SITASAHAU NILIVYOKUMBANA NA MWANAUME WA KIJINI
Nilichozoea kusikia ni kwamba kuna majini wanawake wanaojigeuza
binaadamu na kuwatongoza wanaume.
Wengi wa majini hao hutaka kuishi na
binaadamu kama mke na mume jambo ambalo
baadhi ya watu linawavutia kutokana na tamaa ya kupata utajiri.
Lakini nimekuja gundua kuwa hawapo majini wanawake pekee, bali pia wapo majini wanaume ambao
huwatongoza wanawake wa kibinaadamu na kutaka waishi nao kama
mume na mke.
Hilo ndilo lililonitokea mimi na kuniingiza katika mkasa
uliyoyatatanisha maisha yangu. Nilifikia mahali sasa nilitamani kufa.
Jina langu naitwa Enjo, ukipenda
Engle. Ni mtoto wa tatu katika familia ya mzee Sabastian
Chacha. Wa kwanza alikuwa mwanaume. Jina lake ni
Raymond au Ray kama marafiki zake walivyozoea kumuita.
Yeye anafanya kazi Uingreza. Ameshaoa
na ana watoto wawili. Wa pili alikuwa mwanamke kama
mimi, anaitwa Miriam. Anaishi Dar ninapoishi mimi, naye pia ameshaolewa na ana mtoto mmoja.
Kwa wanaomkumbuka mzee Sabastian Chacha aliwahi kuwa mkuu wa wilaya ya
Handeni kisha
akawa mbunge wa jimbo la Kibaha iliko nyumba yetu.
Mzee Chacha alifariki dunia miaka michache iliyopita kwa ajali ya gari. Miaka
miwili baadaye mama yetu naye alifariki ghafla katika hospitali ya Muhimbili
kutokana na shinikizo la damu.
Baada ya masomo yangu ya chuo kikuu nilipata kazi wizara ya afya. Haikutimia
hata miaka miwili nilifukuzwa kazi kutokana na sababu ambayo haikuelezwa wazi.
Lakini nilijua kuwa nilitofautiana na bosi wangu aliyekuwa akinitaka
kimapenzi nikamkataa. Yeye ndiye aliyenisingizia madai ya kuwa mzembe hadi
nikafukuzwa kazi.
Kulikuwa na mwanaume Mzanzibari ambaye nilikuwa na matarajio naye sana kwamba angekuja
kunioa. Yeye alikuwa akisoma huko Uingreza. Kwa vile alikuwa na ndugu zake huko
ambao walikuwa wakijiweza, alikuwa akinitumia pesa mara kwa mara.
Wakati ule nafanya kazi nilipangisha nyumba huko Sinza. Hiyo nyumba
tulichangia watu wawili. Upande mmoja alipangisha mtu mmoja aliyekuwa na
familia yake na upande mwingine nilipangisha mimi lakini tulikuwa tunatumia
mlango mmoja.
Siku moja nilikuwa nimealikwa katika hafla moja iliyokuwa ikifanyika
katika hoteli moja kule Masaki.
Watu tulikuwa tumekaa kwenye viti tukipata vinywaji. Katika meza ya
pembeni kwangu aliketi mzungu mmoja aliyekuwa akinitazama sana.
Mzungu huyo alikuwa amevaa suti iliyokuwa imempendeza sana na alikuwa amejifunga kikuba cha rangi
nyekundu shingoni. Jinsi alivyokuwa amezichonga vyema ndevu zake alionekana
kama muungwana na mtu aliyejistahi sana.
Alikuwa akinywa kinywaji chake taratibu huku jicho lake likiwa
upande wangu.
Sikuweza kujua ni kwanini alikuwa akinitazama sana. Kwanza
nilidhania pengin e alikuwa amenifananisha na
mtu aliyekuwa anamfahamu au aliniona mahali fulani na alikuwa akijaribu
kunikumbuka.
Lakini nilipomuangalia ili niweze kumuelewa vyema alikuwa akikwepesha
macho yake na kutazama upande mwingine. Na ninapogeuza uso wangu anaanza tena kunitazama
bila kujua kuwa nilikuwa nikimtazama kwa pemebeni mwa macho yangu.
Kusema kweli alinikosesha raha. “Kama
amenipenda angeniambia tu kuliko kunitazama vile” nikajiambia kimoyo moyo
nikiwa nimekasirika.
Kwa vile muda ulikuwa umepita sana
niliona bora niondoke nirudi nyumbani. Lakini kama aliyekuwa amesoma mawazo yangu aliinuka haraka
akanifuata nilipokuwa nemeketi na kuniambia.
“Samahani dada, kuna kitu nataka kukuomba” akanimabia kwa kiswahili fasaha.
Nikahisi alikuwa mzungu mwenyeji kwani alikuwa akiifahamu vyema lugha
yetu.
“Bila samahani, niombe tu” nikamjibu.
“Lakini natanguliza samahani, sijui kama
utaridhika”
“Niambie tu, ni kitu gani?”
“Naomba namba yako”
Nilielewa kuwa alikusudia namba yangu ya simu kwa sababu hiyo ni tabia
ya wanaume wengi, lakini nikamuuliza.
“Namba
yangu ya….?”
“Nilikuwa na maana namba yako ya simu”
“Kama ni hilo
tu hakuna tatizo” nikamwambia.
Nikampa namba yangu. Nilimpa ili anipigie na kunieleza kile alichokuwa
nacho moyoni mwake.
itaendelea kesho usikose
No comments:
Post a Comment