Sunday, July 31, 2016

HADITHI, MWANAMKE SEHEMU YA 50

SIMULIZI ZA FAKI A FAKI
 
MWANAMKE 50
 
ILIPOISHIA
 
Mzee mmoja akachungulia nje. Alimtazama Abdi kisha akanitazama mimi.
 
“Karibuni” akatuambia na kurudi ndani.
 
Abdi akaingia na kuniambia.
 
“”Karibu”
 
Na mimi nikaingia. Tulitokea katika ukumbi mpana kama  darasa. Harufu tuliyokutana nayo humo ndani ni ya udi na marashi.
 
Katikati ya ule ukumbi palitandikwa jamvi. Katika lile jamvi niliona  sinia iliyotiwa vitu mbalimbali kama vile ndizi mbivu, vipande vya miwa, mkate wa mchele, tende na vitu vingine.
 
Katika kila pembe ya lile jamvi kuliwekwa nazi moja. Jumla zilikuwa nazi nne.
 
Yule mzee wa kisomali alikuwa amesimama nyuma ya mlango.
 
Alimwambia Abdi maneno kwa lugha  ya kisomali. Abdi akaniambia mimi.
 
“Twende tukakae pale”
 
Alinionesha lile jamvi.
 
Tukaenda kukaa. Yule mzee wa kisomali alitoka uani. Baadaye akarudi tena akiwa ameshika kitabu kikubwa cha kiarabu na yeye akakaa kwenye lile jamvi.
 
Sasa niliweza kumuangalia vizuri. Nikajiuliza mbona amefanana na yule msomali niliyemuota akinichukua kule chumbani? Alikuwa  mrefu vile vile na pua yake pia ilikuwa ndefu.
 
Nikashangaa sana.
 
SASA ENDELEA
 
Mzee huyo wa kisomali akamtazama Abdi kisha akamuuliza maneno na kwa kisomali.
 
Abdi akanitazama kisha akamwambia.
 
“Amour”
 
Nikahisi labda alimuuliza jina langu.
 
Mzee wa kisomali akanitazama kisha akafungua kitabu chake. Karasa zilikuwa zimegandana akakigusisha kidole chake kwenye ulimi kukitia mate kisha akaufungua  ule ukurasa.
 
Akaanza kusoma maneno ya kiarabu. Sikuwezaa kujua alikuwa anasoma nini lakini nilisikia akitaja jina  la Zena Binti Jabal Keysi. Wakati mwingine akitaja jina langu.
 
Mara kwa mara nilikuwa nikimtazama Abdi kuona kama mwenzangu alikuwa anaelewa chochote. Abdi alikuwa amenyamaza kimya. Alikuwa ametulia kama aliyekuwa anaaguliwa.
 
Ghafla tukaona nazi iliyokuwa katika pembe moja ya lile jamvi inapasuka yenyewe. Mzee alikuwa akiendelea kusoma tu. Naizi ya pili ikapasuka. Ilipopasuka nazi ya tatu ukuta wa uliokuwa mbele yetu ulifanya ufa akatokea mtu.
 
Alikuwa mwanamke aliyevaa vizuri. Gauni alilovaa lilikuwa limedariziwa vimemeta vya dhahabu. Alikuwa amevaa mkufu wa dhahabu na bangili za dhahabu. Masikioni alikuwa amevaa vipuli vya dhahabu.
 
Kichwani kwake nywele zake zilibanwa kwa taji la dhahabu lililomfanya aonekane kama malikia wa visiwa vya Sheba.
 
Alipotokea sote tulishituka tukamtazama. Ilinichukua sekunde mbili au tatu kutambua kuwa alikuwa Zena!
 
Zena alikuwa amependeza kuliko siku zote nilizowahi kumuona. Alikuwa aking’ara kama mwezi mpevu! Sikuweza kujua ni kitu gani kilichomleta pale na kwanini alitokea katika hali tofauti na anavyotokea siku zote.
 
Siku zote nilizokutana naye alinitokea katika hali ya kawaida, si hali kama ile ya kuibuka kutoka kwenye  ufa wa ukuta. Ilikuwa hali ambayo si tu ilinitisha mimi, ilimtisha hata Abdi aliyekuwa ameketi karibu yangu. Nilimuona akimtazama kwa shauku iliyochanganyika na hofu.
 
Mzee wa Kisomali alimtazama kisha alimwambia maneno kwa lugha ya kiarabu.
 
Zena hakusema chochote. Akiwa miguu pekupeku alikuja taratibu hadi ilipokuwa ile sinia iliyokuwa na vitu akaipindua kwa miguu. Sinia ilipinduka, na vitu vyote vilimwagika chini.
 
Alipomaliza kuipindua ile sinia alimfuata yule mzee wa kisomali akampiga kibao cha shavu. Mzee alianguka chini. Hakuinuka tena. Sasa akamfuata Abdi. Abdi alipoona anafuatwa aliinuka haraka akatoka mbio. Na mimi nikainuka na kutoka mbio kumfuata Abdi.
 
Tulitoka kwenye mlango.  Abdi kama ambaye alibadili mawazo alirudi kwenye mlango huo na kuchungulia. Na mimi nikarudi kuchungulia.
 
Zena hatukumuona tena. Tulimuona yule mzee akijiinua na kukaa. Abdi akarudi. Mimi sikurudi.
 
Nilibaki kwenye mlango nikichungulia.
 
Nikawasikia Abdi na yule mzee wakizungumza kwa lugha ya kisomali. Mzee alikuwa akifoka na akimuashiria Abdi aondoke.
 
Abdi akatoka na kuniambia.
 
“Twenzetu”
 
Wakati tunatembea kurudi tulikoliacha gari Abdi hakunieleza chochote na mimi sikumuuliza chochote.
 
Nilibaki kujiuliza mwenyewe ni kitu gani kilichokuwa kimetendeka pale hadi Zena akatokea na kumwaga vile vitu na kisha kumpiga kibao yule mzee? Sikupata jibu.
 
Nilihisi kuwa jibu alikuwa analo Abdi lakini hakuonesha dalili yoyote ya kutaka kunieleza chochote. Na mimi nikashindwa kumuuliza.
 
Niliona uso wake ulikuwa umefadhaika na alikosa raha. Hakuwa hata akinitazama.
 
Tulirudi kwenye gari lake tukajipakia na  kuondoka.
 
Wakati Abdi akiendesha gari kurudi mjini aliniambia.
 
“Nina hoteli mbili. Ile unayokaa wewe na nyingine mpya. Nataka uwe mneneja wa ile hoteli yangu mpya”
 
“Nitawezaje kuwa meneja wa hoteli yako wakati nataka kuondoka?” nikamuuliza.
 
“Huwezi kuondoka bila paspoti. Subiri nikutengezee paspoti”
 
“Utanitengezea lini?” nikamuuliza.
 
“Usiwe na haraka Amour. Ninakuhakikishia kuwa nitakutengezea isipokuwa katika kipindi hiki cha kusubiri paspoti yako iwe tayari nataka uwe meneja wa hoteli yangu. Nitakupa nyumba na gari na kama utahitaji mke wa kisomali nitakutafutia msichana mrembo”
 
Abdi alianza kunitia tamaa ya maisha na kunipa ushawishi wa kubaki Somalia.
 
Hata hivyo moyo wangu ulikuwa mzito kukubaliana naye. Nilikuwa simuelewi japokuwa mipango aliyonieleza ilikuwa ya maana kwa upande wangu.
 
“Unataka kurudi Tanga, kuna nini? Kama utakaa hapa kwa muda mfupi tu Amour unaweza kupata maendeleo makubwa na ukarudi kwenu ukiwa tajiri” Abdi aliendelea kunishawishi.
 
Muda wote nilikuwa nimebaki kimya nikiyatafakari maneno yake. Alipoona nipo kimya na yeye akanyamaza. Sikuweza kujua ni kwanini aliileta ile mada ya hoteli wakati kulikuwa na tukio jingine la kuibuka kwa Zena ambalo ndilo alilopaswa kunieleza.
 
Kwanza kile kisomo alichokuwa anasoma yule mzee hadi nazi zikapasuka na Zena akatokea, nilijiuliza, kilikuwa kiosomo cha nini. Hapo pia sikupata jibu.
 
Dakika chache baadaye Abdi alilisimamisha gari mbele ya nyumba moja iliyokuwa katika mtaa mtulivu.
 
Aliniambia tushuke, tukashuka.
 
“Nifuate” akaniambia.
 
Tuliingia katika geti la ile nyumba tukakuta mafundi wakipaka rangi kwenye kuta. Alizungumza nao kwa kiomali kisha tukaingia ndani ya ile nyumba.
 
Ilikuwa nyumba nzuri na ya kupendeza. Abdi alitazama sehemu zilizokuwa zimeshapigwa rangi, akaniambia.
 
“Hii ni nyumba yangu. Ninaifanyia ukarabati kwa ajili yako. Wewe utakuja kuishi hapa”
 
“Wewe mwenyewe  unaishi wapi?”
 
“Nitakupeleka ukapaone nyumbani kwangu”
 
“Ni lini hii nyumba itakuwa tayari?”
 
“Leo watamaliza kupiga rangi. Labda keshokutwa unaweza kuhamia. Kesho nitakuwekea fanicha mpya”
 
Alifungua milango ya vyumba na kunionesha ndani.
 
“Patakufaa sana hapa” akaniambia.
 
Sikumjibu kitu. Nilikuwa bado ninajadiliana na moyo wangu kuhusu suala la kubaki pale Somalia.
 
“Amour unafikiria nini. Unataka kuiacha bahati kama hii?” Abdi aliniambia kisha akacheka peke yake.
 
“Twenzetu” akaniambia.
 
Tukatoka tena. Tulijipakia kwenye gari tukaondoka.
 
Breki ya kwanza ilikuwa mbele ya hoteli moja iliyokuwa katika mtaa mwingine. Ilikuwa hoteli ndogo ya ghorofa moja, Ilikuwa imeandikwa kwa herufi kubwa. AL ASAD.
 
“Hii ndio hoteli ambayo nitakuachia wewe, itakuwa kama mali yako kwani tutakuwa tunagawana faida kila mwezi na kila mwaka kama utapenda kuendelea kubaki Somalia” Abdi aliniambia tukiwa bado tupo kwenye gari.
 
Alipoona nilikuwa nikiiangalia angalia ile hoteli, aliniambia.
 
“Tushuke uione vizuri”
 
Tukashuka.
 
Tuliingia ndani ya ile hoteli. Kwa kweli ilikuwa imechangamka.
 
“Sasa nani anaiendesha kwa hivi sasa?” nikamuuliza.
 
“Yuko mtu lakini nitamuondoa”
 
“Sasa ni kwanini umuondoe?”
 
“Lengo langu ni kukunufaisha wewe rafiki yangu au nimefanya kosa?’
 
“Hapana. Ni vizuri”
 
Abdi alinitembeza hoteli nzima kisha tukaingia katika ofisi ya meneja.
 
Meneja mwenyewe alikuwa mtu mzima. Kichwa chake kilishaanza kutoka mvi.
 
JE WEWE MSOMAJI UMESHAPATA WAZO GANI KUHUSU HUYU ABDI? MIMI BADO SIMUELEWI! LAKINI HEBU ACHA TUENDELEE TUTAMGUNDUA TU. KWA LEO NAKOMEA HAPA. Kesho ni kama kawa kama dawa!
 

MAYAI YASIYOIVA NI HARTARI

MAYAI YASIPOIVA NI HATARI

Mayai ni moja ya vyakula vyenye viini lishe muhimu kwa ajili ya afya ya mwili wa binadamu. Kwa kawaida mayai kabla ya kuliwa, huandaliwa kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuchemshwa, kukaangwa au kuchanganywa na vyakula vingine kama vipande vya viazi mviringo ambavyo ni maarufu kwa jina la chips.

Pia, kuna baadhi ya watu wanaopendelea kula mayai mabichi kama dawa ya tiba mbadala, kwa ajili ya kulainisha sauti na wengine hupendelea kula mayai ya kukaanga ambayo hayakukaushwa vizuri.
Ukitembelea migahawa mingi utabaini kuwa watu wanakuwa na mitazamo tofauti na wanavyopenda kula mayai.

Mfano kuna wanaoagiza watengenezewe mayai kwa mtindo unaojulikana kama ‘macho ya ng’ombe.’ Ukiagiza namna hiyo, mpishi atataka kuuliza kama ni ‘macho ya ng’ombe’ ya kugeuza.

Ina maana kuwa ‘macho ya ngombe’ ya kugeuzwa ni yale yanayoivishwa pande zote lakini yale ambayo siyo ya kugeuza, huwa linaiva nusu. Upande mmoja unabaki ukiwa mbichi, na ndiyo raha ya baadhi ya watu.

Hata ukienda kwa wakaanga chipsi, utakuta wanawauliza wateja wao kama wanapokaanga na mayai wakaushe au wasikaushe. Hii inaashiria kuna watu wanataka wale chipsi zikiwa na mayai ambayo halijaiva sawasawa.

Kuna watu wengine wanaamini kwamba kula mayai mabichi kunafanya sauti inakuwa nyororo, hivyo wale waimbaji huwalazimu kufanya hivyo ili kufanya nyimbo zao zivutie.

Si hivyo tu, kuna baadhi ya watu huamini pia dawa ya kikohozi ni kunywa yai bichi lililochanganywa na asali. Hizi ni imani ambazo zimejengeka kwenye jamii na watu hufanya hivyo ili kufikia malengo waliyokusudia.

Katika siku za karibuni, imevuma kuwa mayai ya kwale yanatibu magonjwa sugu kama vile kisukari, shinikizo la damu, saratani na kifua.

Katika mpango huo, wanapendekeza wahusika kula mayai mabichi ya kwale tena kwa kutafuna hadi kaka lake, yaani ganda la nje.

Hali hii imesababisha biashara ya mayai ya kwale kuwa kubwa na hata wafugaji wameongezeka mara dufu.
MG

MBINU 7 ZA KUZUNGUMZA MBELE YA UMATI WA WATU

Mbinu Saba(7) Za Kuondokana Na Hofu Ya Kuongea Mbele Ya Kundi Kubwa La Watu

Katika maisha zipo hofu za aina nyingi zinazomtesa binadamu. Lakini mojawapo ya hofu kubwa ambayo inasumbua sana wengi ni hofu ya kuongea mbele za watu. Hii ni hofu ambayo  huwatesa wengi sana, hasa pale wanaposikia kwamba wanakwenda kuzungumza mbele ya umati wa watu.
Wengi wanaposikia suala la kuongea mbele ya watu hali ya hofu kubwa huwaingia ndani mwao. Kutokana na hofu hiyo husababisha kwa wengine kushindwa kula vizuri, kijasho huwatoka na wakati mwingine kuhisi hata kukimbia kama uwezekano huo upo.

Mara nyingi  hofu hii huwatokea wengi sana. Na ni hali ambayo karibu kila mmoja wetu ameshawahi kukutana nayo katika maisha yake au anayo mpaka sasa. Je, inapotokea unashindwa kuongea mbele za watu huwa unachukua mikakati gani? Je, huwa unaacha kama ilivyo au ni hatua gani ambazo unachukua?

Ni muhimu kujiuliza maswali hayo na kupata majibu kwa sababu suala la kuongea mbele za watu ni la muhimu kwa kila mtu na huwezi kulikwepa. Zipo shughuli nyingi ambazo huwa zinatutaka kuwa wasemaji wakuu, hapo unafanyaje kama huwezi kumudu kuzungumza mbele ya umati? Kama kweli nia yako ni kumudu kuongea mbele za watu makala hii itakupa majibu, kivipi?

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kumudu Kuongea Mbele Ya Kundi Kubwa La Watu.

 1. Jiandae.
Ili uweze kufanikiwa vizuri kuongea mbele za watu, kwanza tambua kwa kina kile unachokwenda kukizungumza. Ikiwezekana ukiweke kwenye maandishi, kisha kifanyie mazoezi mara kwa mara. Unaweza ukafanya mazoezi hayo siku tatu kabla au hata moja.

Kwa kadri utakavyozidi kufanyia mazoezi utajikuta unakimdu vizuri na hiyo haitakupa shida sana wakati wa kuzungumza. Kwa kufanya hivyo akili yako itatulia kuliko ambavyo ungekurupuka na kwenda kuzungumza. Maandalizi ni muhimu sana ili kufanikiwa katika hili.

2. Ondoa mawazo ya kukosolewa.
Wengi wanashindwa kongea mbele za watu wengi kwa sababu ya kuogopa kukataliwa au  kuogopa kukosolewa. Wanakuwa wanaamini kwa vyovyote vile ni lazima watakosolewa. Haya ni mawazo hasi yanayowatesa sana na kuwasumbua wengi.
Lakini kwa vyovyote vile, Ukitaka kumudu kuongea mbele za watu wengi, jiamini kwanza wewe. Amini kuwa unaweza na hakuna mtu mwingine mwenye uwezo wa kuzungumza mada hiyo kuliko wewe. Acha kuamini sana katika kukoselewa, hilo litakusaidia kusimama imara.

3. Acha kufikiria watu unaongea nao.
Inaweza ikakupa shida sana kuongea mbele za watu hasa kila unapofikiria kundi kubwa la watu unaloongea nalo. Kundi hilo linaweza kuwa ni la wasomi au watu ambao wamekuzidi umri. Sasa kila ukifikiria kundi hilo unaanza kujiona kama hutaweza kuzungumza kitu.

Badala ya kufikiria kundi hilo, jitahidi kuweka mawazo yako yote kile unachokizungumza. Kiamini unachokizungumza kuwa utakizungumza kwa usahihi. Hapo ndipo mawazo yako unatakiwa uweke hapo na siyo sehemu nyingine. Hiyo itakusaidia kukuondolea hofu kwa sehemu kubwa.

4. Epuka kuongea kwa haraka.
Siri kubwa ya mafanikio ya kuongea mbele za watu ni kujifunza kongea polepole na kwa vituo. Wengi wanashindwa kumudu kuongea mbele za watu kwa sababu ya kutaka kuongea haraka haraka ili wamalize. Hii ni sumu kubwa inawafanya watu wengi washindwe kumudu kuongea mbele za watu kwa ufasaha.

Unapoongea kwa haraka kitu kinachokutokea kwanza, unakuwa unashindwa kupangilia maneno vizuri lakini pia inakuwa inakufanya ushindwe kupumua vizuri na kukufanya uongee kwa tabu. Kwa hali hiyo ni lazima kuepuka kuongea kwa haraka ili kufanikiwa kuongea mbele za watu vizuri.

5. Fikiria unaongea na mtu mmoja tu.
Sumu kubwa ya wengi kushindwa kuzungumza mbele za watu ni kuchukulia unazungumza na kundi kubwa la watu sana. Huu unaweza ukawa ndiyo ukweli halisi, lakini ili uweze kufanikiwa katika hili ni lazima kwako kujidanganya na kuchukulia kuwa unaongea na mtu mmoja.

Hapa ndipo siri ya mafanikio ilipo. Jifanye unaongea na mtu mmoja binafsi ingawa mbele yako lipo kundi kubwa. Wakati wa mazungumzo unaweza ukasisitiza jambo kwa kusema ‘unanielewa ninachosema’ badala ya kusema ‘mnanielewa ninachosema’ Hiyo itakupa nguvu ya kuondoa hofu ndani mwako.
.
6. Tuliza akili na mawazo yako.
Kwa kuwa utakuwa umeshajua kwamba unaonenda kuongea na watu wengi ni vizuri ukajua kuituliza akili yako. Kabla ya kile unachokwenda kuongea kunywa maji mengi, hiyo haitoshi unaweza ukalala zaidi usiku wke kabla ili kuiweka akili yako sawa.

Hayo yanaweza yakawa ni sehemu ya maandalizi ya kile unachokwwenda kukiongea. Ukumbuke pia akili yako inahitaji utulivu huu, ili usiwe na papara za hapa na pale. Hiyo itakusaidia kumudu zoezi zima la kuongea mbele za watu, ikiwa utakuwa makini kwa hilo.

7. Jifunze.
Tafuta namna ya kujifunza na kuweza kuongeza ujuzi wako wa kuongea mbele za watu. Unaweza ukajifunza kupitia vitabu mbalimbali au unaweza ukatafua ‘mentor’ au mshauri ambaye ameboboa katika hilo eneo na akakuongeza na kukusaidia kufikia hatua yaw ewe kuweza kumdu kuongea mbele za watu bila wasiwasi.

Haijalishi wewe ni mbovu kiasi gani wa kuongea mbele za watu. Lakini, kwa makala hii itakuwa chachu au hamasa kwako ya kuweza kukusaidia kuweza kumudu kuongea mbele za watu bila woga. Kitu kikubwa endelea kujifunza, fanyia mazoezi na mwisho wa siku utamudu hili pia na kuwa mshindi.
MG

WAKRISTO WAUNGANA NA WAISLAMU KATIKA IBADA

Waislamu wajiunga na wakatoliki katika ibada

WaIslamu zaidi ya mia moja wamejumuka na Wakatoliki katika sala iliyohudhuriwa na waumini wengi katika Kanisa moja huko Rouen, Ufaransa.
Tukio hilo limewadia , siku tano baada ya kasisi wa kanisa hilo , kuuawa na wapiganaji wa Kiislamu.
Makanisa sehemu mbali mbali za Ufaransa, yaliwaalika WaIslamu wajumike nao kwenye maombi leo, kuonesha wanakanusha mauaji hayo.
Mauaji ya hivi karibu kabisa yaliyotekelezwa na wapiganaji wa Kiislamu, yameshtua Ufaransa.
Kasisi huyo wa umri wa miaka 86, Kasisi Jacques Hamel, aliuwawa akiwa kwenye maombi

CHALSEA KUVUNJA KABATI KUMNUNUA LUKAKU

Chelsea sasa wapo radhi kutoa zaidi ya Tsh Bilioni 190 kwa ajili ya Lukaku

Dirisha la usajili la msimu huu kwa vilabu vya soka barani Ulaya linazidi kuvutia zaidi, hii inatokana na vilabu vingi sasa kutaka kuwarudisha katika timu zao wachezaji wao wa zamani kwa gharama kubwa wakati waliwaacha waondoke kirahisi misimu kadhaa iliyopita.
Man United wanataka kuvunja rekodi ya usajili kwa kumridisha Pogba, Real Madrid wamemrudisha Morata kikosini, Borussia Dortmund tayari wamemrudisha Mario katika kikosi chao, sasa Chelsea inajiandaa kutoa euro milioni 80 kwa ajili ya kuishawish Everton imuachie mchezaji wao wa zamani Romelu Lukaku arejee Stamford Bridge.
Lukaku-Chelsea
Mwandishi Ivan Zazzaroni wa gazeti la dello Sport ameandika katika gazeti kuwa Chelsea wapo tayari kutoa euro milioni 80 kwa ajili ya kumrudisha mshambuliaji wao Romelu Lukaku aliyeondoka Stamford Bridge 2014, Lukaku ameondoka Chelsea akiwa kacheza mechi 10 katika kipindi cha miaka mitatu alipojiunga nayo akitokea Anderlecht.
millardayo

HAPA NI KAZI TU, KAZINI MITAANI NAWAJIBIKA

Afande aliyevalia bikini amkamata mwizi

Afisa wa polisi wa kike aliyevalia bikini amewaogofya wezi mjini Stockholm Sweden baada ya kumnasa mwizi wa simu ya mkononi kwa miereka ufukweni.
 Mikaela Kellner na wenzake ambao pia ni maafisa wa polisi walikuwa wametoka kazini na kwenda   ufukweni kujitanua chini ya jua.
Mara wakagundua mtu mmoja aliyekuwa akinadi vitabu vya watoto yatima . .
Wakashtuka na kuanza kumfuata mbio ufukweni.
watu waliokuwa wakijivinjari ufukweni walidhania kuwa mwanamke huyo aliyekuwa nusura uchi alikuwa akifanya mazoezi kwa jazba.
Kufumba na kufumbua wakashtuka binti huyo aliyekuwa amevalia Bikini ''yaani sindiria na chupi'' pekee alikuwa akikabiliana na mwanaume fulani.
Hapo ndipo walipong'amua haikuwa mazoezi, na walipopeleleza wakagundua kuwa alikuwa ni afisa polisi aliyekuwa akimbana mwizi.
Lakini kwasababu huyo mwizi alijifanya ''dume'' ilimbidi kumbwaga sakafuni kwa mieleka na mateke mazitomazito.
Waandishi wa habari waliofika katika bustani hiyo ya Ralambshov baada ya kushuhudia purukushani hiyo walipigwa na butwaa alipowaeleza kuwa alikuwa ni ''afande'' aliyekuwa kazini kumnasa mwizi.
 Kellner amekuwa maarufu sana baada ya picha yake akiwa na pikini kuchapishwa katika majarida ya habari nchini humo.
Chini ya saa 24 baada ya tukio huyo totoshoo huyo amepokea uungwaji mkono mkubwa miongoni mwa wenyeji.
Ukurasa wake wa Instagram umepata ongezeko la zaidi ya wafuasi 9,000 tayari.

SEKESEKE LA VYETI FEKI, SEKOMU MAMBO SAFI



Tanga.Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (Sekomu),kimesema hakitakumbwa na wimbi linaloendelea linalotokana na mchakato wa Serikali wa kuwafichua wasio na sifa kwa sababu tangu kilipoanzishwa kinajiendesha kwa umakini.

Mkuu wa Chuo hicho,Dr Stephen Munga alitoa maelezo hayo LEO  alipokuwa akizungumza na Tangakumekuchablog mara baada ya kuzindua maonesho ya shughuli zinazoendeshwa na Sekomu yanayofanyika katika tawi lake lililopo jijini Tanga.

Alisema msimamo wa Sekomu wa tangu kilipoanzishwa kutosajili wanafunzi wanapojiunga wasio na sifa ndiyo unaokiweka huru kipindi hiki ambacho Serikali inataka kila jambo liendeshwe kwa utaratibu unaohitajika kwa chuo kikuu.

“Upepo unaovikumba vyuo vikuu nchini hautatukumba Sekomu kwa sababu tumekuwa tukishirikiana na Serikali tangu tulipoanza na msimamo wetu wa kuzingatia kanuni na sheria ndiyo unaotuacha huru hivi sasa”alisema Dr Munga.

Akizungumzia kuhusu maonesho hayo,Mkuu huyo wa Sekomu alisema yana lengo la kukiweka karibu na jamii hasa katika kipindi hiki ambacho kinakaribia kufikisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake lakini pia ni kuonyesha upekee wake nchini na Afrika mashariki kwa ujumla hasa katika utoaji wa elimu maalumu.
“Sekomu ni chuo cha kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki kutoa shahada ya kwanza ya elimu maalumu,wakati tukianza  tulionekana kama chuo cha ajabu lakini tunashukuru sasa hivi vyuo vingi vimeiga kutokana na umuhimu wake katika makundi maalumu”alisema Dr Munga.

Kaimu Makamu Mkuu wa Sekomu,mipango na biashara,Geofrey Kingazi alisema miongoni mwa yanayooneshwa katika maonesho hayo ni machapisho ya kazi za utafiti na kazi zinazofanyika chuoni ukiwamo  mbinu zinazotumika kuwajengea uwezo wanafunzi wa makundi maalumu.

Khalid  Mohamed anayechukua masomo shahada ya elimu katika chuo kikuu cha Sekomu aliupongeza uongozi wa chuo hicho kikuu kwa kuzingatia sheria na kanuni ambapo wakati hivi sasa wenzao wa vyuo vingine wanapohangaika wao hawana wasiwasi kutokana na kutimiza masharti yote yanayohitajika.

                      MWISHO

MAFURIKO YAUWA WATU 100 INDIA

Mafuriko yaua zaidi ya watu 100 India na Nepal

Mafuriko mashariki mwa India na nchini Nepal yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 100 na kuwaathiri mamilioni ya wengine.
Mito iliyojaa maji imesababisha vijiji kufurika na kuwalazimu maelfu ya watu kuhama makwao.
Katika majimbo ya India ya Assam na Bihar, makundi ya uokoaji yanatumia mashua kuwafikia watu ambao wametafuta hifadhi katika makao ya muda kwenye sehemu zilizoinuka.
BBC

Saturday, July 30, 2016

TABIA 10 ZINAZOHARIBU FIGO

Tabia 10 zinazoharibu Figo

Tabia 10 zinazoharibu Figo

  1. Kubana mkojo muda mrefu
  2. Kutokunywa maji ya kutosha kila siku
  3. Kutumia chumvi nyingi kuzidi kiwango
  4. Kula nyama mara nyingi
  5. Kutokula chakula cha kutosha
  6. Kuchelewa kujitibu maambukizi madogo madogo haraka na kwa usahihi
  7. Kutumia visivyo dawa za kutuliza maumivu
  8. Kutumia dawa kwa ajili ya insulin kwa muda mrefu
  9. Kunywa pombe kupita kiasi
  10. Kutopata muda wa kutosha kupumzika


Kunywa glasi 2 za juisi ya parachichi kila siku kutaziweka figo zako katika hali ya usafi na afya.

NAMNA YA KUONDOA SUMU MWILINI

JINSI YA KUTOA SUMU MWILINI

Sumu ni kitu chochote kile ambacho katika mwili huhatarisha utendaji kazi wa mifumo au viungo vya mwili na huweza kupelekea kifo.

Kwa kutegemeana na namna ambavyo sumu huuathiri mwili, tunapata makundi mawili ya sumu; Kundi la kwanza ni aina za sumu ambazo husababisha madhara yasiyorekebishika au tuite ulemavu wa maisha (Irreversible effects), na kundi la pili ni aina za sumu zinazosababisha madhara yanayoweza kurekebishika (Reversible effects).

Miongoni mwa madhara yasiyorekebishika yanayoweza kusababishwa na kundi la kwanza la sumu ni pamoja na, makovu katika ngozi, upofu, matatizo ya akili, matatizo ya damu, kulemaa au kupooza viungo na kuwa kiziwi.

Kundi la pili la sumu husababisha madhara yanayoweza kurekebishika au kutatulika baada ya muda fulani, mfano uvimbe, kuwasha kwa ngozi, ngozi kuwa kavu sana, kutokwa na majibu pamoja na sehemu za mwili kubadilika rangi.

Mpenzi msomaji, kuna vyanzo viwili vya sumu mwilini; chanzo cha kwanza ni kupitia vitu ambavyo vipo nje ya mwili, binadamu huvitumia na matokeo yake humuathiri. Vitu hivi MTU huvitumia pengine kwa kujua au kutokujua kuwa kwake ni sumu, mfano matumizi ya kemikali aina ya zebaki ( mercury) katika shughuli za migodini, uangalifu au umakini mkubwa wahitajika pindi utumiapo kemikali hii kwani huweza kukupa madhara katika mapafu na moyo. Sumu nyingine hujitokeza kwa kukosa au kutozingatia maelekezo tunayopewa juu ya utumiaji salama Wa Dawa za kutibu magonjwa, mtu anazidisha dozi, au ni mama mjamzito lakini anatumia Dawa ambayo siyo salama kwa kiumbe kilichopo tumboni, matokeo yake ni kuhatarisha maisha ya mjamzito, mtoto tumboni au kuja kujifungua mtoto mwenye ulemavu usio rekebishika.

Chanzo cha pili cha sumu ni miili yetu wenyewe, ni katika hali ya kawaida mwili unazalisha sumu mbalimbali kupitia mifumo yake ya Kazi, mfano katika uvunjwaji na usambazaji Wa chakula mwilini, mifumo ya hewa, utengenezaji wa damu, katika Kazi zote hizi na nyingine ambazo mwili hufanya, kuna baadhi ya sumu huzalishwa pamoja na kemikali (free radicals) nyingi ambazo hazitakiwi ziendelee kukaa mwilini, kwani huathiri utendaji Kazi wa kawaida wa mwili.

Uondoaji wa sumu mwilini hutegemeana na aina ya sumu yenyewe. Njia ya kwanza ni matumizi ya Dawa za kuivunja nguvu ile sumu husika ambapo kitaalamu hujulikana kwa jina la antidote, hapa ni baada ya uchunguzi kufanyika na kugundua aina ya sumu iliyokuathiri na kisha utapewa dawa kulingana na majibu ya uchunguzi wa kitaalamu.

Njia ya pili inayoweza kutusaidia kuondoa sumu na hasa zile zinazozalishwa mwilini ni matumizi ya vyakula bora, hivi ni vyakula ambavyo kwa asili yake huwa na virutubisho ambavyo huvunja vunja na kuondoa sumu mwilini, vyakula hivi kitaalamu huwa na vitu vinavyoitwa antioxidants, ambavyo huulinda mwili dhidi ya kemikali hatarishi zinazozalishwa mwilini. Virutubisho hivi ni pamoja na Vitamin A, Vitamini C na Vitamini E. Vitamini hizi hupatikana katika mboga za majani na matunda, mfano mchicha, spinachi, karoti, matembele, machungwa, nanasi, maembe, machenza pamoja na mafuta ya mimea mfano alizeti.

