Wafanyabiashara zaidi ya 300 wakamatwa kwa kutotoa risiti za EFD’S.
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata akizungumza na
waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu mwenendo wa makusanyo ya
mapato nchini.
……………………………………………………………………………………………….
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
imewakamata zaidi wafanyabiashara 300 kwa kosa la kutotumia mashine za
(Electronic Fiscal Devices) EFD’S katika biashara zao.
Akizungumzia na waandishi wa
habari Jijini Dare s Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania(TRA) Alphayo Kidata amesema mamlaka yake imefanya uchunguzi wa
kina na kuwabaini wafanyabiashara hao katika maeneo mbalimbali nchini
wakikiuka agizo la kuwa na mashine hizo.
“ Tumeshaanza kuwapeleka
mahakamani wafanyabiashara ambao wanakwepa kulipa kodi kwa kuuza bidhaa
bila risiti na pia tumetaifisha bidhaa mbalimbali zilizoingizwa nchini
kwa njia ya magendo na kukwepa kodi “ Alisema Kidata.
Kamishna Kidata amefafanua kuwa mamlaka haitowavumilia wafanyabiashara wanaoikosesha mapato Serikali kwa kuuza na kutoa huduma bila risiti za EFD’s kwa makusudi na hasa wale wafanyabiashara wanaouza kazi za wasanii bila stempu za kodi pamoja na wafanyabiashara wanaojihusisha na magendo.
Kamishna Kidata amefafanua kuwa mamlaka haitowavumilia wafanyabiashara wanaoikosesha mapato Serikali kwa kuuza na kutoa huduma bila risiti za EFD’s kwa makusudi na hasa wale wafanyabiashara wanaouza kazi za wasanii bila stempu za kodi pamoja na wafanyabiashara wanaojihusisha na magendo.
Vilevile amefafanua kuwa, kwa
wafanyabiashara waliopelekwa mahakamani mara baada ya kumalizika kwa
kesi zao na kupewa adhabu ya kulipa faini, wakibainika tena kurudia
makosa hayo adhabu kali zaidi zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kifungo
cha miaka mitatu jela kwa kukaidi agizo la Serikali.
Aidha, Mamlaka imetoza faini ya
Shillingi Mil 746 kwa wafanyabiashara waliokutwa na makosa mbalimbali
yakiwemo kutotumia mashine za kielotroniki za EFD’s , kuingiza bidhaa
kimagendo na kuuza kazi za wasanii bila ya stempu ya kodi.
Mamlaka inatoa wito kwa wananchi
wote kuwa mabalozi wa kodi na kichocheo cha ukusanyaji wa mapato
kwakutimiza wajibu wao wa kudai risiti wanaponunua bidhaa au kupatiwa
huduma mbalimbali.Na Raymond
No comments:
Post a Comment