Friday, March 31, 2017

SIMULIZI, NILIKIONA CHA MOTO URITHI WA BABU SEHEMU YA 2

SIMULIZI
 
NILIKIONA CHA MOTO URITHI WA BABU 2
 
ILIPOISHIA
 
“Kuhusu mali za marehemu. Babu yangu alikuwa tajiri lakini katika kumbukumbu zake nimekuta hati ya nyumba moja aliyokuwa anaishi pamoja na hati ya gari alilokuwa akitumia”
 
“Sasa kama hakuna hati wala nyaraka zozote utazijuaje mali zake nyingine?”
 
“Kwanza hizo nyaraka zitakuwa zimekwenda wapi?”
 
“Nenda kapekue vizuri. Inaweekana aliuza baadhi ya mali zake”
 
Kutokana na ushirikiano alionipa wakili huyo kutafiti mali alizokuwa akimiliki marehemu babu yangu, tuligundua kuwa mpaka marehemu anafariki duniani hakuwa na mali yoyote aliyoacha zaidi ya nyumba aliyokuwa akiishi pamoja na gari lake.
 
Hata baada  ya kufungua mirathi mahakamani na  kuthibitishwa kuwa mimi ndiye mrithi wa marehemu, sikukuta pesa ya maana katika akaunti yake ya benki. Akaunti yake ilikuwa na shilingi elfu kumi tu.
 
SASA ENDELEA
 
Kwa Kweli mimi na wakili wa marehemu tulishangaa sana. Kila mtu alikuwa akifahamu kuwa  Mzee Fumbwe alikuwa ni miongoni mwa matajiri wazawa wa jiji la Dar es Salaam. Jinsi alivyokufa akiwa masikini ni jambo ambalo halikueleweka.
 
Katika utafiti nilioufanya baadaye niligundua kuwa Mzee Fumbwe alikuwa ameuza baadhi ya mali zake zikiwemo nyumba na  vituo vya mafuta siku chache kabla ya kufariki dunia.
 
Lakini uchunguzi wangu ulishindwa kubaini marehemu alipeleka wapi pesa zake kwani benki hakukuwa na kitu.
 
Kwa kipindi cha karibu wiki mbili nilikuwa nikiendelea kufanya utafiti kwenye nyaraka za marehemu ili kupata uhakika kwamba kweli babu hakuwa na kitu.
 
Nikaja kugundua kitabu cha kumbukumbu cha marehemu ambacho alikuwa akiandika mambo yake. Nilipopekua karasa na kitabu hicho niliona kulikuwa na watu ambao walikuwa wakifanya biashara na babu na kwamba babu alikuwa akiwadai wafanyabiahara hao pesa nyingi.
 
Nilikuta majina ya wafanya biashara wanne. Katika watu hao ni mmoja tu aliyekuwa akiishi hapo Dar, wengine walikuwa wakiishi nchi za nje. Mwenyewe aliandika kama ifuatavyo
 
Abdul Baraka wa Mbezi Dar es Salaam. Namdai dola milioni moja.
 
(Aliandika na namba ya simu yake)
 
Isaac Chusama wa Harare Zimbambwe. Namdai dola milioni mbili na laki tano.
 
(Aliandika namba ya simu yake na mtaa aliokuwa anaishi)
 
Benjamin Muhoza wa Gaborone Botswana. Namdai dola milioni moja na laki tano.
 
(Aliandika namba ya simu yake na mtaa aliokuwa akiishi)
 
Dumessan Dube wa Cape Town Afrika Kusini. Namdai dola milioni tatu.
 
(Aliandika namba ya simu yake na mtaa aliokuwa akiishi)
 
Hapo nikajua kuwa marehemu babu alikuwa akidai fedha nyingi kwa watu waliokuwa wakiishi nje ya nchi.
 
Kitabu hicho cha kumbukumbu kiliendelea kunjulisha siri ya babu ambayo nilikuwa siifahamu. Babu alikuwa akifanya biashara ya madini. Tena madini ya Tanzanite na kwamba alikuwa akiwauzia wafanya biashara hao.
 
Kumbukumbu za nyuma za kitabu hicho zilionesha ameshawahi kuwauzia madini wafanyabiashara hao kwa thamani ya dola ya Kimarekani. Na kwamba alikuwa akilipwa kwa awamu.
 
Nikajiuliza babu alikuwa akipata wapi madini mengi kiasi cha kumpatia mamilioni hayo ya dola?
 
Swali jingine nililojiuliza ni wapi babu yangu alikokuwa anaficha fedha hizo, isingewezekana afe akiwa hana kitu.
 
Niliitafuta paspoti yake na nikaipekua. Nikagundua kuwa mara kwa  mara alikuwa akitembelea Zimbabwe, Botwana na Afrika kusini.
 
Nilipopekua zaidi kwenye mafaili yake nikaipata mikataba yake na wafanya biashara hao. Alikuwa amelipwa pesa nusu na nusu alikuwa akiwadai.  Tarehe ya kuwafuata wafanya biashara hao wammalizie deni lake ilikuwa imeshapita.
 
Nikajiambia kama nitafanikiwa kupata fedha hizo nitakuwa tajiri mkubwa hapa Dar kwani kwa pesa za Kitanzania dola hizo zilikuwa ni mabilioni ya shilingi.
 
Kwa vile marehemu aliandika namba za simu zao, nikaanza kumpigia Abdul Baraka aliyekuwa hapo Dar. Nilimpigia kwa kutumia laini ya marehemu. Simu yake haikupatikana.
 
Nikampigia Isaac Chusama wa Harare. Simu  iliita kwa sekunde chache kisha ikapokelewa.
 
Nikashangaa kusikia sauti ikinisalimia kwa Kiswahili.
 
“Habari yako Bwana Fumbwe?”
 
“Nzuri lakini mimi siye Bwana Fumbwe. Bwana Fumbwe amefariki wiki tatu zilizopita, mimi ni mjukuu wake. Naitwa Kassim Fumbwe”
 
“Heh! Mzee Fumbwe amefariki?”
 
“Amefariki. Hivi sasa ni wiki tatu zimeshapita”
 
“Oh pole sana”
 
“Asante. Sasa kumbukubu za babu zinaonesha kwamba alikuwa akikudai dola milioni mbili na laki tano. Na mkataba wa makubaliano yenu ninao hapa”
 
“Ndio ni kweli ananidai”
 
“Kwa vile tarahe ya kumlipa imeshapita, ninataka nije Harare unipatie hizo fedha. Mimi ndio mrithi wake”
 
“Sasa nitakuaminije Bwana Fumbwe?”
 
“Nitakuja na hati zote zikiwemo hati za mahakama zinazoonesha kwamba mimi ndiye mrithi wa marehemu, cheti cha kifo chake na mikataba ya makubaliano yenu”
 
Pakapita kimya cha sekunde kadhaa kabla ya sauti ya mtu wa upande wa pili kusikika tena.
 
“Unatarajia kuja lini?”
 
“Baada ya siku mbili tatu. Hivi sasa ninajiandaa kwa safari”
 
“Utakapokuja utanijulisha”
 
“Sawa”
 
Isaac akatangulia kukata simu.
 
Hapo hapo nikampigia Benjamin Muhoza. Nilishukuru naye alipopokea simu.
 
ITAENDELEA kesho usikose nini kitajiri katika Uhondo huu
 
 

AMKA NA MAGAZETI NA FREYS LUXURY COACH TANGA HADI SINGIDA KILA SIKU, 0622 292990


MWILI WA KIM JONG WAWASILI KOREA KASKAZINI

Bwana Kim ni ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea KaskaziniRaia wa Malaysia wakaribishwa nyumbaniMwili wa Kim Jong-nam, ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, umewasili nchini Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini ilikuwa imeomba kupewa mwili huo lakini haikuwa imesema ulikuwa ni wa nani.
Mwili huo ulitolewa kwa Korea Kaskazini kama sehemu ya makubaliano ambapo raia 9 wa Malaysia, waliizuiwa kuondoka Korea Kaskazini waliwasili nyumbani.
Nchi hizo mbili zimekuwa kwenyr mzozo wa kidiplomasia kufuatia mauaji ya Kim, kwenye uwanja wa Kuala Lumpur mwezi uliopita.
Nchi hizo mbili zimekuwa kwenyr mzozo wa kidiplomasia kufuatia mauaji ya Kim, kwenye uwanja wa Kuala Lumpur mwezi uliopita.
Kila nchi ilikuwa imewapiga marugufuku raia wa nchi nyingine kuondoka.
Raia watatu wa Korea Kaskazini wameruhusiwa kuondoka malaysia, kwa mujibu wa mkuu wa polisi wa nchi hiyo.
Korea Kaskazini inashukiwa pakubwa kuhusika kwenye kifo cha  Kim, kwa kutumia kemikali akiwa uwanja wa Kuala Lumpur.
BBC

SPACE X YARUSHA TENA ROKETI KWA MARA YA PILI ANGA ZA JUU

Satelite ya SES-10 iliyosafirishwa na Falcon 9 iliundwa nchini Uingereza na UfaransaFalcon 9 ikiwa tayari kupaa kutoka kituo cha Kennedy Space CenterKampuni ya kuunda roketi za wanasayansi wa anga za juu ya SpaceX iliyo na makao yake huko Carlifonia, Marekania, imefanikiwa kurusha tena roketi yake kwa kutumia moja ya roketi zake aina ya Falcon 9.
Awamu ya kwanza ya roketi hiyo ambayo ilitumika tena miezi 11 iliyopita, ilitumiwa kutuma satellite ya mawasilano kuenda kwa mzingo wa dunia, kutoka kituo cha safari za anga za juu cha Kennedy Space Center.
Hiyo ni hatua kubwa wa kampuni ya SpaceX katika majaribio ya kutumia roketi mara ya pili.

FIFA YAIDHINISHA TIMU 48 KOMBE LA DUNIA

Ujerumani ndio bingwa mtetezi wa kombe la duniaChama cha soka duniani FIFA kimepanga kuwepo kwa michezo sita ili zipatikane timu zitakazoingia katika fainali za kombe la dunia mwaka 2020.
FIFA imefafanua ni kwa namna gani timu 48 zitaweza kushiriki michuano hiyo.
Rais wa shirikisho la soka Ulaya Aleksander Ceferin amesema kuwa amefurahishwa na hatua hiyo na nchi za Ulaya zitawakilishwa vyema.

UCHAGUZI CHADEMA KANDA YA KASKAZINI WAAHIRISHWA

 CHAMA CHA Demokrasia na  Maendeleo (Chadema), kimeahirisha Uchaguzi wa uongozi kanda ya Kaskazini kwa madai ya kuwepo kwa dosari baada ya kubaini kufuatia ziara ya majimbo 35 yaliyotembelewa na viongozi na kada wa Chama hicho kwa siku mbili mfululizi akiwemo kiongozi wa Taifa, Freeman Mbowe.
Viongozi na makada mbalimbali akiwemo Freedik Sumaye alikuwepo kwenye mkutano wa baraza la Uongozi mjini Tanga kushuhudia uchanguzi kama ungelikuwepo.
Katibu wa Chama kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa alithibitisha kuahirishwa kwa uchaguzi huo.


Thursday, March 30, 2017

HADITHI, NILIKIONA CHA MOTO URITHI WA BABU SEHEMU YA 1

SIMULIZI
 
NILIKIONA CHA MOTO URITHI WA BABU, SEHEMU YA (1)
 
Jina langu ni Kassim Fumbwe. Nina umri wa miaka ishirini na minane. Mkazi wa jiji la Dar es Salaam.
 
Wazazi wangu walifariki dunia wakati nikiwa mdogo. Nakumbuka tulikuwa tunasafiri kutoka Dodoma kuja Dar, basi tulilokuwamo likagongana na lori uso kwa uso.
 
Baba yangu na mama yangu pamoja na abiria wengine kadhaa walifariki hapo hapo. Mimi nikanusurika.
 
Nakumbuka nilipata jeraha dogo tu kwenye mkono wangu wa kushoto baada ya kukatwa na vioo vya dirisha vilivyokuwa vimevunjika.
 
Babu yangu mzaa baba, Mzee Fumbwe Limbunga alipopata habari ya ajali ile alitoka Dar kwa gari lake akaja Morogoro. Majeruhi wa ajali ile tulikuwa tumelazwa katika hospitali ya Morogoro.
 
Mimi sikuwa nimeumia sana lakini kwa vile wazazi wangu walikuwa wamefariki ilibidi nibaki hapo hospitali ili niweze kutambuliwa na kuchukuliwa na ndugu zangu.
 
Babu alipokuja akanichukua. Aliichukua pia miili ya marehemu baba yangu na mama yangu.
 
Siku ya pili yake habari za ile ajali zilichapwa kwenye magazeti. Kila gazeti lilikuwa limechapa picha yangu ikielezea jinsi nilivyonusurika kimiujiza.
 
Baada ya msiba huo, nikawa ninaishi na babu. Babu yangu alikuwa tajiri lakini alikuwa hana mke. Aliachana na mke wake tangu alipokuwa kijana na hakutaka kuoa tena.
 
Kwa hiyo alinitafutia mtumishi wa kunihudumia kwa kila kitu ikiwa ni pamoja na kunipeleka shule. Nilipoanza masomo ya sekondari babu akanihamisha katika nyumba yake nyingine. Zote zilikuwa Tegeta lakini zilikuwa mitaa tofauti.
 
Ile nyumba aliyonihamishia upande mmoja ilikuwa na mpangaji, upande mwingine ndio niliokaa mimi.
 
Kila jumatatu babu alikuwa akinipa pesa za kutumia kwa wiki nzima. Baadhi ya siku nilikuwa ninapika mwenyewe nyumbani na siku nyingine nilikuwa ninakula kwenye mikahawa..
 
Baada ya kumaliza masomo yangu nilipata kazi Morogoro. Lakini babu alinishauri niache kazi nifanye biashara. Aliponipa mtaji nikaacha kazi. Nilifungua maduka matatu ya vifaa vya ujenzi pale Morogoro.
 
Yalikuwa maduka makubwa. Niliajiri karibu wafanyakazi kumi na watano. Kila duka lilikuwa na wafanyakazi watano. Biashara ilianza vizuri. Baada ya miezi sita tu nikaja Dar kununua gari la kutembelea.
 
Sasa nikawa nafikiria kutafuta mke nioe. Sikumaliza hata mwaka mmoja ile kasi ya biashara ikaanza kupungua. Maduka yangu yaliyokuwa yamejaa vitu yakaanza kuwa matupu. Haukupita muda mrefu nikaanza kupunguza wafanya kazi. Mwisho kila duka likabaki na mfanyakai mmoja.
 
Nilifikia mahali nikahisi kuwa pengine sikuwa na nyota ya kujiajiri. Nikajuta kuacha kazi niliyokuwa nayo mwanzo. Ikabidi yale maduka mawili niyafunge nikabaki na duka moja ambalo nililisimamia mwenyewe. Duka hilo nalo likafilisika nikalifunga. Nikawa sina kazi.
 
