HADITHI inaletwa kwenu na Candle Education Centre Tanga kituo mahiri cha Kurisiti mitahani kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza kielimu, 0715 772746
SIMULIZI ZA FAKI A FAKI 0655 340572
SITASAHAU NILIVYOGEUZWA PAKA 16
ILIPOISHIA
Siku moja kabla ya kumalizika siku
hizo saba tulipokutana usiku tulikwenda kufukua maiti ya mtoto aliezikwa siku
ile. Kwa mujibu wa wenzangu alikuwa mjukuu wa Yule bibi ambaye alimtoa
mhanga ili afanyiwe karamu ya wachawi.
Pamoja na ukweli huo nilihisi pia
kuwa kulikuwa na njama kati ya mke wangu na yule bibi ya kunilisha nyama ya
maiti. Baada ya mwili wa mtoto kufukuliwa kila mmoja alinyofoa kipande chake
cha nyama mbichi. Akawa anakila hapo hapo tena bila kukunja uso kama vile
anakula paja la kuku wa kukaanga.
Mimi nilinyofolewa kipande na bibi,
akaniambia ‘Kula na wewe”
“Siwezi kula’ nikamjibu”
“Lazima ule pamoja na wenzako”
“Siwezi”
“Utaweza. Kata kipande utafune”
Nilikuwa nimeshika kile kipande cha
nyama nikikiangalia.
Usibishane na mimi, nimekuambia kula
hicho kipande cha nyama.wewe si umekubali kujiunga na sisi.”
Bibi akaniambia huku akiwa
amenitolea macho yake yanayotisha.
SASA ENDELEA
Siku ile ujanja wangu ulikwisha.
Sikuwa na pa kukwepa. Bibi alinikazania nile ile nyama kama wenzangu
walivyokula. Tangu alinibembeleza, mwisho akawa ananilazimisha.
“Tia mdomoni’ akaniambia kwa ukali.
Nikakitia mdomoni kile kipande cha nyama.
“Kata kidogo utafune’”
Nikakikata kipande kidogo kwa meno.
Ilikuwa nyama laini inayozizima. Nikawa naisikiliza ladha yake. Ilikuwa na
ladha ya kuanza kuoza na haikuwa na chumvi.
“Tafuna’ bibi akanihimiza.
Nikatafuna huku mate yakinitoka. Hayakunitoka
kwa sababu ilikuwa ni tamu bali yalinitoka kwa kusababu ya kupata kinyaa.
Sikutaka kumeza mate.
“Sasa meza’ bibi akanihimiza.
Kumeza ilikuwa kazi. Ilibidi
nishikwe ili niweza kumeza kwani mishipa ilikuwa haikubali.
“Kata tena utafune” bibi akaniambia
tena.
“Imetosha’ Nikamwambia .
Haikutosha. Mpaka ukimalize kipande
chote nilichokupa”
“Chote hiki?’’ Nikang’aka.
‘Ndio. Si umeshanza kula. Sasa
unashindwa na nini?”
Nikang’ata kipande kingine na kuanza
kutafuna. Wachawi wote walikuwa wamemaliza kula nyama zao na kunisubiri mimi.
"Sasa tutakuamini kuwa wewe ni
mwenzetu"
Sikuwa nikisikiliza alichokuwa
akiniambia yule bibi. Nilikuwa nikiisikiliza ile nyama ya maiti ya binaadamu
ikiteremka ndani ya tumbo langu. Mdomo ulikuwa nimeuacha wazi ili kutoa
hewa ya ile nyama. Kinywa changu kilikuwa kimeharibika kwa ladha ambayo
niliihisi kama najisi.
Mwili ulinisisimka, nikatikisa
kichwa.
"Ndiyo. Sasa wewe ni
kidume!" yule bibi aliendelea kuniambia alipoona nasisimkwa huku natikisa
kichwa. Alijua fika kuwa ile nyama ilikuwa ikinisisimua kwa sababu haikuwa
nyama ya kuliwa na mwanadamu lakini alitaka kunipa sifa tu ya kipuuzi.
Sifa ya kipuuzi! nikawaza kwa
uchungu.Unanipa sifa kwa kula nyama ya binaadamu mwenzangu tena nyama ya maiti?
Nilikuwa kama niliyepata kichaa
nikanyanyuka pale nilipokuwa nimekaa.Nilitamani nipige makelele lakini
nikajizuia.
"Unakwenda wapi?" Mke
wangu akaniuliza.
"Si tayari nimeshakula"
nikamwaambia
"Sasa unakwenda wapi?"
"Nipo tu"
"Kesho asubuhi uje naye
nyumbani kwangu" bibi akamwaambia mke wangu
"Nitakuja naye"
"Nataka nimkabidhi vitu
vikali"
Baada ya kauli yake ile bibi
aliagiza tutawanyike.
