Matokeo ya Yanga VS Polisi Moro yameamua nani Bingwa TZ Bara… eti Yanga?
Yanga imefikisha
jumla ya pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote
inayoshiriki ligi kuu msimu huu, kwa matokeo hayo basi Yanga wanakuwa mabingwa wa Ligi hiyo.
Mechi hiyo kati ya Yanga na Polisi Moro ilikuwa ikipigwa katika Uwanja wa Taifa Dar.. mechi imekamilika kwa Yanga kutoka kifua mbele kwa goli 4-1.
Hamis Tambwe leo aliweza kuing’arisha Yanga baada ya kupachika magoli matatu ambapo goli la kwanza alifunga dakika ya 40 kufuatia krosi ya Saimon Msuva, goli la pili alilifunga dakika ya 53 na goli la mwisho alifunga baada ya kupokea cross kutoka kwa Mrisho Ngassa.
Msuva alikamilisha idadi ya mabao kwa kupiga bao la nne ambapo baadae dakika ya 83 Polisi walishinda bao la kufutia machozi kupitia kwa Bantu Admini aliyepiga shuti kali akiwa nje ya 18.
Ligi kuu Tanzania Bara inatarajiwa kukamilika mwisho wa wiki katika mechi za kukamilisha ratiba ya ligi hiyo kwa msimu huu.
No comments:
Post a Comment