Kukiwa na usafiri kama huu Dar es salaam utakwenda Town na gari lako kweli?
Wakati
Dar es salaam Tanzania bado inasubiri kuanza kufanya kazi kwa mabasi
yaendayo haraka, sasa hivi nakupeleka moja kwa moja kwenye jiji la
Barcelona Spain, jiji ambalo mpaka mwaka 2011 lilikua na watu zaidi ya
milioni moja na laki sita ndani yake na sasa wanasema kuna zaidi ya watu
milioni 5 ambapo ni jiji la pili kwa ukubwa kwenye nchi ya Hispania.
Unaambiwa
usafiri huu wa Tram ulianza kufanya kazi kwenye mji wa Barcelona toka
mwaka 1872 lakini barabara zilizokua zikitumika na Tram za zamani
zilifungwa ilipofika mwaka 1971 na nafasi yake ikachukuliwa na Mabasi
pamoja na Treni za chini ya ardhi.
Kwenye hii picha ya juu na ya chini ni
muonekano wa Tram za mwanzoni kabisa wakati Barcelona imeanza kutumia
aina hii ya usafiri.
Baada ya mapito yote hayo sasa hivi mji wa
Barcelona unatumia Tram za kisasa zinazopita kwenye njia yake ya reli
kama kawaida na wamezitengenezea sehemu yake iliyo na mvuto zaidi kama
unavyoona kwenye picha hapa chini na barabara hiyo usafiri mwingine
wowote hauruhusiwi kupita.
Usafiri mwingine unaotumika sana Barcelona
ni usafiri wa Treni za chini kwa chini, yani zinapita chini ya ardhi na
kusafirisha watu kwenda sehemu mbalimbali ndani ya mji, ni usafiri
maarufu kwa jina la Metro.
Mfumo wa nauli kwenye Treni hizi za chini
maarufu kama Metro unatumia kadi kama za ATM ambazo unaweza kulipia
safari nyingi na ukifika kwenye mlango wa kuingilia kama huu hapa chini
unaipitisha ile kazi kisha mlango unakuruhusu kupita kuingia kwenye
kituo na kupanda Treni ya safari yako.
, Metro huwa zinatumiwa na watu wengi sababu hakuna foleni na sasa usalama upo japo kuna wale Wanawake wa Romania wanaotajwa sana kuibia watu mifukoni ndani ya hizi Treni, ukiachia hiyo huu ni usafiri salama wa kuutumia na hamna wezi wa kukaba hata iwe usiku wa saa ngapi.
No comments:
Post a Comment