Friday, July 31, 2015

UZINDUZI JEZI MPYA YA SIMBA NA MADUKA YAKE LEO

Club ya Simba SC kwenye headlines moja na Real Madrid, Barca na Manchester United.

BarcelonaKila mwaka klabu ya Simba huwa na utamaduni wa kufanya tamasha la kutambulisha jezi, wachezaji na mipango mingine ya klabu hiyo.Tamasha hilo linalojulikana kama Simba Day  kwa mwaka huu haitakuwa Simba Day bali ni wiki ya Simba. Mabadiliko hayo yametokana na maboresho kadhaa ambayo yamefanywa na uongozi.
Haji-Manara-SimbaUzinduzi huo utafanyika siku ya Jumamosi  August 1 katikati ya jiji la Dar Es Salaam saa 4:30, kwa mujibu wa mkuu wa idara ya habari ya Simba, Haji Manara amethibitisha kufanyika kwa mambo mbalimbali ikiwemo uzinduzi wa maduka yatakayouza jezi za Simba, mabegi, kalamu, kofia na vitu vingine mbalimbali vyenye logo ya Simba ikiwa ni sehemu nyingine ya kuuongeza uchumi wa club.
Kikosi cha SimbaManara amethibitisha kuwepo kwa maduka ya bidhaa za klabu sehemu mbalimbali ikiwemo Mlimani City, huku kilele cha Wiki ya Simba itakuwa August 8 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam kwa Simba kucheza mchezo wa kirafiki na klabu ya FC Leopard ya Kenya. Hata hivyo Manara amekanusha madai yanayosambaa kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi Laudit Mavugo hatokuja Simba.
Simba-Sports-Club“Mavugo nimeona kwenye gazeti nimesikitishwa sana, wiki iliyokwisha gazeti hilohilo liliandika Okwi anarejea Msimbazi hata chezea tena klabu yake ya Denmark wakaandika bila kuweka source bila kubalance story nawahakikishia Mavugo siku ya tarehe 8 August atacheza mechi ya Simba day “>>> Haji Manara
simba-sports-club-dylan-kerr1Ungana nami kwa habari motomoto za papo kwa papo , ni ha hapa hapa tangakumekuchablog

KIPENGA FOMU ZA URAIS CHAPULIZWA

Hii ndio Ratiba ya Kuchukua Fomu za Urais kwa Wagombea wa Vyama Vyote TZ…

1 Tayari headlines za majina ya waliopitishwa na Vyama Kugombea Urais zilichukua uzito sana kwenye stori kubwa Tanzania kwa muda mrefu, baada ya hatua hiyo sasahivi kinasubiriwa kuona Wagombea hao waliopitishwa kuanza kuchukua Fomu kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Kwenye maelezo ya Jaji Damian Lubuva Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi >>> “Tunaanza kutoa Fomu kwa wale wanaogombea urais, kesho (leo) UPDP watakuja kuchukua fomu saa tatu asubuhi wamesema hawana shamrashamra… TLP wao watakuja saa sita mchana wanakuja kwa shangwe… DP wao wanakuja saa nane mchana pia nao wamesema watakuja kwa shangwe pia” >>>>
4
Jumanne August 4 watakuja CCM saa sita mchana watakuja kwa shangwe kama wengine… Jumatano  watakuja ADC saa tatu asubuhi, wao hakuna shamrashamra baada ya hapo watakuja TADEA saa nne asubuhi pia wao hawana shangwe” >>>>
August 17 watakuja ACT- Wazalendo saa tatu asubuhi wanakuja kwa shange pia… muda wa kuandikisha wapigakura kwa mfumo wa BVR unaisha rasmi tarehe August 8 na baada ya hapo Ratiba ya Tume itaendeleakuruhusu Uchaguzi Mkuu” >>>> Jaji Damian Lubuva, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.

MABILIONE 5 LIGI KUU UINGEREZA

Hawa ndio wakali wengine watano Ligi ya Uingereza wenye utajiri mkubwa zaidi, na pichaz zao…

top-5-best-ios-features
Mastaa wa soka wana utajiri wao wa kutosha tu, unaambiwa kutokana na kazi nzuri wanayoifanya hata thamani yao inaongezeka vilevile, ukisikia staa wa soka kanunuliwa kwa pound. Mil 100 Uingereza basi uwe na jibu kabisa kwamba YES jamaa ni jembe la kazi !!
Lakini thamani yake haiishii uwanjani, hata nje ya Uwanja jamaa wa Kampuni kama Nike, PUMA, ADIDAS hawamwachii apite hivihivi wasimpe hata dili moja eti?
Soka na maisha yao nje ya Uwanja vinasababisha wajikusanyie pesa na wawe na utajiri wa kutosha kabisa… karibu uipitie hawa watano ambao wametajwa kuwa na utajiri wa juu zaidi kwenye List ya mastaa wanaochezea Ligi Kuu Uingereza!!
mundial-brasil-2014-1824419w620
No.5: Utajiri wake unakadiriwa kuwa kama Dola Milioni 55, umri wake ni miaka 27 tu lakini tayari kaonesha Ulimwengu jinsi ambavyo ana uwezo mkubwa Uwanjani kitu ambacho kimempa thamani ya juu pia kati ya mastaa wa Uingereza… Jamaa anachezea Klabu ya Manchester City.
bastian-schweinsteiger
No.4: Bastian Schweinsteiger, moja ya Vifaa vya nguvu ambavyo vimeenguliwa kutoka Bayern Munich msimu huu na kujiunga na Man United.. Kama akionesha uwezo zaidi basi huenda akapanda chati na kuuongeza utajiri wake ambao kwa sasa ni kama Dola Mil. 60 hivi.
Chelsea captain John Terry arrives at court for the closing arguments in his racial abuse trial
No.3: Japo umri wake ni mkubwa, miaka 34 lakini hata akisema anastaafu leo Klabu ya Chelsea itakuwa na heshima kubwa kwake kwa mchango mkubwa alioutoa kwa Klabu hiyo kwa miaka mingi ambayo ametumia akiichezea Klabu hiyo. Yuko vizuri pia kwenye nafasi ya tatu akiwa na utajiri wa Dola Mil. 65.
Yaya-Toure-Michael-Regan-Getty-Images-e1438201494864
No.2: Yaya Toure ni nafasi ya pili na ndio staa wa Soka pekeake kwenye hii list ya watano ambae ana asili ya Afrika. Utajiri wake ni kama Dola Mil. 75.. Jamaa ni mmoja wa vichwa ambavyo vinategemewa sana Man City.
soc_waynerooney_640
No.1: Mkali wa Uingereza na mwenyeji wa hapohapo yani.. Kichwa kinachofanya vizuri Manchester United, na ni mmoja ya wakali ambao Uingereza na Man United wanajivunia sana, ukali wake umefanya akae #1 na utajiri wake ni Dola Mil. 110 akimuacha Yaya kwa Dola Mil. 35 hivi !!
Ungana nami kila wakati kupata habari, matukio na michezo papo hapo , ni hapa hapa tangakumekuchablog

AZAM YATINGA NUSU FAINAL

Matokeo ya mechi za nusu fainali, Azam FC katinga fainali? jibu lipo hapa

Nusu fainali ya michuano ya kombe la Kagame imechezwa July 31 kwa timu nne kushuka dimbani, huku timu mbili pekee zitakazoshinda ndio zitakazo cheza mchezo wa fainali jumapi ya August 2 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.
AZAM
Azam FC imekuwa timu ya pili kutinga fainali baada ya kuifunga klabu ya KCCA ya Uganda kwa goli 1-0 bao pekee lililofungwa na Farid Mussa dakika ya 76. Hivyo Azam FC itacheza mchezo wa fainali na klabu ya Gor Mahia ya Kenye ambayo imeifunga Al Khartoum ya Sudan kwa goli 3-0.
Gor-Mahia-team-photo-vs-Congo-UnitedUngana nami kila wakati kukupatia habari, matukio na michezo hapa hapa tangakumekuchablog

MASTAA WA LIVERPOOL WAKIJINOA

Cheki mastaa wapya wa Liverpool walivyoipania ligi kuu…

bbbb
Agosti 8 pazia la ligi kuu ya Engaland linafunguliwa rasmi.
Klabu zote zimeonekana kujipanga vyema ili kukabiliana na mikiki ya ligi hiyo, lakini wachezaji wapya wa Liverpool Christian Benteke na kiungo Mbrazil Firmino wameonyesha wamepania kuiletea klau yao mambo mazuri.
Katika mazoezi ya Liverpool, wachezaji hao na wenzao wamekuwa wakifanya kila kitu kwa juhudi na kuonyesha kupanga kuleta mabadiliko makubwa katika kikosi chao ambacho wao ni sura mpya.
Watazame wakiwa kwenye mazoezi yao…
bente
bente2
bente3
bente4
bente5
bente7

try

Kwa habari, matukio na michezo, ungana nami hapa hapa tangakumekuchablog

WAKALI KUPEPETANA WEMBLEY

Ngao ya Jamii Ligi Kuu England ni Chelsea Vs Arsenal Jumapili hii,wengine je?..

ligi
Kipenga cha kuanza kwa ligi kuu ya England msimu mpya kinatarajia kupulizwa jumapili hii wakati mabingwa Chelsea watakapovaana na Arsenal katika mchezo wa ngao ya jamii.
Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa Wembley,London.
Ligi kuu ya Uingereza inatarajia kuanza Agosti 8 kwa michezo sita ambapo Manchester United vs Tottenham katika uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford wakati Bournemouth vs Aston Villa, Norwich city vs Crystal palace ,Everton vs Watford na Chelsea vs Swansea city.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

OBAMA ZAWADI ZA KENYA HAKIONDOKA NAZO

Rais Obama hakubeba zawadi yoyote aliyopewa nyumbani kwao Kenya.. Sababu ni hii

BO UK
Mgeni Rais Obama alivyoenda kwao Kenya, walijipanga na zawadi kibao ili mtu wao arudi nazo kwa ajili ya Kumbukumbu Marekani… alienjoy vingi Kenya ikiwemo dance ya nguvu na wakali wa Sauti Sol, lakini kumbe zile zawadi hata hakuondoka nazo !!
BO Gifts
Hata usiwaze kwamba labda Barack Obama alidharau zawadi ya Kinyago cha Tembo pamoja na picha mbili za kuchorwa kwa mkono, ishu ni kwamba itifaki au protocol ya Ikulu ya Marekani hairuhusu Rais wao kupokea zawadi yoyote toka kwa Kiongozi yoyote nje ya Marekani !
Hizi ndio pichaz za zawadi zenyewe alizopewa Rais Obama toka kwa Rais Kenyatta.
BO I
BO II
BODuh, japo zawadi hizo hazikuingia kwenye Jet ya Air Force One ya Rais Obama lakini zawadi nyingine aliyoifurahia ni hii, yeye Rais Kenyatta na mkewe.

Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

UZI WA STAND UNITED HUU HAPA

Aina ya jezi za kisasa watakazotumia Stand United msimu ujao picha zipo hapa

Ligi Kuu soka Tanzania bara kwa miaka kadhaa nyuma kabla ya kuzaliwa kwa klabu ya Azam FC ilikuwa ni ligi ambayo ina ushindani wa kweli kwa timu mbili pekee Simba na Yanga ndizo zilizokuwa na uwezo wa kutwaa taji la Ligi Kuu kwa kupokezana kama sio timu moja wapo kutwaa mara mbili mfululizo.
jezi 2
Hali hii haikutokana kwa sababu ya ukubwa wa vilabu, hali hii haikutokana kwa sababu ya kuwa na mashabiki wengi ila ukweli ni  vilabu vingi vilikuwa vikikumbwa na tatizo la kifedha mfano msimu mmoja nyuma tuliwahi kusikia maisha na mazingira mabovu waliokuwa wanaishi wachezaji wa Stand United kitu ambacho kingeweza kuwa kigumu kuleta ushindani kwa Yanga, Simba na Azam FC.
jezi 3
Baada ya kampuni ya ACACIA inayojishughulisha na masuala ya uchimbaji wa madini kuidhamini klabu ya Stand United, yameanza kutokea mabadiliko chanya kiasi kwamba msimu ujao inawezekana Stand United ikafanya vizuri. Baada ya kumleta kocha wa kifaransa Patrick Liewig kuinoa klabu yao, July 30 imeonyesha aina ya jezi za kisasa itakazotumia msimu ujao.
jezi 1
ACACIA ni kampuni inayomiliki migodi mitatu ya uchimbaji dhahabu  Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara, imeingia mkataba wa udhamini na Stand United katika kipindi cha miaka miwili.

SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO, JULY 31TZ

Uchambuzi huu wa magazeti unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Euducation Centre Tanga, kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza kielimu. Kituo kinatoa kozi mbalimbali za kitaaluma na kielimu. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746

HOOOT
MWANANCHI
Wabunge wawili waliohama CCM hivi karibuni, James Lembeli na Ester Bulaya wamepitishwa katika kura za maoni kuwania ubunge kupitia chama chao kipya.
Wakati Lembeli akipitishwa kwa kura za kishindo kuwania ubunge katika Jimbo la Kahama Mjini, Bulaya alishinda katika nafasi ya viti maalumu baada ya kushindwa katika kinyang’anyiro cha Jimbo la Bunda Mjini.
Wanasiasa hao sasa wanasubiri uteuzi wa Kamati Kuu ya Chadema utakaofanyika Agosti 5 na 6.
Katika uchaguzi huo wa juzi, mbunge huyo wa zamani wa Kahama aliwabwaga wenzake 13 aliogombea nao akipata kura 168 kati ya 262 zilizopigwa, akifuatiwa na John Katibu aliyepata kura 45, Peter Shita (17) na Emmanuel Madoshi aliyepata kura 10.
Wengine ni Muta Nyerere (4), Felician Maige (4), Zacharia Obadia (3), Tadeo Mwati (2), Arnold Mtajwaka (2), Prosper Denga (2), Deusdedit Madinda (1), Reuben Macheyeki (1). Victor Mbwana na Richard Makingi waliambulia patupu. Katika uchaguzi wa viti maalumu, Winfrida Mwinula alishinda kwa kura 34 akifuatiwa na Salome Makamba aliyepata kura 30.
Kama isingekuwa ni kura za maoni za viti maalumu zilizomfuta machozi, Bulaya alikuwa tayari ametupwa nje baada ya kuanguka katika Jimbo la Bunda Mjini.
Bulaya aliyekuwa miongoni mwa makada saba wa chama hicho waliokuwa wanawania kuliwakilisha jimbo hilo, alipata kura 37 kati ya 182 zilizopigwa akiwa nyuma ya Pius Masururi aliyeibuka mshindi kwa kura 65 na  Magembe Makoye aliyepata kura 40.
Baadaye katika mkutano wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), uliofanyika baadaye usiku, Bulaya alipata kura 71 kati ya 110 zilizopigwa na kuwabwaga Godliver Masamaki aliyepata kura 31, Joyce Sokombi (4), Minza Shani (3), Dk Jane Nyamsenda (1) na Alice Wandya aliyeambulia patupu.
Awali, Bulaya alikwaa kisiki baada ya jina lake kuwa miongoni mwa waliokatwa na kamati ya utendaji inayosimamia majimbo hayo wakidaiwa ni wageni katika chama; wapenda fujo na matabaka, akiwa pamoja na Chacha Nyamhanga, Sulemani Daudi lakini walirudishwa kundini baada ya kikao cha viongozi na watiania.
Katika Jimbo la Bunda Vijijini, Sulemani Daudi aliibuka mshindi kwa kura 84 kati ya 127 zilizopigwana kuwashinda John Masenza aliyepata kura 14, Dk Lucas Webiro (11), Frank Mongateko (8), Edgar Chibura (5) na Mathias Bandio aliyepata kura mo
MWANANCHI
Tume ya Uchaguzi (NEC) leo imetangaza kuongeza siku nne zaidi za uandikishaji wa wapigakura kwa kutumia teknolojia ya BVR baada ya idadi kubwa ya wakazi wa Dar es Salaam kuitikia wito wa zoezi hilo.
Awali zoezi hilo lilikuwa likamilike kesho, Julai 31, lakini sasa litaendelea hadi Agosti 4, mwaka huu ili kukabiliana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kujiandikisha.
Kwa mujibu wa chombo hicho chenye mamlaka ya kusimamia shughuli zote za uchaguzi nchini, hadi jana, zaidi ya wakazi 1,000,000 walikuwa wamekwishaandikishwa jijini Dar es Salaam.
Ikizingatia matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Nec inatarajia kuandikisha jumla ya wakazi zaidi ya 2.8 milioni wa jiji hilo lenye idadi kubwa ya watu nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva, hadi sasa jumla ya zaidi ya watu 18 milioni wamekwishajiandikisha wakati tume ilitarajia kuandikisha watu kati ya 22 milioni na 23 milioni.
NIPASHE
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), inatarajia kuanza kuwasaka viongozi wa umma waliotumia nafasi zao vibaya ikiwamo kuiba na kujilimbikizia mali ndani na nje ya nchi.
Viongozi hao watasakwa na Takukuru kupitia kitengo maalum kilichoanzishwa mwaka jana ambacho kimeanza kupewa mafunzo nchini Uingereza.
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward  Hoseah (pichani), aliyasema hayo jijini Dar es Salaam juzi alipokuwa akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari.
Dk. Hoseah aliyasema hayo muda mfupi baada ya kufungua mafunzo ya watumishi wa Takukuru ambao wapo katika kitengo hicho ili kuwajengea mbinu na uwezo wa kufanya uchunguzi dhidi ya viongozi walioiba na kujilimbikizia mali.
Alisema kitengo hicho cha Takukuru pia kitakuwa na kazi ya kupambana na masuala ya utakatishaji wa fedha haramu kwa kuwa tatizo hilo linazidi kukua hapa nchini.
Aliongeza kuwa kitengo hicho kilianzishwa rasmi mwaka jana, lakini hakikuanza kazi yake kutokana na kuchelewa kupatikana mtalaam wa kutoa mafunzo kwa watumishi hao.
”Tumejizatiti kukabiliana na viongozi wa umma waliojilimbikizia mali kwa kutumia watalaam wetu ambao wanapatiwa mafunzo,” alisema.
Dk. Hoseah alisema huu ni mwanzo na kwamba watahakikisha wanafanya kazi vizuri ili kuwabaini watu walioiba na kujilimbilikizia mali huku akisema kwamba sheria ni msemeno
Kuhusu wanasiasa wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa hususan katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, Dk. Hoseah alisema mtu yeyote asithubutu kufanya hivyo kwa kuwa Takukuru imesambaa kila wilaya na kwamba watakamatwa.
”Hawa wagombea wasifanye mchezo mchafu, ninawaonya kwa kuwa tutawakamata popote walipo,” alisisitiza.
Aliwaonya wanasiasa wanapita maeneo mbalimbali na kuanza kuchonga barabara na kutoa zawadi nyingine kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa na Takukuru itawashughulikia.
Aliongeza kuwa mtu yeyote atakayepindisha sheria kwamba Takukuru ipo macho muda wote na itawamulika wanasiasa ama wapambe wao ambao watataka kuwahonga wananchi kuwashawishi wawapigie kura.
Hata hivyo, kauli ya Dk. Hoseah imekuwa ya kawaida kutolewa kwa kuwa aliwahi kutangaza vita na wala rushwa wakubwa hapa nchini huku akiahidi kuwaburuza mahakamani, lakini mpaka leo hakufanya hivyo.
NIPASHE
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amekanusha kumshushia kipigo Dk. Joseph Chilongani, ambaye ni mgombea mwenzake katika mchakato wa Chama Cha mapinduzi (CCM), kupata mgombea ubunge Jimbo la Kongwa.
Awali ilidaiwa kuwa Jumatatu jioni Ndugai, alitumia fimbo kumpiga Dk. Chilongani, ambaye alipoteza fahamu kabla ya kupelekwa hospitali ya wilaya hiyo, ambako aliendelea na matibabu mpaka jana aliporuhusiwa.
Mganga Mkuu wa Wilaya, Festo Mapunda, alilieleza NIPASHE jana kuwa walimruhusu kutokana na hali yake kiafya kuwa nzuri.
Naye Naibu Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, hakuwa tayari kueleza ikiwa mpaka jana alikuwa amepokea taarifa rasmi ya tukio hilo kutoka kwa walalamikaji badala yake alisema Dk. Chilongani, jana aliendelea na kufanya kampeni kama kawaida.
Madai dhidi ya Ndugai yalielezwa na Dk. Chilongani, kuwa sababu ya mtafaruku huo ilikuwa mzozo uliyoibuka kati ya Ndugai na mgombea mwingine, Simon Ngatunga, na baadaye Ndugai kumtuhumu Dk.
Chilongani kuwa alikuwa akitumia simu yake ya kiganjani, kumrekodi video ili kusambaza mitandaoni. Hata hivyo Ndugai alisema jana kuwa miongoni mwa wagombea tisa wanaowania nafasi hiyo, baadhi wamepandikizwa kwa lengo la kufanyia fujo.
“Tangu tuanze kampeni, wagombea mapandikizi wanafanya kazi ya kunitukana na kunidhalilisha kila tunakokwenda, mmoja ananiporomoshea matuzi ikitokea nikajibu, wanakuwa wameshapanga mmoja wao wa kunirekodi ili wazidi kunidhalilisha mitandaoni,” alieleza Ndugai
Alisema tukio la Jumatatu, wakiwa kwenye mkutano wa hadhara Ngatunga, alimtukana matusi ya nguoni na kusababisha mzozo kati yao, wakati watu wakiendelea kumsihi ampuuze yule kijana huyo akagundua Dk. Chilongani akitumia simu yake kumrekodi.
“Nilishamuonya mara kadhaa aache kujifanya mwandishi wa habari, kwa kuachukua video tena akinilenga mimi tu, lakini hakusikia nilichofanya niliigonga ile simu aliyokuwa akiitumia kuchukua video,” Ndugai alisema.
“Nikaigonga nikimwambia hebu usiendelee kunichukua video na kikamera chako hicho simu ikaanguka chini, nikashangaa kuona na yeye akijiangusha chini kama wachezaji wa mpira wa miguu,  ambao hujiangusha kwa lengo la kusingizia wamefanyiwa fujo ili wenzao wapewe kadi nyekundu.”
Kwa mujibu wa Ndugai, hakumpiga Dk. Chilongani wala hakujaribu kumpiga Ngatunga.
NIPASHE
Hofu imetanda ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wananchi kwa ujumla kutokana na kutoonekana kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, katika matukio mawili makubwa ya kisiasa yanayohusu mustakabali wa chama hicho.
Dk. Slaa hakuonekana siku ya kihistoria Jumanne wiki hii, iliyokuwa maalum kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kutangaza kujivua uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga Chadema.
Kadhalika, Dk. Slaa hakuonekana jana makao makuu ya chama wakati Lowassa alipofika kuchukua fomu ya kuwania urais kupitia chama hicho akitarajiwa kuwakilisha Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi (Ukawa), katika hafla iliyotikisa jiji la Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wa juu wa Chadema.
Hata hivyo, Dk. Slaa alihudhuria kikao cha dharura cha kamati kuu ya Chadema Jumapili iliyopita ambacho kiliendelea hadi usiku wa manene na hoja kuu ikiwa ni kujadiliana na Lowassa na kumpokea katika chama hicho.
Dk. Slaa alionekana katika baadhi ya picha zilizovuja kutoka katika kikao hicho akiwa na viongozi waandamizi wa Chadema huku akijadili jambo na Lowassa, ambaye katika siku za hivi karibuni ambekuwa gumzo kubwa baada ya kubadili upepo wa siasa za Tanzania.
Tangu juzi kumekuwa na mijadala mirefu ndani ya mitandao ya kijamii, juu ya aliko Dk. Slaa, wengine wakibashiri kuwa ameamua kuacha siasa.
Hata hivyo, Dk. Slaa mwenyewe hajawa radhi ama kupokea simu yake au kujitokeza hadharani kujibu maswali ya umma juu ya kinachomsibu.
Mbali na kutokuonekana Chadema, Dk. Slaa pia hakuonekana kwenye mkutano wa Ukawa, uliofanyika Jumatatu wiki hii makao makuu ya Chama cha Wananchi (CUF), ambao wenyeviti wenza wa umoja huo walimkaribisha Lowassa kujiunga nao.
Wakati wa Dk. Slaa akiadimika kwenye hadhara, viongozi waandamizi wa Chadema kwa nyakati tofauti wameithibitishia NIPASHE kuwa kila kitu “kimedhibitiwa” kuhusu tetesi kwamba kiongozi huyo amesusa.
“Sikiliza brother Dokta yuko freshi. Kila kitu kinakwenda kama tulivyopanga. Hakuna ukweli wa lolote juu ya madai eti Dokta anakwenda CCM,” kilisema chanzo chetu kilichoomba kutotajwa kwa sasa.
Wakati hali ikiwa hivyo, kuna taarifa kwamba Dk. Slaa anashinikizwa sana na watu wa ndani ya familia yake ambao wanadaiwa kusumbuliwa zaidi na ubinafsi, hasa baada ya mabadiliko ya kisiasa ambayo yamekikumba chama hicho kufuatia kujiunga kwa Lowassa.
Watu hao wa ndani wa familia ya Dk. Slaa wanadaiwa kuwa walikuwa wamejiandaa kuwa sehemu ya harakati za katibu mkuu huyo kuwania tena urais mwaka huu kama ilivyokuwa mwaka 2010.
“Sisi tunawaza jinsi ya kuivunjavunja CCM, lakini wapo watu wanawaza jinsi ya kuwa sijui nini sijui nani?
Hapa tunatafuta njia ya kuing’oa CCM hata kama ni kwa kutumia nguvu ya shetani,” alisema kiongozi mmoja wa Chadema.
Lowassa aliamua kujiunga Chadema baada ya kuchoshwa na siasa zilizojaa chuki za kumzuia kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kusaka tiketi ya kuwania urais kupitia CCM.
Katika hatua nyingine, Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu, aliliambia NIPASHE kwamba, Dk. Slaa alishiriki vikao vyote muhimu vilivyoafiki, Lowassa kujiunga na chama hicho.
“Jana (juzi) usiku nilikuwa naye na wiki hii alishirika kikao cha kamati kuu ambacho mliona picha kwenye mitandao,” alisema.
Alipoulizwa alipo, Dk. Slaa, Lissu hakutoa majibu ya moja kwa moja zaidi ya kusema kwamba akiwapo mwenyekiti kwenye kikao chochote inatosha na siyo lazima, viongozi wote wa kitaifa wawepo.
Kuhusu Naibu Katibu wa Chadema, Tanzania Bara, John Mnyika na yeye kutoonekana katika mikutano hiyo, alijibu kwa kifupi kwamba anaumwa.
Licha ya kutafutwa mara kadhaa kupitia simu yake ya mkononi juzi na jana, Dk. Slaa hakupatikana badala yake mtu mmoja mwanamke alipokea na kusema mpigaji amekosea namba.
Alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno ili aeleze kilichomsibu kushindwa kuhudhuria matukio muhimu ya kumkaribisha Lowassa pia hakujibu.
NIPASHE
Mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (pichani),  ameiomba serikali kuendelea kujenga barabara ya lami awamu ya pili hadi makao makuu ya Wilaya ya Simanjiro toka KIA, huku akiwataka Watanzania kukataa watu wanaowatenganisha kwa misingi ya ukabili, dini na vyama vya siasa.
Alitoa wito huo jana wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya lami ya kilomita 26 toka KIA hadi Mererani, Manyara iliyohudhuriwa na  Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Bilal.
Alisema ni vizuri Watanzania wakaendeleza na kuwaogopa baadhi ya watu wanaotaka kuwatenganisha kwa misingi ya vyama, ukabila na udini, kwani hakuna tija kwa Taifa.
“Haya maendeleo hayachagui ukabila, dini wala vyama vya siasa, ndio sababu serikali inajenga barabara kila mahali bila kujali chama gani kipo mahali hapo, hiyo ndiyo misingi tulionayo,” alisema.
Alimuomba Makamu wa Rais kuendeleza barabara hiyo hadi makao makuu ya Simanjiro, katika awamu ya pili baada ya kumalizika awamu ya kwanza.
Dk. Magufuli alisema ujenzi  wa barabara ya KIA hadi Mererani amekabidhiwa mkandarasi China Hennan International Cooperation Group Co. Ltd , ambaye alimtaka kuikamilisha kwa wakati.
Alisema ujenzi wa barabara hiyo utagharimu Sh. bilioni 32.2 na kumtaka mkandarasi huyo kuajiri vijana wa eneo hilo ili nao wanufaike na matunda ya miradi ya eneo lao.
Alisema hadi sasa serikali inaendelea na ujenzi wa barabara za lami kilomita. zaidi ya 17,000 kati ya hizo 5,500 zimekamilika kwa kiwango cha lami, jambo ambalo ni la kupongezwa na kila mpenda maendeleo.
Alisema barabara hiyo ina umuhimu mkubwa kutokana na kuwapo kwa machimbo ya madini ya Tanzanite ambayo yanaingizia mapato makubwa serikalini.
Dk. Bilal alimsifia Dk. Magufuli kuwa ni jembe na anastahili kupeperusha bendera ya urais ya CCM, kutokana na kazi alizofanya bila kutetereka.
Aliwaomba wananchi kuacha kuhujumu mradi huo kwa kuiba vifaa, badala yake wavilinde ili kumpa moyo mkandarasi.
“Lakini nimepokea ombi la Dk. Magufuli la kutaka barabara iendelee awamu ya pili hadi makao makuu ya wilaya na itakuwa hivyo, pia tutafikiria kuyaleta maji eneo hili haraka iwezekanavyo,” alisema.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Patrick  Mfugale, alisema barabara hiyo itakuwa na vituo vya mabasi vitano na madaraja matano na inakadiriwa kudumu kwa miaka 20.’
MTANZANIA
Idara ya uhamiaji nchini imesema inawashikilia wahamiaji haramu 2,048 kutoka nchi mbalimbali kwa tuhuma za kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura.
Naibu kamishna wa uhamiaji na msemaji mkuu wa idara hiyo, Abbas Mussa alisema jana kuwa wahamiaji hao wanatoka nchi za Kenya, Burundi na Uganda.
Alisema walikamatwa katika mikoa 14 wakijifanya ni Watanzania, lakini ilibainika kuwa siyo raia baada ya idara hiyo kufanya uchunguzi kwenye vituo vya uandikishaji.
“Baadhi yao tumewafikisha mahakamani, lakini wengine bado uchunguzi unaendelea na wakibainika nao watachukuliwa hatua,” alisema Mussa.
Aliongeza kuwa wengi ya wahamiaji hao walifika mikoa ya Kagera, Mara, Tanga, Kigoma, Rukwa, Kilimanjaro, Ruvuma, Geita, Shinyanga, Mtwara, Pwani, Mbeya, Morogoro na Dar es Salaam.
“Inasikitisha sana, kwani baadhi ya waliokamatwa walishajiandikisha na kupewa vitambulisho kama raia wa Tanzania,” alisema.
Alisema kutokana na hali hiyo, Idara imeamua kuongeza maofisa katika vituo ili kuendelea kuwabaini wahamiaji hao.
Mussa aliwataka wananchi kutoa taarifa mara wanapobaini watu ambao siyo raia wanajiandikisha.
Aliongeza kuwa maombi ya hati za kusafiria yameongezeka maradufu kutoka hati 4,938 Julai 2014 hadi 8,703 Julai 2015 kwa upande wa Bara na kutoka hati 588 Julai 2014 hadi hati 1,028 Juni 2015 kwa upande wa Zanzibar.
Alisema idara inawataarifu wananchi kuwa siyo lazima kubadilisha hati inapokwisha muda wake, badala yake mmiliki anaweza kubadili na kupatiwa nyingine wakati wowote atakapokuwa akisafiri.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

Thursday, July 30, 2015

WANAOFANYA MGOMO WA KULA GEREANI ISRAEL , KUKIONA

Sheria mpya kwa wafungwa kulishwa chakula wakileta mgomo…

priiiBunge la Israeli, limepitisha sheria ya kuwalisha kwa lazima wafungwa ambao wanashiriki mgomo na kususia kula.
Sheria hiyo ambayo ilikubaliwa na idadi kubwa ya wabunge, inawaruhusu mahakimu kuhakikisha kuwa wafungwa wanalishwa kwa lazima na pia kupata matibabu kwa lazima bila ya ruhusa ya mfungwa ili kunusuru maisha yao.
Raia wa Palestina ambao wanazuiliwa katika magereza ya Israeli wamekuwa wakisusia chakula kama njia yao ya kupinga kukamatwa kwao katika miaka michache iliyopita.
savee
Nchi hiyo inahofu kuwa wafungwa hao ambao wamekataa kula chakula huenda wakafa na kusababisha fujo magerezani.
Sheria hiyo mpya imelaaniwa na chama cha madaktari nchini Israeli, ambacho kinaamini kuwa kuwalisha wafungwa chakula kwa nguvu ni mbinu ya mateso na ni hatari kimatibabu.
Kwa habari,matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

VIMBWANGA VYA WALIMWENGU

Stori ya mwanamke kuripotiwa kufa na baadaye kukutwa hai isikupite mtu wangu…

jullll
Kuna stori moja iliwahi kuripotiwa  Bagamoyo baada ya maiti kuzua taharuki kwa waombolezaji wakidai hajafa licha ya kudhibitishwa na daktari kuwa alifariki.
Huko Ujerumani mwanamke mmoja anayekadiriwa kuwa na miaka 92 ambaye aliaminika kupoteza maisha kisha mwili wake kuhifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti amezua gumzo.
Tayari daktari wa zamu alithibitisha kifo cha mwanamke huyo baada ya kumpima na kuridhika kuwa amefariki ..lakini baada ya masaa machache wahudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti walikuta mwili wa mwanamke huyo ukijigeuza na kugundua alikua hajafariki kama ilivyoripotiwa.
Tukio hilo lilifanya ndugu wa marehemu kushangazwa na hali hiyo huku wakimjia juu daktari aliyewapa taarifa kuwa mgonjwa wao amefariki duniani na kutaka walipwe fidia.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

FACE BOOK KIDEDEA

Facebook Vs Instagram nani ana watumiaji wengi zaidi duniani? Majibu yake haya hapa.

FB3
Kama wewe ni miongoni mwa wale watu wanaohisi Facebook ni mtandao uliopitwa na wakati, basi utapenda kusikia taarifa hii.
Mwishoni mwa mwezi wa sita kampuni ya FB Tech30 ama Facebook ilitajwa kuwa na watumiaji takribani bilion 1.5 kwa mwezi tu, watu wanaoutumia mtandao wa Facebook duniani kwa mwezi tu unazidi matumizi ya mitandao mengine duniani kama Microsoft (MSFT Tech30).
FB7
Ukuaji wa namna hii umeiruhusu Facebook kubuni features tofauti ili kuwezesha kampuni hiyo kukusanya data na taarifa tofauti za watumiaji wa mtandao huo.
Licha ya hayo ofa ya matangazo yanyotolewa na Facebook imewaingizia kampuni hiyo zaidi ya dola Bil 3.8 ambalo ni ongezeko la 43% ya ukuaji wao toka mwaka jana…Ofa ya matangazo ya facebook kupitia simu za mkononi inawaingizia zaidi ya dola Bil 2.9 na zaidi ya 62% ya mapato ndani ya miaka 3.
FB6
Facebook imeendelea kukua na kwa sasa imeweza kuwapiga gepu washindani wake wakubwa kama Twitter (TWTR, Tech30). Jumanne ya wiki hii Interim CEO wa Twitter Jack Dorsey alisema kuwa ukuaji wa Twitter umekuwa ukishuka kwasababu watu wengi hawaelewi kwanini wanahitaji kuutumia mtandao huo.
ig1
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg amesema kuwa mafanikio makubwa ya mtandao huo ni dhamiria rahisi ya kuelewa namna ya kurahisisha mawasiliano na wanajitahidi kukuza na kusupport vitu vinavyo ibeba dhamira hiyo.
ig2
Licha ya Instagram kuwa maarufu sana kwa matumizi ya watu wengi siku hizi idadi ya watumiaji wa mtandao huo ni 26% duniani wakati idadi ya watumiaji wa Facebook duniani ni 71% na kwa zaidi ya miaka 3 iliopita wamekuwa product ya teknolojia inayotumiwa zaidi duniani.
Kwa habai, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

CHEMCHEM ILIYOSAHAULIKA KIJIJI CHA MAJIMOTO AMBONI ,TANGA


Tangakumekuchablog

Tanga, WAKAZI wa kijiji cha Majimoto kata ya Mafuriko halmashauri ya jiji la Tanga, wameshangazwa na Wizara ya Utalii na Maliasili kuacha kuifanya  chemchem inayotoa maji  moto iliyoko kijiji hapo kuwa ya kitalii  hatua ambayo inaikosesha Serikali mapato.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wakazi hao walisema Chemchem hiyo imekuwa kivutio jambo ambalo wageni kutoka mataifa ya nje hufika na kujionea maajabu ilhali Serikali imeshindwa kuitambua.

Alisema kutokana na kutokuwepo kwa utaratibu wageni wa nje na ndani hufika bila kizuizi na kujionea maajabu ya Chemchem hiyo ambayo hutoa maji ya moto pamoja na maajabu mengine yaliyopo eneo hilo.

“Serikali inatambua uwepo wa chemchem hii inayotoa maji moto si usiku wala mchana na haina kiangazi wala masika----raia wa kigeni wanaitambua ila sisi hatuna habari nayo” alisema Hamad Pinto na kuongeza

“Kama Serikali ingeweka utaratibu wa kukiweka kituo hiki katika mazingira ya utalii ingeweza kuongeza mapato yake-----watu wanakuja  bila mpangilio na kupiga picha na kushangaa shangaa” alisema

Kwa upande wake mkazi wa Amboni, Mussa Juma, alisema kuna vivutio vingi vya utalii eneo hilo lakini havitambuliki yakiwemo majengo ya kale na misitu yenye wanyama.

Alisema kama Serikali ingeliviendeleza vivutio hivyo na vijana  kupata ajira na kuondokana na ukaaji wa vijiweni jambo ambalo linawasukuma kujitumbukiza katika viwashawishi.

Alisema vijana wengi hawana kazi na wamekuwa wakikaa vijiweni hivyo kuwepo kwa vivutio hivyo na kuendelezwa ingweza kupunguza wimbi la umasikini na ajira kwa vijana.

“Vinaja wengi hawana ajira wala kazi ya kujiajiri na badala yake wamekuwa wakikaa vijiweni kupiga soga-----kama vivutio vya kitalii vipo kuna sababu gani ya kuacha kuendelezwa” alisema Juma

Alisema ili kuweza kupunguza umasikini ni vyema Serikali kuviendeleza vivutio vyake jambo ambalo linaweza kuingiza mapato na kuweza kupunguza umasikini majumbani.
                                                        Mwisho

 Mkazi wa kijiji cha Majimoto kata ya Amboni Tanga, Hamad Pinto akiwaonyesha waandishi wa habari  maji ya moto katika chemchem iliyopo eneo la Kidugaro  inayotoa maji moto. Chemchem hiyo inadaiwa kuwepo toka mwaka 1935,




MARADONA VITUKO HADI MITAANI

Vituko vya Maradona haviishi!! safari hii kamtuhumu mke wake kumwibia fedha

maraa
Mkongwe wa soka duniani Diego Maradona amerudi kwenye headlines tena baada ya kumtuhumu mke wake wa zamani Claudia Villafane kuwa amemuibia fedha kwenye akaunti yake.
Maradona akizungumza kwenye matangazo ya moja kwa moja ya Televisheni alisema Villafañe ambaye alikuwa mpenzi wake wa zamani ni mwizi na amemwibia kiasi cha dola milioni 9 benki.
Hata hivyo Villafañe amepinga vikali madai hayo na kudai kuwa yeye si mwizi na hakuiba fedha hizo huku akitetewa pia na watoto wake Dalma na Giannina kwenye mtandao wa twitter.
wawil
Maradona akiwa na mke wake Claudia
Wapenzi hao ambao walikutana miaka ya zamani katika mji uliokithiri kwa umasikini huko Buenos Aires kabla ya Maradonna kuwa maarufu na kuwa miongoni mwa wachezaji mahiri duniani katika historia ya soka,waliachana baada ya kutofautiana.
Watoto wao wawili Dalma and Giannina,wamekaririwa kwenye mtandao wa twitter wakimtetea mama yao wazi wazi na kwamba hahusiki na upotevu huo wa fedha za baba yao.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

SOMA KURASA MWANZO MWISHO YA MAGAZETI YA LEO, JULY 30 TZ

Magazeti yanaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza kielimu, Kituo kinatoa kozi mbalimbali za kielimu na kitaalamu zikiwemo za Ufundi wa Computer. Kituo kipo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746