Tuesday, January 31, 2017

AU KUJIONDOA MAHAKAMA YA ICC

AU kujiondoa katika mahakama ya ICC

Jengo la mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC
Umoja wa Afrika umeunga mkono mpango wa kujiondoa kwa pamoja katika mahakama ya ICC ambayo mataifa mengi ya Afrika yanahisi inawalenga viongozi wa bara la Afrika pekee.
Uamuzi huo uliochukuliwa katika kikao cha faragha haujahalalisha hatua hiyo.
Viongozi wa Afrika wanasema kuwa mahakama hiyo ilikosea kumlenga rais wa Sudan Omar El Bashir kwa mauaji ya Darfur na Uhuru Kenyatta wa Kenya kwa kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi.
Mpango huo unapendekeza kwamba mataifa ya Afrika yanafaa kuimarisha mahakama zake na kupanua uwezo wa mahakama ya Afrika kuhusu haki na haki za binaadamu.

CHALSEA,NA LIVERPOOL WALAZIMISHWA SARE, MSIMAMO WA LIGI EPL

Chelsea na Liverpool walilazimishana sare ya 1-1 na msimamo wa EPL ulivyo

Usiku wa January 31 Liverpool waliwakaribisha Chelsea katika uwanja wao wa Anfield kucheza mchezo woa wa 23 wa Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017, Liverpool waliingia katika mchezo huo staa wao Saido Mane akiwa kaanzia katika benchi.
Sadio Mane alikuwa benchi katika mchezo huo uliyomalizika kwa sare ya 1-1 kutokana na kutokuwa fiti kwa asilimia 100, hivyo alikuwa benchi akiwa kawekewa barafu lakini aliingia dakika ya 75 kuchukua nafasi ya Philippe Coutinho.

Chelsea ndio walikuwa wa kwanza kufunga goli dakika 25 kupitia kwa David Luiz aliyefunga goli hilo kwa mpira wa adhabu, ila Liverpool walisawazisha goli hilo dakika ya 58 kupitia kwa Georginio Wijnaldum na kuufanya mchezo huo umalizike kwa sare ya 1-1.
Msimamo wa EPL ulivyo kwa sasa baada ya mechi za January 31 2017

HADITHI, ALIYEMUUA MCHUMBA WANGU SEHEMU YA 24

HADITHI
 
ALIYEMUUA MCHUMBA WANGU 24
 
ILIPOISHIA
 
 “Mwanzo nilijua kuwa atanyongwa lakini baadaye mahakama ilimuachia huru kwa kumuona hakuwa na hatia”
 
“Ndiyo”
 
“Mimi sikutaka tena kurudi kwa yule mwanaume, ninahisi kuwa yeye ndiye amemuua Dokta Kweka”
 
“Unahisi tu au unayo maelezo zaidi ya kutuambia?”
 
“Ninahisi na pia nilimuona jana pale hoteli?”
 
Inspekta Temba akagutuka.
 
“Ulimuona wakati gani na alikuwa wapi?”
 
“Wakati nashuka kwenye teksi nilimuona”
 
“Ulimuona wapi?”
 
“Nilimuona akitoka kwenye mlango wa hoteli”
 
“Halafu akaenda wapi?”
 
“Sikumpatiliza tena, mimi nilijifanya kama sikumuona nikaingia hoteli. Na ndio nikaenda kumkuta Kweka ameuawa kule chumbani”
 
“Yeye alikuona?”
 
“Nina hakika kuwa aliniona”
 
“Alikusemesha chochote?”
 
“Hakunisemesha”
 
“Je aliwahi kukwambia au kumwambia marehemu kuwa atafanya kitu?’
 
“Hakuwahi kuniambia wala kumwambia marehemu kuwa atafanya kitu lakini nina shaka naye”
 
“Ungetuambia tangu jana tungelikwisha mkamata. Anaweza kuwa mtuhumiwa namba mbili. Anapatikana wapi?”
 
“Kwa sasa sijui anapatikana wapi?”
 
“Unadhani tutampataje”
 
“Hapo siwezi kujua”
 
“Una namba yake ya simu?”
 
SASA ENDELEA
 
“Ndiyo ninayo, aliwahi kunipigia”
 
“Alikupigia kukueleza nini?”
 
