Uchambuzi huu wa magazeti unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita wanaofanya mitihani ya Taifa na wale wanaojiendeleza kielimu. Pia kinatoa kozi ya Kiingereza na Computer .Kituo kipo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746
Madaktari katika maeneo yaliyonufaika
na bajaji za kubebea wagonjwa, wamelazimika kuwa madereva wa kuziendesha
baada ya Serikali kushindwa kuajiri madereva.
Mganga Mkuu wa hospitali ya Dodoma Dk. Ezekiel Mpuya alisema Mkoa wa Dodoma ulifanikiwa kupata bajaji 10 na kila Wilaya ilipatiwa mbili lakini zote hazina madereva.
Dk Mpuya alisema madaktari hao licha ya
kuziendesha bajaji hizo hukumbana na changamoto ya ubovu wa barabara
unaowapa wakati mgumu pindi wanaposafirisha wagonjwa wanaopatiwa rufaa
kwenda hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
“Wakati mwingine huwa zinafia njiani kutokana na ubovu wa barabara, kwa upande mwingine naweza kusema sio msaada sahihi ” Dk Mpuya.
Ameiomba Seikali kuzipatia uwezekano wa magari ya wagonjwa hospitali hizo ili kuepuka adha wanayokumbana nayo sasa.
MWANANCHI
Uwezekano wa Kura ya Maoni kufanyika
mwaka huu na hasa sambamba na Uchaguzi Mkuu, umeanza kujionyesha baada
ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza zabuni za ununuzi wa vifaa vitakavyotumika kwenye shughuli hiyo, zikiwamo karatasi za kupigia kura.
Kati ya matangazo hayo mawili, moja
litakamilisha mchakato wa upokeaji maombi ya zabuni Mei 11, mwaka huu na
nyingine kufungwa siku tisa baadaye.
“Serikali
ya Tanzania imetenga fedha kwa ajili ya uendeshaji wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi katika mwaka wa fedha 2014/15. Imepanga kuwa sehemu ya fedha
hizo zitatumika kugharamia ununuzi wa vifaa mbalimbali na huduma zisizo
za kishauri kwa ajili ya Kura ya Maoni 2015,” inasomeka sehemu ya tangazo hilo.
Katika matangazo hayo, NEC imetoa zabuni
sita tofauti zitakazojumuisha ununuzi wa fulana na kofia, ununuzi wa
bahasha zisizoweza kuchakachuliwa, uchapaji na uchapishaji wa karatasi
za kupigia Kura ya Maoni.
Wazabuni hao pia watatakiwa kutoa huduma
mchanganyiko zinazojumuisha vifaa vya ofisini, vifaa vya kuhifadhia
nyaraka na vitu mbalimbali pamoja na taa za chemli.
Pia, wataiuzia NEC chemba za kupigia kura, wino maalumu, lakiri za masanduku ya kura na betri.
Vilevile, Tume inataka wazabuni kufanikisha ununuzi wa kompyuta, skana, printa, modemu, projekta na mashine za kunakili.
Huduma nyingine zinahusisha ununuzi wa vifaa mbalimbali vinavyotumika katika printa na mashine za kunakili.
Katika tenda nyingine, NEC inatafuta
kampuni itakayotoa huduma za kukodisha malori na magari madogo yenye
uwezo wa ‘four wheel’ kwa ajili ya kubebea vifaa vya Kura ya Maoni
katika kata mbalimbali.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva
alisema pamoja na maandalizi hayo, hadi sasa hakuna tarehe maalumu
iliyokubaliwa kufanyika kwa Kura ya Maoni na kwamba nguvu zote
zimeelekezwa kwenye uboreshaji wa Daftari la Wapigakura kwa kutumia
teknolojia ya Biometric Voters Registration (BVR).
MWANANCHI
Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema
amedai kuwa serikali iliyopo madarakani imeshindwa kazi kutokana na
mawaziri na watendaji wengine kumwachia majukumu yote Rais Jakaya
Kikwete.
Akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa
uchaguzi wa chama hicho uliofanyika Dar es Salaam jana, Mrema alisema
kuna mambo mengi ya ajabu yanayojitokeza katika ofisi za Serikali
yanayokatisha tamaa wananchi.
Mrema alisema karibu kila sekta ikiwamo
ya ulinzi na usalama, zinayumba na mbaya zaidi wasaidizi wa Rais bado
hawajaweza kufanya kitu chochote kuikabili hali hiyo.
“Nchi
inaelekea kubaya, kuna matatizo mengi ya kiusalama ambayo hayana majibu,
kuna masuala ya ugaidi, udini, mauaji ya albino, uvamizi, uporaji wa
silaha na mauaji katika vituo vya polisi,” .
Mrema aliyataja matukio mengine kuwa ni
migomo ya madereva na wafanyabiashara na alisema yote hayo yanatokea,
hakuna kiongozi hata mmoja ambaye amejitokeza kuyashughulikia
kikamilifu, kila mmoja anasubiri Rais Kikwete aseme neno au achukue
hatua.
MTANZANIA
Mwili wa mwanafunzi wa kidato cha pili
katika Sekondari ya Matuo, Manyara anayedaiwa kufariki baada ya
kuchapwa viboko na walimu wake Emmanuel Mbigima umefikishwa katika hospitali ya rufaa ya Dodoma kwa uchunguzi.
Wakati mwili huo unafikishwa hospitalini
hapo jana ulikuwa umewekwa kwenye gari la Halmashauri ya Kiteto
ukisindikizwa na baadhi ya ndugu wa karibu wa familia ya marehemu.
Baba wa marehemu Emmanuel Ngowi alisema mwili huo umeletwa hospitalini hapo ili kufanyiwa vipimo ambavyo vimekosekana katika hospitali ya Kiteto.
“Hata
hivyo majibu ya awali yaliyotolewa hospitali hapo yalionyesha jicho la
kulia limevilia damu, pia alikutwa na michubuko miguuni” Ngowi.
Naye Mjomba wa marehemu Michael Ngowi
alisema matukio ya wanafunzi kupigwa hadi kufariki yamekuwa yakitokea
shuleni hapo kila mara kutokana na wahusika kutochukuliwa hatua yoyote.
MTANZANIA
Mwanasiasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mapinduzi ya Zanzibar, Nassor Hassan Moyo amesema hafikirii kujiunga na chama chochote cha siasa, baada ya kuvuliwa uanachama wa CCM.
Wiki iliyopita, Katibu wa CCM Mkoa wa
Magharibi Unguja, Aziza Iddi Mapuri alitangaza kumfukuza mwanasiasa huyo
mkongwe kwa madai ya kukisaliti kwa kukiuka maadili na kutoa matamshi
yasiyokubaliana na sera za chama chake.
Moyo alisema umri wake haumruhusu kujiunga na chama chochote cha siasa, lakini ataendelea kuitetea Zanzibar.
“Sina
mpango wa kujiunga na chama chochote cha siasa kwa sababu umri wangu
hauruhusu, nitaendelea kuungana na wale wote wanaopenda maendeleo ya
Zanzibar na wale wanaounga mkono muundo wa serikali tatu, nitashirikiana
nao vyovyote iwavyo,”a Moyo.
Mzee Moyo aliyepata kushika nyadhifa
mbalimbali, alisema tatizo kubwa linaloisumbua CCM ni kwamba hakitaki
kukosolewa jambo ambalo wanadhani linawapa nguvu wapinzani.
“CCM
wanadhani nchi hii ni yao, kumbe ni ya Tanganyika na Zanzibar. Fikiria
kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Jaji Warioba, tulipeleka maoni
yetu ya kamati ya maridhiano na baadaye tukaiunga mkono, lakini Rais
Dk.Ali Mohamed Shein aliwahi kusema haitambui kamati yetu.
“Hatuna shida na Rais Shein, bali tuna shida na wananchi tu na si
lingine. Sasa wamenifukuza lakini nitaendelea kutetea maoni ya wananchi,”alisema.
Akizungumzia alivyoshiriki mkutano wa Chama cha Wananchi (CUF), alisema hakuibuka tu, bali alialikwa kama mwenyekiti wa kamati ya maridhiano.
HABARILEO
Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge
juzi aliokolewa kwa risasi katika vurugu za kundi la wananchi,
waliomvamia karibu na ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Simiyu na kusababisha taharuki katika ofisi za chama hicho.
Mmoja wa watu waliokuwa kwenye gari la mbunge huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
aliyekuwa na msafara wake kutekeleza shughuli za ubunge jimboni mwake,
ndiye aliyefyatua risasi hewani ili kutawanya umati huo.
Hata hivyo, hali hiyo ilitafsiriwa na
Chadema kuwa ni mkakati wa mbunge huyo wa kuwafanyia fujo katika ofisi
zao, hivyo kulifikisha suala hilo Polisi ambako wamefungua jalada.
Madai ya tukio hilo yaliyotolewa na John Heche, Mwenyekiti wa zamani wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA), yamethibitishwa Jeshi la Polisi ambalo limesema aliyefyatua risasi si Chenge, bali mmoja wa watu waliokuwa kwenye gari lake.
Heche alisema tukio hilo lilitokea jana
majira ya saa 1:30 jioni katika ofisi za chama hicho mkoa wa Simiyu
zilizoko eneo la Salunda.
“Mara
baada ya kumalizika kwa Mkutano wa chama hicho uliohutubiwa na Naibu
Katibu Mkuu Chadema Tanzania Bara, John Mnyika baadhi ya wanachama
walipanda magari na wengine kutembea kwa miguu ili kwenda kwenye ofisi
zao za mkoa ambako watu walishtuka kumuona mbunge huyo akishuka katika
gari lake,” Heche.
“Kutokana
na kitendo hicho, mmoja wa walinzi wa Chadema aliwaomba waondoke eneo
hilo na pia waache kupiga muziki huo kwani kuna kikao cha ndani cha
viongozi wa chama hicho kinachoendelea lakini waligoma.
Kutokana na hali hiyo, viongozi wa
Chadema mkoa wa Simiyu waliripoti tukio hilo Makao Makuu ya Polisi
wilaya ya Bariadi na kutoa malalamiko yao juu ya tukio hilo .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Gemini Mushi
alikiri kutokea kwa tukio hilo, lakini alisema kuwa aliyefyatua risasi
si Chenge, bali ni kijana Ahmed Ismail aliyekuwa katika gari la Mbunge
huyo, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa zamani na Waziri aliyeziongoza
wizara kadhaa, zikiwemo Katiba na Sheria na Miundombinu.
HABARILEO
Uchaguzi wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) mkoa
wa Simiyu uliofanyika jana, nusura uvunjike baada ya baadhi ya
wagombea, kuanza kutuhumiana ndani ya ukumbi wakati wakijieleza kwa
wajumbe.
Mmoja wa wagombea hao ambaye alikuwa akigombea nafasi ya Uwakilishi wa Kamati Tendaji Taifa, Chananja Buluba alipopewa nafasi ya kujieleza, alidai kuwa uchaguzi huo umegubikwa na vitendo vya rushwa.
Alidai kuna baadhi ya wajumbe walipewa
Sh 50,000 hadi Sh 100,000 kutoka kwa wagombea wa nafasi za Uwakilishi wa
Kamati Tendaji Taifa, Mwenyekiti na Mweka Hazina.
Akiwa anazomewa na baadhi ya wajumbe
hao, mgombea huyo alieleza kuwa mbali na kupewa fedha, baadhi ya wajumbe
walilipiwa sehemu za kulala kwa siku tatu pamoja na chakula.
Hali hiyo ilionekana kuwakera wajumbe wa
uchaguzi huo na kumtaka athibitishe mbele yao na kuwataja watu ambao
walipewa pesa, kulipiwa sehemu za kulala pamoja na chakula.
Akiwa tayari kutaka kuwataja wahusika wa
vitendo hivyo, mgombea huyo alizuiliwa na Mratibu wa Uchaguzi huo
ambaye ni Katibu wa CWT mkoani hapa, Fatuma Bakari kwa madai kuwa alikuwa amekiuka taratibu za uchaguzi.
Kitendo cha kuzuiliwa na katibu huyo,
kilionekana kumkera mgombea huyo na kuacha kujieleza mbele za wajumbe
hao, ambapo aliamua kuwaita waandishi wa habari nje ya ukumbi wa mkutano
ili kuwaeleza hali hiyo.
“
Nimechukia sana kitendo cha Mratibu ambaye ni Katibu CWT Mkoa
kunizuia…hali ya uchaguzi huu imechafuliwa sana na rushwa, wagombea
wamegawa pesa kama karanga na sijui wametoa wapi wakati wao ni walimu
kama mimi,” Buluba.
Alibainisha kuwa pesa walizokuwa
wakizitoa wagombea hao, zilikuwa na ufadhili kutoka katika vyama vikubwa
vya siasa, alivyovitaja.
NIPASHE
Chama cha Tanzania Labour (TLP), kimefanya mkutano mkuu wa uchaguzi huku mwenyekiti wake wa Taifa, Augustino Mrema, akitumia muda mrefu kumshutumu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahaman Kinana na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, kwamba wanakihujumu chama hicho ili kianguke.
Alisema hayo jana wakati wa mkutano huo
uliofanyika jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumchagua mwenyekiti wa
Taifa na kumuidhinisha mgombea urais atakayepeperusha bendera ya chama
hicho katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Mrema alisema Kinana alipofanya ziara
katika Jimbo la Vunjo alisema uongo kwa kuwaeleza wananchi kwamba fedha
za mfuko wa jimbo zilizopelekwa na serikali katika jimbo hilo kwa miaka
minne ni Sh. milioni 400 wakati ni Sh. milioni 150 tu.
“CCM
wameamua kuishi kwa uongo, nani atawaheshimu, nani atamuheshimu Kinana,
mbona anamdhalilisha Rais Kikwete, Kinana hafai mbona tembo wanauawa na
meno ya tembo yanaibwa lakini hasemi haya anakaa kimya,” alisema.
Alisema Kinana anashangaza Watanzania
kwani katika ziara zake hazungumzii viongozi waliokula fedha za akaunti
ya Tegeta Escrow badala yake anaiandama TLP na Mrema na kwamba hata
akifanya hujuma hizo kamwe hataweza kuangushwa katika jimbo la Vunjo.
“Kinana
anatukana mawaziri Rais amekaa kimya hamkemei, Kinana anatumia fedha
nyingi kunichafua na sijui kama ni fedha halali, Rais usinyamaze watu wa
Vunjo hawatakubali kuona hujuma zinazofanywa na Kinana dhidi ya TLP,” alisema.
Mrema alisema kutokana na hali hiyo
amemwandikia barua Rais Jakaya Kikwete kumlalamikia Kinana kwa kauli
zake kwamba amejilimbikizia madaraka na kumuomba Rais achukue hatua.
Kuhusu Mbatia, alidai kuwa amekuwa akiendesha kampeni chafu ya kuichafua TLP ambazo zimepewa jina la ‘delete TLP’ katika jimbo la Vunjo kiasi cha kusababisha baadhi ya viongozi wa TLP kuhamia NCCR-Mageuzi.
