Mwenyekiti
wa Shirikisho la Taasisi za Hijja Tanzania (TAHAFE), Sheikh Abdallah
Khalid (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam
jana, kuhusu mchakato wa kwenda kuhiji mwaka huu 2016. Kushoto ni Katibu
wa Taasisi hiyo, Dk. Ahmed Twaha na kulia ni Mjumbe, Hassan Ali.
Katibu wa Shirikisho la Taasisi za Hijja Tanzania (TAHAFE), Sheikh Abdallah Khalid , akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
……………………………………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
OFISI
Kuu ya Hijja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezitangaza taasisi 31
zilizokidhi vigezo vya kupeleka mahujaji kwenda kuhiji kwa mwaka 2016.
Hayo
yalibainishwa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Taasisi za Hijja Tanzania
(TAHAFE) Sheikh Abdallah Khalid wakati akizungumza na waandishi wa
habari Dar es Salaam jana.
Alisema
shughuli zote za utekelezaji wa ibada ya Hijja na Umra hapa nchini
zinasimamiwa, kuratibiwa na kuendeshwa chini ya uongozi wa Biita
inayoundwa na Shirikisho la Taasisi za Hijja Tanzania (Tahefa) na Umoja
wa Taasisi za Hijja Zanzibar (Utahiza).
Alisema
gharama za mahuja kwa mwaka huu kutoka nchi kwenda kuhiji ni dola 3400
hadi 4700 na kuwa malipo ya huduma stahili yanapaswa kupitia benki
zilizoanishwa na Wizara ya Hijja Saudia Arabia.
Sheikh
Khalidi alisema taasisi zote zinatakiwa kuwapima afya mahujaji
watarajiwa mapema kuanzia Agosti 8 au kabla ya hapo na kujaza fomu
maalumu zitakazotolewa na Biita na kuingizwa kwenye mtandao.
No comments:
Post a Comment