Jukwaa Huru la Wazalendo Tanzania limeguswa na hujuma kwa Rais Magufuli
Mei 8 2016 Jukwaa huru la Wazalendo Tanzania limekutana na Waandishi wa Habari Dodoma ili kutoa tamko lao kuhusu hujuma dhidi ya Rais John Pombe Magufuli.
Katibu wa jukwaa hilo Mtela Mwampamba amesema…>>>’Kwa
miaka mingi Watanzania tumekuwa tukipiga kelele tukilia juu ya kero
mbalimbali za Serikali kushindwa kupambana na watumishi wasio wema na
wabadhirifu, mafisadi, wala rushwa na wahujumu uchumi‘
‘Vita
hii tumekuwa tukipigana sisi wanyonge na baadaye ikaungwa mkono na
makundi mbalimbali wakiwemo wanasiasa, Sasa tumempata Rais Magufuli
anayefanya kazi bila kuchoka kuifikisha Tanzania tunakokutaka, wanasiasa
hao wamegeuka na wanaanza kumhujumu‘
‘Tumeshangazwa
zaidi tunaposoma na kusikia katika vyombo vya habari baadhi ya
wanasiasa wakianza kumkejeli Rais Magufuli eti anaendesha nchi kinyume
cha sheria na kuipeleka katika utawala wa kiimla‘
‘Ni
kwasababu hii, sisi wazalendo tunasema hoja za wanasiasa na wasomi
kusema Rais analeta utawala wa kidikteta kwa kutumbua majipu tunaona ni
hali zilizojaa hisia binafsi na zaidi ujasiri wa hujuma‘
Mwampamba hajaacha lipite hili la Sukari, nalo anasema…>>’Baadhi
ya wafanyabiashara kuficha badhaa muhimu ya sukari, tunatumia fursa hii
kuwakumbusha kuwa waachane na hujuma hiyo mara moja.‘
‘Wanaoendesha
uhujumu huo wa uchumi ni sawa na hawa wanasiasa wanaoendekeza hujuma
dhidi ya Rais Magufuli ili asiendeleze mageuzi ambayo Watanzania wenyewe
waliyataka na wameyasubiri kwa muda mrefu‘
Kwa habari, mmatukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment