Friday, April 3, 2015

CHUO KIKUU CHA GHARISSA CHAFUNGWA , KENYA

HEADLINES kubwa toka Kenya bado ni ishu ya magaidi kuvamia Chuo Kikuu GARISSA..

Garissa_2362442fKutokana na shambulio la kigaidi katika chuo cha Garissa kilichopo Kenya, baadhi ya familia bado hawajui watoto wao waliko, mzazi mmoja amesema aliongea na mtoto wake hadi dakika ya mwisho akiwa mikononi mwa magaidi hao baada ya kukamatwa.
Alikuwa akininong’oneza akiniambia yuko chini ya kitanda akaniambia tuu tumuombee akakata simu, saa sita na nusu nikaona hiyo namba ikinipigia nilikuwa naongea naye akaniambia nimeshikwa sina la kufanya akaniambia ndio hawa hapa silaha zao tunaziona, sijui ni bunduki sijui ni silaha gani walikuwa nazo
Akaniambia ndio wanataka kuongea na baba lakini baba amepatikana wako busy sana wanamharasi, tukaongea nae kidogo wakamnyang’anya simu nikaongea na hao magaidi Al Shabaab …
Akiendelea kusimulia; “wakaniambia wee mzee nakupa dakika mbili apige Somalia, akaniambia wee mzee umeshindwa kupiga simu? Kama umeshindwa kupiga simu acha mwanao asali maombi yake ya mwisho mi nasikiliza tu.. akasali maombi yake yote akaniambia umesikia amemaliza kuomba what next we sikiliza, sikiliza mwenyewe hesabu mwenyewe risasi naua kabisa nikasikia three gunshot… na akaniambia nimeuwa chimbeni shimo”– aliongea mzazi wa mwanafunzi mmoja aliyeuawa.
Tukio hili limesababisha wanafunzi 147 kufariki na wengine kujeruhiwa, kwa sasa Chuo hicho cha Garissa kimefungwa kwa muda.

No comments:

Post a Comment