Saturday, April 30, 2016

AMKA NA MAGAZETI NA CANDLE EDUCATION CENTRE

Magazeti Yanaletwa Kwenu Kwa Hisani Kubwa ya Kituo Cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, Candle nui Kituo Maarufu Kinachofaulisha Wanafunzi Kidato Cha Pili hadi Sita na Wanaojiendeleza Kielimu. Candle wapo na Hostel na Gari Maalumu la Kuwapeleka Shule, Wapo Tanga Mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746

LEICESTER CITY HAIKAMATIKI

English Barclays Premier League | LOGS

PosTeamPWDLGFGAGDPts
1Leicester City352210363333076
2Tottenham Hotspur351912465263969
3Arsenal361910759342567
4Manchester City35197966343264
5West Ham United351514660431759
6Manchester United34178942301259
7Liverpool341510958451355
8Southampton351591149371254
9Stoke City36139143852-1448
10Chelsea341211115346747
11Everton351014115549644
12Watford35128153642-644
13West Bromwich Albion361011153246-1441
14Bournemouth36118174363-2041
15Swansea City351010153449-1540
16Crystal Palace36109173646-1039
17Newcastle United3689193964-2533
18Sunderland35711174058-1832
19Norwich City3587203561-2631
20Aston Villa3637262772-4516

GOROFA NAIROBI LAPOROMOKA NA KUUWA WATU SITA

Jengo la ghorofa sita limeporomoka Nairobi na kusababisha vifo

Nairobi Nchini Kenya mvua zinazoendelea kunyesha wiki hii zimesababisha vifo ambapo mpaka sasa imeripotiwa watu 15 kufariki na kati ya hao 7 wamefariki baada ya jengo la ghorofa sita kuporomoka usiku wa April 29 2016 eneo la Huruma na zaidi ya watu 120 wameokolewa.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

.
.
.
.
.
.
nairobi 1.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

AFRICAN SPORTS YAIPELEKA KATIKA TUNDU LA SINDANO COASTAL UNION, YAIBAMIZA BAO 1 BILA

 Timu ya African Sports imevunja ngebe za kaka zao Coastal Union baada ya kuifunga bao moja pekee dakika 28 kwa mshambuliaji wake hatari , Ali Ali.
 Bao hilo la mapema lililodumu hadi kipenga cha mwisho kimewaweka katika wakati mgumu Coastal Union na wako katika tundu la shindani la kubaki ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao.



 Mshambuliaji wa Coastal Union, Miraj Adam akimtoka beki wa African Sports ,Issa Shaban wakati wa mchezo ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa uwanja wa Mkwakwani leo




 , Beki wa Coastal Union Hamis Mbwana akimtoka mshambuliaji wa African Sports, Mussa Chambega wakati wa mchezo ligi kuu Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwani Leo.
  Polisi wa kutuliza ghasia (FFU) wakiimarisha ulinzi baada ya washabiki kutaka kufanya fujo baada ya refarii kumpa kadi nyekundu mchezaji wa African Sports, Ali Ali dakika ya 28,wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya Coastal Union na African Sports zote za Tanga  uliochezwa uwanja wa Mkwakwani leo.

SIO BAHARI, NI MAJI YALIYOZINGIRA NYUMBA ZAIDI YA 70 TANGA



 Wakazi wa Magaoni Tanga wakiangalia athari ya mafuriko baada ya mvua kubwa kunyesha kwa masaa 24 na kulazimika kaya zaidi ya 70 kuhamia shule ya msingi ya magaoni.
Kata ya Magaoni kwa miaka mingi imekuwa wahanga wa mafriko na wadau wa mazingira wamedai kuwa maji hayo yaliyozizingira nyumba sio mafuriko bali hayana miundombinu ya kupita.
Wamedai kuwa kila vipindi vya mvua eneo hilo hutuwaa maji kwa vile hayana pa kwenda hivyo kuomba halmashauri ya mipango miji kuchukua hatua za kuchimba mifereji ya kupita maji na kukomesha hofu kwa wakazi wa eno hilo.





WAPENZI WA SOKA TANGA WAINGIWA NA KIWEWE



Tangakumekuchablog
Tanga, WAPENZI na washabiki wa soka  Tanga wameingiwa na kiwewe cha kuzipoteza timu zao tatu kushiriki ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao na kuwataka viongozi wa Mkoa kuungana kutoa msukumo kwa makocha na viongozi ili kushinda michezo iliyoko mbele yao.
Wakizungumza na Mwanaspoti kwa nyakati tofauti leo, Kamishna wa Chama Cha NCCR Magezi Tanga, Ramadhani Manyeko, alisema tatizo liko kwa viongozi kwani wachezaji wamekuwa wakionyesha kandanda safi uwanjani.
Alisema wachezaji wamekuwa wakionyesha mchezo mzuri uwanjani na wamekuwa wakijituma lakini wamekuwa wakikatishwa tama baada ya kukosa ushirikiano hivyo kutaka kipindi hiki cha lala salama kushikamana na kuwa kitu kimoja.
“Ni jambo ambalo huwezi kuamini timu tatu kutoka mkoa mmoja zinachungulia tanuri, hapa kwetu kuna namna na sisi wapenzi wa soka tunawashushia viongozi wetu” alisema Manyeko na kuongeza
“Timu kama Coastal imeifunga Simba  na kutoa upinzani mkubwa kwa Yanga, hapa utasema timu ni mbovu, hebu tuutafute muarubaini kabla kipenga cha kuisha msimu wa ligi” alisema
Alisema endapo timu zote tatu zitateremka daraja soka la Tanga litakufa na ni ndoto kurudi ligi kuu kwa miaka ya karibuni na wachezaji wengi wataibukia timu za nje ya Mkoa huo.
Kwa upande wake shabiki wa mpira mkazi wa Mikanjuni Tanga, Habib Swaleh, aliwataka viongozi wa Serikali na Mkoa kuzipa ushirikiano timu zote tatu, Coastal Union, African Sports na Mgambo ili ziweze kunusurika na janga la kushuka daraja.
Alisema itakuwa aibu uwanja wa Mkwakwani kuchukuliwa na timu za nje na kuufanya uwanja wa nyumbani ilhali zipo timu tatu ambazo zimekuwa zikionyesha upinzani kwa timu shiriki za ligi kuu Tanzania Bara.
Alisema ili kuweza kuzinusuru timu na soka la Tanga ni wajibu wa viongozi wa mpira na viongozi wa Serikali kukaa chini na kutafakari namna ya kuzinusuru timu hizo kutumbukia janga la kushuka daraja.
“Tuko na uwanja mzuri ambao ni wa pili nchini kwa uzuri na ubora lakini tunashuhudia tukiuwacha uote nyasi ili kupata majani ya kulisha ng’ombe na mbuzi” alisema Swaleh
Alisema kama viongozi wako na dhamira ya kweli timu za Tanga timu mbili zinaweza kubaki ligi kuu msimu ujao hivyo wakazi wa Tanga macho yao yako kwa viongozi wa soka na Serikali.
                                                 Mwisho

HADITHI, SITASAHAU NILIVYOGEUZWA PAKA SEHEMU 6

HADITHI, SITASAHAU NILIVYOGEUZWA PAKA

SIMULIZI ZA FAKI A FAKI, 0655 340572

SITASAHAU NILIVYOGEUZWA PAKA

Asubuhi nilipomuuliza, Chausiku alikasirika akaja juu na kuniambia kuwa alikuwa ametoka barazani kupunga upepo kwa sababu ya joto lililokuwemo ndani.

Nikamwaambia haikuwa jambo zuri kutoka nje peke yake wakati wa usiku kwani anaweza kushambuliwa na fisi wanaozunguka ovyo usiku kucha.

Chausiku akanyamaza kimya.

Siku nyingine aliniaga kuwa anakwenda kwa bibi yake mzaa mama yake aliyekuwa akikaa kijiji cha jirani. Akaniambia atalala hukohuko na atarudi kesho yake.

Lakini akanionya kuwa nisifungue chumba chake ambacho alikuwa akikitumia kama stoo yake. Baada ya kile chumba tulichokuwa tunalala alikuwa na chumba kingine ambacho sikupata kukiingia hata siku moja. Alikuwa akiingia yeye mwenyewe tu kuweka vitu vyake pamoja na vyungu alivyokuwa anatengeza.

Siku ile alipoondoka kwenda kumsalimia bibi yake, usiku wake nikaamua kuingia katika kile chumba alichonikataza nisiingie.

Nilivizia watu wote walikuwa wameshalala. Nikafungua mlango na kuingia huku nimeshika taa ya kandili (Chemli) ili niweze kuona.

Hayo niliyoyakuta humo chumbani sikuyatarajia kabisa. Yalikuwa ni maajabu yaliyonishitua sana!

SASA ENDELEA

Nilipoingia mle chumbani nilishituka nilipomuona Chausiku ameketi kwenye kigoda kilichokuwa katikati ya chumba hicho, ameelekea upande ule uliokuwa na mlango.

Alikuwa ametulia kimya na amefumba macho kama aliyekuwa amelala.

"We Chausiku!" nilimuita kwa kugutuka.

"Kelele!" akaniambia kwa sauti tulivu bila kufumbua macho.   "Si nilikuonya usiingie katika chumba hiki?" akaniuliza.

"Nilikuwa natafuta .....nilikuwa natafuta.....!"

"Toka!" akaniambia kwa ukali akiwa bado amefumba macho yake vilevile.

Nikatoka huku nikitetemeka kwa hofu. Nguvu ziliniishia kabisa mwilini.

Huyu mwanamke aliniaga anakwenda kwa bibi yake tangu asubuhi. Kumbe amejifungia humu chumbani kwenye giza na mbu, anafanya nini? nikawa najiuliza.

Nilirudi chumbani mwetu nikaweka ile taa na kuketi kwenye kiti kutafakari. Baadaye nilimuona akiingia mle chumbani huku akicheka.

"Nimekugundua sasa, kwanza wewe si muaminifu na pili muoga" akaniambia huku akiketi kitandani.

"Kwanini unaniambia hivyo?" nikamuuliza.

"Nilikuonya usiingie katika kile chumba. Ulipoona nimeondoka ukaingia. Je ni uaminifu huo?"

Nikanyamaza kimya. Sikuwa na cha kumjibu.Ni kweli kuwa alinionya lakini nilivyoona ameondoka nikaingia. kumbe na mwenyewe alikuwamo humo ndani.

"Halafu wewe ni muoga sana" akaendelea kuniambia.

"Kumbe ulikuwa unafanya nini mle chumbani?" nikamuuliza

"Nilitaka kukupima wewe nione uaminifu wako kwangu na nione ujasiri wako. Sasa nimeshakugundua"

Nikabaki kuguna tu.

Tukalala. Asubuhi kulipokucha nikaenda zangu shambani kwangu. Ilipofika saa saba mchana mke wangu akaja shamba kuniletea chakula.Ilikuwa ni kawaida yetu siku nikienda shamba mke wangu kuniletea chakula.

Wakati ninakula akaniambia kuwa mtoto wa jirani yetu mzee Juma amagongwa na nyoka na hali yake si nzuri. Habari ile ikanishitua kwa sababu huyo mtoto alizoea kucheza barazani mwa nyumba yetu na alikuwa mtoto mcheshi aliyependwa na kila mtu.

"Amegongwa na nyoka?" nikamuuliza mke wangu huku nikishangaa.

"Amegongwa kama saa tano hivi"

"Wapi?"

"Huko nyumbani kwao.Alikuwa akicheza na wenzake kwenye mti,kumbe palikuwa na nyoka akamgonga"

"Nyoka wa rangi gani?"

"Wenzake wanasema ni nyoka wa rangi ya kijani"

"Nyoka wa kijani wana sumu kali sana. Sasa wamempa dawa gani?"

"Babu yake anajua dawa za nyoka, amemchanja akampaka dawa"

"Lakini umesema hali yake si nzuri?"

"Walichelewa kumpa dawa. Babu yake alikuwa shambani, mpaka anakwenda kuitwa, mtoto alikuwa ameshalegea na mguu umevimba"

"Wangempeleka hospitali Songe"

"Mh! watu wa hapa wanaamini zaidi dawa zao za kiasili kuliko za hospitali"

''Lakini kama mtoto amelegea kiasi hicho wangempeleka hospitali tu"

"Nitakwenda kuwashauri wampeleke hospitali"

"Nikirudi nitakwenda kumuangalia"

Nilipomaliza kula mke wangu alichukua vyombo akarudi nyumbani.