Ili miili yetu iweze kufanya kazi vizuri na tuendelee kuwa na afya njema, inabidi tuepukane na sumu hizi, pale inapo tulazimu zitumike (mfano zebaki, migodini), basi tuzidishe umakini katika kujilinda afya zetu, na pia tubadilishe aina ya maisha au ulaji wa vyakula, matunda na mboga za majani ni walinzi wakubwa sana wa afya zetu.
SOURCE MG BLOG

AMKA NA MAGAZETI NA NEW AGE EDUCATION CENTRE TANGA, 0717 713866

Magazeti yanaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha New Age Education Centre Tanga, New Age ni mabingwa wa kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza kielimu, New Age wanapokea wanafunzi wa kozi mbalimbali na kielimu pamoja na wamakazini, New Age wapo Tanga mkabala na TANESCO  simu 0717 713866



TETESI ZA USAJILI ULAYA

Tetesi za soka Ulaya

Arsenal wataongeza dau na kufikia pauni milioni 35 kumtaka mshambuliaji wa Lyon Alexandre Lacazette, 25, baada ya dau la awali la pauni milioni 29.3 kukataliwa na klabu hiyo ya Ufaransa (Daily Telegraph).
Arsenal pia wanataka kumsajili beki wa Torino, Bruno Peres, 26, huku klabu hiyo ikitaka pauni milioni 16.9 kulingana na (Gazzetta World).
Vilevile klabu hiyo inazungumza na Valencia kutaka kumsajili beki mjerumani Shkodran Mustafi, 24, ambaye ana kipengele cha uhamisho chenye thamani ya pauni milioni 42.1 kwenye mkataba wake (Sky Sports).
Dau la Chelsea la pauni milioni 57, kumtaka mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku, 23, limekatakiwa, huku klabu hiyo ikitaka pauni milioni 75 (Daily Mirror).
Kiungo wa Tottenham Christian Eriksen, 24, amekataa kusaini mkataba mpya, kwa sababu anataka mshahara wake wa pauni 30,000 kwa wiki kuongezwa (Evening Standard).
Nayo Swansea wamepanda dau la kumtaka mshambuliaji wa Sevilla, Fernando Llorente, 31, baada ya Bafetimbi Gomis kwenda Marseille kwa mkopo hadi mwisho wa msimu, na hivyo hawana mshambuliaji rasmi kwa sasa (Daily Mail).
Wakati huohuo Leicester City wako tayari kumpa mkataba wa pauni 100,000 kwa wiki kiungo Riyad Mahrez, 25 ambaye inaaminika anasakwa na Arsenal (Daily Express).
Na hayo yakijiri Manchester United inakaribia kumsajili beki wa kulia kutoka Brazil anayechezea Monaco, Fabinho, 22 (globoesporte).
Aston Villa wanaonekana watamuuza Idrissa Gana, 26, huku Everton wakiwa tayari kukamilisha usajili wa pauni milioni 7.1 kumchukua mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal (Daily Mirror). Vilevile beki wa Manchester United Cameron Borthwick-Jackson, 19, huenda akaondoka Old Trafford na kwenda kucheza kwingineko kwa mkopo (Manchester Evening News).
Everton hawajapanda dau lolote kumtaka beki wa Sunderland Lamine Kone, 27, licha ya taarifa kuzagaa kuwa dau la pauni milioni 14 limetolewa (Sunderland Echo).
Everton wanataka kumsajili beki wa Swansea Ashley Williams, 31, ambaye huenda akagharimu pauni milioni 10 kwa mujibu wa (Daily Mirror).
Nayo Manchester City wanasita kutoa pauni milioni 50 kumsajili beki wa kati wa Everton John Stones, 22, wakitaka kutoa takriban pauni milioni 40 (guardian).
Mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino, 22, yuko tayari kubakia katika klabu hiyo hadi mkataba wake utakapomalizika msimu ujao na aondoke kama mchezaji huru (ESPN).
Klabu ya Galatasaray inataka kumsajili beki wa Manchester City Jason Denayer, 21, na pia kiungo wa Liverpool Lucas Leiva, 29 (Daily Mirror).
Manchester City watathibitisha kuwa Sergio Aguero, 28, atasaini mkataba mpya kabla ya kuanza kwa msimu (Daily Mail).

ASILIMIA 50 YA WATOTO WANA MAGONJWA YA MENO

50% ya watoto Tanzania wana magonjwa ya meno - TDA

Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA), wakati kikiadhimisha Siku ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani mwaka huu kilibaini kuwa zaidi ya asilimia 50 ya watoto walio chini ya miaka 14, wanakabiliwa na magonjwa ya kinywa na meno.

Pia kiilibaini kuwa asilimia 80 ya watanzania wanakabiliwa na matatizo ya ugonjwa wa fizi.

Katika kukabiliana na hali hiyo, wadau mbalimbali wameanza kutoa elimu ya afya ya kinywa ikiwa ni pamoja na watengenezaji wa dawa ya meno ya whitedent wa namna ya kujikinga na magonjwa ya kinywa.

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliozungumza na East Africa Radio wanasema kumekuwa na upuuziaji mkubwa katika usafishaji wa meno, ulimi na kinywa kwa ujumla hali inayochangia watu wengi kung'oa meno yao.

FAIBER YA KISASA YATENGENEZWA TANGA, ITAKUWA NA UWEZO WA KUBEBA ABIRIA 80

 Mafundi wakiunda Faiber ambayo kukamilika kwake itakuwa na uwezo wa kuchukua abiria zaidi ya 80 waliokaa na kuondosha kero ya Usafiri kati ya Pemba na Tanga.
Faiber hiyo ambayo itakuwa ya kwanza kutengenezwa Tanzania hususani Tanga tofauti na ilivyo huwa inaagiziwa kutoka nje ya nchi.
Faiber hiyo inayotengezwa na Mtaalamu, Hemed Said mkazi wa Kojani Pemba.
Inatajwa kuwa Faiber hiyo ambayo kukamilika kwake itakuwa msaada mbali ya kubeba abiria pia inaweza kufanya uokozi kutokana na kuwa na Spidi kubwa  kufika kwenye tukio.





Hii ndio Faiber ambayo kukamilika kwake itakuwa na uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 80 na kuwa na uwezo wa kutembea kwa kasi zaidi ya vyombo vyengine baharini

LEICESTER CITY YAIBANIA ARSEANL KWA MAHREZ

Mbinu za Leicester City kumzuia Mahrez kujiunga na Arsenal

Mabingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 2015/2016 klabu ya Leicester City bado inaendelea kupambana ili kulinda kikosi chake kilichoisaidia kutwaa Ubingwa wa England kisibomolewe,  baada ya Leicester City kutwaa taji la England vilabu vingi vikubwa England vinahangahika kuhakikisha vinasajili nyota wa kikosi hiko.
Leicester City wameripotiwa na gazeti la Daily Express kuwa wameamua kumuongezea mshahara winga wa kimataifa wa Algeria anayeichezea klabu hiyo Riyad Mahrez ili asishawishike kujiunga na Arsenal ambao nao wamepanga kumlipa mshahara wa pound 100,000 kwa wiki, hivyo Leicester City wanataka kumlipa mshahara huo ili asiondoke.
nogo-811x1024
Riyad Mahrez ambaye ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa PFA, anawindwa na Arsenal na tayari wameripotiwa kuwa wapo tayari kutoa pound milioni 37 kwa Leicester City ili wampate nyota huyo, ambaye aliwahi kukaririwa kwa wiki za hivi karibuni akisema kuwa bado hajajua msimamo wake kuhusu kuondoka au la.

Friday, July 29, 2016

HADITHI, MWANAMKE SEHEMU YA 49

SIMULIZI ZA FAKI A FAKI 0713 340572
 
MWANAMKE 49
 
ILIPOISHIA
 
Baada ya kuwaza sana nilipitiwa na usingizi. Sikujua nililala kwa muda gani lakini nilihisi kama nilishituka katikati ya usiku au nilikuwa katika ndoto. Nikaona kama mlango wa chumba nilichokuwa nimelala unafunguliwa taratibu.
 
Kitendo hicho kilitokea nikiwa na kumbukumbu kamili kichwani mwangu kwamba mlango wa chumba hicho niliufunga kwa ndani na kuhakikisha kuwa ulikuwa umefungika.
 
Mlango ulipokuwa wazi nilimuona mtu akiingia. Alikuwa mzee mwembamba na mrefu. Wembamba wake ulichanganyika na kukonda. Alikuwa na nywele ndefu, nyeupe tupu.
 
Alikuwa amejifunga shuka nyeupe kiunoni na mabegani alijitanda shuka nyingine nyeupe kuziba kifua na tumbo lake. Hata hivyo upande mmoja wa kifua chake ulikuwa ukionekana. Mbavu zake zilikuwa zimetokeza na kuhisabika.
 
Akaingia mle chumbani kwa kunyata. Wakati akiingia nilikuwa nikijiuliza nilikuwa ninaota au nilichokuwa kitendo  nakiona kilikuwa ni kweli.
 
Muda huo niligundua kuwa  sikuwa sawa. Nilikuwa kama niliyepatwa na jinamizi. Mwili wangu haukuwa na uwezo wa kufanya chochote hata kupiga kelele.
 
Kadhalika akili yangu ilikuwa imepoteza uwezo wake na nilikuwa kama taahira au zezeta. Sikuweza kujua ni kwanini nilijihisi kuwa vile.
 
Yule mzee wa kisomali alikuja hadi karibu na kitanda nilichokuwa nimelala.
 
Nilimuona vizuri. Alikuwa na pua ndefu na macho makali na madogo. Akasimama na kuniita.
 
“Amour!”
 
Nikanyamaza kimya. Nikamuona anasema maneno fulani kwa lugha  ya kisomali kisha akanyoosha mkono wake na kupapasa kitanda nilichokuwa nimelalaa akashika mkono wangu na kuubana.
 
SASA ENDELEA
.
Aliubana kwa nguvu nikaona kama nilishikwa kwa koleo.
 
“Inuka” akaniambia.
 
Kwa sababu nilikuwa kama taahira nisiyejielewa nikainuka kweli.
 
“Shuka kwenye kitanda” akaendelea kuniambia.
 
Nikashuka kwenye kitanda. Nilikuwa nimevaa chupi tu. Akaichukua ile shuka aliyoitanda mabegani mwake akanifunga nayo kiunoni kisha akanishika tena mkono na kuniambia.
 
“Twende”
 
Nikatoka naye mle chumbani.
 
Tulishuka ngazi, akatumia mlango wa nyuma wa hoteli kunitoa. Nilikuta gari limewekwa sambamba na mlango. Nikafunguliwa mlango wa nyuma wa gari, nikajipakia bilakuambiwa.
 
Mzee naye aliingia katika siti ya nyuma. Kulikuwa na mtu aliyekuwa kwenye siti ya dereva ambaye sikuweza kumuona vizuri. Sikujua alikuwa nani.
 
Kama ningemchunguza ningeweza kumjua lakini akili yangu haikuona umuhimu wa kutaka kumjua wala kujua nilikuwa napelekwa wapi.
 
Gari likapigwa moto na kuondoka. Safari ikaanza. Mji ulikuwa kimya na hakukuwa na watu wowote walioonekana barabarani zaidi ya walinzi wa maduka waliokuwa wakisinzia.
 
Baada ya mwendo wa karibu kilometa tano nilihisi kuwa tulikuwa tumeuacha mji kwani sikuona  tena majumba ya ghorofa isipokuwa nyumba ndogo ndogo.
 
Tulikuwa tumeingia  katika maeneo ya ambayo kwa lugha ya kwetu tungeyaita ‘uswahilini’
 
Mwanga wa gari tulilokuwemo ulimulika mapaka yaliyokuwa yakirandaranda kutafuta vyakula vilivyotupwa kwenye mapipa ya takataka. Ingawa ilikuwa usiku maji taka yalikuwa yakitiririka kutoka kwenye majumba ya watu na kuunda vidimbwi vya  maji taka kandokando ya barabara.
 
Wakati wote nilikuwa nashindana na akili yangu. Nilikuwa naona kichwa kizito kama niliyelemewa na usingizi, wakati huo huo sikutaka usingizi unichukue.
 
 Kila muda nilikuwa najigutuka na kukaza macho yangu ili nisilale. Lakini mwisho wake nilizidiwa nguvu, usingizi wa moja kwa moja ukanichukua ghafla.
 
Hata sikuweza kujua tena lile gari lilielekea wapi.
 
Lakini nilipokuja  kuzinduka nilijiona mimi na yule mzee tumekaa kando ya shimo lililokuwa mbele yetu. Shimo hilo lilichimbwa usawa wa kaburi kando ya mti mkubwa. Mahali tulipokuwa palikuwa ni porini.
 
Kulikuwa na taa ya chemli iliyokuwa inawaka pembeni mwa kaburi hilo na kufanya sehemu ile tuliyokuwa iwe na mwanga kwani eneo lote lilikuwa na kiza totoro.
 
