Pale ambapo mbwa anaamua kutembelea mgonjwa Hospitali
Kwa
nchi za wenzetu mbwa ni sehemu ya familia, huduma anayopewa ni sawa tu
na binadamu yoyote ambaye anaishi kwenye nyumba husika.
Hii inaweza kukushangaza kiasi fulani kutoka Marekani, mbwa ambaye jina lake ni Sissy aliona muda unakwenda hamuoni mlezi wake, akaamua kwenda hadi hospitali alikokuwa amelazwa mlezi wake huyo.
Nancy Frank ambaye ndiye aliyemfuga mbwa huyo alikuwa amelazwa katika hospitali ya Mercy Medical Center
akitibiwa cancer kwa muda wa wiki mbili huku mbwa wake akiwa amemuacha
nyumbani kwake, kilichomshtua ni kitendo cha mbwa huyo kumfuata mpaka
hospitali.
Mbwa alifika Hospitali akiwa na maelezo kwenye shingo, walinzi walimtambua na kumpeleka kwenye chumba alichokuwa amelazwa Nancy.
Mara nyingi wanyama kama mbwa na paka
wana uwezo wa kurudi nyumbani wanakofugwa hata kama wakipelekwa mbali,
lakini hii ya mbwa kumtafuta anayemfuga hospitali alikolazwa ni kitu
kilichoshangaza wengi.
Hakuna Stori itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment