Saturday, January 31, 2015

POKEA CHETI KAMANDA



Mkurugenzi wa Tangakumekuchablog,Salim Mohammed (kushoto),akitunukiwa cheti cha kuhitimu masomo ya Ulinzi na Usalama Utetezi wa Haki za Binadamu Tanzania  (Tanzania Human Rights Defenders Coalition THRD) kutoka kwa Mratibu wa THRDS ,Onesmo Olengurumwa hafla iliyofanyika Land Mark Hotel jijini Dar es Salaam

FURAHA YA AFRICAN SPORTS KUPANDA DARAJA

 Washabiki na wapenzi wa timu ya African Sports ya Tanga tawi la Wagosi wa ndima Makorora, wakimchuna mbuzi ikiwa ni sherehe ya kufurahia timu yao kupanda daraja na kucheza ligi kuu Tanzania bara baada ya kuifunga timu ya Mlale JKT juzi uwanja wa CCM Mkwakwani.





Washabiki hawa wakimchuna mbuzi ikiwa ni furaha ya timu yao African sports kupanda daraja na mwakani kucheza ligi kuu Tanzania bara

SHETANI AWA KIDHIBITI MAHAKAMANI

Pale ambapo jamaa wanamtaja shetani Mahakamani kwa kesi ya uhusiano wa jinsia moja…

Handcuffs_shutterstock_3
Moja ya ishu ambazo zilikuwa na mijadala mikubwa duniani mwaka 2014 ni suala la ndoa za jinsia moja, mvutano bado ni mkubwa zipo nchi ambazo ziliidhinisha na zipo ambazo zilipiga marufuku kubwa kwenye hiyo, wakapitisha na sheria kali kuzuia ikiwemo nchi ya Uganda.
Story kutoka Nigeria ni kwamba jamaa wawili Edwin Kelechi na Khulid Ibrahim wamefikishwa Mahakamani kwa kosa la kujihusisha na uhusiano wa jinsia moja.
Paul anatajwa kuwa na kosa la kumshawishi Edwin kufanya nae tendo hilo na kumuahidi kumlipa Naira 2000 ambayo ni kama 20,000 Tshs, lakini jamaa hakutimiza ahadi hiyo kitu kilichofanya wapigane na Polisi wakawakamata baadaye wakagundua kuwa walifanya kosa hilo.
Tunaomba tusamehewe kwa kosa hilo, ni shetani alitupitia… Hatutorudia kosa hilo tena,” walijitetea jamaa hao wakiwa Mahakamani, hukumu yao imetajwa kutolewa February 4, 2015.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,www.tangakumekucha.blospot.com

REAL MADRID YAIADHIBU REAL SOCIETED

Wakicheza bila Ronaldo – hiki ndicho Madrid walichoifanya Real Societed

(null)
Ligi kuu ya Hispania maarufu kama La Liga imeendelea tena jana jioni  kwa mchezo ambao ulivihusisha vilabu vya Real Madrid na Real Sociedad.
Mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la Santiago Bernabeu, ulikuwa ndio wa kwanza kwa kocha wa zamani wa Man United – David Moyes katika uwanja huo.
Huku wakicheza bila mshambuliaji wao tegemeo Cristiano Ronaldo ambaye amesimamishwa mechi mbili – Real Madrid  wameiadhibu Sociedad magoli 4-1.
Sociedad ndio walioanza kuziona nyavu za Madrid katika dakika ya kwanza tu ya mchezo lakini dakika mbili baadae Real walisawazisha kupitia James Rodriguez.
Ramos aliongeza lingine dakika ya 36, na Benzema akashindilia misumari ya mwisho dakika ya 51 na 76.
TIMU ZILIPANGWA HIVI
Real Madrid: Casillas, Carvajal, Varane, Ramos, Marcelo, Irrallamendi, Kroos (Khedira 81), James (Jese 74), Isco, Bale, Benzema (Hernandez 81)
Subs not used: Navas, Coentrao, Arberloa, Nacho
Scorer(s): James 3, Ramos 36, Benzema 51, 76
Booked: Irrallamendi 30, Marcelo 70, Khedira 87
Real Sociedad: Rulli, Aritz (Bergara 63), Gonzalez, Inigo Martinez, Yuri, Gorka Elustondo, Ruben Pardo, Xabi Prieto, Granero, Canales (De la Bella 46), Vela (Agirretxe 17)
Subs not used: Finnbogason, Zubikarai, Castro, ZaldĂșa
Scorer(s): Aritz 1,