“Kuna madiwani wa TLP ambao waliasi
hadharani na wakawa wanampigia debe Mbatia na waliingia katika kampeni
hiyo na walikuwa wakidai uamuzi wa kumuunga mkono Mbatia ni uamuzi wa
Mungu,” alisema.
Alisema watu ambao wamekuwa wakimuombea
mabaya afe ili wagombee jimbo la Vunjo wahesabu kuwa wameumia kwani hivi
sasa yupo ‘fiti’ na kuwahakikisha wajumbe wa mkutano huo kwamba
atagombea jimbo hilo na kuchaguliwa kwa mara nyingine tena.
Mbatia alipopigiwa simu yake ilikuwa inaita bila kupokelewa na alipotumiwa sms alijibu kuwa yupo kwenye mkutano.
“Hali
ya kisiasa katika nchi si nzuri, nchi inaelekea kubaya, kuna matatizo
mengi kama vile ugaidi, udini, mauaji ya albino, uvamizi wa vituo vya
polisi, mauaji ya polisi na kuporwa bunduki. Sioni kiongozi
anayejitokeza kukabiliana na matatizo hayo,” .
NIPASHE
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinari Pengo, amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kugombea urais, ili wananchi wapate wigo mpana wa kuchagua anayefaa kuiongoza nchi.
Kardinali Pengo alitoa wito huo jana
jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, baada ya
kumalizika kwa mahafali ya saba ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph Tawi
la Dar es Salaam (SJUIT).
Alisema iwapo watajitokeza wagombea
wengi wa urais, itawasaidia wananchi kuwafahamu wagombea wao vizuri,
kuwapima kwa kulinganisha sifa zao kabla ya kuchagua mmoja kuwa kiongozi
wa nchi.
Alisema kujitokeza kwa watu wengi wenye
nia ya kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka
huu ni jambo jema, kwani watakapojitokeza wachache au mmoja, wananchi
wanaweza kuchagua kiongozi asiye na sifa.
“Mimi
nadhani ni jambo zuri kwa watu wengi kujitokeza kugombea nafasi ya
urais, akijitokeza mtu mmoja kugombea urais wananchi watashindwa
kufahamu kama anafaa kwani hakutakuwa na wa kumlinganisha naye,”.
Baadhi ya makada ndani ya vyama vya siasa wametangaza nia ya kuwania nafasi hiyo na wengine wanatajwa.
Kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
makada kadhaa wamejitokeza kutangaza nia ya kumrithi Rais Jakaya
Kikwete atakapong’atuka Oktoba mwaka huu.
Waliotangaza nia hadi sasa ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu; Mbunge wa Nzega, Dk. Khamis Kigwangalah na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye alitangaza akiwa ziarani nchini Uingereza na kueleza kuwa alifanya hivyo kimya kimya.
Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Prof. Mark Mwandosya na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, aliyetangazia nia hiyo nchini Uingereza.
Viongozi wanaotajwa kuwania nafasi hiyo ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa; Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira.
Wengine ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli; Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta; Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro; Mbunge wa Sengerema, Willium Ngeleja na Mbunge wa Songea Mjini, Dk. Emmanuel Nchimbi.
Kwa upande wa Tanzania Labour Party
(TLP) aliyejitokeza na alitarajiwa kupitishwa na Mkutano Mkuu ulioanza
jana jijini Dar es Salaam ni Macmillan Lyimo.
Vyama vya Chadema, CUF, NCCR- Mageuzi na
NLD vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimepanga
kusimamisha mgombea mmoja wa urais.
Wanaotajwa katika vyama hivyo ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba.
Kadhalika, Kardinali Pengo
aliwatahadharisha wananchi dhidi ya wagombea wa nafasi ya urais wanaotoa
rushwa ili waingie Ikulu, kwani uongozi wa taifa hauwezi kununuliwa.
Kila siku asubuhi na mapema tangakumekucha inakupatia yote yaliyojiri magazetini, usiwe mbali nami kwa mengi mazuri nia hapa hapa
No comments:
Post a Comment