Wednesday, November 30, 2016

AMKA NA MAGAZETI NA FREYS COACH, TANGA HADI SINGIDA KILA SIKU 0622 292990



TANZANIA
UK

NAIBU WAZIRI SULEIMAN JAFO, ALIPOKUWA KOROGWE UKAGUZI WA MIRADUI YA MAENDELEO

 Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Robarts Gabriel akitoa maelezo ya jengo la vyumba vya madarasa shule ya Sekondari ya Mnyuzi Wilayani humo wakaati wa ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo,(kushoto mwenye suti ya blue) wakati w aziara yake mwishoni mwa wiki .
Ziara hiyo ikiongozwa na Wabunge wa Korogwe mji, Merry Chatanda na Profesa MajiMarefu wa Korogwe Vijijini.






Tuesday, November 29, 2016

TIMU 8 ZILIZOPATA AJALI MBAYA YA NDEGE

Ajali nane za ndege zilizokumba timu za mpira

Ndege iliyokuwa imebeba timu ya Manchester United ilianguka mjini MunichMabaki ya ndege yalipatikana kwenye mto uliokuwa karibuNdege iliyokuwa imebeba timu ya soka ya Brazil imeanguka wakati ilipokuwa ikikaribia mji wa Medellin nchini Colombia na kuwaua karibu watu wote 81 waliokuwa ndani yake.
Ndege hiyo ilikuwa na wachezaji wa timu ya Chapecoense, waliokuwa safarini kwenda kucheza fainali ya mashindano ya kimataifa ya vilabu vya Amerika ya Kusini.
Chapecoense ndicho klabu ya hivi punde kukumbwa na mkasa kama huo.
Mikasa mingine inayokumbukwa ni:
1949 Il Grande Torino
Mwezi Mei mwaka 1949 ndege iliyokuwa imeibeba timu ya Torino ilianguka eneo la milima karibu na Turin na kuwaua watu 31.
Wakati huo timu ya "Il Grande Torino" ilikuwa klabu kubwa nchini Italia baada ya kupata ushindi mara tano.
Kablu hiyo hikuweza kujikwamua kufuatia ajali hiyo ambayo iliangamiza karibu kikosi chote.
1958 Ajali ya Munich
Ndege iliyokuwa imebeba timu cha Manchester United ambayo ilikuwa wakati huo ilijulikana kama "the Busby Babes" ilianguka ilipokuwa ikipaa wakati timu ilikuwa ikirudi kutoka mechi ya bara ulaya dhidi ya klabu ya Red Star Belgrade.
Wachezaji 8 wa United na watu wengine 15 waliaga dunia.
1961 timu ya kuteleza kwenye theluji ya Marekani
Wanachama wote 18 wa timu ya kuteleza kwenye theluji ya Marekani walikuwa miongoni mwa watu 73 waliokufa baada ya ndege yao kuanguka karibu na uwanja wa ndege wa Brussels wakati ilipokuw ikitua.
Timu hiyo ilikuwa safarini kwenda mji wa Prague, huko Czechoslovakia, kushiri mashindano na dunia ambayo wakati huo yalifutwa.
1972 Alive
Siku ya Ijumaa tarehe 13 Oktoba mwaka 1972, ndege iliyokuwa imebeba timu ya Old Christians ambayo na timu ya raga ya Uruguay, ilitoweka ilipokuwa safarini kutoka mji wa Montevideo kwenda Santiago nchini Chile.
Miezi miwili baadaye jeshi la wanahewa wa Chile waliwapata manusura 14 kutoka kwa ajali hiyo. Wengine wawili walikuw wametembea kwa siku 10 kabla ya kukutana na wafugaji katika milima ya Andean.
Mkasa huo ulindikwa kwenye vitabu na baadaye kutengenezwa vilamu ,ALIVE, iliyoeleza jinsi manusura walikula nyama ya binadamu kuepuka kufa njaa.
1979 FC Pakhtakor Tashkent
Mwezi Agosti mwaka 1979 wanachama 17 wa timu ya soka la Pakhtakor Tashkent waliuawa wakati ndege yao iligongana na ndege ngingine katika anga ya Ukrain.
Watu wote 178 waliokuwa ndani ya ndege zote mbili waliangamia.
Timu zingine kwenye muungano ya usovieti zilichangia wachezaji wa klabu hiyo kukiwezesha kumaliza msimu.
1987 Alianza Lima
Timu ya soka ya Alianza Lima, moja ya vilabu vyenye mafanikio makubwa zaidi ilikuwa ikirejea mjini Lima wakati ndege yao ilianguka kwenda baharini dakika chache kabla ya kutua
Timu yote wa Alianza Lima iliyokuwa miongoni mwa watu 43 iliangamia. Ni rubani tu wa ndege hiyo aliyeweza kunusurika.
1993 Timu ya Soka ya Zambia
Wanachama 18 wa timu ya taifa ya Zambia waliuawa wakati ndege ya jeshi la Zambia ilianguka karibu na Gabon tarehe 28 mwezi Aprili mwaka 1993, walikuwa wikielekea kucheza mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia nchini Senegal.
Ripoti rasmi kuhusu mkasa huo miaka kumi baadaye ilitaja matatizo ya kimitambo kwenye injini moja ya ndege hiyo.
2011 timu ya magongo ya Lokomotiv Yaroslavl
Timu hiyo ambayo ilikuwa ndio mabingwa mara tatu nchini Urusi ya Lokomotiv Yaroslavl, iliangamia kwenye ajali ya ndege mwezi Septemba mwaka 2011.
Ndege hiyo ilikuwa ikielekea nchini Belarus kwa mechi ya kwanza ya msimu wakati ilianguka na kushika moto.
Wachezaji 36 na maafisa waliaga dunia pamoja na wahudumu 7. Mchezaji mwingine aliaga dunia akiwa hospitalini.

YAMENIKUTA SALMA MIE SEHEMU YA 34

HADITHI
 
YAMENIKUTA SALMA MIE
 
ILIPOISHIA
 
Nilikaa pale hospitali kwa wiki mbili. Sikumuona Sikuzani wala Mariam aliyekuja kunitazama hata siku moja, wakati nilikuwa na hakika kuwa walipata habari kuwa niligongwa na gari na niko Muhimbili.
 
Baada ya wiki hizo mbili, kidonda kilichokuwa mguuni kwangu kilikuwa kimepona ingawa hakikuwa kimekauka kabisa. Kadhalika sehemu za mwili wangu nilizoumia nazo zilikuwa zimepona. Hapo hospitali nilipewa magongo mawili ya msaada ili niweze kuendea msalani.
 
Daktari aliyekuwa katika wodi yangu alinipa ruhusa lakini aliniambia niende nikatafute msaada wa pesa sehemu yeyote ile ili niweze kupelekwa India kufanyiwa operesheni ya jicho kabla ya wiki nne kumalizika.
 
Nilitoka hapo hospitali nikiwa sijui pa kwenda.Vile nilivyofikishwa pale hospitali ndivyo nilivyotoka, sikuwa na kitu chochote zaidi ya mfuko wa plastiki na shilingi elfu tano nilizosaidiwa na daktari kwa ajili ya usafiri.
 
SASA ENDELEA
 
Sikuwa na pakwenda zaidi ya kupanda daladala na kurudi kule Sinza kwa kina Mariam.
 
Nilipofika Sinza, wakazi wa nyumba niliyokuwa ninaishi waliponiona walipatwa na mshangao. Kwanza hawakunitambua mpaka nilipojitambulisha.
 
Nikaambiwa kuwa Mariam na Sikuzan hawakuwepo.
 
"Wamekwenda wapi?" nikawauliza
 
"Wamefungwa" dada mmoja aliyekuwa shoga mkubwa wa kina Mariam akaniambia. Nikashituka.
 
"Wamefungwa kwa kosa gani"?nikamuuliza.
 
"Walikamatwa usiku.Wakashitakiwa kwa kosa la kuendesha biashara ya umalaya"
 
"Ilikuwa lini?"
 
"Siku ya pili baada ya siku ile uliyopata ajali"
 
"Wamefungwa kwa miaka mingapi?"
 
"Si miaka, ni miezi sita tu kila mmoja"
 
Hapo nikajua sababu ya kutomuona Mariam wala Sikuzan kuja kunitembelea hospitali nilikokuwa nimelazwa.
 
"Siku waliyohukumiwa nilikwenda mahakamani.Mariam alinipa funguo ya chumba chao akaniambia kama utatokea nikupe"
 
"Shida yangu ilikuwa ni kutoa vitu vyangu ili niviuze nipate nauli ya kunirudisha Tanga. Siwezi tena kuishi Dar" nikamwaambia
 
"Sasa ngoja nikupe huo ufunguo"
 
Dada huyo aliyekuwa akiitwa Agnes aliingia chumbani mwake akanitolea ufunguo na kunipa.Nikafungua ule mlango na kuingia mle chumbani. Nikafungua dirisha ili niweze kuona vizuri. Agnes naye akaingia.
 
Nikaanza kukusanya vitu vyangu. Kulikuwa na mabegi yangu mawili ya nguo.Nikayafungua na kutoa nguo zote zilizokuwemo.Nilichagua nguo chache tu, nikazirudisha kwenye begi moja. Nguo zingine nikamwaambia Agnes ninaziuza.
 
"Nitafutie wateja, nataka nipate nauli"
 
"Nauli ya shilingi ngapi?"
 
"Nataka nipate kama shilingi laki moja hivi kwani huko niendako sijui kukoje. Hivi vyombo vingine pia ninaviuza,sitavichukua"
 
Agnes akachukua baadhi ya vyombo na kuchagua nguo alizozipenda, akaniuliza anipe kiasi gani.
 
"Nipe utakazo nipa dadaangu"
 
"Elfu themanini, sijui kama utaridhika nazo kwa hivyo vitu nilivyochukua"
 
"Nipe tu dadaangu"
 
Agnes aliponipa pesa hizo, nilimuambia akanitafutie wateja wengine wa kununua vile vitu vilivyobaki.
 
"Labda nichukue hizi nguo niende nazo hukohuko.Sasa niambie bei yako"
 
"Bei yoyote dadaangu,elfu kumi, kumi na tano, wewe uza tu"
 
Agnes akachukua zile nguo na kutoka nazo. Nikabaki mle chumbani kwa karibu masaa mawili. Aliporudi alikuwa hana nguo hata moja. Akanipa shilingi laki moja.
 
"Nimekwenda kuziuza kwa majirani" akaniambia.
 
"Nakushukuru dadaangu. Hivi vyombo vyangu vilivyobaki nitawaachia mashoga zangu kina Mariam.Wakitoka jela watakuja kuvikuta. Utawaambia nimetoka hospitali na nimerudi Tanga”
 
"Sawa mdogo wangu. Nitakuja kuwaambia"
 
"Tatizo langu kubwa ni huu mguu wangu uliokatwa na haya macho yangu. Hili jicho langu moja limeharibika kabisa. Hili jingine nimeambiwa limeingia kipande cha kioo huku pembeni, nalo linaweza kuharibika kama sitapelekwa India.Na siku nilizoambiwa zimebaki wiki mbili tu.Sijui nitafanya nini?"
 
"Ukifika Tanga utawaeleza ndugu zako. Natumaini watakuchangia"
Sikumjibu kitu. Niliguna tu kisha nikanyanyuka.
 
"Dadaangu ndiyo natoka naenda Ubungo. Gari lolote nitakalo lipata ndilo nitakaloondoka nalo"
 
Agnes alinishindikiza hadi kwenye kituo cha daladala.Tukaagana hapo, nikapanda daladala na yeye akarudi.
 
Nilipofika Ubungo moyo wangu ulikuwa mzito sana kurudi Tanga. Kwa muda nikawa nimesimama nikitafakari.Nilihisi kurudi Tanga ilikuwa sawa na kujimaliza kabisa.Tatizo langu sasa lilikuwa kupata msaada wa kuokoa jicho langu. Nilikuwa na uhakika kwamba huko Tanga nisingepata ndugu yeyote wa kunisaidia pesa hizo hasa kutokana na visa nilivyovifanya.
 
Kama kuna mahali pa kupata msaada, nilijiambia, ni hapa hapa Dar es salaam.
 