Yule mzee wa kisomali aliingia kwenye lile kaburi akasimama na kuniambia.
 
“Ingia”
 
Na mimi nikaingia.
 
“Kaa hapo chini”
 
Akanionesha mahali pa kukaa, nikakaa. Nikaona analishika sikio langu la upande wa kulia na kusema maneno kwa lugha ya kisomali kama mtu aliyekuwa anasoma dua kisha akaniinamia na kukigandamiza kichwa chake kwenye komo langu.
 
Alinishika na kunigandamiza kwa nguvu sana mpaka nikasikia maumivu ya kichwa. Nilitaka  kupiga kelele nilipomuona amerushwa na kuanguka chini. Alikuwa kama aliyerushwa na umeme.
 
Akainuka taratibu na kutoka kwenye lile kaburi. Kilichofuatia baada  ya hapo sikukifahamu, nilishitukia tu nikiamka kitandani pale hoteli nilipokodiwa chumba na Abdi.
 
Nikahisi kwamba labda nilikuwa katika ndoto. Moyo ulikuwa ukinienda mbio. Nikainuka na kwenda kuutazama  mlango wa mle chumbani. Niliukuta umefungwa kwa ndani. Kitu ambacho kiliashiria kuwa hakukuwa na mtu aliyeingia humo chumbani.
 
Lakini ni ndoto gani ile? Nikajiuliza. Kila kitu nilikiona waziwazi kama vile kinatokea kweli.
 
Kama ilikuwa ndoto ilikuwa ya ajabu sana, nikajiambia.
 
Wakati ule nilipoamka kulikuwa kumekucha. Nikaingia maliwatoni. Nilipotoka nikavaa nguo. Nilivaa  suti ile ile niliyonunuliwa na Abdi.
 
Nikashuka chini na kuingia mkahawani. Nilipatiwa kifungua kinywa. Wakati nakunywa chai nikamuona Abdi akiingia.
 
“Amour salaam alaykum” akanisalimia kwa bashasha huku akinipa mkono.
 
“Alayka salaam. Habari ya  tangu jana?”
 
“Nzuri bwana, umeamkaje?”
 
“Nashukuru, nimeamka salama. Sijui wewe”
 
Na yeye akaagiza kifungua kinywa.
 
“Kuna sehemu nataka twende” akaniambia.
 
“Wapi?”
 
“Mogadishu ni kubwa sana. Kuna sehemu nyingi nataka kukuonesha”
 
“Sawa”
 
Tulipomaliza kunywa chai tukatoka.
 
“Jana nilikufuata usiku nikakuta umelala” Abdi aliniambia wakati tunatoka.
 
“Nililala mapema kwa sababu ya uchovu”
 
“Niliwambia wale wasichana wasikuamshe. Nilijua ulikuwa na uchovu mwingi”
 
Tulitoka nje ya hoteli tukajipakia kwenye gari. Lilikuwa ni gari la aina nyingine sio lile la jana yake.
 
Baada ya kujipakia tukaondoka.
 
“Nataka uuone mji wetu vizuri” Abdi alikuwa akinizungumzisha huku gari likiwa katika mwendo  wa taratibu au wa kinyonga . Nilikuwa sijui tunakwenda wapi.
 
“Mji wenu ni mzuri sana. Una majumba makubwa na umejengeka sana” nikamwambia.
 
“Bado. Kuna maeneo mengi hujayaona”
 
“Inavyoonekana mmepiga hatua kubwa ya maendeleo”
 
“Sana”
 
Baada ya mwendo wa karibu nusu saa tuliingia katika maeneo ya mashamba. Nilikuwa nikijiuliza alikuwa akinipeleka shambani kwake au alitaka kunionesha kitu gani?
 
Tulitokea katika mtaa mmoja uliokuwa umezagaa uchafu. Tulipishana na mbuzi, kondoo na kuku wa kienyeji. Abdi alikuwa akikata kona ovyo kukwepa mashimo na vidimbwi vya maji machafu.
 
“Tuache gari hapa” Abdi akaniambia huku akifunga breki pembeni mwa njia. Bila shaka alishindwa kuendesha kutokana na barabara yenyewe kujaa mazagazaga.
 
Tulishuka tukatembea kwa miguu. Tulizipita nyumba mbili za ghorofa. Zilikuwa nyumba zilizoonekana zimeshapitwa na muda wake wa kuishi watu kwani zilichakaa sana. Huenda zilijengwa miaka mia moja iliyopita. Enzi za utawala wa kikoloni.
 
Tuliingia mtaa mwingine uliokuwa na tifutifu jingi. Tukapita msikiti. Tulikwenda mbele kidogo, Abdi akasimama mbele ya mlango wa nyumba moja iliyokuwa imepakwa rangi nyeupe.
 
Mlango wake ulikuwa umechorwa picha ya nyota na mwezi.
 
Abdi alibisha mlango huo. Baada ya muda kidogo mlango ukafunguliwa.
 
Mzee mmoja akachungulia nje. Alimtazama Abdi kisha akanitazama mimi.
 
“Karibuni” akatuambia na kurudi ndani.
 
Abdi akaingia na kuniambia.
 
“”Karibu”
 
Na mimi nikaingia. Tulitokea katika ukumbi mpana kama  darasa. Harufu tuliyokutana nayo humo ndani ni ya udi na marashi.
 
Katikati ya ule ukumbi palitandikwa jamvi. Katika lile jamvi niliona  sinia iliyotiwa vitu mbalimbali kama vile ndizi mbivu, vipande vya miwa, mkate wa mchele, tende na vitu vingine ikiwemo chupa kubwa lenye  asali.
 
Katika kila pembe ya lile jamvi kuliwekwa nazi moja. Jumla zilikuwa nazi nne.
 
Yule mzee wa kisomali alikuwa amesimama nyuma ya mlango.
 
Alimwambia Abdi maneno kwa lugha  ya kisomali. Abdi akaniambia mimi.
 
“Twende tukakae pale”
 
Alinionesha lile jamvi.
 
Tukaenda kukaa. Yule mzee wa kisomali alitoka uani. Baadaye akarudi tena akiwa ameshika kitabu kikubwa cha kiarabu na yeye akakaa kwenye lile jamvi.
 
Sasa niliweza kumuangalia vizuri. Nikajiuliza mbona amefanana na yule msomali niliyemuota akinichukua kule chumbani? Alikuwa  mrefu vile vile na pua yake pia ilikuwa ndefu.
 
Nikashangaa sana.
 
KUNA NINI HAPA? HUYU MZEE NI NANI? ANA MIPANGO GANI NA ABDI? MAJIBU Y MASWALI  HAYO UTAYAPATA KESHO