Hadithi hii inaletwa kwenu kwa hisani kubwa na Mkombozi Sanitarium Clinic, Mabingwa wa Tiba Asilia. Mkombozi wanatibu magonjwa sugu yakiwemo homa za mara kwa mara, magonjwa ya tumbo, Bawasiri na maradhi ya moyo. Mkombozi wako na Mashine ya kupima kipimo cha mwili mzima na kugundua maradhi yaliyofichikana. Wapo Chuda Tanga mkabala na Kampuni ya usafirishaji abiria (Raha leo) simu 0654 361333
ILIPOISHIA
Siku ya pili yake nilimchukua
rafiki yangu nikaenda naye kupeleka pesa hizo.
Mipango ya harusi ikafanywa.
Baada ya wiki mbili nikaenda
Ponwe kumuoa Halima.
Baada ya kuoana na Amina
ndipo nilipoanza kufaidi maisha ya ndoa. Kuse,ma kweli yalikuwa matamu kinyume
na kuishi kihuni.
Kwanza gharama ya maisha
ilipungua sana.
Pesa ambayo hapo mwanzo nilitumia peke yangu kwa siku kwa kula kwenye mikahawa, ilitumika kwa siku
mbili nilipokuwa na mke wangu.
Kadhalika nilikuwa na
mwenzangu wa karibu wa kuniliwaza, kunishauri na kunisaidia pale nilipohitaji
mwenza wa kunisaidia.
Kwa kweli nilihisi raha na
nilijilaumu kwa kuchelewa sana
kumuoa Halima.
SASA ENDELEA
Niliendelea na kazi yangu ya
teksi. Fedha nilizopata ntulitumia, kiasi kingine tuliwek kama
akiba yetu. Miezi michache tu baad ya kuoana, ndoa ilijibu. Halima akapata
ujauzito.
Halima alinijulisha usiku
kuwa alikuwa mjamzito. Wakati tunataka kulala aliniambia.
“Subiri”
“Nisubiri nini?” nikamuuliza.
“Subiri nikuoneshe kitu”
“Kitu gani?”
“Una haraka gani?”
Halima akasimama mbele yangu
na kuushika mkono wangu kisha akaushikisha kwenye tumbo lake chini
ya kitovu. Akawa anautomasisha kwenye tumbo lake.
“Unaona nini?” akaniuliza.
“Sioni kitu” nikamjibu.
“Huoni kitu kigumu gumu?”
“Nakiona, ni nini?”
Halima akauachia mkono wangu
kisha akapanda kitandani. Wakati anavuta shuka nilimuuliza.
“Mbona hukiambii ni nini?”
“Mimba!” akanijibu huku
akiendelea kijifinika.
“Hiyo ni mamba?”
Ndiyo”
“Mbona ndogo sana?”
“Si ndio inaanza, ina mwezi
mmoja. Ujue mwezi uliopita sikupata siku zangu”
Ni kweli ilikuwa mamba ya
mwezi mkmoja. Ilitupa furaha sote wawili. Tukaona karibuni tutaitwa baba na
mama.
Lakini kadiri siku
zilivyoendelea Halima alikuwa akiniambia anapolala usiku anaota ndoto
amejifungua watoro wawili mapacha. Watoto hao ni wazuri na weupe kama wazungu!
Nikadhani labda ni kweli
atajifungua mapacha. Mimba ilipoiza miezi mitatu Halima aliota akifanya tendo
la ndoa na mwendawazimu. Alipoamka akaanza kuumwa tumbo!
“Una nini?” nikamuuliza
nilipomuona akifurukuta.
Akanihadithia ile ndoto
aliyoota kasha akaniambia alipoamka aliona tumbo linamuuma.
Wakati ananieleza hali
ilizidi kuwa mbaya. Nikafikiria nimpeleke hospitali lakini ile mamba ikatoka
muda ule ule.
Sikujua alikuwa amepatwa na
tatizo gani. Ilikuwa saa kumi na mbili asubuhi. Nikatoka naye na kumpakia
kwenye teksi, tukaenda hospitali ya Bombo.
Tulipofika hospitali
nilimpigia simu rafiki yangu Dk Augostino Kweka. Kwa bahati njema alikuwa pale
pale hospitali, akaja kumtazama mke wangu kisha
akaniambia.
“Anahitaji kusafishwa. Mimba
haikutoka yote”
Dk Kweka alinisaidia sana. Alilichukua jukumu
lile kirafiki. Mpaka inafika saa tatu mke wangu alikuwa ameshasafishwa.na
kupelekwa wodini. Mimi mwenyewe nilikuwa hapo hapo hospitali muda wote.
Baada ya kupelekwa wodini Dk
Kweka aliniita, nikaenda wodini na kumuona mke wangu. Hali aliyokuwa nayo
wakati anapelekwa kufanyiwa usafishwaji, siyo aliyokuwa nayo wakati ametolewa.
Alikuwa na afadhali sana.
Nikamshukuru Dk Kweka nay eye
akanishukuru pia.
“Unaweza kurudi naye
nyumbani” akaniambia.
“Tatizo lake limekwisha
kabisa?” nikamuuliza.
“Limekwisha isipokuwa kila
wiki umlete kuangalia maendeleo yake”
“Lilikuwa ni tatizo gani?”
“Mimba ilikuwa haikushika
sawa sawa. Ana udhaifu kwenye kizazi chake. Katika hali kama
hiyo anapopata mshituko, hofu au fadhaa, mara moja mimba inaweza kutoka”
Nikahisi ile ndoto aliyoota
ndiyo iliyomshitua na kusababisha mimba hiyo kuporomoka.
“Asante dokta, sasa unatushauri
nini?”
“Kama
nilivyokwambia kila wiki mlete hapa hospitali, nione maendeleo yake”
“Sawa dokta, nitafanya hivyo”
ITAENDELEA
NILIJUA NIMEUA

|
|
Friday, April 24, 2015
NILIJIA NIMEUA SEHEMU (6)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment