Monday, February 29, 2016

UNYONYESHAJI WATOTO WALALAMIKIWA

HALI YA UNYONYESHAJI WATOTO NCHINI SIO NZURI

DSC_0599Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini,  Maniza Zaman akitoa neno la ufunguzi katika warsha iliyoandaliwa na UNICEF ili kujadili jinsi uwekezaji mkubwa zaidi katika kunyonyesha maziwa ya mama kunaweza kusaidia maendeleo kiuchumi na kuokoa maisha ya watoto nchini.(Picha zote na Rabi Hume wa Modewjiblog)
DSC_0630Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline Kaganda katika warsha iliyoandaliwa na UNICEF akielezea hali ya unyonyeshaji kwa watoto ilivyo nchini.


Imeelezwa kuwa wastani wa unyonyeshaji kwa watoto walio chini ya miezi sita nchini sio mzuri na hivyo kuwa na uwezekano wa watoto kudhoofika kwa kukosa maziwa ya mama ambayo yanakuwa na virutibisho muhimu kwa ukuaji ya mtoto.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline Kaganda katika warsha iliyoandaliwa na UNICEF ili kujadili jinsi uwekezaji mkubwa zaidi katika kunyonyesha maziwa ya mama kunaweza kusaidia maendeleo kiuchumi na kuokoa maisha ya watoto nchini.
Dkt. Kaganda amesema wastani wa unyonyeshaji kwa watoto walio chini ya miezi sita ni asilimia 42 na wastani huo ni mdogo hivyo kuashiria kuwa hali sio njema kwa watoto ambao hawapati maziwa ya mama.
Amesema kiafya inatakiwa mtoto aanze kunyonya nusu saa baada ya kuzaliwa na mtoto anyonye maziwa ya mama yake kwa kipindi kisichopungua miezi sita na baada ya hapo anaweza kuanza kuwa anachanganya na vyakula vingine kama uji na maji.
“Hali sio nzuri ukiangalia wastani wa wamama ambao wanawapa watoto wao maziwa ya kunyonya ni wachache na labda inawezekana wengi wakawa hawatambui matatizo yanayoweza kutokea kama hawatawanyonyesha watoto wao,” amesema Dkt. Kaganda.
Aidha Dkt. Kaganda amesema kazi zinachangia kina mama wengi kushindwa kuwanyonyesha watoto wao lakini wanaweza kuweka utaratibu wa kuwa wanakamua maziwa yao na kuyahifadhi sehemu nzuri ili hata kama wanapokuwa mbali na watoto wao, msimamizi anayemuangalia mtoto aweze kumpa mtoto ili kumfanya apate virutubisho muhimu kutoka kwenye maziwa ya mama yake.
Nae Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman amesema katika kusaidia Tanzania kuongeza wastani wa watoto ambao wananyonya wamekuwa wakitoa elimu kwa kina mama wanaonyonyesha pamoja na familia zao ili wajue umuhimu wa mtoto kunyonya maziwa ya mama.
Alisema watoto wengi wamekuwa wakipoteza maisha kwa matatizo ambayo yanatokana na kukosa maziwa ya mama zao na hivyo ili kuzidi kushughulikia tatizo hilo wanataraji kuanza kutoa elimu kwa watumishi wa afya katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe na wanataraji kutembelea zaidi maeneo ya vijijini kutokana maeneo hayo kuonekana kutokuwa na elimu hiyo zaidi.
“Watoto wamekuwa wakipata matatizo na kupoteza maisha na hiyo inachangiwa na kutokunyonya kwa mama … tumeshirikiana na serikali tunataraji kutoa elimu katika vijiji zaidi ya 15,000 kwenye mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya na tutafundisha pia mama na familia umuhimu wa mtoto kunyonya,” alisema Bi. Zaman.
Alisema baada ya kumalizika kwa mikoa hiyo wataendeleza utoaji wa elimu nchi nzima ili jamii ya Tanzania itambue umuhimu wa watoto kunyonya maziwa ya mama na pia kuwaomba waandishi wa habari kutumia nafasi yao katika jamii ili kuwaelimisha watanzania kuhusu tatizo hilo.
Katika makala zilizoandikwa katika jarida la habari za afya la The Lancet linaonyesha kuwa uboreshaji wa kunyonyesha maziwa ya mama kunaweza kuokoa maisha zaidi ya watoto 820,000 kila mwaka duniani na Dola za Kimarekani Bilioni 302 kila mwaka.
Imendaliwa na Rabi Hume wa Modewjiblog
DSC_0622Baadhi ya wadau wa sekta ya afya waliohudhuria katia warsha hiyo wakifatilia kwa makini ripoti zilizokuwa zikitolewa.
DSC_0654Mshauri Mwandamizi wa maswala ya watoto wadogo na unyonyeshaji kutoka Makao Makuu ya UNICEF, New York, Dr. France Begin akielezea kuhusu makala za The Lancet juu ya uwekezaji mkubwa zaidi katika kunyonyesha maziwa ya mama jinsi kunavyoweza kusaidia maendeleo ya kiuchumi na kuokoa maisha ya watoto nchini.
DSC_0655Mshauri Mwandamizi wa maswala ya watoto wadogo na unyonyeshaji kutoka Makao Makuu ya UNICEF, New York, Dr. France Begin akiwaonyesha wahudhuriaji wa warsha hiyo ripoti ya utafiti uliofanywa na jarida la The Lancet linalohusika na kuandika habari za afya.
DSC_0661Viongozi wa Taasisi mbalimbali waliofika katika warsha hiyo wakifatilia ripoti ya utafiti uliofanywa na jarida la The Lancet. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Dkt. Vicent Assey, Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu,Obey Assery Nkya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline Kaganda na Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman.
DSC_0665Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Obey Assery Nkya akielezea hatua ambazo serikali imechukua ili kupunguza idadi ya kina mama ambao hawanyonyeshi watoto.
DSC_0674Viongozi wa Taasisi mbalimbali waliofika katika warsha hiyo wakisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wadau wa sekta ya afya na waandishi wa habari. Wa kwanza kulia ni Mshauri Mwandamizi wa maswala ya watoto wadogo na unyonyeshaji kutoka Makao Makuu ya UNICEF, New York, Dr. France Begin, Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Dkt. Vicent Assey, Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu,Obey Assery Nkya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline Kaganda na Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini,  Maniza Zaman.
DSC_0696Mkuu wa kitengo cha fedha na malipo nchini kutoka Benki ya Dunia, Douglas Pearce akiuliza swali katika warsha hiyo.
DSC_0711Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini,  Maniza Zaman akitoa neno la shukrani kuashiria kumalizika kwa warsha

