea kwa moto.
Hii ishu ilikuwa kubwa sana, unaweza kuona hapa hali ilivyokuwa baada ya moto huo kuwashwa..
No comments:
Post a Comment