Wiki hii
kuliripotiwa kutokea kwa kimbunga kikali kiliambatana na mvua pamoja
upepo mkali ambao umevikumbuka visiwa hivyo. Kimbunga kilichopewa jina
la Hurricane Matthew kimesababisha madhara makubwa kwa kuharibu miundo mbinu, majumba ya kuishi, watu wamepoteza maisha na wengine makazi ya kuishi.
Ripoti
ya Umoja wa Mataifa, Kimbunga hicho kimeacha madhara kwa watu
takribani 350,000 na kuirejesha Haiti kwenye kumbukumbu mbaya ya aina
hiyo iliyowahi kujitokeza miaka sita iliyopita.
Mwakilishi wa UNICEF
nchini Haiti, Marc Vincent amesema kimbunga Matthew ni kibaya zaidi
kuwahi kushuhudiwa nchini humo katika miongo ya karibuni na bila shaka
madhara yake yatakuwa makubwa.
Kimbunga Mathew ambacho ndicho kubwa
zaidi katika visiwa vya Carebean kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita,
kimepiga taifa la Bahamas baada ya kupitia Haiti na Cuba.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linashirikiana na serikali ya Haiti na wadau wengine kusambaza vifaa vya usaidizi kwa waathirika wa kimbunga Matthew kilichopiga Haiti hii leo. UNICEF inasema misaada hiyo ni pamoja na vidonge vya kutakasisha maji na vya kujisafi, wakati huu ambapo watoto zaidi ya Milioni Nne wanatarajiwa kuwa wameathiriwa na zahma hiyo.

No comments:
Post a Comment