Monday, October 31, 2016

KAMA ULIKOSA PAMBANO LA ARFICAN SPORTS NA FRIENDS RANGERS , NIMEKUSOGEZEA PICHA HAPA



Kiungo wa African Sports ya Tanga, Idd Hassan, akiumiliki mpira katikati ya wachezaji wa Friends Rangers ya Magomeni Dar es Salaam wakati w amwezo ligi daraja la kwanza uliofanyika uwanja wa Mkwakwani juzi, Timu hizo zilitoka suluhu 0, 0.


  Refarii wa mchezo wa African Sports ya Tanga na Friends Rangers ya Magomeni Dar es Salaam, Mohammed Theophil, akimuonyesha mshambuliaji wa African Sports eneo ambalo alipaswa kuweka mpira na kupiga langoni mwa Friends Rangers ya Magomeni Dar es Salaam, wakati wa mchezo ligi daraja la kwanza uliofanyika Mkwakwani juzi, timu hizo zilitoka suhulu 0, 0.

Wachezaji wa Friends Rangers ya Magomeni Dar es Salaam, wakigombea mpira na wachezaji wa African Sports ya Tanga wakati wamchezo ligi daraja la kwanza uliofanyika uwanja wa Mkwakwani juzi. Timu hizo zilitoka suluhu , 0 ,0.

BONDIA ALIEUWAWA AACHA GUMZO KILA KONA

Bondia Mashali ameuawa siku chache baada ya kubadili dini, jina lake la kiislamu limetajwa

Wapenda ngumi nchini wako katika majonzi makubwa baada ya kifo cha bondia nyota, Thomas Mashali.
Tokeo la picha la thomas mashali
Mashali au Muhammad kama ambavyo anatajwa baada ya kusilimu bondia huyo inaelezwa kutoka vyanzo vya habari  kuuwawa katika kifo cha kutatanisha.
Taarifa zimesema kuwa Mohammad alipigiwa kelele za mwizi na kuelezwa kuwa kupigwa hadi mauti kumfika.
Mashali ameuwawa katika moja ya viunga vya jiji la Dar es Salaam, ikielezwa aliokotwa eneo la Kimara ingawa kuna wengine wanasema ameokotwa eneo la Tabata.
Kitu ambacho Watanzania wengi hawakukijua ni kwamba, wakati mauti yanamkuta, Mashali alikuwa amebadili dini siku chache, kutokuwa kuwa Mkristo hadi Mwislamu, akaamua kuacha kutumia jina la Thomas na alikuwa akitumia jina la Mohammed.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa (PST), Anthony Rutta amesema, Mashali kweli alibadili dini.
"Kweli alikuwa anaitwa Mohammed, hili alitueleza mwenyewe kwamba aliamua mwenye kwa hiari yake kuwa mwislamu," alisema Rutta.

HADITHI, YAMENIKUTA SALMA MIE SEHEMU YA 25

HADITHI
 
YAMENIKUTA SALAMA  MIE (25)
 
ILIPOISHIA
 
“Usiniapize mwana wa mwenzio. Binaadamu haishi kuumbwa maana yake nini?” nikamuuliza kwa ukali.
 
Ibrahim hakujibu kitu. Nikaendelea kumwaambia.
 
“Sasa kama mimi nimeshakuwa Malaya, nina wanaume je wewe unachukua uamuzi gani?”
 
“Uamuzi unao wewe mwenyewe” Ibrahim akaniambia kwa sauti iliyonyeea.
 
“Basi nipe talaka yangu niondoke. Huo ndiyo uamuzi wangu. Kwanza nimeshachoka na maisha ya kuhangaika!”
 
Ibrahim akanyamaza kwa vile nilikuwa nimemfikisha mahali asipopataka.
 
“Usijitie kunyamaza, umeyataka mwenyewe. Nipe talaka yangu!” nikaendelea kumwaambia.
 
Lakini Ibrahim aliendelea kubaki kimya, nikawa ninasema peke yangu. Mwishowe na mimi mikanyamaza.
 
Asubuhi kulipokucha nikajitia kufura. Sikusafisha nyumba wala sikuchemsha chai. Nilitoka bila kumuaga mtu nikaenda kwa Rita..Nilikunywa chai huko huko kisha nikaingia chumbani mwake nikalala mpaka saa sita. Nilipoamka nikarudi nyumbani.
 