Nilirudi kutoka shamba majira ya saa kumi jioni. Sikuona dalili nzuri nyumbani kwa mzee Juma.Nilikuta watu wamejazana barazani na huko ndani kulikuwa na sauti za watu wanaolia. Hapo hapo nikajua nini kimetokea. Niliingia nyumbani mwetu nikaweka jembe. Mama mmoja mkazi wa mle ndani akaniambia  "Nyumba ya pili kumefiwa"

"Nani aliyekufa?" nikamuuliza lakini tayari nilikwisha jua

"Ni Hamisi, mtoto wa mzee Juma.Amegongwa na nyoka asubuhi, wamemchelewesha kumpeleka hospitali hivi jioni amekufa"

"Na mke wangu yuko hukohuko?"

"Tulikuwa naye hukohuko kwenye msiba. Mimi nimerudi mara moja tu kumpikia mume wangu.Je unataka nikuitie?"

"Hapana.Mimi pia nitakwenda hukohuko.Mke wangu alikuja shambani kuniambia kuwa Hamisi amegongwa na nyoka. Nikamwaambia kwanini baba yake hakumpeleka hospitali. Kumbe wamemuacha mpaka amekufa"

"Babu yake alikuja kumpa dawa lakini haikusaidia"

"Nyoka wa kijani wana sumu kali sana"

Baada ya kuzungumza na yule mama nikatoka kwenda kumpa pole mzee Juma na kumuuliza juu ya mipango ya maziko.Akaniambia wamepanga kumzika mtoto wao kesho yake asubuhi.

Asubuhi mimi na mke wangu tukaenda kwa jirani yetu kuhudhulia maziko.Muda ulipowadia jeneza lilibebwa kuelekea eneo la makaburi ambalo halikuwa mbali sana.Tukamzika yule mtoto kisha tukarudi

Siku ile tulishinda nyumbani kwa mzee Juma kumfariji mwenzetu.Mke wangu alikuwa miongoni mwa akina mama waliokuwa wakishughulika kupikia wageni kama ilivyo kawaida ya mahali panapotokea msiba. Ilipofika usiku mimi na mke wangu tukarudi nyumbani kulala.

Nilikuja kushituka usiku wa manane. Nikamuona mke wangu anashuka kitandani. Nikanyamaza kimya na kujifanya kama nimelala.Akajifunga upande wa kaniki kisha akaniita mara tatu.

lakini sikumjibu kitu. Akatoka mle chumbani.Alipotoka na mimi nikashuka kitandani, nikanyata hadi mlangoni kumchungulia. Nikamuona ameingia katika kile chumba cha pili. Baadaye kidogo akatoka, mimi nikarudi kitandani. Akaingia tena mle chumbani na kunichungulia.Mkononi alikuwa ameshika kitu ambacho sikuweza kukiona vizuri kwa sababu nilikuwa namwaangalia kwa kumuibaiba.

Nilitulia kimya pale kitandani, nikasikia akifungua mlango wa nje.Nikainuka na kwenda kumchungulia.Nikamuona anatoka na kuufunga mlango.Nilisubiri kwa dakika chache kisha nikaenda kwenye mlango huo. Nikaufungua taratibu na kumchungulia.Nikamuona anapotea kwenye kiza upande wa kushoto mwa nyumba yetu ambako palikuwa na pori.

Yule msichana anakwenda wapi usiku huu? nikajiuliza kwa mshangao bila kupata jibu. Nikatoka nje na kuufunga mlango.Niliamua kumfuatilia ili nijue anakwenda wapi.

Kulikuwa na baridi l;akini sikuisikia kwa sababu ya kutaharuki. Nilipoingia kwenye lile pori nilimuona Chausiku ametokea upande wa pili wa pori hilo na kuendelea kwenda.Nami niliendelea kumfuatilia taratibu huku nikijifichaficha kwenye miti ili asinione.

Nikaendelea kumfuatilia hadi kwenye eneo la makaburi mahali ambako kwa usiku ule palikuwa panatisha kweli kweli na isingekuwa rahisi kwa mtu yeyote mwenye akili zake timamu kufika mahali hapo wakati ule usiku akiwa peke yake tena bila taa na akionekana hana wasiwasi.

Mh! Makubwa! Haya huyo msichana anakwenda wapi usiku huo? Hebu endelea kufuatilia  hadithi hii ya kusisimua  katika blogy hii hapo kesho.