CHALSEA YAZIDI KUCHANJHA MBUga

Chelsea vs Man City – wamekipiga jana matokeo haya hapa

(null)
Baada ya Liverpool na Manchester United kupata ushindi jana jioni y – vilabu vingine vikubwa kwenye ligi kuu ya Uingereza Chelsea na Man City navyo vilikuwa vikichuana katika vita kugombea uongozi wa ligi hiyo.
Mechi hiyo ambayo ilipigwa jijini London katika dimba la Stamford Bridge imemalizika muda mfupi uliopita huku Chelsea wakiweza kuendelea kuustawisha uongozi wao kwenye msimamo wa ligi.
Matokeo ya mechi hiyo ni sare ya 1-1 ambayo imeendelea kuipa Chelsea uongozi wa pointi 5 zaidi ya Man City wanaoshika nafasi ya pili.
Chelsea walianza kufunga goli kupitia Loic Remy ambaye alimalizia kazi nzuri ya Eden Hazard katika dakika ya 40 – lakini muda mfupi baadae David Silva akaisawazishia City baada ya kumalizia pasi ya Sergio Aguero.
Mpaka mwisho wa mchezo huo matokeo yalikuwa yakisomeka 1-1.

MANCHESTE YALIPIZA KISASI KWA LECEISTER CITY

Je Man U wameweza kurudisha kisasi kwa Leceister? Cheki matokeo hapa

IMG_1311-1.PNG
Kumbukumbu za mchezo wao uliopita – Louis Van Gaal anasema ni kitu ambacho angependa kukisahau, wakiwa wanaongoza kwa magoli 3 mechi ikaishia kwa kufungwa 5-3 na Leicester City.
Leo hii miezi takribani minne tangu mechi hiyo ya kwanza ya EPL kuchezwa, Leceister walisafiri mpaka jijini Manchester kwenda kucheza na Man United.
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Old Trafford jana umemalizika kwa Louis Van Gaal kuiongoza United kuweza kulipa kisasi kwa kuifunga Leceister kwa magoli 3-1.
Magoli ya United yalifungwa na Van Persie, Radamel Falcao na moja la kujifunga kwa Leceister wenyewe.
Mpaka timu hizo zinaenda mapumziko United walikuwa wanaongoza 3-0.
Kipindi cha pili United walipunguza kasi na Leceister wakajaribu kufanya maajabu ya kusawazisha magoli na hata kupata ushindi kabisa lakini siku haikuwa yao – wakaishia kupata goli moja tu lilofungwa na Wasilewski.
MANCHESTER UNITED (4-1-2-1-2): De Gea 6; Valencia 7 (Mata 77, 6), Jones 6.5, Rojo 7, Shaw 7; Blind 7.5; Rooney 7, Januzaj 6.5; Di Maria 7; Van Persie 8 (McNair 68, 6), Falcao 7.5 (Wilson 80, 6)
Subs not used: Valdes, Smalling, Herrera, Fellaini
Goal: Van Persie 27, Falcao 32, Morgan OG 44
LEICESTER (4-4-2): Schwarzer 6; Simpson 5, Wasilewski 6.5, Morgan 5; De Laet 6; Vardy 5 (Cambiasso 46, 6), Drinkwater 5, King 6, Schlupp 5; Ulloa 5 (Nugent 62, 6), Kramaric 5 (Albrighton 62, 6.5)
Hutopitwa na habari yoyote mtu wangu, niko tayari kukutumia kila kinachinifikia kupitia, www.tangakumekucha.blogspot.com

MATOKEO YA SIMBA NA JKT RUVU HAYA HAPA



Simba SC Vs JKT Ruvu imemalizika. Matokeo na Pichaz nimekusogezea hapa…

DSC08908
Ligi Kuu Tanzania Bara imeendelea leo January 31 katika viwanja mbalimbali ikiwemo Uwanja wa Taifa Dar, ambapo timu ya Simba Sports Club walikuwa wakipambana na JKT Ruvu kusaka point tatu muhimu za ushindi.
Mpaka dakika tisini zinakamilika matokeo yalikuwa hivi, Simba SC walikuwa na goli 2 wakati JKT Ruvu walishinda goli 1.
Matokeo hayo ni nafuu kwa Simba kupata point tatu muhimu baada ya timu hiyo kutokana na kutoa sare mechi saba, kufungwa mbili na hii imekuwa ni ya tatu kwao kupata ushindi katika ligi hiyo.

DSC08892
DSC08894
DSC08897
DSC08898
DSC08900
DSC08908
DSC08910
DSC08915
DSC08917
DSC08918
DSC08919
DSC08920
DSC08925
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,www.tangakumekucha.blogspot.com

HALIMA MDEE ACHACHAFYA BUNGE

Sikia hoja za Mbunge HALIMA MDEE Bungeni, ishu ni UDA na CHENGE kuhusishwa na MIKATABA MIBOVU

UDA
Kikao cha Bunge kilianza siku ya Jumanne January 27, Kamati mbalimbali zilikuwa zikiwasilisha taarifa za Ripoti tangu kuanza kwa kikao hicho, Kamati ya PAC iliwasilisha taarifa iliyotokana na Ripoti ya CAG ambayo ilibaini ubadhirifu kwenye taasisi mbalimbali, Wabunge wakaanza kuchangia kuhusu taarifa ya ripoti hiyo.
Tulijadili ESCROW suala lilikuwa MAHAKAMANI, tulijadili LIPUMBA suala lilikuwa MAHAKAMANI leo tunakuja kujadili UDA ambalo lina mustakabali wa mkubwa wa Mkoa wa Dar es Salaam mnasema suala liko MAHAKAMANI. Hili suala linazuiwa kwa sababu kuna wakubwa nyuma…”— Halima Mdee.
Mdee II
Mwenyekiti wa Bunge Mussa Zungu akamkatisha Mbunge huyo;“Mheshimiwa Halima we still respect you.. najua concern yako.. mimi sina tofauti na Jaji hapa, nikitoa ruling una sehemu ya kwenda kulalamika. Hili ni BUNGE la heshima na katika watu wanaheshimika wewe ni mmojawapo. Hoja za MAHAKAMA ziache!
Halima Mdee aliendelea kuzungumzia ishu hiyo tena, Mwenyekiti huyo akamkatisha kwa mara nyingine; “Halima kama utakosa priviledge yako ntazuia…  Hata mimi jana nimezuiwa, nimeanza ikabidi nisalimie watu nikakaa chini kwa kuheshimu mamlaka. Itabidi nifanye action ambayo sipendi kufanya, nna adi ya manjano na kadi nyekundu. Za manjano zishachoka sasa zinaanza kugeuka rangi.”
Baada ya hapo Halima Mdee akaendelea kuchangia; “ Ukiangalia nani ambaye alohusika kwenye mkataba wa 2007/08, Chenge alikuwa Waziri wa Miundombinu alikuwepo. Chenge na mikataba ya nchi hii ya madini mibovu yupo.. na IPTL yupo… hatuchukui hatua mambo yanaenda tu. Mtafanya wananchi wataanza kuchapa watu barabarani, wakianza kuchapwa hawa nd’o discipline itakuja…
Baada ya hapo Andrew Chenge naye alipata nafasi kujibu hoja ya Mdee; “Nimemvumilia sana mheshimiwa anayechangia hoja, kama ana ushahidi  wa hayo anayoyasema kanuni zetu zinatutaka ayawasilishe tu mbele hapo
.
Mbunge Andrew Chenge.
Kuna utaratibu wa kikanuni vielelezo nikitakiwa kuleta nitavileta haina tatizo”—Halima Mdee.

SOMA HABARI KUU ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO,TZ

Leo January 31, STORY kubwa  kutoka zilizopewa uziti magazetiya leo,TZ

Glasses & PapaersMWANANCHI
Wabunge wameendelea kuwalipua mawaziri, huku wakimtaka Waziri wa Fedha, Saada Mkuya kufukuzwa kutokana na kukiuka Katiba, huku Mbunge Andrew Chenge akikumbana na kadhia ya kudaiwa kuwa anahusika kwenye kila mikataba mibovu, jambo lililosababisha Chenge kusimama na kutoa kauli ya kutaka ‘kuheshimiana’.
Hayo yalitokea Bungeni Dodoma wakati Wabunge wakichangia taarifa za Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ya mwaka ulioishia Juni 30 mwaka 2014.
Mkuya alitajwa kubadili matumizi ya fedha zilizotengwa na Serikali kwa ajili ya matumizi mengine, kitendo kinachomaanisha kuwa alivunja Katiba.
Fedha ambazo ziko kwenye ring fence (mfuko maalumu), hazitakiwi kutumika kwa matumizi mengine kwa mujibu wa sheria. Kwa mujibu wa Katiba, Waziri umevunja Katiba kwa mujibu wa ibara ya 135 na ibara ya 136 ni Tanzania peke yake (Waziri Mkuya) unabaki salama. Hupaswi hata kupewa heshima ya kujiuzulu, unafukuzwa kazi,” – Esther Bulaya.
Bulaya, ambaye amekuwa mmoja wa wabunge wachache kutoka chama tawala wanaoihoji Serikali, alisema wizara hiyo imeshindwa kukata fedha kwa ajili ya chai, suti na sambusa na badala yake inakata fedha zilizokuwa ziende kupeleka umeme vijijini.
Bulaya alikuwa akizungumzia Sh180.7 bilioni zilizokusanywa kulipia gharama za mradi kutokana na mauzo ya mafuta ili ziweze kupeleka umeme vijijini.
Wakati wa kuhitimisha mjadala wa ripoti hizo, Naibu Waziri wa Fedha (Sera), Mwigulu Nchemba alikiri kuwa wizara iliyumba katika eneo hilo kutokana na hali ya kifedha ya Serikali.
“Mwaka huu ni hapa tu ambako tuliyumba, (katika) eneo hili la matumizi ya fedha za miradi,” alisema Mwigulu na kuongeza kuwa wizara yake inaandaa utaratibu utakaowezesha makosa hayo kutojirudia.
MWANANCHI
Hofu imetanda kwa wazazi wa watoto ambao wanasoma shule za msingi za Kabasa A na B Wilaya ya Bunda, Mara baada ya kubuka kwa ugonjwa wenye dalili za kupanda ‘mapepo’ ambao unawaathiri wanafunzi wa kike pekee.
Kutokana na ugonjwa huo kuhusishwa na Imani za kishirikina uongozi wa Wilaya uliwataka viongozi wa kijiji kukaa na wazee wa kimila ili kumaliza tatizo hilo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya hiyo, Boniface Maiga alisema Serikali haiamini ushirikina, kwa kuwa tatizo limeanzia kwenye jamii basi jamii hiyo hiyo inapaswa kumaliza tatizo hilo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kabasa B alisema ugonjwa huo ulianza kati ya January 21 na 28 huku wakidhani kuwa ugonjwa huo ni Malaria.
NIPASHE
Sakata la uchotwaji wa zaidi ya Shilingi bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow limeibuka tena bungeni na kuzua malumbano makali baina ya Mwanasheria Mkuu mpya wa Serikali, George Masaju na Mbunge Tundu Lissu ambaye alimwambia Masaju kuwa ni mshauri wa serikali na si  mshauri wa Bunge kuhusu masuala ya kisheria.
Wakati huohuo Lissu alisema licha ya Bunge kumwondoa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuwafukuza mawaziri, waliochukuliwa hatua ya kufikishwa mahakamani ni watu wadogo waliopewa milioni 80, huku wale waliogawana mabilioni ya fedha wakidunda mitaani.
“Watu wanafanya makosa makubwa dhidi ya umma hakuna hatua inayochukuliwa, waheshimiwa wabunge mnaweza mkauliza, lini mtu  amewahi kuwajibika, nani kachukuliwa hatua, yupi amefungwa, tunajua wanajiuzulu ili wakafaidi matunda ya wizi wao, sheria zetu zinasema wajiuzulu, wafilisiwe, washitakiwe na wakipatikana na hatia wafungwe, nani ameshitakiwa, kufilisiwa au kufungwa?”—Tundu Lissu.
Mbunge huyo alisema kuwa Bunge liliazimia majaji waliohusika na sakata hilo Bunge wawajibishwe, lakini Rais Kikwete hajawachukulia hatua  kwa madai kuwa majaji hao wanatakiwa kuchukuliwa hatua na mahakama, huku akishangaa nani anayemshauri Rais masuala ya kikatiba na sheria.
“Maazimio ya Bunge lako ni kwamba serikali  ilete taarifa ya utekelezaji maazimio kabla ya kumalizika kwa Bunge la Bajeti lakini hata kabla halijaanza… kanuni zinakataza kumhusisha mheshimiwa Rais kujenga hoja kwa namna ya kejeli, kwa hiyo mimi naomba kushauri kuwa tunapopata fursa ya kuchangia tujikite kwenye hoja yetu na tutumie lugha ya  staha kwa sababu ndivyo kanuni  zinavyoelekeza,” Mwanasheria Masaju.
Lissu aliongeza kuwa ameipata taarifa ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye alimwita mrithi wa Jaji Fredrick Werema huku akimweleza kuwa ni mshauri wa serikali na si  Bunge kuhusu masuala ya kisheria ambapo Mwenyekiti wa Bunge, Mussa  Zungu alisimama na kumtaka Lissu kutotumia lugha za vijembe badala yake ajenge hoja.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Masaju alisimama kuomba mwongozo na kumtaka Lissu kuendelea kuheshimu mihimili mingine kwa kutozungumzia mambo yaliyo mahakamani. 
MTANZANIA
Bibi kizee anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 70 asiyejulikana jina wala makazi yake ameanguka akiwa hajavaa nguo yoyote nyumbani kwa mtu mkoa wa Shinyanga jambo ambalo limehusishwa na Imani za kishirikina.
Suzana Mwandu ambaye ni mwenye nyumba ambayo kikongwe huyo alianguka anasema alimkuta akiwa nje ya jiko llake ambapo baada ya kumsemesha bibi huyo alizinduka na kuanza kuongea vitu visivyoeleweka ambapo mashuhuda walihisi kwamba alikuwa akifanya ushirikina.
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa  Waziri Issa amekiri kuwepo kwa tukio hilo ambalo lilikusanya umati wa watu ambapo muda mfupi baadaye Polisi walifika na kumchukua ili kumnusuru bibi huyo kupigwa na wananchi wenye hasira.
MTANZANIA
Mbunge Godbless Lema jana alimshambulia kwa maneno makali Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja kuwa anaweza kuwa anashirikiana na majambazi wanaovamia vituo vya polisi na kupora silaha.
Lema aliliambia Bunge kuwa Chagonja anaweza kuwa anahusika katika matukio ya ujambazi katika vituo vya polisi kwa sababu anataka kudhoofisha utendaji kazi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu huku akifananisha taifa na chumba kinachotumiwa na vijana wa kihuni kuishi ambacho hakina utaratibu.
“Mheshimiwa Mwenyekiti, geto ni mahali ambapo watu wanaishi bila kufuata utaratibu, yaani katika geto, wakati wa kulala anayewahi ndiye anayelala kitandani. Geto chakula kinapopikwa kinaweza kuliwa hata kama hakijaiva, kwa hiyo nchi hii naifananisha na geto kwa sababu watu wanaiba fedha za umma kama wanavyotaka…” Godbless Lema.
“Katika ripoti za Bunge zilizosomwa hapa jana (juzi) zimejaa wizi, kila ukurasa wa taarifa ya Zitto ni wizi tu, wizi tu, hivi huu wizi utakwisha lini? Hata zile bunduki zinazoibwa katika vituo vya polisi zinaweza kuwa ni ‘sabotage’ (hujuma), zinazofanywa na Chagonja dhidi ya IGP,” alisema Lema.
Alisema amefanya uchunguzi wake binafsi uliobaini kuwa Jeshi la Polisi limegawanyika na kwamba haamini kama Rais Kikwete amekwishafanya mabadiliko ya uongozi ndani ya jeshi hilo.
Alisema ikitokea mawaziri wa Tanzania wakapelekwa nchini Tunisia wangeishachukuliwa hatua kali kwa sababu Serikali ya nchi hiyo haiwavumilii wabadhirifu wa fedha za umma.
MTANZANIA
Zitto Kabwe ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwigulu Nchemba, Mbunge wa Iramba Magharibi na pia Naibu Waziri wa Fedha jana walialikwa kushiriki mahojiano katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC) ambapo katika mjadala huo kila mmoja kumsifia mwenzake kwa utendaji kazi uliotukuka.
Zitto alikwenda mbali zaidi kwa kutangaza kumuunga mkono Mwigulu, ambaye amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa wanasiasa vijana wanaoendesha harakati za chini kwa chini za kuwania urais baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza muhula wake wa pili wa urais mwishoni mwa waka huu.
Katika mjadala huo, ni Mwigulu ambaye ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyeanza kummwagia sifa Zitto kwa jinsi ambavyo amekuwa akitekeleza majukumu yake ya kiuongozi katika nafasi yake ya uenyekiti wa Kamati ya PAC.
Mwigulu alisema Zitto na kamati yake kwa ujumla wamekuwa wakifanya kazi kubwa na nzuri ya kibunge na pia kuishauri vizuri serikali na hasa Wizara ya Fedha.
Zitto alijibu pongezi hizo muda mfupi kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala huo kwa kueleza kuwa iwapo Mwigulu ataonyesha nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa baadaye mwaka huu atamuunga mkono, kwa sababu ameonyesha kuwa ni kiongozi mzalendo na mwenye uwezo mkubwa wa kuelewa matatizo ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.
Alisema ameamua kumuunga mkono kwa sababu yeye anabanwa na umri wake ambao unamwondolea sifa ya kikatiba ya kuwania wadhifa huo, tofauti na Mwigulu ambaye tayari amekwishatimiza miaka 40 inayotajwa kwenye Katiba kama moja ya sifa ya kumwezesha mtu mwenye nia ya kugombea urais kutekeleza matamanio yake hayo.
Alisisitiza kuwa uamuzi wake huo umetokana na tathmini aliyoifanya kuhusu mwenendo wa utendaji kazi wa Mwigulu ndani ya serikali ulioonyesha kuwa ana uwezo mkubwa wa kiuongozi.
Zitto na Mwigulu wameonyesha dhamira ya kuunganisha nguvu zao ili kutekeleza malengo yao ya kisiasa, huku kukiwa na mitazamo mbalimbali ndani na nje ya jamii kuhusu wanasiasa vijana waliokwishaonyesha nia ya kuwania madaraka hayo ya juu ya Dola.
Kitengo cha jarida la The Economist cha The Intelligence Unit ambacho hufanya ufuatiliaji wa siasa za kimataifa, mwishoni mwa mwaka jana kilimtaja Zitto kuwa ni mmoja wa wanasiasa vijana wa kambi ya upinzani ambaye nguvu za kisiasa.
The Intelligence Unit kilieleza kuwa umaarufu wa kisiasa wa Zitto unatokana na nafasi yake ya kiongozi wa kamati nyeti ya Bunge ambayo imekuwa ikiibua mambo mazito na yenye athari katika taifa, hivyo licha ya kuwa na mgogoro na baadhi ya viongozi wenzake ndani ya CHADEMA, bado anao ushawishi mkubwa wa kisiasa kwa wadhifa alionao ndani ya Bunge.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,www.tangakumekucha.blogspot.com

Friday, January 30, 2015

YALIYONIKUTA TANGA (8)

HADITHI
 
YALIYONIKUTA TANGA (8)
 
ILIPOISHIA TOLEO LILILOPITA
 
Nikairudisha ile simu mfukoni. Wakati nairudisha ilikuwa kama ninaizima akili yangu kwani hapo hapo sikujielewa tena. Sikujua kama nilipotewa na fahamu au nilipitiwa na usingizi wa ghafla. Sikuweza kujua.
 
Nilipozinduka nilijiona nimechoka, kitu ambacho kilinipa dalili kuwa nililala kwa muda mrefu pale kwenye kochi. Nikatazama saa yangu na kuona ilikuwa saa tisa usiku. Nikataharuki. Mwenyeji wangu hakuwepo. Nilikuwa bado niko peke yangu.
 
Nikajiuliza Maimuna alikuwa amekwenda wapi tangu muda ule. Nikanyanyuka na kuanza kumtafuta mwenyeji wangu. Niliingia ukumbini nikaita “Maimuna!”
 
Lakini sikupata jibu. Nikasukuma mlango wa chumba cha kwanza ambao ulikuwa wazi. Nikachungulia ndani. Chumba kilikuwa kitupu lakini kulikuwa na boksi kubwa lililowekwa nyuma ya mlango.
 
Nilichungulia ndani ya lile boksi nikaona kitu kilichonishitua. Nikaingia mle chumbani na kutazama vizuri. Ndani ya lile boksi niliona kichwa cha binaadamu, tena kilikuwa kichwa cha Sajenti Erick!
 
SASA ENDELEA
 
Kwa kweli nilipatwa na mshituko mkubwa. Vile ambavyo nilitoka usingizini nilijihisi kama nilikuwa kwenye ndoto ya kutisha. Kwa kutoamini macho yangu nilikitazama kile kichwa tena na tena. Akili yangu ilinithibitishia kuwa sikuwa kwenye ndoto na nilichokiona ni kichwa cha binaadamu na ni cha Sajenti Erick!
 
Nikawa najiuliza Sajenti Erick alichinjwa muda gani na alichinjwa na nani na kwanini kichwa chake kipo pale? Nikakumbuka kwamba nilipigiwa simu na kachero mwenzangu aliyenieleza kuhusu kutoonekana kazini kwa Sajenti Erick mchana kutwa wa siku ile.
 
Kile kichwa kwa jinsi kilivyoonekana hakikuchinjwa muda mrefu. Jeraha lake lilikuwa bado bichi na lilikuwa linavuja damu. Macho ya Sajenti Erick yalikuwa wazi kuonesha kuwa wakati anachinjwa alikuwa ameshituka.
 
Akili ya kupelelezi ikaanza kunijia. Nikazungusha macho yangu kwenye kile chumba. Sikuona mahali popote palipokuwa na damu, hali iliyoonesha kuwa Sajenti Erick hakuchunjwa mle chumbani.
 
Wakati nayarudisha macho yangu kwenye lile boksi nikaona magazeti kwenye pembe moja ya kile chumba. Nikaenda kuyatazama. Yalikuwa magazeti mawili yaliyowekwa pamoja. Juu ya magazeti hayo kulikuwa na kete tatu ambazo nilishuku zilikuwa kete za kokeni.
 
Nilizishika na kuzinusa. Kwa vile nilikuwa na uzoefu na unga huo haramu niligundua harufu yake. Ilikuwa ni kokeni. Nikaziweka kando. Sasa nilishika yale magazeti. Nilianza kuangalia mojawapo. Kwenye ukurasa wa mbele kulikuwa na habari ya ajuza (kikongwe) aliyekamatwa Tanga na kete za madawa ya kulevya.
 
Picha yake ilikuwa imechapwa. Nilipoitazama nikagundua ilikuwa ni ya yule mwanamke tuliyemkamata siku ile mimi na Sajenti Erick. Kumbe habari zake zilichapwa kwenye gazeti. Nikatazama tarehe ya lile gazeti nikaona ni la siku za nyuma.
 
Nikashika lile gazeti jingine. Katika ukurasa wake wa mbele kulikuwa na habari iliyohusu kifo cha yule kikongwe ambacho kilitokea katika mahabusi ya polisi.
 
Mpaka muda ule nilikuwa sijaelewa kitu. Nilikuwa nikijiuliza mengi ambayo hayakuwa na majibu. Wakati naliweka lile gazeti nikaona kitone cha damu kikidondoka kwenye kiganja changu. Nikashituka na kutazama juu.
 
Huko juu niliona kitu cha kushitusha. Niliuona mwili wa Sajenti Erick usio na kichwa ukiwa umening’inizwa kwenye miti iliyopaulia nyumba! Lile jeraha la kwenye shingo ndilo lililotonesha tone la damu  lililotua kwenye kiganja changu.
 
Mwili ule uliunda picha ya kutisha sana hasa kwa vile mtu mwenyewe nilikuwa namfahamu. Ujasiri wa kipolisi niliokuwa nimebaki nao uliniishia pale pale. Kama nisingekuwa makini ningekurupuka na kutoka mbio kwani hisia zangu zilishanusa hali ya hatari.
 
Nilijua kuwa hata mimi maisha yangu yalikuwa hatarini. Mahali nilipoingia palikuwa sipo!. Nikainua hatua ili nitoke katika kile chumba. Baada ya kupiga hatua mbili nilikanyaga mahali palipotitia! Nikajiona natumbukia chini.
 
Lilikuwa shimo la urefu wa kama futi nne. Miguu yangu ilipotua chini nikaona kitu kinanizongazonga kwenye miguu kikinipandia juu. Nikajaribu kukishika. Nikaona nimeshika kichwa cha nyoka!
 