SASA ENDELEA
 
Sikujua kuwa walichemsha chai asubuhi au walikaa hivyohivyo, sikutaka kujua. Nilifikia sebuleni nikawa naangalia tv.
 
Kumbe nilipokuwa kwa Rita mmoja wa marafiki wa Ibrahim alikuja nyumbani akampa Ibrahim shilingi elfu kumi. Ibrahim alipogundua kuwa nimerudi, alikuja pale sebuleni akanipa ile elfu kumi aliyopewa.
 
“Chukua hii elfu kumi uende sokoni. Rafiki yangu Martin alikuja kunijulia hali akanipa” akaniambia.
 
“Mpe ndugu yako umtume huko sokoni” nikamwaambia kijeuri.
 
Ibrahim akamuita Zacharia akampa ile pesa.
 
“Shemeji yako atakuagiza vitu vya kununua” akamwaambia.
 
“Shemeji yupi!” nikamuuliza kwa kung’aka na kunyanyuka pale nilipokuwa nimekaa.
 
Huku nikielekea zangu uani nilimwambia. 
 
“Wewe muagize vitu mnavyotaka. Mimi nimuagize nini?”
 
Nikaenda kukaa uani. Sikujua Ibrahim alizungumza nini na mdogo wake lakini baada ya muda kupita Zacharia alikuja uani na kuniambia amesharudi kutoka sokoni.
 
“Vitu viko jikoni” akaniambia.
 
“Mimi sipiki, nenda ukapike mle na kaka yako”
 
Nilipomwaambia hivyo Zacharia aliondoka. Sikujua walivyozungumza na kaka yake lakini baadaye acharia aliingia jikoni na kupika. Mimi nikaingia chumbani nikalala.
 
Baada ya muda Ibrahim aliingia chumbani na kuniuliza.
 
“Unaumwa?”
 
Sikumjibu kitu.
 
Akasimama simama karibu ya kitanda kisha akatoka. Nilikaa humo chumbani hadi saa kumi jioni nilipoingia bafuni na kuoga. Nilipotoka bafuni nikajipara na kuvaa viwalo vya gharama kisha nikavaa baibui langu nikatoka. Sebuleni nilimkuta Ibrahim peke yake akiwaza. Sikujua alikuwa akiwaza nini. Nikafungua mlango na kutoka. Wakati naufunga mlango, nilimsikia akiuliza.
 
“Wewe nani Zacharia?”
 
Sikumjibu chochote, nikaondoka. Ilikuwa safari ya kuelekea kwa Chinga.
 
Nilipotoka hapo nyumbani, nilikwenda kukodi pikipiki ya bodaboda ikanipeleka Makorola nyumbani kwa shangazi yangu. Nilijifanya nilikwenda kumsalimia, kumbe nilikuwa na langu jambo.
 
Vile nilivyomsingizia kuwa anaumwa nilimkuta kweli anaumwa. Akaniambia alikuwa ameshikwa na malaria kwa karibu wiki nzima lakini baada ya kutumia dawa ndiyo ameanza kupata nafuu.
 
Nilitoa shilingi elfu kumi nikampa shangazi kisha nikajidai kumlalamikia kuhusu gubu la mume wangu na jinsi anavyonishutumu kuwa nina wanaume wa nje.
“Yaani tangu apate ule upofu tabia yake imebadilika. Kila siku tunagombana, akiniona ninatoka anajua ninakwenda kwa mwanaume. Akiniona nimepigiwa simu anaitegea sikio akidhani nimepigiwa na mwanaume” nikamueleza shangazi.
 
“Mvumilie. Ile hali yake ndiyo inayomfanya anaona kama umemgeuka” Shangazi akaniambia.
 
“Nimemvumilia sana lakini sasa naona uvumilivu utaisha. Si hilo tu, mume hana pesa anategemea ndugu na jamaa wamsaidie, siku nyingine tunakula mlo mmoja tu halafu ananiletea kero kama hilo”
 
“Sasa utafanyaje? Kuwa naye hivyo hivyo ndiyo kilimwengu. Maisha yana majaribu mengi”
 
“Mh! Mimi naona maisha yatanishinda. Usishangae shangazi ukija kusikia nimemuacha yule mwanaume!”
 
