Tangakumekuchablog
Tanga,
JESHI la Polisi Tanga, limesema mtu
ambaye hakufahamika ameuwawa na watu wenye hasira kali eneo la Daraja Bovu kata
ya Mikanjuni baada ya kutuhumiwa kurusha vitu vilivyodhaniwa kuwa ni mabomu ya mkono na kurusha ovyo
barabarani.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo, Kamanda wa Polisi Tanga, Leornard Poul, alisema tukio hilo lilitokea jana
saa 2 ; 30 usiku na kusema kijana huyo aliekuwa na zaidi ya umri wa miaka 30
alikufa wakati akipelekwa hospitali ya Bombo.
Alisema wakati kijana huyo akirusha
mabomu ovyo wananchi walitoa taarifa kwa kituo cha polisi na wakati jeshi hilo
lilipofika walimkuta kijana huyo akiwa hoi baada ya kupokea kipigo kutoka kwa
wananchi.
“Polisi ilifika eneo ambalo kijana
ambaye hakufahamika jina lake akiwa yuko hoi baada ya kupokea kipigo, alikuwa
akirusha ovyo mabomu njiani muda ambao wananchi wanarejea majumbani kutoka
katika majukumu na swala ya Isha kwa Waislam” alisema Poul na kuongeza
“Yule kijana alikuwa na pikipiki na
mwenzake mmoja ambapo yule wa nyuma alikuwa anadondosha moja moja, watu
walishtushwa baada ya kuona moshi mzito na gesi kama ambalo limegoma kuripuka”
alisema kamanda
Alisema wakati polisi ikimpeleka
hospitali kijana huyo ambaye hakufahamika jina lake mara moja alikufa akiwa njiani
baada ya kupokea kipigo kizito kutoka kwa wananchi.
Kamanda Poul alisema kipindi hiki
cha kuwasaka majambazi jeshi la polisi limefanikiwa kuwatia mbaroni watu wengi
na wengine bado wanaendelea kusakwa na kusema kuwa wote waliojihusisha na
ujambazi na mauaji watashikwa.
Jiji la Tanga limekuwa katika hali
ya simanzi na woga baada ya kutokea matukio mfululizo ya mauaji kwa kutumia
silaha na uporaji katika maduka na vituo vya huduma ya mafuta.
Hali hiyo imekuwa ikiwaweka katika
hali ya Sintofahamu wananchi na hivyo kulitaka jeshi hilo kuhakikisha
inawakamata na kukomesha matukio hayo na wananchi kufanya shughuli zao kwa
amani.
Wananchi hao wameiambia
tangakumekuchablog mapema leo kuwa kipindi hiki cha ufufuaji wa uchumi na
viwanda Tanga kunahofu ya wawekezaji kubadilisha malengo yao.
Itakumbukwa hivi karibuni Tanzania
ilikuwa katika ushindani mkubwa ya ujengaji wa bomba la mafuta na kugombewa na
Kenya na hatimaye Tanzania kushinda mtanange huyo hivyo bomba hilo kujengwa
Tanga.
Wananchi wamelitaka jeshi la Polisi
na Usalama wa Taifa kuangalia kwa jicho la pili vitendo vinavyotokea Tanga
kwani huenda ni hujuma ili sera ya Serikali kufufua viwanda na ujengaji wa
bomba la mafuta uwe ndoto
Kwa habari, matukio na michezo ni
hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment