Sunday, January 31, 2016

MGAMBO JKT YATOKA SULUHU NA NDANDA FC 1 1



Mshambuliaji wa Ndanda, Kasham Ponera, akigombea mpira na kiungo wa Mgambo, Bakari Abdalla, wakati wa ligi kuu Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwani Tanga Leo


  Mshambuliaji wa Mgambo, Ramadhani Malima akijaribu kumtoka kiungo wa Ndanda, Omari Mponda wakati wa ligi kuu Tanzania Bara Vodacom Uwanja wa Mkwakwani Tanga leo.
Mshambuliaji wa Mgambo, Ramadhani Malima akijaribu kumtoka kiungo wa Ndanda, Omari Mponda wakati wa ligi kuu Tanzania Bara Vodacom Uwanja wa Mkwakwani Tanga leo.

TIMU YA SAMATTA YASHINDA BILA YEYE KUWEPO UWANJANI

Huu ndio ushindi walioupata KRC Genk ya Mbwana Samatta January 30


Siku moja baada ya klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji imsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa anaichezea klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Samatta, January 30 ilishuka dimbani ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani Cristal Arena kuikabili klabu ya Kortrijk.
Licha ya kuwa Samatta hakuwa kwenye kikosi, kwa sababu hakufanya mazoezi na timu, KRC Genk imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na mshambuliaji mwenye asili ya Zaire Christian Kabasele dakika ya 21, hizi ni taarifa na mapokezi mema kwa Samatta ambaye ndio kwanza ametua Ubelgiji kuanza maisha yake ya soka.
642x999_59395959 (1)
Mchezo wa mwisho kabla ya ushindi dhidi ya Kortrijk, KRC Genk ilicheza dhidi ya Mechelen na kutoka sare ya goli 1-1, kwa sasa KRC Genk ipo nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi. KRC Genk watarudi uwanjani February 6 kucheza dhidi ya Mouscron-Peruwelz na huenda mchezo huo Mbwana Samatta akawepo.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

AMKA NA MAGAZETI NA CANDLE EDUCATION CENTRE TANGA

Magazeti yanaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, Kituo kinaendelea kupokea wanafunzi wa QT na wakidato cha nne hadi sita na wanaojiendeleza kielimu, Kituo kipo Tanga mkabala na bank ya CRDB simu 0715 772746

Saturday, January 30, 2016

RAHA YA KUSAFIRI ANGANI NA NDEGE UKIWA PEKE YAKO

Utajisikiaje siku unajikuta unasafiri pekeyako kwenye ndege kubwa? Imemkuta jamaa Ufilipino..

Inaweza kutokea unasafiri kwenye gari hivi labda toka Dar mpaka Morogoro kwenye basi la abiria pekeyako, unaweza kujifariji kwa kuchekicheki nje mazingira, ukachezea simu yako au ukaendelea zako na safari kwa kusikiliza muziki au kuangalia TV kwenye basi, kwenye ndege je inakuwaje?
Jamaa mmoja Alex Simon mtalii kutoka Austria, alijikuta kwenye level za kistaa hivi au mtu fulani VIP kwenye ubora wake baada ya kujikuta akiwa ndio abiria pekeake ndani ya ndege ya abiria zaidi ya 100… alitoka zake  Manila kwenda Boracay ndani ya Ufilipino kwa ajili ya kutalii tu !!
Baada ya Simon kuingia kwenye ndege alianza kupiga stori na marubani baadae akaungana na wahudumu wawili wa ndege wakiendelea na stori mpaka alipotua

Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

COASTAL UNION YAIPIGA 2 YANGA MKWAKWANI


 Kipa wa Coastal Union ambaye alikuwa mchezaji bora wa mchezo huo akinyaka mpira wa kona leo uwanja wa Mkwakwani ambapo timu yake imeshinda magali 2, 0
 Kipa wa Coastal Union ya Tanga Fikirini Bakari akimuonyesha mkono Refarii Endu Shamba jereha alodai kulengwa jiwe na washabiki wa Yanga leo wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara ambapo Coastal Union imeshinda magali 2 , 0
 Mshambulia wa Coastal union ya Tanga, Abdisallam Achidebile akitafuta kumtoka kiungo wa Yanga, Osvcar Joshua wakati wa mchezo ligi kuu Tanzania Bara leo uwanja wa Mkwakwani ambapo Coastal Union imeshinda magali 2, 0



Friday, January 29, 2016

YANGA WAFANYA MAZOEZI GALANOSI TANGA ASUBUHI HII

 Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi uwanja wa Shule ya Sekondari ya Galanozi kujiandaa na kipute uwanja wa Mkwakwani kumenyana na Coastal Union ya Tanga.
Yanga ambayo itakuwa na kibarua kigumu baada ya Coastal kuendelea kuwa chambo ya pointi tatu kwa kila timu inayokutana nayo.
Upinzani huo unatokana na maandalizi na kuikamia kuibuka na ushindi ili kuwapa faraja washabiki wake hasa wakiwa uwanja wa nyumbani