Wednesday, August 31, 2016

AMKA NA MAGAZETI NA NEW AGE EDUCATION CENTRE TANGA


JACK WILSHERE HATIMAE ATIMKIA BOURNEMOUTH

Jack Wilshere kujiunga na Bournemouth

Jack Wilshere kujiunga na Bournemouth
Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere anakaribia kujiunga na klabu ya Bournemouth kwa mkopo wa muda wa msimu uliosalia baada ya mpango wa kuijiunga na klabu ya Roma kuzuiwa na Arsenal.
The Gunners ilikataa kufanya biashara na Roma kwa sababu ya vile walivyochukulia uhamisho wa beki Kostas Manolas mapema msimu huu.
Wilshere mwenye umri wa miaka 24 alifanya mazungumzo na Bournemouth na Crystal Palace.
Anatarajiwa kufanyiwa ukaguzi wa kimatibabu na The Cherries.

JOHN KERRY AKUMBANA NA FOLENI NEW DELH

John Kerry akwama kwenye foleni Delhi, India

Indian Prime Minister Manmohan Singh's official motorcade arrives to attend the Beating the Retreat ceremony in New Delhi on January 29, 2011.Travellers face traffic congestion on NH-24 as Kanwadias (Dak Kawad) carry holy water for Lord Shiva collected form the River Ganga, on August 1, 2016 in New Delhi, India. (PWaziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry alipofika Delhi kwa mashauriano na maafisa wa serikali Jumatatu jioni, hakuwa na bahati.
Mvua kubwa ilinyesha na 'kukosa kutambua cheo chake'.
Badala ya magari yake kupitia barabara zilizo wazi, msafara wake wa magari ulikwama kwenye foleni zaidi ya saa moja.
Lilikuwa jambo lisilo la kawaida kwa sababu maafisa wa usalama huondoa magari barabarani kutengeneza njia ya kutumiwa na wageni mashuhuri.

BARABARA YA KOROGWE ROAD ENEO LA KWAFUNGO MUHEZA



Gari aina ya Carry ikiwa imepakiza abiria kupitiliza wakipandisha mlima wa Kwafungo   Muheza Tanga na mbele yao waendesha bodaboda wakiendesha pikipiki wakiwa hawana kofia ngumu ya kichwani.
 








UKUTA WAAHIRISHA MAANDAMANO KESHO

 Upinzani waahirisha maandamano

Viongozi wa upinzani wakati wa kikao na wanahabari Dar es Salaam
Bw Lowassa, ambaye aliwania urais kupitia ChademaMuungano wa vyama vya upinzani nchini Tanzania umeahirisha maandamano ya kitaifa ambayo yalikuwa yamepangiwa kufanyika kesho.
Viongozi wa upinzani, akiwemo Edward Lowassa wa Chadema, wametangaza hatua hiyo kwenye kikao na wanahabari Dar es Salaam.
Wamesema wameahirisha maandamano hayo kwa kipindi cha mwezi mmoja baada ya kusikia ombi la viongozi wa kidini na wadau wengine waliowaomba kukumbatia na kuyapa muda mazungumzo.
Viongozi wa chama hicho walikuwa wameitisha maandamano na mikutano ya kisiasa Septemba Mosi kupinga walichosema kuwa ni ukandamizaji unaoendelezwa na serikali.
Baada ya mkutano wa kikao cha Kamati Kuu ya chama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mwishoni mwa Julai, viongozi walisema: "Yapo Matukio ambayo yamekua yakifanywa na kukandamiza demokrasia na misingi ikipuuzwa na kudharauliwa.
"Si nia ya Chadema kugombana na Serikali bali ni kazi ya Chama Pinzani kuisaidia Serikali iongoze kwa kufuata misingi ya Katiba," chama hicho kilisema.
Maandamano hayo yalipewa jina Ukuta, ikisimamia Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania.
Serikali ilipiga marufuku mikutano yote ya kisiasa, ya hadhara na ya ukumbini. Baadhi ya viongozi wa upinzani wamekamatwa na kuzuiliwa kwa muda.

MKUU WA WILAYA HANDENI GODWEN GONDWE AWATAKA WAKULIMA KULITUMIA SOKO LA (EAC)

 Tangakumekuchablog

Handeni, MKUU wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe, amewataka wakulima wa machungwa Wilayani humo kutafuta masoko nje likiwmo soko la pamoja la Afrika Mashariki (EAC) kuepuka kulanguliwa na walanguzi wanaowafuata mashambani.
Akizungumza katika kikao mara baada ya kukabidhiwa mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) kwa halmashauri ya Wilaya hiyo jana, Gondwe alisema wakulima wa machungwa  wanashindwa kuwa wakulima wa kisasa baada kushindwa kuthubutu kutafuta masoko nje.
Alisema soko la pamoja na Jumuiya ya Afrika Mashariki lipo lakini wanashindwa kulitumia badala yake wafanyabiashara wa nje huja mashambani kwao na kuwalangua kwa bei ya hasara.
“Kila mtu ndani na nje ya nchi wanajua kuwa Handeni inalima kilimo cha cha machungwa kwa wingi na wafanyabiashara huja , ila niwaambieni kuwa munalanguliwa kwa woga wa kwenda kutafuta masoko ” alisema Gondwe na kuongeza
“Soko la pamoja lipo wazi bila vikwazo vyoyote sasa ni kitu gani kinachotufanya kushindwa kulitumia na kuwaachia wenzetu kuja kwetu na kutulangua kwa bei ya kutupa hebu jamani tuondoe woga na tuwe tayari” alisema
Aliwataka wakulima kuacha woga na badala yake kuwa tayari kutafuta masoko ndani na nje ya nchi na kuwa wakulima wakubwa na kuacha kulanguliwa na wafanyabiashara mashambani ilhali fursa zipo.
Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Wafanyabiasha wa Machungwa Segera, Hussein Diamballa, aliwataka wafanyabiashara hao kucha kuuza machungwa yaliyopepewa na kusema kuwa kufanya hivyo kunaondosha sifa ya machungwa kituoni hapo.
Alisema kuna wachuuzi ambao wamekuwa wakiuza machungwa yaliyopepewa na kuchanganya mabovu na hivyo kuwataka kuacha kufanya hivyo kwani watafanya ukaguzi wa mtu mmoja mmoja.
Alisema umoja huo uko mbioni kusajili wanachama ambao utakuwa na utaratibu wa kutoa namba na sare hivyo kuwataka kufanya biashara ya halali na kuacha udanyanyifu.
“Tunataka kuondosha ile dhana ya kituo chetu kuuza machungwa ya kupepea na kubambika mabovu, hii inatuletea sifa mbaya wakati hapa tunalima machungwa mazuri yenye maji mengi” alisema Diambala
Aliwataka wafanyabiashara hao kuwafichua wachuuzi wenye kufanya udanganyifu na kuwaletea sifa m,baya kwa wateja ilhali kituo hicho ni muunganisho wa magari yaendayo Mikoani jambo ambalo linaweza kuuza na kupata mitaji na kuwa wafanyabiashara wakubwa.
                                            Mwisho



Wakulima wa machungwa Kabuku Wilayani Handeni Tanga wakiwa katika semina ya kilimo cha machungwa na halizeti wakati wa kujadili andiko la makabidhiano ya mafanikio wa mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) jana.
.

 Mkulima wa machungwa Kabuku Handeni Tanga, Rajab Lusewa akizungumza wakati wa warsha la andiko la makabidhiano ya mafanikio wa mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) jana.
 Mkulima wa machungwa Kabuku Handeni Tanga, Bakari Mgaza, akizungumza wakati wa warsha la andiko la makabidhiano ya mafanikio wa mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) jana.
Mkulima wa machungwa Kabuku Wilayani Handeni Tanga, Said Msagati akizungumza wakati wa warsha la andiko la makabidhiano ya mafanikio wa mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI) jana.