HALI BADO TETE: PICHA TOKA AFRIKA KUSINI!
Raia wa kigeni wakiamua kujihami kwa kuchukua silaha kupambana na wenyeji.Baaadhi
ya raia ya kigeni wakiwa wamehifadhiwa katika kambi baada ya kukimbia
fujo na kuepusha maisha yao. Nchi jirani na Afrika Kusini zimeanza
matayarisho ya kuwaondoa raia wao kutoka nchi hiyo wakati Umoja wa
Mataifa ukieleza wasi wasi wake mkubwa kutokana na mashambulio hayo ya
chuki dhidi ya wageni .
Mashambulio ambayo yamesababisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao,
Ghasia
hizo dhidi ya wageni, ambazo zilianzia katika mji wa mashariki wenye
bandari wa Durban, zimesababisha kiasi cha watu sita kuuwawa na kusambaa
hadi katika mji wa kibiashara wa Johannesburg.
"Nchini
Afrika Kusini, mashambulizi ya chuki dhidi ya wageni katika muda wa wiki
tatu zilizopita, yamesababisha watu zaidi ya 5,000 raia wa kigeni
kukimbia makaazi yao," lilisema shirika la Umoja wa Mataifa la
Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) na kuongeza kuwa lina "wasi wasi mkubwa".
Makambi ya muda
Raia hao wa kigeni wanajihifadhi sasa katika makambi ya muda.
Nchi
jirani ya Zimbabwe, Malawi na Msumbiji zimetangaza mipango ya
kuwarejesha nyumbani raia wao, wakati ghasia hizo zimesababisha hasira
miongoni mwa nchi za eneo hilo.
Balozi wa
Zimbabwe nchini Afrika kusini, Isaac Moyo amesema hatua ya kuwarejesha
nyumbani kiasi ya Wazimbabwe 1,000 kutoka Durban itaanza Jumapili
(19.04.2015).
Katika
mji mkuu wa Zimbabwe, Harare , waandamanaji walipita katika ubalozi wa
Afrika kusini wakishutumu kile walichokiita "mauaji ya kiwendawazinmu na
ya kikatili" ya Waafrika wenzao.
Nchini
Msumbiji , kundi la watu wapatao 200 jana Jumamosi lilizuwia kivuko cha
mpakani cha Lebombo kuelekea nchini Afrika ya Kati.
Hutopitwa na habari inayonifikia na niko tayari kukutumia muda wowote kupitia hapa hapa www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment