Umeisikia ya waumini kusali wakiwa hawana nguo?? Kilichofuatia je?
Malalamiko yalikuwa mengi tangu kufunguliwa kwa kanisa hilo la Healing Ministry
katika Kaunti ya Machakos, Kenya.. wanawake wanaingia kwenye migogoro
na wanaume zao kisa ibada, wakatu mwingine walikua wanaenda kulala
hukohuko.
Hii kitu ikaleta migogoro mingi kwenye
baadhi ya familia, baadae kukawa na malalamiko kwamba wanawake wanaosali
kwenye Kanisa hilo wanasali wakiwa wamevua nguo zote.. siku moja watu
wa eneo hilo wakavamia kanisani hapo usiku, wakakuta wanawake wakiwa
wanasaliwa huku wamevua nguo zote.. Kasisi akajitetea kwamba alikuwa
akiwafanyia ibada maalum.
Mwenyekiti wa muungano wa wafanyabiashara eneo hilo Duncan Mutua amesema; “Tulivamia kanisa hilo na kumfumania Kasisi akiwamwagilia wanawake maji wakiwa uchi wa mnyama alijitetea akisema alikuwa akiwafanyia maombi spesheli,”.
Amesema wasiwasi kuhusu shughuli za
Kanisa hilo uliongezeka baada ya wanawake wa eneo hilo kutumia muda wao
mwingi Kanisani na hata kuwaacha waume wao usiku na kwenda kwenye ibada
za mkesha.
No comments:
Post a Comment