Nikajiuliza sasa niende wapi kutafuta msaada huo? Niende Ikulu…niende wizara ya afya…au niende kwa mbunge?
 
Wakati naendelea kutafakari nikamuona Mzee mmoja mwenye asili ya Kiasia amesimama karibu yangu akizungumza na simu. Alipomaliza kuzungumza nikamfuata.
 
“Shikamoo Baba” nilimwamkia.
 
“Marahaba” akanijibu.
 
Nilimuhisi alikuwa akinidhania kuwa nilikuwa ombaomba  niliyetaka kumuomba msaada.
 
Nikamuona akijipekua mifukoni.
 
“Sihitaji pesa baba, kuna maneno nataka kukwambia. Naomba unisikilize.” nikamwambia.
 
Mzee huyo akanishangaa kidogo.
 
 “Unasemaje?” akaniuliza.
 
“Baba kama unavyoniona nina matatizo lakini tatizo kubwa ninalotaka kukueleza ni kuhusu jicho langu hili” nikamwambia na kumuonyesha lile jicho langu linaloona.
 
“Mimi nilipata ajali ya gari hivi karibuni iliyosababisha mguu wangu mmoja ukatwe na jicho langu moja kuharibika.
 
“Sasa hili jicho langu ambalo linaona lilingia kipande cha kioo kwa pembeni. Madaktari wa Muhimbili wameniambia ni chembe ndogo sana ya kioo. Sasa tatizo liliopo ni kwamba natakiwa kupelekwa India kufanyiwa upasuaji kabla ya wiki mbili. Madakdari wameniambia baada ya wiki mbili kumalizika jicho hili nalo litaharibika kabisa na nitakuwa kipofu”
 
Yule mzeebaada ya kunisikiliza kwa makini aliniuliza.
 
“Sasa ulikuwa unahitaji nini?”
 
“Nilikuwa nahitaji msaada wa kupelekwa India kutibiwa” nikamjibu haraka .
 
“Kwani wewe huna ndugu?”
 
“Ninao lakini ndugu zangu ni maskini, hawawezi kupata pesa zinazohitajika.”
 
“Zinahitajika kiasi gani.”
 
“Nimeambiwa zinahitajika shilingi milioni nane”
 
“Bado si tatizo kwa sababu zipo taasisi zinazosaidia watu kama nyinyi. Kuna taasisi moja ya misheni ilianzishwa mwaka jana. Ishapeleka watu wengi nchini India kutibiwa maradhi yaliyoshindikana hapa kwetu.”
 
ITAENDELEA

TIMU YA SOKA YAPATA AJALI WENGI WAHOFIWA KUFA

Maamuzi ya timu iliyokuwa icheze na Chapecoense fainali kabla ya kupata ajali


Klabu ya Atletico Nacional ya Colombia ambapo ilikuwa icheze mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Sudamericana kesho Jumatano ya November 30 2016 Colombia dhidi ya klabu ya Chapecoense ya Brazil imetangaza maamuzi tofauti.
1480397623_017517_1480398498_noticia_normal
Atletico Nacional ambapo ndio wangekuwa wenyeji wa mchezo huo wa fainali ya kwanza, wameomba shirikisho la soka la America Kusini (CONMEBOL) kuwa kutoa Kombe hilo kwa timu ya Chapecoense ya Brazil kama sehemu ya heshima.
a-nacional-sampiyon-chapecoense-ilan-edilsin-8079098
Msafara wa watu 72 wa timu ya Chapecoense ya Brazil wamepata ajali ya ndege asubuhi ya leo  wakiwa Colombia, ndege hiyo imepata ajali ikiwa na jumla ya watu 81 kati ya hao watu 9 ni wafanyakazi wa ndege, katika list ya watu 81 ni watu watano tu ndio wamefanikiwa kutoka salama.

UKAGUZI WA SOKO LA MBOGAMBOGA NA MATUNDA LUKOZI, LUSHOTO

 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo, akikagua ujenzi wa soko la mbogamboga na matunda Lukozi Wilayani Lushoto Mkoani Tanga wakati wa ziara yake mwishoni mwa wiki, Jaffo alikuwa Tanga kuangalia miradi ya maendeleo ya wananchi  kwa kutembelea Wilaya zote za Mkoa huo.