Baada ya
jana kukubali kichapo kingine cha bao 3-1 katika uwanja wao wa nyumbani
dhidi ya Liverpool, mashabiki wa Chelsea waliamua kuimba huku wakimtaja
jina kocha wao Mourinho wakati wote wa mechi.Tajiri wa Chelsea, Roman
Abramovic hakuwepo uwanjani wakati mechi hiyo iliyotajwa kuwa ya mtego
kwa Mourinho lakini bila shaka aliwasikia mashabiki wakimsapoti kocha
wao kupitia television nyumbani kwake.
Baada ya
mechi, pamoja na kudai hana cha kuongea huku akijibu majibu ya mkato
sana, kocha Jose Mourinho alidai kwamba haondoki klabuni hapo huku
akisema mashabiki hawakua vichaa kumuimba jina lake kwani wanajua jinsi
yeye na wachezaji wanavyojaribu kupata matokeo.
Kwa
utamaduni wa Chelsea tangu kununuliwa na tycoon Roman Abramovic, amekua
akiwasikiliza zaidi mashabiki wake wanasema nini kabla ya yeye kufanya
maamuzi, historia inaonesha Andres Vila Boas na Rafael Benitez
walifukuzwa asubuhi baada ya jana yake kuimbiwa nyimbo za kutotakiwa na
mashabiki Stamford Bridge na Abramovic akawasikiliza.
No comments:
Post a Comment