Tuesday, October 31, 2017

RIWAYA, KAMA UNATAKA FEDHA ZA MAJINI SEHEMU YA 11

RIWAYA

KAMA UNATAKA FEDHA ZA MAJINI 11

ILIPOISHIA

Wengine walikuwa wakisema.

“Nahodha utatuua wewe, kuna watoto humu!”

“Alikuwa akivuta bangi, huyo hana akili!” Mwanamke mmoja alisema kwa hasira.

Pamoja na kelele zote hizo nahodha huyo hakumsikiliza mtu yeyote, aliendelea kukielekeza chombo hicho kwenye mawimbi. Ile dharuba iliyokuwa ikitupiga haikumtia hofu hata chembe.

Pale ndipo nilipogundua sababu ya baadhi ya manahodha kuvuta bangi, ni kutaka kupata uwezo wa kiakili wa kukabiliana na ile hali endapo itatokea.

Yule mtu alionekana kama mwehu. Wimbi linapokuja linatutosa. Na yeye alitota chapa chapa lakini hakuonesha kupata hofu wala kujali. Siku ile niliapa kuwa sitasafiri tena na jahazi na sikujua kama tungefika salama Pemba.

Yale mawazo ya kufa yakanifanya nimkumbuke mke wangu. Nikakumbuka kwamba nilimuahidi kumtumia nauli na nikahisi kwamba angenipigia simu kuniulizia tena.

Nikatoa simu yangu na kuizima ili akipiga simu asinipate.

SASA ENDELEA

Upande mmoja wa akili yangu ukaniambia kuwa hatua hiyo ingeweza kumzidishia wasiwasi mke wangu, jambo ambalo linaweza kufanya aamue kukopa pesa ya nauli ili aje anifumanie.

Kama atafanya hivyo, nilijiambia, akifika Korogwe hatanikuta na hivyo atawapa nafasi wale majini wamtoe kafara.

Kile nilichokuwa sikitaki ndicho kitakachotokea, nilijiambia.

Nikakumbuka pia nilikuwa nimewaacha na njaa wale viumbe kule kwenye pango na nikapata hofu kuwa wanaweza kufa.

Ilimradi nilijikuta nimesongwa na mawazo mengi lakini niliomba Mungu tufike salama ili nijue nitafanikiwaje kulitatua lile tatizo lililokuwa linanikabili.

Mungu si Athumani wala si Huseni. Pamoja na dharuba zilizotupiga baharini tulifika salama Pemba. Tatizo ni kuwa tulifika usiku.

Ikanibidi nitafute gesti. Mji huo haukuwa na gesti nyingi kama ilivyo huku bara. Hata hivyo nilifanikiwa kupata gesti moja katikati ya mji wa Chakechake Pemba. Nikalala hapo hadi asubuhi.

Kulipokucha ndipo nilipoulizia kwa wenyweji kilipo hicho Kisima cha Giningi.

“Kipo Kendwa” Kijana aliyenipokea pale gesti ndiye aliyenijibu. Kabla sijamuuliza huko Kendwa ni wapi akaendelea kuniuliza.

“Unataka kwenda Giningi?”

“Ndiyo nataka niende nikapaone”

“Wewe unataka ufike katika hicho kijiji au hapo kwenye kisima?”

“Nataka nifike hapo kwenye kisima”

“Magari yapo yanayokwenda huko”

“Nitayapata wapi?”

Kwa msaada wa yule kijana aliyegundua kuwa nilikuwa mgeni ninayetoka bara nikafanikiwa kupata daladala iliyonipeleka katika kijiji hicho kilichokuwa maeneo ya mashambani.

Nilipofika nilipata kijana mwingine aliyenichukua kwa baskeli ya bodaboda hadi kilipokuwa kisima hicho cha Giningi.

Kinapotajwa Kisima cha Giningi mtu angeweza kudhani kuwa kilikuwa kisima cha kisasa na kilichokuwa katika mazingira ya kupendeza. Lakini hakikuwa hivyo. Kisima chenyewe kilikuwa ni cha kale sana na kilionekana kama hakikuwa kikitumika tena.

Kwa mujibu wa mzee mmoja niliyemkuta hapo, kisima hicho ni cha kale sana na haikufahamika kilichimbwa katika enzi ipi. Lakini kilipata umaarufu kutokana na baadhi ya wenyeweji kuamini kuwa mahali hapo palikuwa na asili ya kimizimu na majini. Hivyo watu mbalimbali walikuwa wakifika mahali hapo kufanya matambiko na mambo mengine ya kiuganga.

Nilimsikiliza kwa makini yule mzee kabla ya kujitambulisha kwake na kumueleza kuwa nimetoka bara na nilikuwa na shida na mzee aliyekuwa anaitwa Habib Sultani.

“Ulikuwa unamtaka wa nini?” Mzee huyo akaniuliza.

“Nina shida naye”

“Shida gani?”

“Nilisikia huyo mzee anashughulika kuwapa watu majini ya kuwatajirisha”

“Ni kweli. Kwa hiyo wewe ulikuwa unataka upate utajiri?”

“Hapana. Nina tatizo jingine”

“Nataka nikufahamishe kuwa huyo mzee uliyemtaja ameshakufa”

Nikashituka na kumuuliza.

“Alikufa lini?”

“Ni muda sasa. Inafika miaka mitatu”

Nikatikisa kichwa changu kusikitika. Nikaona safari yangu ya kwenda Pemba ilikuwa ya bure.

“Ungenieleza mimi shida yako labda ningekusaidia”

“Kwani wewe pia unahusika na mahali hapa?”

“Mimi ndiye muangalizi wa eneo hili. Mimi ndiye ninayefagia hapa kila siku na kusaidia watu shida mbalimbali”

“Huyo Habib Sultani alikuwa ni nani?”

“Yeye alikuwa mganga na ndiye aliyeachiwa siri ya mahali hapa na babu yake”

“Sasa sijui utanisaidiaje mzee wangu…”?

“Niambie tu shida yako wala usihofu”

Nikamueleza yule mzee matatizo yangu mwanzo hadi mwisho.

Yule mzee hakushituka hata kidogo isipokuwa aliinama akafikiri kwa muda kidogo kabla ya kuniuliza.

“Una maana kuwa marehemu baba yako kabla ya kufa kwake hakuwa amekuarifu kuwa alikuwa na jini kutoka hapa Giningi linalompatia pesa?’

“Hakuniarifu. Nilizikuta zile pesa baada ya yeye kufa na yule jini alinifuata usiku akanifahamisha kuwa alinunuliwa na baba yangu kutoka hapa na akataka mimi nimrithi”

“Na wewe hukutaka?”

“ Sikutaka na sitaki!”

“Yule mke wake na yule mwanao waliotolewa kafara bado wapo?”

“Wale bado wapo hai lakini wakati wowote wanaweza kufa. Isitoshe nimeambiwa akifa mama, mke wangu naye atachukuliwa. Ndiyo maana nimeharakisha kuja huku”

“Tangu nianze kuwa msimamizi wa kisima hiki leo ndio mara ya kwanza kuona mtu anakataa pesa za majini ambazo watu wengi wamekuwa wakizitafuta”

“Mimi ni mtu tofauti sana, Najali utu wa watu, sijali pesa. Bora nife masikini kuliko kuwatoa muhanga binaadamu wenzangu”

“Basi usiseme maneno mengi, nataka nikuulize swali moja umeshatumia kiasi gani katika hizo pesa?”

“Sijatumia hata senti tano”

“Sasa mwanangu, mimi ni muangalizi tu wa eneo hili. Mimi sina uwezo wa kumpa mtu jini wala kumtoa jini na sijui kama jambo hilo unalolitaka linawezekana…”

“Mzee uliniahidi kuwa utanisaidia” nikamkatiza yule mzee.

“Msaada wangu utaupata. Nitakupeleka kwa mwana wa huyo Habib Sultani ambaye ameachiwa mikoba na huyo baba yake. Sasa msaada zaidi utaupata kwa huyo”

“Sawa, basi nipeleke kwa huyo aliyeachiwa hiyo mikoba”

“Lakini kuna mawili, anaweza akusaidie au asikusaidie”

“Mimi ninachotaka wachukue pesa zao pamoja na yule jini wao”

“Kwa sababu yeye siye aliyemtoa huyo jini, sina uhakika kuwa ataweza kulifanya jambo hilo lakini twende ukamsikilize mwenyewe’

Yule mzee akanipeleka katika nyumba moja iliyokuwa katika kitongoji kile kile cha Kendwa.

Tulimkuta mtu mmoja aliyekuwa amekaa kwenye kiti cha uvivu akivuta tasbihi. Alikuwa amevaa kanzu nyeupe na kichwani alijifunga kilemba kikubwa.

“Maalim asalaam alaykum” Yule mzee akamsalimia. Na mimi pia  nikamsalimia.

“Waalaykum salaam” Mtu huyo akatujibu.

“Tumepata mgeni kutoka bara. Alikuwa na shida na marehemu Habib Sultani. Nimemwambia Sheikh Habib allishafariki kitambo lakini yuko mwanawe”

Yule mtu akanitazama na kuniambia.

“Karibu mgeni?”

“Huyo ndiye mwanawe  marehemu Shikh Habib Sultani na yeye pia anaitwa Sultani. Unaweza kumueleza shida yako” Yule mzee akaniambia.

Tangu nilipomuona mtu huyo sikutarajia kuwa angekuwa  ndiye huyo mwana wa Habib Sultani. Kwa vile niliambiwa ni mwana, nilitarajia kumuona kijana mdogo. lakini yeye hakuwa kijana mdogo. Alikuwa mtu mzima na kiumri alikuwa amenizidi hata mimi.

“Mtolee kiti” Mtu huyo akamwambia yule mzee niliyekwenda naye.

Yule mzee akaingia ndani ya ile nyumba na kutoka  na kiti akaniwekea na kuniambia.

“Karibu ukae”

Nikakaa mbele ya yule maalim.

“Haya nieleze shida yako”

Nikaanza kumueleza mtu huyo matatizo yangu mwanzo mpaka mwisho.

“Nadhani kulikuwa na makosa yalifanyika kati ya marehemu Habib na baba yako” akaniambia.

“Makosa gani?”

“Huyo jini alimuhusu baba yako tu na hizo pesa zilimuhusu baba yako tu. Lakini bila shaka baba yako alikutaja wewe kama mrithi wake na ndio maana huyo jini alikufuata. Sasa kwa bahati mbaya mzee Habib ameshakufa”

“Nimeambiwa kuwa wewe ndiye mrithi wake. Nilitarajia kuwa ungeweza kunisaidia”

“Kwani usichotaka wewe ni kitu gani, ni pesa au jini?” akaniuliza.

“Silitaki hilo jini?”

“Na pesa je?”

Je nini kitatokea? Tukutane kesho

Monday, October 30, 2017

RIWAYA, KAMA UNATAKA FEDHA ZA MAJINI SEHEMU YA 10

RIWAYA

KAMA UNATAKA FEDHA ZA MAJINI  10

ILIPOISHIA

Mke wangu akakata simu. Badala ya kuwa na furaha ya kuzungumza na mke wangu, moyo wangu ukajaa machungu.

Kile nilichokuwa nikikihofia sasa kilikuwa kinakaribia kutokea.

Mke wangu umeng’ang’ania kuja huku lakini huku kuna matatizo ambayo siwezi kukuambia kwa sasa, nikajikuta nikisema peke yangu.

Nikajiambia kama mke wangu atakuja hapo kesho huenda huo ukawa ndio mwisho wake.

Licha ya kutambua bayana  madhara ambayo yangeweza kumkuta mke wangu nilishindwa kumzuia asije. Mwenyewe ameshaanza shutuma zisizo na msingi, hajui jinsi dakika zake zilivyokuwa zinakaribia.

Wakati nikiwaza hivyo kichwa changu kilikuwa kipo kwenye mchakato wa haraka haraka kutafuta ufumbuzi wa suala hilo. Nikakumbuka ile ndoto niliyoiota kwamba nilikwenda Pemba mahali panapoitwa Giningi na kukutana  na yule mwanamke wa kijini.

SASA ENDELEA

Nilikuwa nikifahamu kuwa  jini huyo alichukuliwa na baba yangu kutoka  mahali hapo ambapo ndipo alipopatia utajiri wake. Nikakumbuka kuwa yule jini alinieleza kuwa hapo Giningi kuna mzee mmoja anayeitwa Habib Sultani ambaye ndiye anayewauzia watu majini wanaozalisha pesa.

Hao majini wanamuita mzee huyo “baba.”, yaani wanamfanya kama baba yao na ndiye huyo ambaye katika ile ndoto niliambiwa amekwenda shamba.

Nikapata wazo moja. Wazo hilo lilikuwa ni kwenda Pemba kumtafuta mzee huyo na kumueleza hali halisi kuhusu matatizo yaliyokuwa yananikabili. Ikiwezekana nimrudishie pesa zake na yeye achukue majini wake.

Wazo hilo likanipa nguvu, nikaona ndio wazo pekee ambalo litanipatia ufumbuzi wa matatizo yangu.

Sasa kama nataka kusafiri kwenda Pemba, nikajimbia, muda ulikuwa ndio ule. Sikuwa  na muda tena wa kupoteza kwani mke wangu angefika kesho yake.

Nikiianuka kwenye kitanda nikaenda bafuni kuoga. Nilipomaliza nilirudi ndani nikavaa nguo nyingine za safari. Nilichukua begi langu nikatia nguo mbili za akiba nikatoka na kufunga mlango wa nyumba.

Sikumuaga mtu yeyote nikaanza safari ya miguu kuelekea stendi ya mabasi. Nilipofika nilipanda basi la kwenda Tanga.

Wakati nimo safarini kuelekea tanga likanijia wazo jingine kuwa endapo sitampata huyo mzee nitafanya nini. Kwa kweli hapo sikuwa na jibu lakini waswahili wanasema “Mfa maji hushika maji” Na mimi kwa vile nilikuwa mfa maji nikaamua kushika maji.

Nilipofika Tanga nilikwenda kwenye duka la mkazi mmoja wa Pemba ambaye nilikuwa nikimfahamu, nikamuulizia kuhusu usafiri wa kwenda Pemba. Akaniambia maneno ya kunikatisha tamaa.

“Usafiri wa kwenda Pemba unafanyika kwa wiki mara moja, inabidi ukae hadi jumamosi ndio utapata usafiri wa Pemba” Mtu huyo akaniambia.

Siku ile ilikuwa ni jumatano. Kwa maneno yake ni kwamba nilipaswa kukaa hadi siku ya jumamosi ndipo niondoke kwenda Pemba wakati nilihitaji kufika Pemba siku ile ile.

Hapo nikagwaya. Jasho lilikuwa linanitoka kwenye uso wangu.

“Kwani wewe ulihitaji kwenda lini?” mtu huyo akaniuliza.

“Nilihitaji kufika leo”

“Labda uende Pangani. Kule kuna usafiri wa kila siku wa kwenda Pemba na Unguja”

“Si kitu, naweza kwenda Pangani”

“Lakini usafiri wa huko ni wa majahazi. Utaweza kusafiri kwenye jahazi?”

“Nitaweza. Acha jahazi hata kwa dau nitakwenda”

Mpemba huyo akacheka.

“Kwani una dharura kubwa sana?” akaniuliza.

“Nina dharura kubwa, ni muhimu nifike leo”

“Basi wewe nenda Pangani. Mabasi ya Pangani yapo wakati wote”

Kutokana na muongozo wa rafiki yangu huyo sikuhangaika tena kwenda bandarini kuulizia usafiri wa Pemba, nikaenda katika kituo cha mabasi nikapanda basi la Pangani. Nililikuta basi hilo limejaa na lilikuwa tayari kuazna safari. Ikanibidi nisimame baada ya kutopata siti.

Mpaka nafika Pangani ilikuwa saa tisa alasiri. Nilikuwa na matumaini madogo sana ya kufika Pemba kwa siku ile.

Ile ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kukanyaga katika mji huo wa kihistoria niliokuwa nikiusikia na kuusoma kwenye ramani. Nilikuwa na shauku ya kwenda kupaona mahali palipokuwa na soko la watumwa ambapo pamekuwa ni kivutio kikubwa cha watalii lakini muda haukuniruhusu.

Nilishuka pwani nikakuta kulikuwa na majahazi kibao.

Ili nijue taratibu za usafiri wa hapo nilimfuata mtu mmoja nikamuulizia kuhusu usafiri wa Pemba.

“Muulize mtu yule pale”

Mtu huyo naye akanielekeza kwa mtu mwingine aliyekuwa amekaa pembeni chini ya mti akivuta sigara.

Jinsi alivyokuwa amevaa alionesha alikuwa mmoja wa manahodha wa zile jahazi. Nikamfuata.

Wakati namkaribia nilianza kusikia kupuo la harufu ya bangi. Yule mtu alikuwa akizidi kupuliza moshi. Nilipofika karibu yake nikagundua kuwa sigara aliyokuwa akivuta ilikuwa bangi.

Alikuwa akivuta kwa uhuru bila kujali kuwa alichokuwa akivuta kilikuwa haramu. Mpaka ninamfikia hakuonekana kushituka. Alikuwa akiendelea kuvuta.

“Habari ya saa hizi?” nikamsalimia mtu huyo aliyekuwa na mwili mfupi uliokakamaa.

Alikuwa na macho madogo yaliyoiva kwa bangi.

Mtu huyo akanitazama kisha akanijibu.

“Nzuri”

“Nilikuwa naulizia usafiri wa kwenda Pemba”

“Wewe ndiye unayetaka kwenda Pemba?” akaniuliza.

“Ndiyo.

“Jahazi ile pale, tutaondoka sasa hivi”

Alinionesha jahazi moja iliyokuwa baharini ambayo tayari ilikuwa  imejaa watu.

“Kwa hiyo niende nikajipakie”

“Lipa nauli kwanza”

“Ni kiasi gani?”

“Elfu saba”

Niliona kilikuwa kiasi kidogo sana. Nikatoa kiasi hicho na kumpa.

Nilimpompa pesa hizo alizima bangi yake. Kipisi kilichobaki alikitia mfukoni kisha akainuka.

“Haya twende” akaniambia.

Nikafuatana naye kuelekea baharini.

“Sega suruali yako isiingie maji” akaniambia.

Nikasega suruali yangu. Tukaenda kupanda jahazi pamoja. Kumbe alikuwa akisubiriwa yeye avute bangi kwanza ndipo jahazi liondoke.

Nilitafuta mahali nikakaa na kuanza kuitafakari safari hiyo ambayo ilishaanza kunitia mashaka.

Nahodha mwenyewe ameshavuta bangi, jahazi limejaa abiria na mizigo na bahari ilionekana haikuwa shwari.

Lakini kutokana na umuhimu wa safari yenyewe ilibidi niende tu. Ingawa mimi nilipata hofu kidogo lakini usafiri huo ndio unaotumiwa siku zote na baadhi ya abiria kwa vile unapatikana kila siku na nauli yake ni nafuu.

Yule mtu alikuwa ndiye nahodha. Akiwa kwenye ile jahazi alikuwa na lugha chafu na alikuwa mkali kama pilipili.

Dakika chache  tu baada ya kujipakia sisi safari ikaanza. Jahazi iliondoka polepole, tukaanza kuiacha pwani ya Pangani. Baada ya masaa mawili mji wa Pangani hatukuuona tena.

Ghafla upepo mkali ukaanza kuvuma tukawa tunakutana na mawimbi makubwa makubwa. Nikaona baadhi ya  abiria wanawake wakianza kupiga kelele. Huku baadhi wakitapika hasa watoto.

Chombo chetu kilikuwa kikiinuliwa na mawimbi na kisha kurudishwa chini kwa kishindo. Abiria mmoja ambaye nilikuwa nimekaa naye akaanza kutapika.

Nahodha alikuwa amesimama ameshikilia kamba. Kazi yake ilikuwa ni kulielekeza jahazi kulielekea wimbi linapotokea. Sikujua ilikuwa ni kwanini alifanya vile. Mimi niliona ilikuwa  vyema kulikwepa wimbi na sio kulifuata.

Wakati anapolielekea wimbi ndipo jahazi linapoinuliwa na kisha kurudishwa chini na hapo ndipo watu wanapotapika na  kupiga kelele.

Hali ilizidi kuwa mbaya mpaka mimi mwenyewe nikaona matumbo yamenichafuka. Nikasikia baadhi ya abiria wakipiga kelele kumwammbia nahodha.

“Rudisha chombo bandarini!  Rudisha chombo bandarini! Hali si shwari”

Wengine walikuwa wakisema.

“Nahodha utatuua wewe, kuna watoto humu!”

“Alikuwa akivuta bangi, huyo hana akili!” Mwanamke mmoja alisema kwa hasira.

Pamoja na kelele zote hizo nahodha huyo hakumsikiliza mtu yeyote, aliendelea kukielekeza chombo hicho kwenye mawimbi. Ile dharuba iliyokuwa ikitupiga haikumtia hofu hata chembe.

Pale ndipo nilipogundua sababu ya baadhi ya manahodha kuvuta bangi, ni kutaka kupata uwezo wa kiakili wa kukabiliana na ile hali endapo itatokea.

Yule mtu alionekana kama mwehu. Wimbi linapokuja linatutosa. Na yeye alitota chapa chapa lakini hakuonesha kupata hofu wala kujali. Siku ile niliapa kuwa sitasafiri tena na jahazi na sikujua kama tungefika salama Pemba.

Yale mawazo ya kufa yakanifanya nimkumbuke mke wangu. Nikakumbuka kwamba nilimuahidi kumtumia nauli na nikahisi kwamba angenipigia simu kuniulizia tena.

Nikatoa simu yangu na kuizima ili akipiga simu asinipate.

Je nini kitatokea? tukutane kesho hapahapa kumekucha.com

Thursday, October 26, 2017

RIWAYA, KAMA UNATAKA FEDHA ZA MAJINI SEHEMU YA 9

KAMA UNATAKA FEDHA ZA MAJINI 9

ILIPOISHIA

“Nikwambie ukweli tatizo lako ni gumu. Kama nitajidai kuwa naweza kukusaidia ninaweza kupata matatizo kwani hao majini wanaokalia hizo pesa ni majini hatari. Ni majini wa jamii ya Subiani. Sisi huwaita Subiani Damisi au jini maiti. Wanaweza kukukata mara moja”

Ustaadhi huyo aliponiambia hivyo alinitisha. Uso wangu ulifadhaika hapo hapo.

Hapo nikaona nimuhadithie kile kisa cha yule mganga aliyetandikwa bakora.

Utaadhi huyo alipokisikia kisa hicho aliangua kicheko.

“Huyo mganga alipata tamaa. Alitaka kuzichukua pesa hizo akiamini kuwa alikuwa na majini wanaoweza kumlinda. Lakini huyo jini wa baba yako alipomfuata, majini wa huyo mganga walisambaratika. Ni bahati yake alitandikwa bakora. Angeweza kumuua kabisa”

“Kwa hiyo utanisaidiaje” nikamuuliza tena mganga huyo huku sauti yangu ikiwa imenywea.

“Sikufichi, hakuna mganga yeyote atakayeweza kukusaidia kwa tatizo hilo labda akudanganye tu”


SASA ENDELEA


“Una maana kwamba mke wangu naye atafanywa taahira”

“Hilo ni lazima muda wake ukiwadia”

“Mpaka dakika hii sioni faida ya zile pesa kwa sababu zimeshagharimu maisha ya mama yangu na mwanangu na bado zitagharimu maisha ya mke wangu. Ni afadhali niende nikazitupe, zisiwe mikononi mwangu”

“Hao majini wa pesa hizo hawatakubali uzitupe kwa sababu baba yako alikwenda kuzitafuta huko Zanzibar na alikubali masharti aliyopewa”

“Lakini ni yeye aliyezifuata huko Zanzibar na mwenyewe ameshakufa. Mimi hazinihusu”

“Zinakuhusu kwa sababu baba yako alikutaja kama mrithi wake na ndio maana zilikuja kwako”

Ustaadhi huyo alizidi kunichanganya, nikainamisha kichwa changu na kukitikisa.

“Baba yangu atakuwa na hatia kubwa mbele ya Mungu” nikajisemea kwa hasira.

“Wakati wewe unasema hivyo, wako watu wanaozitafuta pesa hizo kwa udi na uvumba lakini hawajafanikiwa kuzipata”

“Hawajali kuwapoteza wake zao na watoto wao?”

“Mbele ya pesa hawajali”

“Sasa huu ulimwengu unakwenda wapi!”

“Unajua binaadamu tuna roho tofauti. Pesa zimewabadili watu na zimeubadili ulimwengu wetu mpaka umekuwa hivyo”

“Sasa sijui niende wapi?”

“Pata muda wa kutafakari zaidi”

Ustaadhi aliponiambia hivyo nikainuka. Kwa kweli nilikuwa nimechnaganyikiwa na kuchoka.

“Nimeshatafakari vya kutosha. Lengo langu ni moja tu kumuokoa mke wangu na kumkomboa mama yangu na mwanangu” nikamwambia huku nikitoka nyumbani kwake bila kumuaga.

Ni vizuri nikiri kuwa nilikabiliwa na mtihani mgumu katika maisha yangu. Kulikuwa na kila dalili kuwa nisingeweza kushinda mtihani huo.

Lilikuwa ni tatizo lililohitaji elimu ambayo sikuwa nayo. Waganga ambao ndio niliokuwa nikitegemea wanipe msaada wao walikuwa wananikatisha tamaa.

Wakati natoka nyumbani kwa yule mganga, akilini mwangu niliunda picha ya mama yangu na mwanangu wakienelea kuteseka kwenye lile pango hadi wanakufa kwa dhiki.

Vile  vile niliunda picha ya mke wangu niliyekuwa nikimpenda naye akichukuliwa kafara na kuwekwa katika pango hilo.

Kama hali itakuwa hiyo, nilijiambia. Sitaweza tena kurudi kazini kwangu. Nitalazimika kubaki hapo hapo Korogwe nimhudumie mke wangu hadi naye atakapokufa.

Na bila shaka, nikaendelea kujiambia, hivyo ndivyo wanavyofanya watu wanaomiliki pesa za majini kama alivyokuwa baba yangu. Wanaendelea kuwahudumia watu wao waliowatoa makafara huku wakifurahia pesa za bure walizopewa na majini.

Hili jambo halikuingia akilini mwangu kabisa. Niliona sawa na kumfanyia unyama binaadamu mwenzako ilimradi tu umiliki pesa.

Mtu unapomlaumu jambazi kuwa anatumia bunduki kuua watu na kupora fedha, akumbuke kuna na huyu jambazi mwingine anayemtoa kafara mke wake ili apate pesa.

Nilipofika nyumbani niliingia chumbani kwangu nikajilaza kitandani na kuendelea kuwaza.

Nilikuwa mtu wa kuwaza tu wakati wote. Nikiwa hapo kitandani niliwaza sana lakini licha ya kupoteza muda mwingi sikuwa nimepata ufumbuzi wowote.

Pengine utashangaa kuwa niliwaza kila kitu lakini wazo la kuwa tajiri halikupita akilini mwangu kabisa. Nilitaka niendelee kuishi nikiwa masikini vile vile na nife nikiwa masikini. Mshahara wangu ninaolipwa kila mwezi na jeshi ulitosha kabisa kuendesha maisha yangu.

Utajiri ule wa pesa zilizokuwa chini ya kitanda nilichokuwa nimekilalia wakati ule, sikuuhitaji. Ni kweli kuwa hakuna mtu asiyetaka utajiri lakini utajiri wa kuangamiza maisha ya watu haukuwa utajiri. Ni sawa na ujambazi tu.

Baada  ya kuwaza kwa muda mrefu, usingizi ulinipitia hapo hapo nikalala. Wakati nimelala nikaota ndoto. Niliota nimesafiri na boti kwenda Pemba. Nikafika katika kijiji kinachoitwa Giningi. Nikakuta kisima kilichochimbwa miaka mingi iliyopita.

Wakati nakishangaa kile kisima nilisikia sauti ya mwanamke ikiita jina langu.

Nilipogeuka niliona mwanamke amesimama kando ya mti akiniashiria kwa mkono nimfuate pale. Nikamfuata. Nilipofika karibu yake nikagundua kuwa alikuwa ni yule mwanamke wa kijini aliyekuwa mke wa baba yangu.

“Umefuata nini huku?” akaniuliza.

“Nimekuja kumtafuta yule mzee aliyempa pesa baba yangu”

“Nyumba yake ile pale”

Mwanamke huyo akanionesha nyumba iliyokuwa mbali kidogo na mahali tulipokuwa.

Wakati naitazama ile nyumba akaendelea kuniambia.

“Lakini hivi sasa hayuko amekwenda shamba”

“Na wewe unafanya nini hapa?” nikamuuliza na yeye.

“Hapa ndipo nilipotoka mimi. Na mzee uliyemuuliza ndiye baba yangu. Nataka nikukumbushe kitu, karibuni mama yako atakufa nimekuja kuchukua idhini kwa baba yangu ili tumtoe kafara mke wako achukue nafasi ya mama yako”

Maneno hayo yakanishitua.

“Sisi tunataka kuondoka kurudi Dar, mke wangu huwezi kumpata”

“Hamuwezi kuondoka tena, mtabaki pale pale Korogwe. Mke wako ataishi kwenye pango na ni wewe utakayemuhudumia”

“Likizo yangu ikiisha nitatakiwa kazini”

“Hatutakuruhusu uendelee na kazi yako kwa sababu tumeshakupa utajiri”

Ndoto yangu ikaishia hapo hapo. Nikajikuta nimezinduka kutoka usingizini. Kumbe kilichonizindua zilikuwa kelele za simu yangu iliyokuwa inaita. Si unazijua simu hizi za kichina zilivyo na sauti kali.

Nikaitoa simu hiyo kwenye mfuko wa shati langu na kutazama skirini ya simu. Nikaona aliyekuwa akinipigia alikuwa mke wangu. Sikujua ni kwanini moyo wangu ulishituka ukawa unanienda mbio.

Nikaipokea ile simu.

“Hello!”

“Ulikuwa  umelala?” Sauti ya mke wangu ikauliza.

“Simu yako ndiyo imeniamsha”

“Naisikia sauti yako umekuwa nzito kama una mafua”

“Nilikuwa nimelala. Hamjambo?”

“Hatujambo. Nataka kukujulisha kuwa kesho nakuja huko”

Nikaduwaa kwa sekunde kadhaa kabla ya  kujibu chochote. Akilini mwangu niliwaza kwamba mke wangu akija Korogwe tu amekwisha.

“Kwani hali ya baba inaendelea vizuri?”

“Ndiyo, yuko vizuri. Yeye ndiye anayenihimiza nirudi kwa mume wangu. Ameniambia nimekaa kwake kwa muda mrefu”

Nilishindwa kumwambia mke wangu kuwa asije, angeniuliza sababu na nisingekuwa na jibu kwa wakati ule.

“Mume wangu mbona umenyamaza, hutaki nije huko?” Sauti ya mke wangu ikauliza.

“Hapana. Nilikuwa nameza dawa. Kichwa kinaniuma. Wewe njoo tu” nikajisemea baada ya kushutumiwa.

“Au una mwenzangu huko, niambie tu usinifiche”

“Hapana mke wangu.Mimi niko kwenye msiba wa baba, nitafute mwanamke wa nini!”

“Naona tangu jana nikikwambia suala la kuja huko unasitasita”

“Sijasitasita ila wasiwasi wangu upo kwenye hali ya mzee. Kama unasema hivi sasa anaendelea vizuri basi unaweza kuja tu”

“Nitumie nauli”

“Nitakutumia”

“Ni hapo kesho tutakapokutana”

“Mungu akituweka hai”

Mke wangu akakata simu. Badala ya kuwa na furaha ya kuzungumza na mke wangu, moyo wangu ukajaa machungu.

Kile nilichokuwa nikikihofia sasa kilikuwa kinakaribia kutokea.

Mke wangu umeng’ang’ania kuja huku lakini huku kuna matatizo ambayo siwezi kukuambia kwa sasa, nikajikuta nikisema peke yangu.

Nikajiambia kama mke wangu atakuja hapo kesho huenda huo ukawa ndio mwisho wake.

Licha ya kutambua bayana  madhara ambayo yangeweza kumkuta mke wangu nilishindwa kumzuia asije. Mwenyewe ameshaanza shutuma zisizo na msingi, hajui jinsi dakika zake zilivyokuwa zinakaribia.

Wakati nikiwaza hivyo kichwa changu kilikuwa kipo kwenye mchakato wa haraka haraka kutafuta ufumbuzi wa suala hilo. Nikakumbuka ile ndoto niliyoiota kwamba nilikwenda Pemba mahali panapoitwa Giningi na kukutana  na yule mwanamke wa kijini.

Je nini kitatokea? Usikose kuwa nami kesho hapahapa kumekucha.com

Wednesday, October 25, 2017

RIWAYA, KAMA UNATAKA FEDHA ZA MAJINI SEHEMU YA 8

RIWAYA

KAMA UNATAKA FEDHA ZA MAJINI 8

ILIPOISHIA

Bado kulikuwa na lile suala la kufanya mapenzi na yule mwanamke wa kijini juu ya kaburi saa nane za usiku. Jambo hilo nalo kwa upande wangu lilikuwa haliwezekani kabisa.

Baada ya kuwaza sana, niliona ufumbuzi ni kuacha zile pesa kisha nifunge nyumba na kumfuata mke wangu turudi Dar.

Nilijiambia kama nitaondoka pale Korogwe na kutoshughulika na zile pesa, huenda matatizo yataniepuka.

Lilikuwa wazo zuri lakini hapo hapo niligundua kuwa lilikuwa wazo la kutapatapa kwa mfamaji. Nilijiuliza endapo nitandoka pale Korogwe, nitamuachia nani mama yangu na mwanangu wanaoteseka kule pangoni?
Pango lenyewe liko Magoma na ni kipande cha kuchapuka--- Nani atawapa chakula au nani atakuja kuwaokoa?

Nikaona nisingeweza kuondoka hapo Korogwe kabla  ya kupata ufumbuzi yakinifu kuhusu mama yangu na mwanangu.

Niliendelea kuwaza hadi asubuhi. Ulionikurupusha kitandani ulikuwa ni mlio wa simu yangu ya mkononi. Niliketi kitandani nikaichukua simu yangu na kutazama namba  ya aliyekuwa akinipigia.

Nikaona alikuwa mke wangu. Nikaipokea simu.

SASA ENDELEA

Baada ya kuulizana hali na mke wangu nilitaka kumueleza kuhusu lile tatizo lililotokea.

Lakini nikajizuia baada ya kuona ningemtia hofu mke wangu.

“Umesema Baba anaendelea vizuri kwa sasa?” nikamuuliza.”

“Anaendelea vizuri. Namtazamia kwa siku mbili, tatu. Kama hali yake haitabadilika naweza kumuacha nikaja huko”

Mke wangu aliponiambia hivyo nilishituka kidogo. Mimi nilikuwa sitaki afike tena pale Korogwe. Nilihisi kama atakafika ungekuwa ndio mwisho wake.

“Usiharakishe. Huku hakuna lolote. Muuguze kwanza mzee. Likizo bado ndefu”

“Nimesema nitakuja kama ataendelea kupata nafuu”

Nilitaka kumwambia asije kabisa. Nikaona kama nitamng’ang’aniza sana kwenye suala hilo, aingeweza kupata wasiwasi. Angeweza kushuku kuwa nimepata msichana mwingine.

“Basi sawa. Ukijiona unataka kuja tuwasiliane kwanza. Umenielewa?”

“Nimekuelewa mume wangu”

Baada ya hapo tuliagana nikaiweka ile simu kwenye kitanda. Ingawa tulikuwa tumemaliza kuzungumza lakini moyo wangu bado ulikuwa na wasiwasi. Lile suala la yeye kuja pale Korogwe sikulipendelea.

Nilihisi kwamba ningemkosa mke wangu kama atakuja hapo Korogwe kwani majini wa zile pesa za marhemu baba yangu walishaniambia kuwa wanataka kumtoa kafara mke wangu pindi mama yangu atakapokufa.

Kutokana  na hali ya mama nilivyoiona wakati ule, anaweza kufa wakati wowote.

Katika  hali isiyokuwa ya kawaida nilijikuta nikimuombea baba mkwe wangu aendelee kuumwa ili mke wangu abaki Dodoma hadi nitakapoondoka pale Korogwe.

Ilikuwa dua mbaya lakini sikuwa na jinsi. Ilibidi nimuombee hivyo kutokana na usalama wa binti yake.

Nikawaza kwamba kuna wazee waliowaachia watoto wao urithi wa majumba, magari, mashamba na pesa za halali. Na kuna wazee wengine huwaachia watoto wao urithi wa hatari. Kuna wanaorithi mikoba ya uganga wa mashetani. Kuna wanaorithi uchawi na kuna wanaorithi pesa lakini ni pesa za majini zenye masharti mabaya kama pesa zile za baba yangu.

Urithi kama ule wa kuangamiza roho za watu tena watu wanaokuhusu haukuwa urithi unaofaa asilani! Nikajiambia.

Niseme ukweli hizi pesa za majini ziliniendesha puta kweli kweli. Ziliniendesha puta kwa sababu nilizikataa lakini niliamini kuwa zingeniendesha puta hata kama ningezikubali.

Kwa upande wangu nilipania kufa na kupona kuhakikisha kuwa urithi wa pesa zile unanitoka ingawa mpaka muda ule nilikuwa sijui ningefanya nini.

Baada ya siku ile zilipita siku tatu. Nilikuwa nikifikiria nifanye nini. Katika siku zote hizo tatu nilikuwa nikiwapelekea chakula wale wahanga waliokuwa kule pangoni.

Siku ya nne yake ndipo nilipokutana na mtu mmoja ambaye alinipa matumaini kidogo. Nilikutana naye kwenye mkahawa ambako huenda kula chakula kila siku.

Ilikuwa subuhi, nilikwenda kwenye mkahawa huo kunywa chai. Wakati nakunywa chai kulikuwa na watu wawili ambao pia walikuwa wanakunywa chai kibakuli cha maharege na kipande cha mkate wa ajemi huku pembeni wakiwa  na kikombe cha chai ya rangi, walikuwa wakizungumza kuhusu mwenzao mmoja aliyeponeshwa kichaa na mganga wa majini.

“Alikuwa amepigwa jini, yule jini alitolewa mbele yetu. Hivi sasa huyo bwana ni mzima kabisa” Mtu mmoja akamwambia mwenzake.

“Kumbe kile kichaa kilikuwa  ni cha jini?” Mwenzake akamuuliza.

“Tena jini mwenyewe alitumiwa na ndugu yake”

“Walikuwa wanagombania nini?”

“Wanagombania nyumba ya urithi”

“Umtie mwenzako kichaa kwa sababu ya nyumba tu!”

Wakati watu hao wakizungumza, mimi nilikuwa nikiwasikiliza. Yule mtu aliyekuwa akielezewa mkasa ule alitangulia kuondoka akabaki yule aliyekuwa akieleza.

Nilipoona yupo peke yake nikamwambia.

“Samahani, nilikusikia ukizungumza kuhusu mganga aliyemtoa mtu jini”

“Ndiyo nilikuwa ninamueleza yule rafiki yangu kuhusu mwenzetu mmoja aliyekuwa na kichaa” Yule mtu akanijibu.

“Hivi sasa amepona kabisa?”

“Amepona, ni mzima anaendelea na shughuli zake”

“Nilikusikia  ukisema alikuwa ametupiwa jini?” nikamuuliza yule mtu.

“Ndiyo, alitupiwa jini na ndugu yake lakini ametolewa na huyo mganga”

“Inaonekana huyo mganga ni hodari sana?”

“Kwa kweli ni hodari, sisi hatukutarajia kama angeweza kumponesha yule mtu. Alidumu na kichaa kwa miaka miwili”

“Sasa ningekuomba unielekeze kwa huyo mganga, na mimi nina matatizo yangu kuhusiana na majini”

“Naweza kukupeleka hadi nyumbani kwake, ni mtu ambaye tunafahamiana”

“Kwa kweli nitakushukuru sana”

Tulipomaliza kunywa chai, yule mtu alinipeleka hadi kwa huyo mganga.

Alikuwa ni ustaadhi moja aliyekuwa amevaa kanzu nyeupe na kofia iliyodariziwa.

“Karibuni” akatukaribisha.

Yule mtu niliyekwenda naye alimueleza kuwa alikuwa amenipeleka mimi ili aweze kunisaidia.

“Naomba umsikilize, ana matatizo yake”

“Sawa. Nitamsikiliza”

Baada ya hapo yule mtu aliyenipeleka akaondoka na kuniacha. Nikamueleza yule ustaadhi matatizo yaliyokuwa yananikabili kuhusiana na zile pesa za majini.

