Saturday, February 28, 2015

UNDANI WA KIFO CHA JOHN KOMBA

UNDANI WA KIFO CHA KEPTENI JOHN KOMBA!


Marehemu Kapteni Komba.
Picha ya kwanza ya Marehemu komba mara baada ya kufariki dunia.
…Komba enzi za uhai wake.
MBUNGE wa Mbinga Magharibi, Kapten John Komba amefariki dunia jioni hii jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, hata hivyo hakuwa tayari kuelezea kwa undani kwa madai kuwa taarifa hizo zimemfikia sasa hivi.
Mmoja wa watoto wa Komba ambaye aliyejitambulisha kwa jina la Herman amethibitisha kutokea kwa msiba huo na akasema, huku akilia, msiba wa baba yake upo nyumbani kwake Mbezi Tangi Bovu, Dar.
Habari zinasema asubuhi ya leo Komba alikwenda kwenye shughuli zake za kikazi kama kawaida lakini baadaye akajisikia vibaya, hivyo akaamua kurudi nyumbani ambako alizidiwa ndipo familia yake ilipoamua kumkimbiza Hospitali ya TMJ lakini alipopimwa na madaktari ikathibitika kuwa alikuwa tayari ameaga dunia. habari zaidi zinasema kuwa hivi sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo.
Kapteni Komba ambaye pia ni Mkurugugenzi wa Kikundi cha Maigizo cha Tanzania One Theatre (TOT),  ambacho kina kikundi cha taarabu na bendi  inayokwenda na mtindo wa Achimenengule, amekuwa akikisaidia sana chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kampeni zake wakati wa uchaguzi kwa kutunga nyimbo za kuhamasisha wapiga kura na kushiriki kupiga live kwenye majukwaa ya kisiasa.
…alipokuwa bungeni
Enzi za uhai wake alitamani  sana na kufanya juhudi kubwa ili mtindo wa Achimenengule uwe wa kitaifa lakini ikashindikana,  na badala yake Watanzania sasa tuna muziki wa Mduara ambao umekuwa kama mtindo wa muziki wetu kwa sababu zifuatazo.
Kwanza, ni mtindo halisi wa Kitanzania uliochipuka kutoka mahadhi ya kimwambao ya Tanzania. Pili, ndiyo mtindo pekee uliowahi kutumiwa na bendi nyingi baada ya kuasisiwa na ‘mabingwa’ wa muziki wetu, wana Njenje, The Kilimanjaro Band.
Baada ya bendi hiyo kuuasisi, mtindo huo, tayari umepigwa na bendi kama TOT Plus, Chuchu Sound, Pamo Sound, Inafrika Band, wana mipasho kadhaa na mwanamuziki mahiri lakini asiyethamini kiwango chake kikubwa cha muziki, Bob Haisa.
Sababu ya tatu ni kwamba mtindo huo umekuwa wa kupigwa na bendi nyingi, vikundi vingi na wanamuziki wengi si kwa kulazimisha bali kwa mapenzi tu ya mashabiki wa muziki wa Tanzania.
Kapteni Komba awali alikuwa mwalimu wa shule ya msingi kabla ya kuingia jeshini na kuwa kiongozi wa kikundi cha maonesho cha jeshi na baadaye Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akamshawishi aachane na jeshi na kujiunga na CCM wakati wa mfumo wa vyama mingi ulipoingizwa mwaka 1992.
“Mzee Mwinyi ndiye aliyenifanya niache jeshi wakati huo nikiwa na cheo cha ukapteni. Aliniomba nikisaidie chama kwa kuanzisha kikundi ambacho lengo lake lilikuwa kukipigia debe CCM,” aliwahi kusema hivyo Kapteni Komba.
Ameshiriki kampenzi za marais Ally Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa na aliye madarakani hivi sasa, Jakaya Mrisho Kikwete. Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi hadi kifo kinamchukua.
Licha ya siasa Kapteni Komba alikuwa anamiliki shule na pia alikuwa na biashara kadhaa.
Mwaka 2012 Komba aliwahi kupelekwa India kwa matibabu ambapo alifanyiwa upasuaji wa nyonga baada ya kupata ugonjwa uliosababisha mifupa kusagana sehemu hiyo ya nyonga.
Baada ya kurejea nchini alisema upasuaji huo ulichukua saa tano na ulifanyika katika Hospitali ya Apollo, India na alikanusha kuwa alikuwa na ugonjwa wa figo.Ugonjwa uliomuua ni shinikizo la damu ambalo lilikuwa likimsumbua kwa muda mrefu.
..marehemu Komba akiongea na wanahabari nyumbani kwake Mbezi tangi Bovu akielezea kuimarika kwa afya yake aliporejea kutoka India kwenye matibabu, Julai 27, 2012.
Marehemu Komba ameacha mjane, Bi Salome, ambaye ni mwalimu kitaalumu na watoto kadhaa. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi- ameen!

KAULI YA MWISHO YA JOHN KOMBA

Alichofanya Kapteni Komba kwa familia yake siku mbili kabla ya kifo chake.

capt KombaKifo cha Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa CCM kapteni John Komba ambaye amefariki dunia akiwa hospital ya TMJ jana 28 kilitanguliwa na kitu ambacho kinadhaniwa kama kilikua ni ishara ya siku yake ya mwisho.
Claudia John Komba ambaye ni mtoto wa 9 kati ya watoto 11 wa marehemu John Komba amesema nna kuelezea baadhi ya vitu ambavyo kwao imekua kama kauli ya mwisho kutoka kwa Baba yao ambayo aliitoa siku ya sherehe ya kuzaliwa kwake.
Claudia ‘Taarifa ilinifikia mida ya saa 9 akasema anajisikia vibaya ambapo wakati yupo njiani akawa anaweweseka sana, tulipofika TMJ hospital walipofanya vipimo walisema ameshafariki’
Claudia John Komba: ‘Zilikuwepo baba alikua amekaa ilikua mida ya asubuhi akawa analalamika anajisikia vibaya tukampeleka hospitali, tukagundua sukari imepanda sana na presha imepanda sana, akatolewa akawa anaendelea vizuri’
‘Juzi tarehe 26 february ilikua siku yangu ya kuzaliwa, akaita watoto wote akasema nataka kufanya birthday sababu birthday nyingi huwa zinanipita nakua nipo nje, akatukusanya watoto wote, aliongea maneno ya mwisho akatusihi watoto tupendane tusiweke  matabaka kwamba huyu mdogo huyu mkubwa alisema yeye hana mkataba na Mungu’.

AMKA NA MAGAZETI NA KUMEKUCHABLOG

KURASAMWANZO MWISHO ZA MAGAZETI YA LEO MARCH 01 YANALETWA KWENU KWA HISANI KUBWA YA KITUO CHA ELIMU CHA CANDLE EDUCATION CENTRE KILICHOPO TANGA MKABALA NA BANK YA CRDB, WANAFUNDISHA KOZI MBALIMBALI KIDATO CHA PILI HADI CHA SITA. WAKO NA WALIMU WALIOBOBEA MASOMO KWA MASOMO YOTE, SIMU 0715 772746


Kama kawaida tangakumekuchablog inakuletea kurasa za mwanzo mwisho za magazeti kila siku kupitia www.tangakumekuchablogspot.com

MATOKEO LIGI KUU ENGLAND JANA

Nimekuwekea matokeo ya EPL hapa, yakiwemo ya Man UTD vs Sunderland

(null)
Baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo yasiyo ya kuridhisha katika ligi kuu ya England tangu kuanza kwa mwaka 2015, klabu ya Manchester United leo iliwakaribisha kwenye uwanja wao wa nyumbani Sunderland.
Mchezo huo wa raundi ya pili ya EPL, umemalizika muda mfupi na kikosi cha Louis van Gaal kimepata ushindi wa magoli 2-0.
Wayne Rooney alifunga magoli yote mawili na kuweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya ligi hiyo kufunga magoli zaidi ya 10 katika misimu 11 mfululizo.
Matokeo mengine kwenye ligi hiyo yapo kama inavyoonekana kwenye picha:
(null)

TAARIFA YA HIVI PUNDE

Taarifa iliyonifikia kuhusu MBUNGE aliyefariki leo Dar es Salaam

mshumaaMbunge wa Mbinga na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa CCM, Kapteni John Komba amefariki leo, taarifa iliyotolewa kwenye ukurasa wa Twitter wa Chama cha CCM, hajawamesema chanzo cha kifo chake.
Katika Tweet hiyo imeandikwa kwamba Mbunge huyo amefariki akiwa hospital ya TMJ.
Marehemu Kapteni Komba alikuwa kiongozi wa bendi ya TOT.
Naendelea kufuatilia taarifa hii na kila kitakachonifikia nitakuwa nakufahamisha pia hapahapa.

Komba
Kapteni John Komba enzi za uhai wake akiwa kwenye kikao cha Bunge.
ripkomba

KAPTEN JOHN KOMBA AFARIKI

Taarifa kuhusu kifo cha Kapteni Komba.

mshumaaMbunge wa Mbinga na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa Ccm Kapteni John Komba amefariki leo,taarifa iliyotolewa kwenye mtandao na Chama Cha Mapinduzi CCM haijaeleza chanzo cha kifo chake na amefariki akiwa kwenye hospital ya TMJ,Kapteni Komba pia alikua kiongozi wa bendi ya TOT.
ripkomba
 Hutopitwa na habari na niko tayari kukupatia wakati wowowte kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

SOMA HABARI KUU ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO,TZ

Uchambuzi huu unaletwa kwenu kwa hisani Kubwa ya kituo cha elimu cha Candle Education centrte. Mabingwa wa ufaulishaji kidato cha pili hadi cha sita. wapo Tanga mkabala na CRDB, 0715 772746