“Yesu wangu!” nilishituka na kukivuta juu. Haikuvutika kwani sehemu yake ya mkia ilikuwa imenizonga kwenye mguu. Nilitaka kuwania kupanda juu ya lile shimo nitoke  lakini nilijiambia nikikiacha kile kichwa nyoka yule atanigonga.
 
Nikakipeleka kichwa hicho chini ya mguu mwingine kisha nikakikanyaga kwa kupiga mguu wangu chini. Kile kichwa kilipasuka. Ndipo nilipoweza kutoka kwenye lile shimo. Nilikuwa nahema kama niliyekuwa nafukuzwa.
 
Nilipotoka tu kwenye shimo hilo nilikwenda ukumbini nikaelekea kwenye mlango wa nje. Nilipoushika ili niufungue nikaona ulifungwa kwa nje. Mlango haukufunguka!
 
Nikasikia sauti za watu waliokuwa wakizungumza huko nje. Sauti ya mwanaume na mwanamke. Zilikuwa zikisikika kwa mbali lakini zilikuwa zikikaribia kwenye ule mlango. Nikajua ni watu  wanakuja.
 
Nikatega masikio kuwasikiliza.
 
“Sasa mama yuko wapi?” Ilikuwa sauti ya kiume iliyouliza.
 
“Mama yuko uani, anachimba kaburi kabisa” Sauti iliyojibu niliitambua, ilikuwa ni ya yule msichana aliyenikaribisha mle ndani.
 
“Na huyo polisi mwingine aliyewabambikia kesi yuko wapi?” Ile sauti ya kiume ikauliza tena.
 
“Nilimuacha ukumbini amelala, sijui kama atakuwa ameamka”
 
“Sasa acha tumshughulikie na yeye kama mwenzake”
 
“Mama yangu, nimekwisha!” nikajiambia niliposikia maneno hayo. Kumbe tatizo lilikuwa ni ile kesi tuliyombambikia yule mwanamke.
 
Sasa akili yangu ilitanzuka. Nilimkumbuka yule msichana. Alikuwa ndiye yule aliyekuwa na yule mwanamke kwenye ile nyumba tulipokwenda kuwakamata. Yule msichana alikimbia, tukamshikilia mama yake peke yake.
 
Kwa hofu kwamba ningeuawa kama alivyouawa Sajenti Erick, nilikimbilia kwenye mlango wa uani. Niliukuta mlango upo wazi, nikatoka uani ambako kulikuwa kiza lakini kulikuwa na mbalamwezi.
 
Kwenye pembe moja ya ua huo nilimuona bibi mmoja ameshika shepe akichimba shimo. Nilipomuona tu nikakumbuka yale maneno ya yule msichana niliyemsikia akisema “Mama yuko uani, anachimba kaburi kabisa”
 
Nikajiuliza lilikuwa kaburi langu au ni la Sajenti Erick? Wakati namtazama yule bibi nikamkumbuka. Alikuwa ni yule mwanamke tuliyemkamata na kumbambikia kesi ya kumkuta na madawa ya kulevya.
 
Jambo ambalo lilinishangaza ni kuwa mwanamke huyo alikufa akiwa mahabusi lakini muda ule nilimuona akiwa hai tena akionekana akiwa na nguvu za kutosha.
 
 Kitu ambacho kilikuwa cha ajabu zaidi ni kuwa bibi huyo alikuwa uchi wa mnyama na mwili wake ulikuwa umejaa manyoya meupe marefu. Nikaiona miguu yake, ilikuwa na kwato kama miguu ya punda!
 
Je nini kitatokea? Usikose kuendelea na hadithi hii kesho.
 Na usisite kutembelea blog hii kila wakati kwa habari nyingi nzuri na za kusisimua, ni tangakumekuchablog

AMKA NA MAGAZETI NA KUMEKUCHA BLOG

MAGAZETI YA LEO JAN 31 YANALETWA KWENU KWA HISANI YA KITUO CHA ELIMU CHA NEW EGE EDUCATION CENTRE TANGA, WANAFUNDISHA KOZI MBALIMBALI NA MASOMO YA FORM 4 FORM 5 NA FORM 6. PIA HUDUMA ZA HOSTELI ZINAPATIKANA, WASILIANA NAO KWA SIMU NO, 0717 713866





















                   Niko tayari kutumia muda wangu wakati wowote mtu wangu ili kukupata habari zinazojiri kila wakati na usiste kutembelea, www.tangakumekuchablogsspot.com