Wakati namueleza Ustaadhi huyo alikuwa ametulia kimya akinisikiliza kwa makini. Ule utulivu wake peke yake ulinipa matumaini.

Nilimuelezea kila kitu kuhusiana na zile pesa pamoja na wale watu waliotolewa muhanga kule pangoni ambao nilikuwa ninawapelekea chakula kila siku.

Sikutaka kumueleza kuhusu yale yaliyomkuta yule mganga wa kwanza kwa kuogopa ningemtia hofu.

Ustaadhi baada  ya kunisikiliza aliniambia.

“Fedha za majini zipo. Kuna feha ambazo majini wanakupa kwa kukuchunuka wao wenyewe lakini pia kuna fedha ambazo watu wanaozitaka hupewa masharti na majini na wakikubaliana nao hupewa pesa hizo”

Ustaadhi alinyamza kidogo lakini nilijua kuwa kulikuwa na kitu ambacho alitaka kunieleza.

“Sasa kama alivyokueleza huyo jini aliyekuwa na baba yako kuwa baba yako alikwenda Zanzibar mahali panapoitwa Kisima cha Giningi na kuomba kupata pesa hizo kwa  masharti ya kumtoa kafara mke wake na kumiliki mke wa kijini” akaendelea kunaimbia baada ya kimya kifupi.

“Ndiyo hivyo” nikamjibu.

“Hapo Kisima cha Giningi, mimi niliwahi kufika. Ni sehemu ambayo hufanyika matambiko na mambo ya kiasili. Ni sehemu ambayo huaminika kuwa ni ya uchawi na majini”

“Kumbe wewe umeshawahi kufika mahali hapo?’ nikamuulliza.

“Nimeshawahi. Nilikwenda kumuagua mtu. Huyo mtu niliondoka naye hapa hapa. Uganga wake ulitakiwa kufanyika mahali hapo. Nikaenda naye”

“Kwanini uganga wake ulitakiwa kufanyika mahali hapo?’

“Ni kwa sababu jini aliyekuwa ametumiwa alinunuliwa mahali hapo. Na jini huyo alitoa sharti kwamba aende akatolewe mahali hapo hapo alipotoka”

“Na ni kweli alitoka?”

“Ndiyo alitoka”

“Sasa utanisaidiaje  hili tatizo langu?”

“Nikwambie ukweli tatizo lako ni gumu. Kama nitajidai kuwa naweza kukusaidia ninaweza kupata matatizo kwani hao majini wanaokalia hizo pesa ni majini hatari. Ni majini wa jamii ya Subiani. Sisi huwaita Subiani Damisi au jini maiti. Wanaweza kukukata mara moja”

Ustaadhi huyo aliponiambia hivyo alinitisha. Uso wangu ulifadhaika hapo hapo.

Hapo nikaona nimuhadithie kile kisa cha yule mganga aliyetandikwa bakora.

Utaadhi huyo alipokisikia kisa hicho aliangua kicheko.

“Huyo mganga alipata tamaa. Alitaka kuzichukua pesa hizo akiamini kuwa alikuwa na majini wanaoweza kumlinda. Lakini huyo jini wa baba yako alipomfuata, majini wa huyo mganga walisambaratika. Ni bahati yake alitandikwa bakora. Angeweza kumuua kabisa”

“Kwa hiyo utanisaidiaje” nikamuuliza tena mganga huyo huku sauti yangu ikiwa imenywea.

“Sikufichi, hakuna mganga yeyote atakayeweza kukusaidia kwa tatizo hilo labda akudanganye tu”


Itaendelea kesho Usikode Uhondo huu

Tuesday, October 24, 2017

SIMULIZI, TAMAA MBELE MAUTI NYUMA SEHEMU YA 9

SIMULIZI

TAMAA MBELE, MAUTI NYUMA 9

ILIPOISHIA

Eneo la Lang’ata lilikuwa kando kidogo ya jiji hilo. Lilikuwa eneo linaloishi watu wa vipato vya chini kama Herieth. Lwanzo alimpeleka msichana huyo hadi mlangoni mwa nyumba aliyokuwa anaishi.

Lakini walikuta kitu kilichowashitua.

Kwanza waliona gari la polisi lililokuwa limesimama pembeni mwa mlango. Halafu waliona polisi watatu wakitoka ndani ya nyumba hiyo pamoja na mtu mmoja aliyevaa kiraia ambaye alikuwa akifoka.

“Tutamkamata tu hata ande wapi. Kwao ninakujua ni Kiambu na hana pengine pa kukimbilia!”

“ Haa! Njoroge yule!” Herieth akamaka na kugwaya

“Amefuata nini nyumbani kwako?” Lwanzo akamuuliza.

Msichana akabetua mabega yake.

“Sijui. Tena amekuja na polisi!”

SASA ENDELEA

Lwanzo alilisimamisha gari nyuma ya gari la polisi.

“Hebu tushuke, tuwasikilize” lwanzo akamwambia Herieth huku akifungua mlango wa gari.

“Sijui huyu mwanaume ananitafuta nini mimi” Herieth alilalamika.

“Shuka tu, kama ni kesi yenu, tayari iko mahakamani. Hakuna sababu yoyote ya kuwa na wasiwasi”

Herieth akafungua mlango. Wakati anashuka kwenye gari, mtu aliyekuwa anafoka alimuona.

“Huyo hapo amefika “ akasema huku akimnyooshe kidole Herieth.

“Wewe Njoroge unanitafuta nini lakini…?” Herieth alimuuliza kwa hasira baada ya kushuka kwenye gari.

“Unajua wewe uko huru kwa dhamana, leo ulitakiwa kufika mahakamani lakini hukufika, umekiuka dhamana yako!”

“Wewe inakuhusu nini?”

Lwanzo akaingilia kati.

“Msibishane. Huyu msichana wakati anakuja mahakamani asubuhi alipata ajali ya gari, ametenguka mguu. Mimi ndiye niliyemsaidia kumpeleka hospitali”

“Sasa sisi hatujui. Tunajua kuwa amekiuka dhamana. Polisi wamekuja kumkamata”

“Lakini Njoroge hii ni kazi ya polisi na mahakama, wewe inakuhusu nini?” Herieth akafoka.

“Herieth nyamaza msogombane” Lwanzo alimtuliza.

“Anajifanya hodari sana wa kusema lakini safari hii jeuri yake itakwisha” Njoroge alimwambia Herieth kwa jeuri.

“Wewe unatakiwa kukamatwa kwa sababu mahakama haina taarifa kuwa umepata ajali. Sisi tumekuja kukukamata” Mmoja wa wale polisi akamwambia Herieth.

“Ndio mumkamate mkamuweke ndani hadi kesho atakapofikishwa tena mahakamani chini ya ulinzi wa polisi” Njoroge akasema.

“Hapa tunatoka mahakamani. Ameshatoa taarifa na ametakiwa kufika tena kesho” Lwanzo akawambia.

Polisi mmoja  aliposikia hivyo alimgeukia Njoroge.

“Kama mahakama ina taarifa kuwa alipata ajali hatuwezi kumkamata tena” akamwambia.

“Wewe angalia sana!” Njoroge akamwambia herieh huku akimnyooshea kidole cha onyo.

Herieth hakumjibu kitu, alimtazama tu kisha akapanda kwenye baraza ya nyumba. Njoroge na wale polisi walishuka kwenye baraza wakajipakia kwenye gari na kuondoka.

“Karibu ndani kaka” Herieth akamwambia Lwanzo.

“Asante. Sitaingia ndani. Nitaishia hapa ila kesho asubuhi nitakufuata hapa nikupeleke mahakamani”

“Sawa. Asante kaka”

“Haya kwaheri”

“Karibu sana”

Lwanzo akarudi kwenye gari akaliwasha na kuondoka.

Wakati akiendesha kurudi nyumbani kwake aliwaza kwamba sheria zimeshindwa kuzuia unyanyasaji dhaidi ya wanawake kwa sababu pesa imewekwa juu ya sheria.

Aliendelea kujiambia, kwa sababu ya pesa mtu anaweza kutumia hata vyombo vya dola kumdhalilisha binaadamu mwenzake bila huku akijua fika kuwa hana kosa.

“Udhalilishaji dhidi ya wanawake bado ni tatizo ambalo linahitaji kufanyiwa kazi na jamii nzima” Lwanzo akajiambia.

Hata hivyo alikuwa amepanga kumsaidia yule msichana hadi dakika ya mwisho ili ahakikishe kuwa haki imetendeka.

Herieth baada ya kuingia chumbani kwake alikaa kwenye kochi na kuanza kuufikiria mguu wake. Alijiambia alipoondoka asubuhi mguu wake ulikuwa mzima kabisa na hakufikiria kuwa angerudi nyumbani akiwa na P.O.P.

“Kweli binaadamu haishi kuumbwa” alijiambia huku akimshukuru Lwanzo, mtu ambaye hakuwa akimfahamu kabla, kwa msaada aliompa kumpeleka hospitali na kisha kumuwekea wakili.

“Kama si yule kaka, sijui ningekuwa katika hali gani leo?” alijiuliza bila kupata jibu.

Taratibu alianza kukumbuka jinsi wazazi wake walivyofariki huko kwao Kiambu na yeye kuamua kwenda jijini Nairobi kutafuta kazi. Alifika Nairobi akiwa na nguo moja tu ya akiba aliyokuwa ameitia kwenye mfuko wa plastiki.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kufika katika jiji hilo na lengo lake lilikuwa kutafuta kazi, kazi yoyote tu ambayo angejaliwa kuipata, iwe kazi ya ndani au ya uchuuzi wa vitu vidogo vidogo.

Ilimchukua karibu saa nzima kuzunguka katika eneo la stendi la Nairobi akiwa hajui aende wapi. Alikuwa akizungumza na kila msichana aliyemuona anafanya biashara ndogondogo.

Hatimaye alikutana na msichana mmoja aliyekuwa akitembeza  vitu vidogo vidogo.

“Naweza kupata kazi kama yako?’ akamuuliza.

“Kwani wewe unatoka wapi?”

“Natoka Kiambu, ndio nimefika sasa hivi”

Msichana huyo aliyeonekana kukomaa lakini mwenye umbo dogo alimtazama Herieth kuanzia kichwani hadi miguuni.

“Unataka kazi?” akamuuliza.

“Unaweza kunipatia?”

“Mimi pia nimeajiriwa kuuza hivi vitu, si kazi yangu”

“Na mimi pia nahitaji”

“Usifikiri ni rahisi, hapa haturuhusiwi kufanya biashara ndogo ndogo tunaibia tu, askari wa jiji wakija tunakimbia. Utaweza?’

“Nitaweza”

“Basi subiri nikiondoka nitakupeleka kwa mama mmoja anayetaka msichana wa kumuuzia biashra yake”

Ndipo Herieth alipopelekwa kwa mama mmoja wa Kijaluo ambaye alimwambia Herieth kuwa alikuwa anataka msichana wa kumsaidia katika kazi yake ya kuuza majungu katika soko moja lililokuwa kando kidogo ya jiji la Nairobi eneo la Kibera.

“Mimi sichagui kazi. Kazi yoyote utakayonipa nitafanya” Herieth alimwambia mwanamke huyo ambaye alimpokea Herieth na kumuajiri kazi ya kuuza majungu.

Herieth hakumaliza hata mwezi mmoja, akajakukutana na msichana mmoja aliyeitwa Sara ambaye alikuwa akiishi jirani na mwanamke huyo wa Kijaluo.

Herieth na Sara wakawa marafiki.

“Kwani mwenzangu unafanya kazi wapi?” Siku hiyo Herieth akamuuliza Sara.

“Nauza baa”

“Huyu mwanamke ninayemfanyia kazi yake ananinyanyasa sana. Nikipata mahali pengine nitamkimbia”

“Utaweza kuuza baa”

“Kwanini nisiweze?”

“Tena una umbo zuri la kuvutia wateja, nikikupeleka kwa tajiri yetu atakupokea mara moja”

“Sasa unajua tatizo ni nini?”

“Ni nini?”

“Ni mahali pa kulala. Hivi sasa nalala kwa yule mwanamke, nikiacha kazi kwake itabidi niondoke kwake”

“Kama ni kulala tu si tatizo, utala na mimi chumbani kwangu”

Siku ya pili yake Herieth akamtoroka yule mwanamke wa Kijaluo. Sara alimpeleka mjini katika baa aliyokuwa anafanya kazi ya ubaamed.

Mmiliki wa baa hiyo ambaye alikuwa ni mtumishi wa serikalini alipomuona Herieth alimpokea mara moja. Harieth akaanza kazi ya ubaamed.

Ni wakati huo ushamba ulipomtoka Herieth na kuonekana kama msichana wa mjini. Kutokana na pesa ndogo ndogo za chenji alizokuwa akiachiwa na bia za ofa ambazo alikuwa akiziuza kwa wateja wengine kwa kisingizio kuwa hawaruhuiwi kulewa wakiwa kazini, mara moja Herieth alibadilika. Aliweza kununua nguo za thamani na kuweza kujiwekea akiba.  Urafiki  wake na sara ukazidi kuwa mkubwa.

Siku moja  Sara akataka kumchuuza mwenzake kwa mwanaume aliyekuwa akimtaka.

“Kuna jamaa atakuja usiku ana visenti vyake mbuzi, nataka ukamchune” Sara alianza kumwambia herieth mara tu walipoingia kazini saa kumi na mbili jioni.

“Ni jamaa gani?”

“Atakuja saa tatu usiku utamuona, ameniambia anakupenda sana”



ITAENDELEA kesho Usikose Uhondo huu hapahapa kumekucha.com