Magazeti
JAMBO LEO
Aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM Dar, John Guinita na Mwenyekiti wa Chama hicho Singida, Mgana Msindai wameanga kumfikisha Mahakamani Mkuu mpya wa Wilaya ya K’ndoni, Paul Makonda kwa kuwatolea lugha za kashfa huku wakimtaka Rais Kikwete kutengua uteuzi wa DC huyo.
Guinita amesema amefikia uamuzi kenda Mahakamani baada ya Makonda kugoma kuwaomba radhi; “Tulimtaka Makonda atuombe radhina kufuta kashfa zake dhidi yetu kupirtia vyombovya habari kwa kwa wanasheria wetu.. Makonda alijibu kuwa ametumwa na chama na alikuwa anafanya kazi ya chama..”—Guinita.
Mwanasheria kutoka BM Attorneys amesema kisheria maneno ya Makonda ni ya udhalilishaji hivyo ni lazima achukuliwe hatu.
JAMBO LEO
Mmoja wa vigogo waliosimamishwa kazi Shirika la Ndege ATCL amesema kwamba katika tuhuma za ubadhirifu wa fedha za Shirika hilo alikuwa na baadhi ya vigogo wengine waliopo kwenye idara nyeti lakini wenzake wamemgeuka.
Mmoja ya viongozi hao (akamtaja) alichukua mgao wa kwanza Novemba19 mwaka 2014, .. mwenzetu alichukua dola 12,100 na Januari 19 mwaka huu akachukua tena dola 2,700”, amenukuliwa kigogo huyo.
Tulikubaliana kuwa tutauificha menejiment kuhusu uchotaji huo wa fedha na kasha waowawashe moto kuishitaki Kampuni hiyo ya Kenya kwa kukiuka mkataba na kuidhalilisha kampuni yetu..
Kigogo huyo anasema wenzake walimgeuka na kumfanya yeye mbuzi wa kafara wakati wanafahamu ukweli.
JAMBO LEO
Madiwani wa Manispaa ya Dodoma walilazimika kuvunja Kikao cha Baraza lao na kutoka nje kwenda kumwadhibu kibaka aliyeiba kofia za gari ya mtangazaji wa TBC, Victoria Patrick lililokuwa limeegeshwa nje ya Ukumbi wa Manispaa.
Kibaka huyo, Ladislaus Haule mkazi wa Kizota, alikurupushwa na kupewa kichapo kabla ya kukabidhiwa mikononi mwa Polisi.
HABARI LEO
Kobe wadogo 250 wamekamatwa Uwanja wa Ndege wa Abeid Aman Karume wakiwa wanasafirishwa kwa njia ya magendo kwenda Malaysia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkadam Khamis Mkadam amesema; “Tumekamatra kobe 250 wakiwa wamehifadhiwa vizuri katika masanduku yakiwa yameingizwa maembe ndani yake tayari kusafirishwa kwenda Malaysia
Kamanda huyo amesema kwa sasa hawako tayari kumtaja mtuhumiwa kwa kuwa itaharibu upelelezi wao.
Kumekuwa na matukio ya wizi wa kobe kutoka Z’bar kwenda sehemu nyingine duniani ikiwemo Tanzania Bara ambapo wanyama hao wako kwenye orodhaya viumbe vilivyo hatarini kutoweka duniani nawanalidhwa na sheria za Kimataifa.
HABARI LEO
Ndege ya Jeshi la Wananchi JWTZ iliyokuwa katika mazoezi imeanguka jana na kuteketea moto huku rubani wake akiumia wakati akijiokoa Uwanja wa Ndege Mwanza.
Taarifa kutoka Kurugenzi ya Habari na Uhusiano ya Jeshi hilo Dar imesema ndege hiyo iliwaka moto baada ya ndege mnyama kuingia katika injini yake moja wakati ikiruka hivyo imeungua moto katika hali ya kawaida.
Ajali hiyo ilitokea wakati ndege hizo zikiwa kwenye mazoezi, Rubani Meja Peter Lyamunda alipoona ndege inawaka aliruka kwa kutumia vifaa maalum na hakupata jeraha kubwa zaidi ya kuumia mguu.
TANZANIA DAIMA
Vijana ambao wanadaiwa kuwa ni ndugu wa Mwalimu wa Kibasila, Gaudensia Albert aliyeishi na kinyesi kwa muda wa miaka miwili juzi walikwenda kudai vyombo vilivyokuwa vimehifadhi uchafu huo.
Mwenyekiti wa mtaa, Yahya Bwanga amesema; “Juzi usiku walikuja vijana kwenye Ofisi yetu ya Serikali ya Mtaa wakati mimi sikuwepo .. walimkuta mjumbe akawahoji wakaonekana wamekuja kuchukua vile vyombo vilivyokuwa na uchafu kwamba walitumwa na yule dada..
Bwanga amesema waliwajibu kwamba vyombo vile havikuwepo kwa kuwa kazi ya kuteketeza uchafu huo ilifanywa na Manispaa.
Hapa ndipo penye utata, juzi tumeambiwa kuwa yuko Muhimbili Muhimbii anapimwa akili leo tunaambiwaanadai vyombo vyake.. tumewaambia waende Manispaa..”Bwanga.
Mwalimu huyo hakuweza kupatikana kwa kuwa tangu siku ya tukio hilo simu yake imekuwa ikiita bila kupokelewa.
TANZANIA DAIMA
Kauli ya Prof. Anna Tibaijuka kuwa shilingi mil. 10 ilikuwa hela ya mboga imezua gumzo kila mahali Dodoma ambapo kila kona ya kijiwe kulikuwa na mabishano na kila mmoja akisema lake kuhusu kauli hiyo wengine wakisema ni ya udhalilishaji wa Serikali na kuwadharau Watanzania.
Kweli sasa Watanzania tunatakiwa kutambua kuwa hatuna viongozi na hizi sasa ndizo dalili tosha za kufanyika mabadiliko, haiwezekani kiongozi ambaye anatuhumiwa kutafuna mabilioni ya fedha bila aibu anasema kuwa sh. Mil 10 ni kwa ajili ya kununua mboga”—alisema mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Ally.
Dada mmoja mjasiriamali alisema; “ Inasikitisha kumuona dada mbunge huyo anavyowabeza Watanzania , sh. Mil. 10 akanunue mboga, mboga gani hiyo? Mimi hapa sijui kama nitakuja kuzipata katika maisha yangu..”—Catherine Mhinte.
TANZANIA DAIMA
Waziri wa Ujenzi Dk. Magufuli amefanya ukaguzi wa Kivuko kipya cha Mv Dar es Salaam kitakachofanya safari kutoka Dar kwenda Bagamoyo ambapo kitasaidia kuondoa kero ya usafiri inayosababishwa na foleni.
Kivuko kimenunuliwa kwa fedha za Watanzania.. ni vema wakatumia rasilimali yao kwa kulipa hela kidogo na wakafaidika, pia wawahi sehemu zao za majukumu”—Dk. Magufuli.
Waziri Magufuli amesema Rais Kikwete atakizindua na ndani ya siku 10 mpaka 15 kitakuwa kimeanza kazi hukuakiahidi kushughulikia changamoto mbalimbali zinazokikabili kivuko cha Mv Magogoni.
MWANANCHI
Ujenzi wa majengo marefu kila kona ya Dar kunaliweka Jiji katika hali mbaya iwapo majanga yatatokea na hivyo kudaiwa kusababishwa maafa makubwa iwapo majanga yatatokea.
Katika kongamano lililofanyika kujadii ujenzi wa majengo na nyumba lililoandaliwa na Bodi ya Wahandisi, Profesa Kumbwaeli Salewi alisemahali sio nzuri Dar kutokana na ujenzi wa maghorofa pasipo kuweka maeneo ya maegesho ya magari, huku wengine wakisema kwamba maeneo kama ya Mitaa ya Samora na barabara ya Bibi Titi ilitakiwa kuwa maeneo ya wazi.
Wataalamu hao wameshauri kwamba weledi unahitajika ili madhara ya maafa yasiwe makubwa na pia kuangaliwa kwa mfumo wa utendaji ili kulinda watu na mali zao.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