POLISI WAZIMA MAANDAMANO YA WANAFUNZI, SONGEA


01
Mmoja wa vijana ambaye anasadikiwa ndiye aliyekuwa kinara wa kuhamasisha maandamano ya wanafunzi wa vyuo vya Mtakatifu Joseph vya Tawi la Songea vilivyofungwa na serikali  akiwa chini ya ulinzi wa kikosi cha kuzuia fujo FFU kutokana na kufanya maandamano kinyume cha utaratibu wakitaka kwenda kumuona Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi wakati walipodhibitiwa maeneo ya shule ya Bunge posta wakielekea wizarani leo.
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ilifuta kibali kilichoanzisha vyuo vikuu viwili vishiriki vya Mtakatifu Joseph ambavyo ni Chuo Kikuu kishiriki cha Sayansi ya Kilimo na Teknolojia (SJUCAST) na Chuo Kikuu kishiriki cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (SJUIT) vilivyopo Songea.
1
Baadhi ya askari wakijiandaa kuzuia maandamano ya wanafunzi hao leo maeneo ya wizara ya Fedha na Mipango Posta  jijini Dar es salaam.
2
Wanafunzi hao wakifurumushwa na polisi mara baada ya kuktwa wakiandamana bila kibali kwenda kumuona  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi
3
Wanafunzi hao wakitoka mbio baada ya kuamriwa na polisi kuondoka eneo hilo na kutawanyika.
4
Askari polisi wakizunguka maeneo mbalimbali kuangalia hali ya usalama.
5
Polisi wakiwazuia wanafunzi hao na kuwaamuru kutawanyika kabla ya kuchukuliwa kwa hatua zaidi.
6
Mmoja wa polisi akiwaamuru wanafunzi hao kutawanyika eneo hilo.
Kwa habari, matukio bna michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

BWENI SHULE YA SEKONDARI IYUNGA MBEYA LAUNGUA MOTO


Moto ukiendelea kuteketeza Bweni la Wavulana (Mkwawa ) katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya ambapo chanzo chake kimetajwa kuwa ni hitilafu ya umeme ambapo moto huo ulizuka majira ya saa 3 asubuhi february 29 mwaka huu wakati wanafunzi wakiwa madarasani.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa mwenye suti akisaidiana na kikosi cha Zima moto kuuzima moto ulioteketeza Bweni la wavulana katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya linalolaza wanafunzi 95 February 29 mwaka huu ambapo hakuna  

Muonekano wa bweni la Wavulana katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya mara baada ya kuteketea kwa moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme majira saa3 asubuhi ambapo hakuna mwanafunzi yeyote aliyejeruhiwa kutokana na ajali hiyo ya moto. .
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa akizungumza na Walimu pamoja na wanafunzi (hawapo pichani )katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya mara ya baada ya kukumbwa na tukio la kuungua kwa moto kwa mabweni ya wavulana ya (Mkwawa) February 29 mwaka huu.

Kamati ya ulinzi na Usalama wilaya ya  Mbeya na baadhi ya viongozi wakitizama athari zilizotokea mara baada ya mabweni ya wavulana katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya kuungua moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme February 29 mwaka huu .

Afisa elimu Mkoa wa Mbeya Charles Mwakalila akizungumzia athari zilizojitokeza mara baada ya mabweni ya wavulana katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya ambayo yaliteketea kutokana na hitilafu ya umeme majira ya saa3 asubuhi wakati wanafunzi wakiwa madarasani .
Baadhi ya wanafunzi waliofanikiwa kuokoa vifaa vyao kwa masaada wa watu wa zima moto wakiwa nje wakisubiri utaratibu mara baada ya bweni lao kuteketea kwa moto.

Baadhi ya wanafunzi wakiwa  nje kusbiri utaratibu mara baada  waliofanikiwa kuokoa baada ya bweni lao kutektea kwa moto  

MAKAMO WA RAIS AFUNGUA KONGAMANO LA PILI LA UNESCO

su1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
su2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO kanda ya Afrika Firmin Matoko katikati na mwakilishi Mkaazi wa UNESCO Tanzania Zulmira Rodrigues kabla ya kufungua rasmi Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
su3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Balozi wa Korea kusini Nchini Geum-Young Song kabla ya kufungua rasmi Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
su4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Cheti kiongozi wa Spice kutoka Zanzibar ambae ni mmoja kati ya washiriki Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
su5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Cheti Judith Mwambela mmoja kati ya washiriki Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
su6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.

IBRAHIM AJIB MWEZAJI BORA WA MWEZI

Katika kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri, Klabu ya Simba ilianzisha Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi wa Septemba 2015.
Mshindi wa mwezi wa Disemba, 2015 ni Ibrahim Ajib ambapo amepata kura nyingi zaidi zilizopigwa na mashabiki na wapenzi wa Simba na soka wa Tanzania kwa ujumla kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya Simba News.Akikabidhiwa tunzo pamoja na pesa taslim Tsh 500,000/= na Mkuu wa kitengo cha biashara na mipango kutoka EAG Group ambao ni washauri na watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba, Richard Mvula, Ibrahim Ajib alisema “kila siku nimekuwa nikiendelea kujitahidi kufanya vizuri zaidi ili nami ifike siku niweze kukabidhiwa tunzo hii, kwakweli ni heshima kubwa sana kwangu, napenda kuchukua fursa hii kuupongeza uongozi mzima wa Simba kwa kuanzisha utaratibu huu, pia napenda kuwashukuru mahsbiki wangu ambao wamenipigia kura, wachezaji wenzangu kwenye kikosi cha Simba ambao kila siku tumekuwa tukishirikiana katika kazi yetu hii ya mpira, napenda kushukuru kwa sapoti kubwa ninayoipaa kutoka kwa familia yangu na mwisho napenda kumshukuru Allah kwa kuendelea kunibariki na neema zake kila siku”
Akimakabidhi tunzo hiyo Mkuu wa kitengo cha biashara na mipango kutoka EAG Group Richard Mvula alisema “kama mtakumbuka utaratibu huu ulianzishwa kwa ajili ya kuwapa motisha wachezaji wetu na sasa umekuwa ni utamaduni wetu katika kuwapongeza na kuonesha kuthamini jitihada zinazofanywa na wachezaji wetu katika kuutafuta ushindi wa msimu huu”
Napenda kuwakumbusha wanachama na wapenzi wa Simba kuendelea kuwapa sapoti wachezaji wetu kwani kwa sapoti yao ndio mafanikio ya timu yetu yanapopatikana, aliongeza Mkuu wa kitengo cha biashara na mipango kutoka EAG Group Richard Mvula
Akizungumza jinsi tunzo ya mchezaji bora itakavyoendeshwa, Mkurugenzi Mkuu wa EAG Group, Imani Kajula alisema “Wanachama na wapenzi wa Simba na wapenda michezo ndio watakao kuwa wanachagua mchezaji bora wa mwezi kwa kutuma jina la mchezaji wanayempendekeza kwenda kwenye namba 15460, Ni wale tu ambao wamejiunga na Simba News kupitia mtandao wa Voda na Tigo wataweza kupiga kura kuchagua mchezaji bora wa mwezi wa Simba”.
Tukumbuke kuwa unaweza kumchagua mchezaji bora wa mwezi ukiwa umejiunganisha na huduma ya Simba News kwa kutuma jina la mchezaji kwenda namba 15460. Zoezi la kumchagua mchezaji bora wa mwezi wa Januari, 2016 litaanza February 29 2016. Piga kura mara nyingi zaidi kuweza kumpata mchezaji wako bora wa Mwezi Januari, 2016.
Simba News ni huduma iliyoanzishwa na Simba ili kuwapa wapenzi wa Simba habari mbalimbali za Simba popote pale walipo ikiwemo matokeo, majina ya wachezaji wanaocheza mechi, usajili na habari nyingine za klabu ya Simba. Kujiunga na Simba News tu

