Tangakumekuchablog
Tanga, KOCHA
msaidizi wa Azam FC, Dennis Kitambi, amesema wachezaji wake wameiva kuikabili
African Sports ya Tanga na anatambua kuwa wagozsi hao watakuwa mbogo kutokana
na kuwa katika mstari mwekundu wa kushuka daraja.
Akizungumza mara baada ya mazoezi
uwanja wa Mkwakwani mapema leo, Kitambi alisema ushindi leo ni lazima ili
kujihakikishia kumaliza ligi nafasi ya pili na kusema kuwa mchezo huo
anautabiria kuwa mkali.
Alisema timu hiyo imeongozana na
wachezaji 22 na watano (hakuwataja) wamebaki Chamazi kwa mazoezi madogomadogo
na kusema hakuna majeruhi yoyote na wote wako fiti.
“Mchezo wa leo nautabiria utakuwa
mkali kwani wagosi watapambana mwanzo hadi mwisho kuepukana na kuungana na ndugu
zao ambao wameshanawa mikono, cha kufurahisha tuko na jeshi la wachezaji
ishirini na mbili” alisema Kitambi na kuongeza
“Kuna wachezaji watano wamebakia
Chamazi na wanajifua kama ujuavyo ligi inaendelea, hawa waliopo hapa
wamedhamiria kunyakua pointi tatu muhimu zitakazotuwezesha na kuwa na uhakika
wa kumaliza nafasi ya pili mwisho wa ligi” alisema
Kwa upande wake, Kepteni wa Azam,
Himid Maona, alisema wako tayari kwa mchezo wa African Sports na kusema kuwa
wataondoka na pointi tatu leo hivyo wapinzani wao wasitarajie ushindi.
Alisema cha msingi ambacho
kitawapelekea kuibuka na ushindi ni kuwa timu hiyo iko katka janga la kushuka
daraja hivyo watakuwa wamenyong’onyea na kuwa rahisi kuwafunga.
“Ushindi leo ni mweupe kwani
natambua mtu akijeruhiwa hupoteza mwelekeo na hiki ndicho ambacho kitaonekana
leo na niseme kuwa tutamaliza ligi katika nafasi ya tatu na ushindi ni lazima”
alisema Kitambi
Aliwataka washabiki wa timu hiyo
kuwashangilia kwa nguvu na kuingia uwanjani kwa wingi kuhakikisha wanatoa hamasa ya ushindi kwa wachezaji uwanjani.
Mwisho
Kocha Muingereza wa Azam FC, Stewart Hall, akiwapa mbinu wachezaji wake
mara baada ya kumaliza mazoezi uwanja wa Mkwakwani kujiandaa na mchezo wake na African
Sports leo.
No comments:
Post a Comment