Friday, February 27, 2015

YALIYONIKUTA TANGA SEHEMU YA (21)



HADITHI

YALIYONIKUTA TANGA (21)

IIPOISHIA TOEO IIOPITA

“Sawa. Leo kamilisha taratibu za kuanza likizo, kesho utaondoka” afande wangu aliniambia.

“Nashukuru afande”

Nikamuaga na kutoka.

Siku ya pili yake nikaanza likizo yangu. Na siku ya tatu nikaondoka kwenda Dar nikiwa nimekichukua kile kisanduku cha dhahabu. Nilikitia kwenye begi langu.

Nilipofika Dar siku iliyofuata nikatafuta usafiri wa kuelekea Kagera. Mpaka ninafika kijijini kwetu ilinichukua siku mbili. Japo nilikuwa nimekutwa na madhila huko Tanga, nilipata furaha kukutana tena na wazazi wangu pamoja na ndugu zangu ambao tuliachana kwa karibu miaka mitatu iliyopita.

Iliuwa ni siku iliyofuata nilipowakusanya ndugu zangu wawili ambao walikuwa wakubwa zangu pamoja na wazazi wangu na kuwaeleza mkasa uliokuwa umenitokea huko Tanga.

Niliwaeleza wazi makosa ambayo tuliyafanya mimi na Sajenti Erick ya kumbambikia kesi mwanamke ambaye alikuwa ni jini baada ya kukataa kutupa rushwa. Lakini nilijitetea kuwa aliyepanga mpango huo alikuwa mkuu wangu wa kazi ambaye alichinjwa kama kuku.

Pia nilificha kuwaeleza habari ya kile kisanduku cha dhahabu ambacho nilikuwa nimekiiba nyumbani kwa yule mwanamke na ambacho nilikwenda nacho Kagera.

Baada ya kuwaeleza mkasa huo ambao uliwashangaza na kuwatia hofu, wazazi wangu waliniambia ni lazima tutafute mganga tumueleze suala hilo halafu tumsikilize atatuambia nini.

SASA ENDELEA

Baada ya mazungumzo yetu mama alinichukua tukaenda kwa mganga. Mganga mwenyewe alikuwa kijiji cha pili na tulikwenda kwa miguu.

Wakati tunatembea pole pole, mama aliniambia nilifanya vyema kuwahi kurudi kijijini hapo na kuwaeleza mkasa huo kwani kama ningechelewa majini hao wangenichinja kama aivyochinjwa Sajenti Erick.

“Tangu zamani tulikuwa tunasikia sifa za mji wa Tanga, ni mji wenye majini wa hatari. Kumbe wengine wanaishi na binaadamu na wanafanya biashara za dhahabu!” Mama aliniambia.

“IIitokea bahati kwamba likizo yangu ilikuwa ipo tayari, nilicheleweshwa na hayo matatizo tu”

“Bahati yako mwanangu”

Tulipofika kwa mganga nilishangaa kukuta mganga mwenyewe niiyesifiwa kuwa hodari kwa matatizo ya majini alikuwa mwanamke tena akiwa bado msichana.

Hatukukuta watu, tulikuwa ni sisi tu. Baada ya kusalimiana naye alitukaribisha ndani kwani tulimkuta nje ya nyumba yake.

“Tumekuja tuna shida” Mama alianza kumwambia mganga huyo mara tu tulipoingia kweye chumba chake cha uganga kilichokuwa uani mwa nyumba yake.

“Shida gani?” mwanamke huyo akatuuliza.

“Wewe ndiye mtaalamu, tunataka utuambie shida yetu” Mama akamwambia.

“Mimi si mtaalamu, mimi ni mtumishi tu wa wenyewe. Ngojeni niwaite mzungumze nao”

Mwanamke huyo baada ya kutuambia hivyo alichukua upande wa kaniki akajifunika kisha akanusa ugoro. Baada ya kuunusa mara tatu alipiga chafya kisha akatikisa kichwa chake kwa mfululizo.

Wakati anatikisa kichwa alitupa mkono na kutusalimia kwa lugha ya kikwetu ambayo ndiyo iliyokuwa ikitumika zaidi pale kijijini. Lakini wakati ule sauti yake ilikuwa imebadilika na kuwa ya kiume.

Akatuambia kwamba yeye  ndiye mganga mwenyewe na amekuja kusikiliza shida yetu.

“Mimi ni jini wa kiti, mwenye uganga huu. Nataka kusikiliza shida zenu” akatuambia.

“Tunataka ramli” mama akamwambia.

“Oh mnataka ramli…mtapata” akatuambia na kutazama juu ya dari ya miti ya chumba tulichokuwemo.

Aliangalia boriti za ile dari kwa sekunde kadhaa kama aliyekuwa akiangalia kitu kisha akakishusha kichwa chake na kututazama.

“Ramli inakwenda kwa kijana” akatuambia.

“Taire” Mama alitumia neno la kinyumbani lenye maana ya neno hilo taire.

Mwanamke huyo aliinua tena kichwa chake, safari hii hakuchelewa sana akakishusha taratibu.