Nilifikiria kwenda kumueleza babu ili anipe mtaji mwingine lakini nilishindwa kwani nilijua asingekubali tena kunipa pesa zake. Nikauza lile gari. Siku ile nauza gari babu akanipigia simu na kunijulisha kuwa alikuwa anaumwa na alikuwa amelazwa katika hospitali ya Aga Khan.
 
Nikapanda basi kuja Dar. Nilipofika Dar nilikwenda moja kwa moja katika hospitali katika hospitali ya Aga Khan..
 
Vile nafika tu na babu yangu anakata roho. Hata sikuwahi kuzungumza naye lolote.
 
Kifo chake babu hakikunishitua sana kwa sababu alikuwa na mali na mimi ndiye ambaye ningemrithi.
 
Dereva wake nilimkuta hapo hapo hospitali, alinieleza kuwa Mzee Fumbwe alianza kuumwa siku tatu zilizopita lakini usiku uliopita ndio alizidiwa. Presha ilikuwa juu na sukari ilipanda. Hali ikawa mbaya.
 
Kwa kushirikiana na dereva huyo tuliuchukua mwili wa Mzee Fumbwe siku ya pili yake kwa ajili ya maziko. Baada ya maziko nikaanza mchakato wa kukagua mali za marehemu.
 
Nilichokuwa nikikifahamu awali ni kuwa babu yangu alikuwa na maduka kadhaa Dar es Salaam. Alikuwa na vituo vitatu vya mafuta na malori sita.
 
Pia alikuwa na nyumba alizokuwa amezipangisha ambazo sikujua zilikuwa ngapi.Nilikuwa nikijua nyumba mbili tu, ile aliyokuwa akiishi yeye na ile niliyokuwa nikikaa mimi kabla ya kuhamia Morogoro.
 
Mali zake nyingine alikuwa akizijua yeye mwenyewe. Niliingia chumbani mwake nikafungua makabati na kuanza kupekuwa nyaraka zake alizozihifadhi kwa lengo la kutambua mali hizo.
 
Jambo ambalo lilinishangaza, nilikuta hati ya nyumba yake aliyokuwa akiishi na hati za gari alilokuwa akilitumia. Sikukuta hati wala nyaraka nyingine zinazohusu mali zake.
 
Wakili wake nilikuwa namfahamu. Nikaenda ofisini kwake barabara ya Samora na kumjulisha kuhusu kifo cha mteja wake.
 
“Oh mzee amefariki?” akaniuliza kwa mshituko.
 
“Amefariki juzi, tumemzika jana”
 
“Alikuwa mgonjwa?”
 
“Wakati anaumwa mimi nilikuwa Morogoro. Juzi akanipigia simu yeye mwenyewe akaniambia kuwa anaumwa na amelazwa hospitali. Muda ule ule nikapanda gari kuja kumuona. Mpaka nafika Dar nikakuta ameshafariki”
 
“Oh pole sana. Aliwahi kuniambia kuwa mwanawe alifariki dunia”
 
“Mwanawe ni baba yangu. Alifariki mimi nikiwa mdogo”
 
“Kwa hiyo mrithi wake utakuwa wewe. Kwa maana hakuwahi kuandika wasia wowote ila alinieleza kuwa hakuwa na ndugu wala mtoto mwingine isipokuwa mjukuu”
 
Wakili alipoleta suala la urithi akawa amenirahisishia tatizo lililokuwa limenipeleka kwake.
 
“Hilo ndilo lililonileta kwako”
 
“Umefanya vizuri kuja kunifahamisha. Sasa unatakiwa ufungue mirathi mahakamani ili uweze kumrithi babu yako”
 
“Kabla ya kufungua mirathi kuna suala moja ambalo limenishitua sana”
 
“Suala gani?”
 
ITAENDELEA kesho hapahapa tangakumekuchablog, Usikose uhondo huu nini kitaendelea
 

AMKA NA MAGAZETI NA FREYS LUXURY COACH TANGA HADI SINGIDA KILA SIKU, 0622 292990