Huyu mrembo alifariki baada ya kunywa dawa za kupunguza uzito, mama yake kayasema haya
April 12 2015 ndio ilikua siku yake ya
mwisho duniani baada ya kulazwa hospitali na chanzo cha kifo chake
kikiaminika ni hivyo vidonge ambavyo inasemekana vilikua na sumu.
Mama yake mzazi ameongea na kusema
Madaktari wasingeweza kuokoa maisha yake, kunywa hizo dawa ni sawa na
kujisogeza karibu na kifo, zinasababisha pia mwili upate joto kupitiliza
na kusababisha pia ini kushindwa kufanya kazi.
Haikufahamika ni vidonge vingapi alimeza na
alivitumia kwa muda gani lakini Polisi wa Uingereza wametoa onyo kwa
yeyote mwenye mpango wa kununua dawa online aachane nao tena sanasana
kupitia websites ambazo hazijasajiliwa.
No comments:
Post a Comment