“Nimeona” akatuambia na kuongeza.

“Nimeona matatizo makubwa sana, yametokea mbali na amekuja nayo hapa”

Mimi na mama tukatazamana.

“Matatizo gani?” Mama akauliza haraka.

Mganga akatazama tena juu.

“Wewe na mwenzako mlifanya makosa, naona damu nyingi…” akatuambia baada ya kukishusha kichwa chake kisha akatazama tena juu.

Iikuwa kama vile pale juu ndipo alipokuwa anasoma habari zetu.

“Mtu mmoja ameuliwa na mmoja amechukua mali, ile mali ni ya majini” mwanamke huyo aliendelea kutuambia.

Tukanyamaza kimya huku tukiendeea kumsikiliza. Niishayatafsiri maneno yake kwamba mtu aliyeuliwa ni Sajenti Erick na aliyechukua mali ni mimi. Mali ilikuwa ile dhahabu iliyokuwemo kwenye kisanduku.

Mwanamke huyo baada ya kutazama juu alishusha kichwa chake na kunitazama mimi.

“Hebu nieleze, nini kimetokea” akaniambia.

Kwa vie aishaigusia habari yenyewe nikaona nimueleze. Nikamueleza.

Mwanamke huyo akapiga mluzi wa mshituko.

“Hatari!” akasema na kuongeza.

“Wewe pia ungekufa. Umri wako bado mrefu”

Akaendelea kutuambia.

“IIe nyumba inakaa majini. Mwenyewe amekwishakufa. Majini wa pwani wanafanya biashara. Wewe unapenda sana kutongoza wasichana. Sasa umetongoza jini. Alikuwa anakutafuta akukomeshe”

Nilimuelewa alichomaanisha. Alikuwa na maana kwamba mimi napenda kutongoza kwa sababu nilimtongoza yule msichana wa kijini kwenye simu, kumbe msichana mwenyewe naye alikuwa ananitafuta baada ya kumkamata mama yake na kumbambikia kesi ya uongo.

“Sasa nifanye nini ili niweze kusalimika” nikamuuiza mwanamke huyo.

Niipomuuliza hivyo alitazama juu. Baadaye aliurudisha chini uso wake akatuambia.

“Wenyewe wanataka dhahabu yao”

“Hakuna namna ya kufanya nikabaki nayo mimi?” nikamuuliza.

“Mimi utanipa nini?”

“Nitakupa pesa utakayoitaka”

“Sawa. Kesho lete kile kisanduku, nitakufanyia uganga wake. Hao majini hawatakufuata tena na wewe utabaki na dhahabu yako”

“Hivyo ndivyo ninavyotaka. Basi tutakuja kesho. Nitakileta na kile kisanduku” nikamwambia.

Yule jini alipoondoka, yule mwanamke alituuliza tulichozungumza, tukamueleza.

“Sasa kesho mtakuja?” akatuuliza.

“Tutakuja kesho asubuhi” nikamjibu.

“Ngoja nikupe dawa yangu” akatuambia na kuinuka.

Aikwenda pembeni mwa chumba hicho. Alikuwa ameweka makorokoro yake ya kiganga. Akachukua pembe moja ya mnyama aliyokuwa ameifunga kitambaa cheusi. Ule upande uliokuwa na shina la ile pembe aliukung’uta kwenye kiganja chake, ukatoka unga mweusi.

Alinifungia unga huo kwenye kikaratasi.

“Usiku utatia dawa hii kwenye maji yako ya kuoga halafu utaoga” akaniambia.

Nikakichuku kile kikaratasi na kukitia mfukoni.

“Niitie yote au niibakishe?” nikamuuliza.

“Tia yote”

“Sawa”

Je nini kitaendelea? Usikose kuendelea na hadithi hii katika toleo lijalo. 
Niko tayari kukutumia habari inayonifia na niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com