Alipotoka jela alinipigia kuniuliza niko wapi, ndipo nilipomjibu kuwa nimeolewa na mwanaume mwingine”
 
“Akakwambia nini?”
 
“Alisikitika tu”
 
“Sasa tupe namba yake”
 
“Simu yangu mnayo nyinyi, nilinyang’anywa tangu jana”
 
“Sawa. Tutakupatia utupe namba yake”
 
Temba alimuagiza yule polisi mwanamke akalete simu ya Vicky. Polisi huyo alikwenda kuichukua simu ya Vicky na kumpa Temba.
 
“Mpe mwenyewe” Temba alimwambia.
 
Vicky alipopewa simu aliiwasha. Baada ya sekunde chache akaisoma namba ya Simon.
 
“Sasa sikiliza, ninataka umpigie umwambie mkutane sehemu muda huu ili akija tuweze kumkamata”
 
“Nimwambie tukutane sehemu gani”
 
“Wewe unafikiri wapi anaweza kuja haraka”
 
“Kwa hapa kwenye kituo hataweza kuja”
 
“Si hapa. Sehemu nyingine yoyote hata kama ni kwenye hoteli. Tunaweza kwenda kumsubiri”
 
Vicky akampigia Simon.
 
“Utamwambia mkutane wapi?” Temba akamuuliza huku simu inaita.
 
Kabla ya Vicky kujibu simu ilikwishapokelewa.
 
“Hallo…Simon nahitaji kukuona” Vick akasema kwenye simu.
 
“Uko wapi?” Sauti ya Simon ikasikika.
 
“Niko hapa New Africa Hotel”
 
“Nisubiri hapo hapo, ninakuja”
 
“Sawa”
 
“Twende New Africa Hotel, anakuja” Vicky akamwambia Temba.
 
Simon alikuwa ndio amemaliza kuvaa akiwa kwenye chumba cha gesti aliyokuwa amepangisha chumba tangu alipoachiwa na mahakama kutokana na kesi ya mauaji iliyokuwa inamkabili.
 
Katika hisia zake aliamini kuwa Vicky hakuwa tena na pa kushika baada Dokta Kweka kuuawa. Hivyo alikuwa anamuita ili wazungumzie tofauti zao.
 
Pia Simon alijua kuwa Vicky alishaachiwa na polisi baada ya kukamatwa jana yake katika hoteli ya Suzy ambako Dokta Kweka alikuwa ameuawa
 
Hisia kwamba Vicky alitaka kurudisha uhusiano wao na ndio sababu amempigia simu, ilimfariji Simon kutokana na ukweli kwamba bado alikuwa akimpenda. Hivyo aliharakisha kuvaa akatoka na kujipakia kwenye gari alilokuwa amelikodi kwa kazi ya kumuua Dokta Kweka.
 
Aliificha bastola yake chini ya siti aliyokuwa amekaa kwani kazi yake ilikuwa imekwisha. Alikuwa akisubiri apewe pesa na James airudishe alikoikodi.
 
Akaliwasha gari hilo na kuliendesha hadi New Africa Hotel akiwa na tamaa ya kumpata Vicky. Wakati huo Vicky alikuwa ameketi kwenye ukumbi wa nje wa New Africa akiwa katika meza ya peke yake akinywa soda aliyonunuliwa na Inspekta Temba.
 
Katika meza ya jirani yake kulikuwa na makachero watatu ambao walikuwa wakizungumza.
 
Inpekta Temba mwenyewe alikuwa akisubiri kwenye gari lililokuwa jirani na hoteli hiyo maarufu.
 
Wakati Vick akiendelea kunywa soda simu yake ikaita. Alipoitazama aliona namba ya Simon. Akaipokea.
 
“Hallo Simon…vipi?”
 
“Umekaa sehemu gani?”
 
“Niko kwenye ukumbi wa nje wa hoteli, ukiingia tu utaniona”
 
“Okey, ninakuja”
 
“Kwani umeshafika”
 
“Nimeshafika”
 
“Sawa. Ukiingia tu kwenye huu ukumbi wa nje utaniona” Vicky alimwambia Simon na kukata simu.
 