Mimi na mke wangu tukarudi
nyumbani.Siku ile sikupata usingizi kwa mawazo.Kama ningejiingiza katika uchawi
kwa hiari yangu ningekubali kila kitu. Lakini nimelazimishwa.
Ilikuwa kufuru (kosa) kubwa kula
nyama ya binaadamu mwenzako aliyekufa.Lakini sikula kwa kupenda kwangu.Sikuwa
na jinsi.Nilikuwa kama mateka niliyekuwa sina hiari.
Ningeweza kwenda kwa wazazi wa
Chausiku kumshitaki lakini nilihisi huo uchawi umo katika familia yake.Kwani
nilivyojifunza ni kuwa uchawi unapokuwa katika familia unarithiwa kama mkoba wa
uganga.
Sasa ningekwenda kumshitakia nani,
wakati familia nzima ina jadi ya uchawi?
Isitoshe hata kama uchawi huo
ulikuwa ni wa Chausiku peke yake, kwenda kumshitaki kungesababisha chuki na
uhasama ambao ungepelekea na yeye kwenda kuniripotia polisi.
Niliwaza sana usiku huo.Kwa kweli
sikupata usingizi wa maana kabisa.Kulipokucha baada ya kuoga na kunywa chai,
mke wangu akaniambia twende kwa yule bibi kigagula.
Kwa vile bibi huyo aliniambia niende
na mke wangu tukaenda.
Tulipofika tulimkuta bibi akinywa
uji ukumbini. Uji huo ulikuwa kwenye kijungu.Alikuwa akiuchota kwa upawa na
kuutia kwenye kifuu cha nazi.Hicho kifuu kimekuwa ndiyo kikombe chake
alichonywelea.Pembeni mwake alikuwa ana bakuli lililokuwa na mafuta mazito
yalioganda.
Kila alipotia uji kwenye kifuu ili
anywe huudodeza na yale mafuta na kuyachanganya kwenye uji anaokunywa.
Baada ya kusalimiana naye bibi
alitukaribisha tunywe uji.
"Karibuni uji lakini hauna
sukari. Ni uji wa chimvi tu" akatuambia
"Endelea kunywa tu bibi. Sisi
tumesha kunywa" nikamwaambia
"Niwatilia kidogo muonje?"
"Kunywa tu bibi.Tumekunywa chai
tayari" nilimuambia tena.
Bibi akalichukua lile bakuli la
mafuta akadodeza mafuta kidogo kwenye uji wake kisha akanywa.
"Ni mafuta ya nini bibi
unayoyachanganya?"
Bibi akacheka. "Muulize
mke wako anajua"
Nikamtazama Chausiku na
kumuuliza "Ni mafuta ya nini?"
"Akwambie mwenyewe"
"Kwani jana usiku tulikula
nini?" bibi akaniuliza
"Ile ilikuwa nyama"
nikamjibu
"Sasa haya ni mafuta yake"
"Mafuta ya nyama
ya.......!" nikauliza kwa mshangao bila kumalizia sentensi yangu. Nilishindwa
kusema "Nyama ya maiti"
"Tunakamua tunaweka" bibi
aliendelea kuniambia
"Mbona sikuona ukikamua?"
"Nakamulia nyumbani
kidogokidogo"
Ndani ya moyo wangu nilishituka
lakini nilijifanya niko kawaida tu
"Unataka uonje kidogo?"
"Nitaonja siku nyingine"
"Ameshayaonja sana. Nimeshamtilia
kwenye mchuzi mara nyingi. Mwenyewe akausifia ule mchuzi akasema ni mtamu
kweli" mke wangu akasema.
Nikashituka tena
"Kumbe wewe pia unayo?"
nikamuuliza Chausiku kwa sauti tulivu ili wasione kuwa nilikuwa mpinzani wa
vitendo vyao
"Nilikuwa nayo, niliyamaliza
jana kwenye mchuzi"
Kumbe nalishwa vingi? niliwaza
kimoyo moyo
Kama vile bibi huyo aliyasoma mawazo
yangu aliangua kicheko kisha akanitazama, na mimi nikajifanya nacheka uongo
"Sasa kazi utaiweza tu.Usiwe na
wasi wasi na wala usiwe na haraka.Tunakwenda hatua kwa hatua. Hata mke wako
tulitoka naye mbali" bibi akaniambia baada ya kunitazama
Sikumjibu kitu. Moyo wangu ulikuwa
umesha fadhaika
"Subirini ninywe uji twende
chumbani"
HAYO NDIYO MAMBO YA BLOG YA TANGA
KUMEKUCHA. TUONANE TENA HAPO KESHO.
No comments:
Post a Comment