Msichana afanyiwa ukatili na kuuawa Mbeya
Tukio la mauaji limetokea Mbeya, inahusu tukio la mwanaume mmoja kumuingila kinguvu msichana wa miaka 8.
Mwanaume huyo alimuita msichana na
kumuagiza dukani akamnunulie mafuta, aliporudi alimuingilia kinguvu,
akamuua halafu akautupa mwili wake kwenye shimo.
Mama wa mtoto huyo amesema alirudi
mwenye mizunguko yake lakini hakumkuta mtoto huyo, akaanza kumtafuta..
alipowauliza wenzake walisema alikuwepo nyumbani baada ya kurudi shule
lakini hawajui baada ya hapo alielekea wapi.
Akaamua kutoa taarifa Polisi na kwa
Balozi wa nyumba kumi, wakaitisha kikao.. baadae vijana wakaanza
kumtafuta na kukuta mwili wake ukiwa kwenye shimo.
Baada ya siku tatu wanakijiji walianza
msako na kukuta baadhi ya vitu vya marehemu nyumbani kwa mwanaume mmoja
zikiwemo nguo pamoja na damu, kwa hasira wakaanza kumshambulia kwa
kipigo na kuchoma moto nyumba hiyo hadi Polisi walipofika na kuwazuia.
Polisi walimchukua mtuhumiwa huyo na kumpeleka kituoni.Ni halali yako kupata taarifa yoyote inayonifikia na niko tayari kukutumia muda na wakati wowowte kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment