Hadithi hii inaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya Mkombozi Sanitarium Clinic, Mabingwa wa Tiba Asilia. Kituo kinatoa huduma za magonjwa mbalimbali yaliyoshindikana yakiwemo Kisukari, Bawasiri, Magonjwa ya Matumbo. Wako na mashine ya kupima mwili mzima na madaktari waliobobea katika Tiba ya magonjwa. Wapo Chuda Tanga mkabala na Kampuni ya usafirishaji abiria Raha Lao. simu 0654 361333
NILIJUA NIMEUA
ILIPOISHIA
Nikatoka na kumkuta amesimama
pembeni mwa nyumba yangu. Nikamkaribisha ndani.
“Nilikuwa nimepotea, kama nisingeiona ile teksi yako pale barazani,
nisingeitambua hii nyumba” akaniambia wakati tumo chumbani.
“Lakini hapapotezi, labda
wewe hufiki sana
huku Msambweni”
“Labda. Unajisikiaje kuumwa?”
“Sijambo kidogo, nikuletee
soda?”
“Acha tu. Unaumwa na nini?”
“Kichwa. Kichwa kinauma sana. Siwezi hata
kuendesha gari. Sijui waswahili wameniroga?”
SASA ENDELEA
“Acha kuamini sana uchawi. Umepima
malaria?”
“Nimepima, sina malaria”
“Umetumia dawa gain?”
“Nimeandikiwa dawa na
daktari, ndizo ninazotumia tangu jana”
“Tangu utumie hizo dawa,
unajisikiaje?’
“Kwa sasa nina nafuu,
nashukuru sana”
“Pole sana”
“Asante”
“Hii ni nyumba yako au
umepangisha?”
“Ni nyumba yangu?”
“Unaishi na wazazi wako
humu?”
“Hapana. Wazazi wangu
wameshafariki”
“Hawa watu waliomo humu ndani
ni akina nani?”
“Ni wapangaji wangu”
“Wewe mwenyewe umechukua
chumba kimoja tu”
“Kinanitosha. Sina mke wala
motto”
Tulipofika hapo msichana
akanyamaza kimya. Alikuwa kama anayewaza.
“Mbona kama unawaza, unawaza
nini?” nikamuuliza.
“Nikwambie kitu?”
“Niambie”
“Si unanitaka mimi, sasa mimi
nakupa sharti la kukukubali”
“Sharti gani?”
“Wafukuze wapangaji wote
halafu uikarabati hii nyumba” nikamwambia.
“Unataka tuishi peke yetu?”
“Ndiyo. Sitaki kero. Chumba
kimoja uweke sebule”
“Kwa vile nakupenda nitafanya
hivyo”
Baada ya wiki moja
nikaufanyia kazi ushauri wa Halima. Niliwapa notisi wapangaji wote,
nikaikarabati nyumba na kuweka chumba kimoja kama
sebule.
Nilikuwa na shamba langu la
minazi. Fedha nilizopata kutokana na mauzo ya nazi zilinisaidia sana kukamilisha nyumba
yangu.
Halima aliendelea
kunitembelea mara kwa mara. Alipohakikisha nimetimiza matakwa yake akanielekeza
kwa wazazi wake nipeleke barua ya uchumba.
Wazazi wa Halima walikuwa
wakishi Pongwe, mwendo wa karibu kilometa kumi na tano kutoka Tanga mjini. Baba
yake Halima mzee Moto Bwagizo alikuwa mtu mzima sana. Niliambiwa kuwa Halima alikuwa mtoto
wake wa mwisho na alizaliwa bila kutegemewa kwani tayari baba yake alikuwa mzee.
Mama yake mzazi alishafariki.
Mzee Moto Bwagizo alikuwa na
wake wawili, mama yake Halima na mke mwingine. Baada ya kufariki mama yake
Halima, mzee Moto aliendelea kuishi na mke wake wa pili.
Niliwasilisha ujumbe wangu
kwa wazazi wa Halima. Baba mkwe aliponiona aliniambia hazitambui mila za kutuma
barua ya uchumba kwani mimi sikuwa nikiomba kazi. Ukiomba kazi ndio unatuma
barua.
“Mila ninazizijua mimi za
kutpka enzi na enzi ni za kutuma mshenga, anakuja na maneno tu”
“Samahani baba yangu, sikujua
ndio kama unanielimisha”
Mzee akacheka.
“Umenijibu vizuri. Sasa
fungua barua yako unisomee”
Nikafungua ile barua yangu na
kumsomea yale niliyoandika.
Mzee akafurahi akaniambia.
“Nimekuelewa. Unataka kuunga
udugu na sisi. Mimi kama baba wa Halima nakujibu hapa hapa kuwa nimekukubali.
Halima ni mchumba wako tangu sasa”
Mzee Moto alinitajia kiasi
cha pesa alichotaka ili aniozeshe binti yake.
Siku ya pili yake nilimchukua
rafiki yangu nikaenda naye kupeleka pesa hizo.
Mipango ya harusi ikafanywa.
Baada ya wiki mbili nikaenda
Ponwe kumuoa Halima.
Baada ya kuoana na Amina
ndipo nilipoanza kufaidi maisha ya ndoa. Kusema kweli yalikuwa matamu kinyume
na kuishi kihuni.
Kwanza gharama ya maisha
ilipungua sana.
Pesa ambayo hapo mwanzo nilitumia peke yangu kwa siku kwa kula kwenye mikahawa, ilitumika kwa siku
mbili nilipokuwa na mke wangu.
Kadhalika nilikuwa na
mwenzangu wa karibu wa kuniliwaza, kunishauri na kunisaidia pale nilipohitaji
mwenza wa kunisaidia.
Kwa kweli nilihisi raha na
nilijilaumu kwa kuchelewa sana
kumuoa Halima.
ITAENDELEA kesho na usikose uhondo huu wa kusisimua ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment