Japan kwenye headlines nyingine tena.. Huyu ROBOT hana tofauti na mtu kabisa..
Bado dunia nzima inazungumzia teknolojia
ya JAPAN, ile treni ambayo imevunja rekodi jana APRIL 21 kwa kutembea
kasi ya kilometa 603 kwa saa, leo iko nyingine.. unajua tumezoea
kukutana na yale masanamu kwenye maduka ya nguo, unakuta limevalishwa
kabisa nguo.. vipi siku unakutana na sanamu la aina hiyo hiyo alafu
linakusalimia au linakuongelesha???
Bado JAPAN imeendelea kukaa kwenye
headlines.. ni upande huo huo wa teknolojia, mpya niliyokutana nayo leo
ni hii ya robot ambalo linafanana kabisa na binadamu, tumezoea yale
mengine ya kwenye movie ambayo mengi tunayaona ni marobot ya chuma hivi,
hili liko kama binadamu.. ukikuta limesimama hivi hata huwezi
kutofautisha na mtu wa kawaida.
Wajapan wamelipa robot jina la Aiko Chihira,
lina uwezo wa kuongea, kusalimia, kuimba.. Kampuni ya Toshiba
wamelitengeneza hili mwaka 2014 lakini Jumatatu April 20 2015 kwa mara
ya kwanza liliwekwa dukani Tokyo, ilikuwa burudani yani watu
wanasalimiwa kama wamekutana na mtu !!
Kwa sasa robot hilo lina uwezo kuongea lugha chache ikiwemo Kijapan na Kichina.
No comments:
Post a Comment