Sunday, February 28, 2016

MAJI MAREFU ASAIDIA VILABU VYA MICHEZO KOROGWE VIFAA MILIONI 5



Tangakumekuchablog
Korogwe, MBUNGE wa jimbo la Korogwe Vijijini, Stivin Ngonyani, maarufu kama Profesa Majimarefu, ametoa jezi seti tano, mipira mitatu vyenye thamani zaidi ya shilingi laki 5 kwa timu ya mpira ya vijana wa Makuyuni Wilayani Korogwe lengo likiwa ni kukuza vipaji.
Vifaa hivyo kwa mujibu wa Mbunge huyo vimekuja kufuatia maombi ya vijana wa Makuyuni kumtaka kusaidia ili kuweza kuimarisha timu yao na kuingia ligi ngazi ya Wilaya hadi Mkoa.
Alisema msaada huo hautoishia hapo lakini atapenda kuona timu hiyo inafanya vizuri ligi ngazi ya Tarafa na kuahidi kuisaidia kwa hali na mali hivyo kuwataka kuonyesha moyo na mapenzi na timu.
“Leo nawapeni jezi na mipira kumaliza kilio chenu kwani nakumbuka barua yenu muloniandikia nikiwa bungeni na mukaiacha kwa katibu wangu pale ofisini, niwaahidi kuwa mimi kama mbunge wenu nitakuwa nanyi bega kwa bega” alisema Majimarefu na kuongeza
“Nitahakikisha timu yenu inaingia mashindano ya Wilaya hadi mkoa na mimi kuwa mlezi wenu na musisite kunieleza kwa lolote” alisema
Kwa upande wake Kocha wa timu hiyo, Mbaraka Kiondo, alimshukuru mbunge huyo na kusema kuwa msaada wake huo aloutoa utatumika kama ilivyo na kumuahidi kuwa hawatamuangusha katika mashindano ya ligi.
Alisema awali walikuwa wanatumia mipra mmoja huku wakiwa hawana jezi na badala yake kila mchezaji alikuwa anatumia fulana yake jambo ambalo lilikuwa kero wakati wa uchezaji na kutoelewana.
“Mheshimiwa Mbunge hatuna la kukulipa na hatuna la kusema kwani hatujui tuanze wapi ila nimalize kwa kusema asante sana na Mungu ndie atakakulipa na kukubariki” alisema Kiondo
Aliwataka wachezaji wake kuzingatia muda wa kufanya mazoezi baada ya kupata vifaa hivyo na kuwataka kupiga kambi ili kushikilia usukani wa ligi hiyo ngazi ya Tarafa na msimu wa ligi kuingia ngazi ya Wilaya.
                                                Mwisho

PICHA 5 UJIO WA MAKAMO WA RAIS TANGA

MAKAMO WA RAIS SAMIA SULULU HASSAN ALIPOWASILI TANGA JANA
LU1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Mwantum Mahiza alipowasili uwanja wa ndege wa Tanga kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku Mbili Mkoani humo .LU2
Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa Tanga akimvisha Skafu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipowasili uwanja wa ndege wa Tanga kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani hum .jana.
LU3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Vijana wa Chipkizi wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa Tanga alipowasili uwanja wa ndege wa Tanga kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani humo jana.
LU4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Tanga baada ya kupokea Taarifa ya Mkoa huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Mwantumu Mahiza.
LU5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Mwantumu Mahiza jana Februari 28, 2016. Makamu wa Rais yupo Mkoani Tanga kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili.

AMKA NA MAGAZETI NA CANDLE EDUCATION CENTRE TANGA

Magazeti yameletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu cha Candle Education Centre Tanga, kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza kielimu. Candle wanaendelea kusaili wanafunzi wapya wanaorisiti na wanaojiendeleza kielimu. Candle wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746