Simon alikuwa amelisimamisha gari kwenye eneo la kuegesha la hoteli akafungua mlango na kushuka. Alitembea hadi kwenye mlango wa kuingilia ambapo alitupa macho kwenye ukumbi huo na kumuona Vicky aliyekuwa ameketi katika meza ya peke yake.
 
Aliingia na kutembea hadi kwenye meza hiyo akavuta kiti na kuketi.
 
“Hujambo mke wangu” Simon akamsalimia Vicky kwa tabasamu.
 
“Sijambo. Na wewe hujambo?”
 
“Mimi sijambo. Tatizo langu lilikuwa kwa upande wako kwani bado naamini wewe ni mke wangu”
 
Vicky aligeuza uso akawatazama makachero waliokuwa wameketi kwenye meza ya karibu kisha akaurudisha uso wake kwa Simon.
 
“Na mimi pia ninaamini hivyo, ndio maana nimekuita tuzungumzie hilo”
 
Ghafla Simon akajikuta amezungukwa na makachero. Kachero mmoja alimuonesha kitambulisho chake na kumwambia.
 
“Sisi ni askari wa upelelezi, tunakuhitaji kituo cha polisi!”
 
Simon akashituka na kuwatazama makachero hao.
 
“Kuna nini tena?” akawauliza.
 
“Utaelezwa, usiwe na wasiwasi” Kachero mmoja akamwambia.
 
Simon akamtazama Vicky.
 
“Wewe ndio umepanga njama hizi?’ akamuuliza.
 
Vicky akabetua mabega yake bila kusema chochote.
 
Simon akainuliwa kwenye kiti.
 
“Kuwa mstaarabu, jaribu kutekeleza kile unachoambiwa” Kachero mmoja alimwambia Simon.
 
Baada ya kumtupia jicho kali Vicky Simon aliongoza njia. Alitolewa nje ya hoteli na kupakiwa kwenye gari la polisi ambalo ndani yake alikuwemo Inspekta Temba.
 
Vicky naye alipakiwa kwenye gari hilo hilo, wakaondoka.
 
Walipofika kituo cha polisi, Vicky na Simon walitenganishwa. Vicky alirudishwa mahabusi, Simon akapelekwa ofisini kwa Inspekta Temba.
 
Simon hakuwekwa kwenye kiti, alikaa chini.
 
“Msichana uliyekuwa ukiongea naye pale hoteli mnafahamiana vizuri?” Temba akamuuliza.
 
“Ndiyo tunafahamiana vizuri”
 
“Unaweza kunieleza uhusiano wenu ulivyo?”
 
“Yule ni mke wangu”
 
“Ni mke wako hadi hivi sasa?”
 
“Tulikuwa tumetengana kidogo…”
 
“Kwa vipi?”
 
“Niliwahi kupata matatizo kidogo ya kipolisi nikashitakiwa kwa kuhisiwa kuwa nilifanya mauaji ya msichana mmoja lakini mahakama ikaona sikuwa na hatia ikaniachia huru. Sasa niliporudi uraiani Vicky akaniambia kuwa alidhani ningenyongwa hivyo ndoa yetu alishaivunja kwa Padre”
 
“Unamfahamu mtu anayeitwa Kweka?”
 
Simon alishituka alipoulizwa swali hilo. Mshituko wake ulionekana waziwazi.
 
Akajiambia akijibu kuwa hamfahamu atajiingiza katika matatizo kwani hakujua Vicky aliwaeleza nini polisi.
 
“Namfahamu” akajibu baada ya kusita kidogo.
 
“Tueleze unavyomfahamu?”
 
“Ni rafiki yangu”
 
“Ni kweli kwamba alimuoa mke wako baada ya wewe kuwekwa ndani kutokana na kesi iliyokuwa inakukabili?’
 
Simon aligundua kuwa hilo swali lilikuwa la mtego.
 
“Vicky aliwahi kunieleza kuwa aliolewa na mtu mwingine lakini nilimwambia kuwa hakupaswa kuolewa”
 
“Alikwambia aliolewa na nani?”
 
ITAENDELEA

AMKA NA MAGAZETI NA TANGAKUMEKUCHABLOG, FEBR01, 2017