“Usifanye hivyo mwanangu, si vizuri. Dunia yote itakusema wewe. Umekuwa naye katika raha na uwe naye pia katika shida”
 
“Shangazi mume hana kazi hana bazi, nisitoke nikatafute kazi mahali au biashara, nikae tu pale. Si tutakufa kwa njaa shangazi?”
 
“Hamtakufa. Kama ni kutafuta kazi au kufanya biashara sidhani kama atakukataza”
 
Nilivyoona shangazi hakuwa akiliunga mkono wazo langu la kuachana na Ibrahim  japo nilimtolea visingizio chungu nzima vya uongo, nikanyanyuka na kumuambia. 
 
“Vikizidi sana nitaondoka. Utakuja sikia
nimeshaondoka”.
 
Hapo hapo nikamuaga na kuondoka. Nilikwenda saluni nikatengezwa nywele na uso wangu kwa karibu saa moja. Hapo salumi palikuwa panauzwa kashata za kungu. Nilikuwa nazifahamu ingawa sikuwa na ushabiki wa kuzila. Kabla sijaolewa na Ibrahim ndiyo niliwahi kuzitumia sana lakini nilipoolewa nikaziacha.
 
Kashata hizo zinazochanganywa na unga wa mbegu inayoitwa kungumanga unapozila hukulegeza macho na kukulainisha mwili. Wakati mwingine ukila nyingi zinaweza kukulewesha na kukufanya usitosheke na tendo la ndoa.
 
Baadhi ya wanawake hupenda kuzila wanapokuwa na ahadi na wanaume zao. Na sana sana ni wale wanawake makahaba.
 
Nilipoona wasichana wenzangu wanazinunua huku wakizitolea sifa na mimi nikanunua nne na kuzila hapohapo saluni.
 
“Shoga ukitaka uzipatie mpaka uzinuilie, unazila kwa madhumuni gani” msichana aliyekuwa akinishughulikia aliniambia.
 
“Unazinuilia vipi?” nikamuuliza
 
“Unazinuilia vile unavyotaka, kama unataka zikulegeze macho, zikutie kilevi au zikufanye usitosheke na….” hakumaliza sentensi yake akaishia kucheka.
 
“Usipozinuilia hazifanyi kazi?” nikamuuliza.
 
“Zinafanya lakini hao makonkodi wenyewe huzinuilia.Vile unavyozinuilia ndivyo zinavyokufanya lakini kwa vle umeshazila basi”
 
“Nitakuja kuzinunua siku nyingine unifundishe hivyo zinavyonuiliwa” nikamwaambia.
 
Baada ya kutengezwa nywele zangu sikuondoka haraka hapo saluni, Nilimpigia simu Chinga na kumjulisha kuwa ninakwenda kwake, akaniambia ananisubiri
 
Ndipo nilipotoka nikakodi tena pikipiki ya bodaboda, ikanipeleka Mtendele Hotel.
 
Jambo la ajabu lililojitokeza kwa upande wangu ni kuwa safari ile niliingia mle hotelini bila kujali chochote kama vile nilikuwa mwenyeji. Nilimjulisha tu msichana aliyekuwa mapokezi kuwa ninakwenda kumuona Chinga chumba namba kumi na tano. Akaniruhusu.
 
Na hata nilipoingia chumbani kwa Chinga sikumuona haya kama ninavyomuona siku zote. Nilifikizia kujitupa kitandani. Kichwa changu kilikuwa kizito kama niliyekunywa kilevi. Mwili ulikuwa umenilegea na macho yalikuwa yamenilegea kiasi kwamba nilishindwa kutazamana na Chinga. Nikajua hali hiyo ilitokana na zile kashata nilizokula. Nikajiuliza je kama ningezinuilia ingekuwaje?
 
Kama kawaida yake nilimkuta Chinga kwenye kochi akinywa bia. Kwa mara ya kwanza siku ile Chinga alifanikiwa kunishawishi ninywe bia. Katika maisha yangu sikuwahi kunywa bia hata siku moja. Siku ile ndiyo niliionja na kuijua ladha yake. Nilikunywa chupa moja tu lakini kwa sababu nilishakula kashata nne za kungu nilionekana kama niliyekunywa chupa nne.
 
Si kwamba nilikuwa siwezi kusimama au kutembea bali nilikuwa nikiropoka maneno mengi ambayo kwa akili yangu ya kawaida nisingeweza kuyatamka huku nikijifanya nampenda sana Chinga.
 
Ghafla Chinga alinikata kilevi chote nilichokuwa nacho aliponiambia kuwa anatarajia kuondoka kesho yake kurudi Dar es salaam kwa vile mwenzake anayeshirikiana naye katika biashara zao alimpigia simu na kumueleza kuwa anahitajika Dar.
 
“Tutakwenda sote” nikamwaambia Chinga nikiwa nimemkumbatia.
 
Sikuwahi kumkumbatia Ibrahim namna ile hata siku moja tangu apate upofu.
 
“Siwezi kukuchukua wakati ni mke wa mtu” Chinga akaniambia.
 
“Mtu gani…..yule kipofu? Yule tumeshaachana tangu jana usiku” nikamwambia kwa sauti ya kupayuka.
 
“Mmeachana?” Chinga akaniuliza huku akishangaa
 
“Tumeachana jana, mimi si mke wake tena”
 
“Hebu nieleze vizuri, alikwambia anakuacha?”
 
“Ndiyo ameniambia”
 
“Ilikuwaje mpaka akakuacha?”
 
“Ulitokea ugomvi kati yetu. Jana asubuhi tulipokuwa tunazungumza kwenye simu alitusikia akanyamaza hadi usiku alipoanza kunitukana kuwa mimi ni malaya,  nina wanaume wa nje. Nikamwaambia kama mimi ni malaya anipe talaka yangu, ndipo akanipa”
 
“Iko wapi hiyo talaka aliyokupa?”
 
ITAENDELEA kesho hapahapa tangakumekuchablog

MKALI WA MUVI, RAMBO AIBUKA GYM YA PACQUIAO

Rambo alivyomuibukia Pacquiao Gym

Bondia Mfilipino, Manny Pacquiao akiwa na gwiji wa filamu za kibabe Marekani, Sylvester Stallone maarufu kama Rambo au 'Bondia Rocky' mjini Las Vegas, Marekani. Pacquiao yupo katika maandilizi ya mwisho na pambano na Jessie Vargas Novemba 5 mjini Las Vegas uzito wa Welter na mwishoni mwa wiki alitembelewa na Rambo katika gym ya Wild Card mjini Hollywood

MAJINA YA MANAJESHI WALIUWAWA WAKATI WA VITA YA KWANZA YA DUNIA TANGA



Wakazi wa Usagara Tanga, Joseph Kimani, Martin Kiarie na Ali Hamis  wakiangalia majina ya askari wa Uingereza na India waliouwawa  Tanga wakati wa vita ya kwanza ya Dunia mwaka 1914, jumla ya askari 270 waliuwawa na majina yao kuwekwa katika kituo kilicho katika uangalizi cha Commonwealth War Graves Cammission (CWGC)




  Mkazi Usagara Tanga, Joseph Kimani, akiangalia majina ya askari wa Uingereza na India waliouwawa wakati wa vita ya kwanza ya Dunia ambapo jumla ya askari 270 waliuwawa Tanga wakati wa vita hivyo vilivyopiganwa mwaka 1914.Majina hayo yamehifadhiwa na Commonwealth War Graves Cammission (CWGC)

Mkazi wa Usagara Tanga,Devid Charles, akiangalia majina ya askari wa Uingereza na India waliouwawa wakati wa vita ya kwanza ya Dunia mwaka 1914 majina yaliyohifadhiwa na Commnwelth War Graves Commission (CWGC)

Sunday, October 30, 2016

TENDO LA NDOA MARA TATU NA FAIDA ZAKE

KUFANYA MAPENZI  MARA 3 KUNAPUNGUZA KUPATA SHAMBULIO LA MOYO (HEART ATTACK) KWA ASILIMIA 50% WANA SAYANSI WAMESEMA

Utafiti umebainisha kwamba kufanya mapenzi angalau mara tatu kwa wiki kunapunguza uwezekano wa kupatwa Heart Attack (Shambulio la Moyo) kwa 50% ukilinganishwa na yule ambaye anapitisha wiki nzima bila kupiga mambo yetu. Pia utafiti huo unasisitiza ya kwamba mwenye Kufanya Mapenzi killa siku anaondoa uwezekano wa kupata Heart Attack kwa Asilimia 100%

ZIJUE FAIDA ZA KUFANYA MAPENZI

Kiafya
Tendo la ndoa ni moja kati ya mazoezi ya mwili. Wataalamu wanasema kwamba, unapofanya tendo hilo mara tatu kwa wiki husaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini na pia endapo mtu
atafanya tendo mara tatu kwa wiki kwa kipindi cha mwaka mzima ni sawa na kukimbia maili 75.

Tendo la ndoa huongeza takriban vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo ni sawa na kukimbia dakika 15 kiwanjani.

Kuongeza mwendo wa damu
Tendo la ndoa husaidia kuongeza kasi ya mtiririko wa damu kwenye ubongo na sehemu nyingine ya viungo vya mwili, hii huchangia kuongeza kasi ya mapigo ya moyo na kuboresha mfumo wa upumuaji. Msukumo thabiti wa damu mpya yenye oxygen na homoni zenye chembe chembe hai zinapopenya kwenye mishipa ya damu husaidia katika uunguzaji wa chakula, pia huondoa kiasi cha uchafu ambao ungesababisha mishipa na kushindwa kufanya kazi na kumfanya mwanadamu apate maumivu ya mwili.

Hupunguza mafuta yenye kileo (Cholesterol)
Tendo la ndoa huweka sawa uwiano wa mafuta yenye kileo (Cholesterol) nzuri na cholesterol mbaya na wakati huo hupunguza kwa ujumla kiasi cha mafuta yenye kileo mwilini.

Kupunguza maumivu
Wakati wa kufanya mapenzi, homoni iitwayo oxytosin huzalishwa mwilini ambayo husababisha kuzalishwa kwa homoni iitwayo endorphin ambazo hupunguza maumivu kama vile kuvimba sehemu za viungo (arthritis) maumivu ya shingo (Whiplash) na maumivu ya kichwa.

Ulinzi wa tezi ya kibofu (mwanaume)Majimaji yanayozalishwa katika tezi ya kibofu (prostate) yakizidi husababisha kuleta matatizo mwilini. Tendo la ndoa la mpangilio huondoa uzalishaji wa majimaji hayo yenye madhara.

Mabadiliko ya ghafla ya tendo la ndoa huelekea kuleta matatizo yahusianayo na tezi ya prostate.

Kupunguza mfadhaiko wa moyo
Kujitosheleza na kupumzisha mwili baada ya tendo la ndoa ni muhimu kwa kutuliza akili na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini. Watu wenye kushiriki tendo la ndoa wanatajwa kushinda mfadhaiko na kupata usingizi mnono hasa mara baada ya kumaliza kufanya mapenzi.

Huongeza uzalishaji wa homoni za kiume(testosterone) na za kike (Oestogen)
Faida nyingine inayopatika ni kuongeza uzalishaji wa homoni za kiume na za kike likiwemo suala zima la msukumo wa kufanya tendo hilo ambapo mhusika hutosheka zaidi ya yule ambaye hana mazoea ya kufanya mapenzi. Hata hivyo, baadhi ya madaktari wamegundua kwamba ongezeko la homoni za kiume/ kike huweza kuwakinga wanadamu na magonjwa ya moyo.

Kuishi muda mrefu huku ukionekana kijana
Wakati wa tendo la ndoa homoni iitwayo DHEA huzalishwa mwili mzima. Hii husaidia msisimko wa mapenzi kuongezeka.

Kutokana na elimu hiyo DHEA ni kemikali yenye nguvu duniani ambayo husaidia kuweka sawa kinga ya mwili, huongeza ufahamu, kuimarisha mifupa, kutengeneza na kuimarisha afya na kuimarisha mishipa ya moyo (Cardiovascular).

Hupunguza baridi na mafua
Elimu inaonesha kuwa wanaofanya tendo la ndoa mara moja au mbili kwa wiki huongeza 30% ya uzalishaji wa chembe chembe hai za mwili ziitwazo Immunogloulin A ambazo huwa na kazi ya kuulinda mwili dhidi ya magonjwa.

Hizo ni faida chache tu za kufanya tendo la ndoa.
NB: Jambo kubwa la kuzingatia ni kuwa faida hizi hupatikana kwa ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na hofu ya kufumaniwa au kuumbuliwa

mgblog