Thursday, March 31, 2016

AMKA NA MAGAZETI NA MKOMBOZI SANITARIUM CLINIC TANGA

Magazeti yanaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Tiba Asilia cha Mkombozi Sanitarium Clinic Tanga, Mkombozi ni mabingwa wa kutibu magonjwa sugu na kutoa ushauri wa uhakika. Mkombozi wako na vifaa vya kisasa vya kupima magonjwa na mwili mzima. Wapo Tanga barabara ya 12 Ngamiani Tanga mkabala na Ofisi za Kampuni ya Mabasi ya Freys yaendayo Moshi, Arusha hadi Singida. Simu 0654 361333


LICHA JOTO NA JUA KALI, TMA YASEMA MVUA IPO PALE PALE


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imesema licha ya kuongezeka kwa joto katika maeneo mengi ya nchi hakutaathiri utabiri wa msimu wa masika uliotolewa mwezi Machi mwaka huu.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa baraza la wafanyakazi wa TMA, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi amesema maeneo yaliyotolewe taarifa za mvua za wastani, Juu ya wastani au chini ya wastani yataendelea kuwa hivyo japo uwezekano wa kuwepo jua upo kutokana na ongezeko la joto.

Dkt. Kijazi ameongeza kuwa Mamlaka hiyo itaendelea kutoa taarifa za hali ya hewa zenye uhakika na kusema utabiri wa msimu wa vuli mwaka jana,TMA ilitabiri kwa usahihi uliofikia kiwango cha asilimia 85.8.

Mkurugenzi huyo wa Mamlaka ya Hali ya Hewa ametumia fursa hiyo kuishukuru serikali kutambua umuhimu wa TMA na kuboresha mashine za kufanyia utabiri na kuajiri wataalamu ambao kwa pamoja wanashirikiana kutumia mitambo ya kisasa kuufamisha umma.

Aidha, Dkt. Kijazi ameongeza kuwa wako katika mkakati wa kuongeza vitu vya hali ya hewa nchi nzima ambapo wataanza na Dar es Salaam ambako kuna vituo viwili tu huku mahitajia yakiwa ni vituo zaidi ya 10

WABUNGE WATATU WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

 
Pichani kutoka kushoto ni Mbunge wa Mwibala,Mh.Kangi Lugola,Mbunge wa Mvomero Mh.Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa jimbo la Lupa Mh.Victor Mwambalaswa
 Wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wamefikishwa mahakama ya Kisutu hivi punde kwa tuhuma za rushwa,Wabunge hao kama waoenekanavyo pichani ni Mbunge wa Mwibala,Mh.Kangi Lugola,Mbunge wa Mvomero Mh.Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa jimbo la Lupa Mh.Victor Mwambalaswa

REA WAJIBU MSAADA WA MCC

Majibu ya REA baada ya MCC kukatisha msaada wa TRILIONI 1 kwa Tanzania

Siku kadhaa zilizopita bodi ya Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC) ilisitisha msaada wa awamu ya pili wa kutoa zaidi Trilioni 1.4 kwa Tanzania kutokana na kile lilichosema kuwa ni malalamiko ya uchaguzi wa Zanzibar na sheria mpya ya makosa ya mitandao Tanzania ikisema Tanzania iliendelea na uchaguzi wa marudio Zanzibar ambao haukushirikisha wote na haikujali malalamiko ya Marekani na jamii ya kimataifa.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijini ‘REALutengano Mwakahesya amezisikia taarifa kwamba moja ya miradi ambayo itakosa pesa hizo za msaada ni REA na sasa anatamka yafuatayo >>> ‘REA haijawahi kupata fedha za MCC, REA imekuwa ikiendeshwa kwa fedha za serikali ambapo imekuwa ikichangia kwenye mfuko huo kwa karibu 90% ya fedha zote tunazofanyia kazi na  hizo 10% ndio zinatoka kwa wahisani’
>>>’Shughuli za REA haziwezi kusimama naserikali inatarajiwa kutoa fedha nyingi kwenye bajeti hii kwa hiyo kasi itakuwa kubwa zaidi’ – Mwakahesya.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekcuhablog

BAADA YA MCC NA HAWA WENGINE WAMETANGAZA

Baada ya MCC, hawa ni wengine waliotangaza kusitisha misaada kwa Tanzania kisa uchaguzi wa Znz

March 29 2016 bodi ya shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC) ilisitisha msaada wa awamu ya pili wa kutoa zaidi Trilioni 1.4 kwa Tanzania kutokana na kile lilichosema kuwa ni kufanyika kwa uchaguzi Zanzibar licha ya malalamiko ya uchaguzi huo lakini pia sheria mpya ya makosa ya mitandao Tanzania.
Sasa leo March 31 2016 shirika la utangazaji la Uingereza BBC kupitia bbcswahili.com limeandika ripoti ifuatayo >>>kundi la watoa misaada 10 kutoka nchi za magharibi limetangaza kusitisha ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania, hii inafuatia uamuzi wa shirika la utoaji misaada la serikali ya Marekani kuondoa msaada kutokana na uchaguzi wa Zanzibar ulivyoendeshwa
Karibu theluthi moja ya bajeti ya Tanzania ilitegemea msaada mwaka uliopita, kwa hivyo hatua hizo za hivi punde ni pigo kwa mipango ya maendeleo ya serikali mpya‘ – BBC SWAHILI.
Kwa habari matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

Wednesday, March 30, 2016

AMKA NA MAGAZETI NA MKOMBOZI SANITARIUM CLINIC TANGA

Magazeti yanaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Tiba Asilia Cha Mkombozi Sanitarium Clinic Tanga, Mkombozi ni mabingwa wa kutibu magonjwa na hutoa ushauri wa uhakika. M,kombozi pia wako na vifaa vya kisasa vya kupimia mwili mzima. Wapo Tanga barabara ya 12 Ngamiani Tanga. simu 0654 361333























ABIRIA WA NDEGE APIGA PICHA MTU ANAEDAIWA KUWA MTEKAJI

Selfie ya Egyptair

Mtu aliyepiga picha na anaedaiwa kuwa mtekaji  wa ndege ya kampuni ya EgyptAir aliyevalia mkanda bandia wa mlipuaji wa kujitolea muhanga amesema kuwa alitaka kuuona vizuri ukanda huo.

Picha hiyo ya Ben Innes ,akitabasamu karibu na mtuhumiwa huyo katika ndege hiyo ya EgyptAir imesambazwa katika mitandao ya kijamii.

  Innes anayeishi Aberdeen pia aliliambia gazeti la Jumapili la Sun kwamba alitaka kuonyesha tabasamu mbele ya shida.

Alisema kuwa picha hiyo iliochukuliwa na mfanyikazi mmoja wa ndege hiyo ilikuwa ''selfie bora zaidi''.

Ndege hiyo ilikuwa ikibeba abiria 55,ikiwemo raia 26 wa kigeni waliotoka Alexandria kueleka Cairo.

Wengi wa wale waliokuwa wameabiri ndege hiyo waliwachiliwa baada ya ndege hiyo kutua katika uwanja wa ndege wa Lanarca lakini mtekaji huyo aliwazuia watu saba kabla ya kisa hicho kukamilika kwa amani.

UMMY MWALIMU AKEMEA WANAOJICHUKULIA SHERIA MIKONONO

Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula kufuatia tukio la mmoja wa Madaktari kupigwa na mwananchi. Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi.
………………………………………
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akemea tabia inayotaka kujengeka ndani ya jamii ya kuwashambulia watumishi wa afya hasa Madaktari na Wauguzi.
Amevitaka vyombo ya dola kuwachukulia hatua wananchi wanaojihusisha na vitendo hivi ambavyo vitaathiri utoaji wa huduma za afya kwa wananchi hasa wa kipato cha chini.
Mhe Ummy amewasili Mtwara jana akiongozana na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi ambapo alifanya mazungumzo na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.
Amewaonya wananchi kutoitumia vibaya dhamira ya dhati ya Rais Dkt. John Magufuli na Serikali ya kuimarisha nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma kwa kujichukulia sheria mkononi.
Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na mmoja wa wazee aliyefika kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula mara baada kuwasili hospitalini hapo kuzungumza na wafanyakazi.
Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na baadhi ya wananchi waliokusanyika nje ya hospitali kufuatia tukio la mwananchi kumpiga daktari.
Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akisikiliza maoni kutoka kwa mmoja wa wananchi aliyefika hospitalini hapo.
Ummy Mwalimu
Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula kufuatia tukio la mmoja wa Madaktari kupigwa na mwananchi. Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi.
Ummy Mwalimu
Baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula wakimsikiliza Mh. Ummy Mwalimu (hayupo pichani).
Ummy Mwalimu
Mh. Ummy Mwalimu akisikiliza hoja mbalimbali za madktari wa hospitali hiyo.
Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akikagua neti ya mmoja wa mama aliyejifungua katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.
Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akifurahi kumuona mmoja wa watoto aliyezaliwa katika wodi ya wazazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula mara baada ya kufanya mazungumzo na watumishi wa hospitali hiyo.
IMG-20160329-WA0058
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akifurahi jambo na mmoja wa kina mama alipotembelea wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.
Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungukia baadhi ya maeneo ya hospitali hiyo.